Head

✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass

Dalili za Uric Acid Kuzidi Mwilini, Ishara, Takwimu na Vyanzo vyake

Uric acid ni taka inayozalishwa mwilini baada ya kuvunjwa kwa kemikali zinazoitwa purines, ambazo hupatikana kwenye baadhi ya vyakula na pia hutengenezwa na mwili. Kwa kawaida, uric acid hutolewa kupitia figo kwa njia ya mkojo. Hata hivyo, kiwango chake kinapozidi (hyperuricemia), kinaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya kiafya.

Takwimu duniani

  • Tafiti zinaonyesha kuwa takriban asilimia 20 ya watu wazima duniani wana kiwango cha juu cha uric acid, ingawa wengi hawana dalili mwanzoni.
  • Kati ya watu wenye uric acid nyingi, karibu asilimia 20–25 wanaweza kupata ugonjwa wa gout katika maisha yao.
  • Ugonjwa wa gout unaathiri zaidi ya watu milioni 55 duniani, na idadi inaendelea kuongezeka kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

Dalili za uric acid kuzidi mwilini

1. Maumivu makali ya viungo

Dalili maarufu zaidi ni maumivu ya ghafla kwenye viungo, hasa kidole kikubwa cha mguu. Maumivu yanaweza kuwa makali kiasi cha kushindwa kutembea.

2. Kuvimba na wekundu wa kiungo

Kiungo huvimba, huwa chekundu na kuwa cha moto au kupata hali ya joto/kuhisi kuungua kutokana na mkusanyiko wa uric acid.

3. Kiungo kuwa kigumu kusogeza

Baada ya shambulio la gout, kiungo kichoathirika kinaweza kuwa kigumu kukunja au kunyoosha. Mfano Kidole cha Mguu au Kidole cha Mkono n.k.

4. Maumivu ya mara kwa mara hasa usiku

Mashambulizi mengi ya gout hutokea usiku na yanaweza kumwamsha mtu usingizini.

5. Vinundu chini ya ngozi (Tophi)

Kwa watu wenye uric acid nyingi kwa muda mrefu, hujitokeza vinundu vigumu kwenye vidole, masikioni, mikononi au kwenye viwiko.

6. Mawe kwenye figo(Kidney stones)

Uric acid nyingi inaweza kuathiri figo zako kwa njia mbali mbali ikiwemo kutengeneza mawe kwenye figo(kidney stones) na kusababisha:

  • Maumivu makali ya mgongo au ubavu.
  • Kukojoa Damu kwenye mkojo.
  • Maumivu wakati wa kukojoa.n.k.

7. Kupungua uwezo wa figo kufanya kazi

Iwapo hali itaendelea bila matibabu, inaweza kuharibu figo polepole.

Nini husababisha uric acid kuongezeka?

  • Kula nyama nyekundu kwa kiwango kikubwa na maini mara kwa mara.
  • Kunywa pombe, hasa bia.
  • Vinywaji vyenye sukari nyingi.
  • Unene uliopitiliza.
  • Kuwa na Ugonjwa wa figo.
  • Kuwa na matatizo kama vile Kisukari na shinikizo la damu.
  • Kutumia Baadhi ya dawa kama jamii ya diuretics.

Nani yuko kwenye hatari zaidi?

  • Wanaume.
  • Wanawake baada ya kukoma hedhi.
  • Wenye historia ya gout kwenye familia.
  • Watu wenye uzito mkubwa.
  • Wenye magonjwa ya figo au kisukari.

Jinsi ya kupunguza uric acid

  • Kunywa maji ya kutosha kila siku.
  • Punguza nyama nyekundu na vyakula vyenye purines nyingi.
  • Epuka pombe na vinywaji vyenye sukari nyingi.
  • Punguza uzito ikiwa una uzito uliopitiliza.
  • Fanya mazoezi mara kwa mara.
  • Tumia dawa ulizoandikiwa na daktari ikiwa kiwango ni cha juu au una gout.

Bonus point;

Uric acid nyingi mwilini inaweza isiwe na dalili mwanzoni, lakini ikiachwa bila kudhibitiwa inaweza kusababisha gout, mawe kwenye figo na hata uharibifu wa figo. Ukipata maumivu makali ya viungo, hasa kwenye kidole kikubwa cha mguu, ni muhimu kufanyiwa vipimo na kuanza matibabu mapema.

Je,Unachangamoto hii? Kwa Ushauri Zaidi na Tiba tuwasiliane +255758286584.

Reference;

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584