✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass
Tukio La Afya Lililowafanya Wachezaji Wote Kulia Uwanjani
Mwaka 2003, dunia ya soka ilitikiswa baada ya mchezaji wa Cameroon, Marc-Vivien Foé, kuanguka ghafla uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Colombia kwenye michuano ya Confederations Cup. Hakuguswa na mchezaji mwingine… alianguka mwenyewe katikati ya mchezo.
Madaktari walijaribu kumuokoa kwa haraka lakini baadaye ilitangazwa kuwa amefariki kutokana na tatizo la moyo. Wachezaji walilia uwanjani, baadhi wakishindwa hata kuendelea na mchezo kutokana na majonzi makubwa.
Tukio hilo lilibaki kuwa moja ya simulizi za kusikitisha zaidi katika historia ya mpira wa miguu duniani.
Taja tukio Lingine hapa......


Post a Comment