Head

✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass

Kifo cha mwanamitindo maarufu wa OnlyFans, Christina Ashten Gourkani, mjadala kuhusu usalama wa upasuaji wa urembo umeibuka

Baada ya hukumu ya kifungo cha miaka minne kutolewa dhidi ya mwanamke aliyepatikana na hatia ya kusababisha kifo cha mwanamitindo maarufu wa OnlyFans, Christina Ashten Gourkani, mjadala kuhusu usalama wa upasuaji wa urembo usio rasmi umeibuka tena nchini Marekani.

Vivian Alexandra Gomez, mwenye umri wa miaka 53, alihukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia pamoja na kufanya shughuli za kitabibu bila leseni. Waendesha mashtaka walieleza kuwa Gomez alifanya sindano za silicone kinyume cha sheria kwa Christina Ashten Gourkani, ambaye alifariki mwaka 2023 kutokana na matatizo makubwa ya kiafya yaliyotokana na utaratibu huo.

Gourkani, aliyekuwa na umri wa miaka 44 wakati wa kifo chake, alijulikana mtandaoni kwa kufanana kwa sura na mwonekano na mwanamitindo maarufu . Ripoti zinaeleza kuwa alipatwa na kushindwa kupumua pamoja na kuganda kwa damu kwenye mapafu baada ya kufanyiwa utaratibu wa kuongeza umbo la makalio unaojulikana kama Brazilian Butt Lift.

Kesi hiyo imeibua tahadhari mpya kuhusu hatari za sindano za silicone zinazofanywa na watu wasio na sifa za kitabibu. Madaktari bingwa wa upasuaji wa plastiki wameonya kuwa silicone inaweza kusambaa mwilini, kusababisha maambukizi, kuharibu tishu na hata kuingia kwenye mfumo wa damu, jambo linaloweza kuziba mishipa na kuhatarisha maisha.

Wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa watu wanaotaka kufanyiwa upasuaji au matibabu ya urembo wanapaswa kuhakikisha huduma hizo zinafanywa katika vituo vilivyosajiliwa na wataalamu wenye leseni halali, ili kuepuka madhara makubwa yanayoweza kusababisha ulemavu au kifo.

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584