✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass
Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa huashiria nini? Ukiona usaha halisi, au Vitu kama kamasi nene, ya manjano/nyeupe iliyochanganywa na kinyesi chako, mara nyingi inaonyesha mwitikio wa kinga mwili dhidi ya maambukizi, hali ya uvimbe, au jipu kwenye njia yako ya kumeng'enya chakula n.k. Ni muhimu kutofautisha hili kwa kujua aina ya uchafu unaotoka sehemu ya haja kubwa na unaashiria nini.
Wakati mwingine ni kawaida kuwa na hali ya Kamasi(mucus) kwenye kinyesi chako. Lakini kamasi yenye chembechembe za damu au nyeupe au njano inaweza kuwa dalili ya ugonjwa kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Na hali kama vile tatizo la kupata choo kigumu/kukosa choo(Constipation) au kuharisha zinaweza kusababisha kamasi kwenye kinyesi. Lakini pia kamasi au kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa inaweza kuwa dalili ya magonjwa makubwa. zaidi.
Chanzo cha Kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa
Sababu kubwa za hali hii ya kutokwa na Usaha kwenye haja kubwa ni pamoja na;
- Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.
- Uwepo wa Inflammatory Bowel Disease (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn's disease pamoja na ulcerative colitis
- Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
- Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
- Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa n.k.
Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?
Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?
1.Kunywa maji mengi Kila Siku
2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)
3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya
Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;
-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi
-Unapata maumivu ya Tumbo
-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3
-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika
-Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana
-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?
Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?
Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
Reference;
https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101
https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool


Post a Comment