Choo chenye makamasi,chanzo cha kujisaidia choo chenye makamasi au Usaha
Chanzo au Sababu za Choo chenye makamasi au Usaha
- Maambukizi ya Bacteria au Parasite, ndyo mana ukiwa na Magonjwa kama Vile Amoeba unaweza kupata choo chenye vitu kama Kamasi.
- Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa-Sexually Transmitted Infections (STIs);Mfano wa magonjwa kama Chlamydia endapo yatashambulia eneo la haja kubwa(Rectal infection) huweza kusababisha hali ya kujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na Vitu kama Makamasi(Mucus) au Usaha.
- Kuwa na Jipu au Majibu kwenye eneo la haja kubwa, hii pia huweza kuchangia ukajisaidia kinyesi chenye vitu kama Makamasi au usaha
- Tatizo la Fistula Sehemu ya haja kubwa(Anal Fistula)
- Magonjwa ya uchochezi wa utumbo (Inflammatory Bowel Disease – IBD), (IBD),hapa nazungumzia hali kama vile Crohn's disease pamoja na ulcerative colitis, ambayo yanaweza kusababisha makamasi kwenye choo, damu na maumivu ya tumbo.
- Ugonjwa wa Irritable Bowel Syndrome (IBS), ambapo baadhi ya wagonjwa hupata choo chenye makamasi hasa bila damu.
- Na Wakati mwingine mzio wa chakula(Allergy) au hali ya kutovumilia baadhi ya vyakula(Food Intolerance) inaweza pia kuongeza ute kwenye choo.
Nini cha kufanya ukiwa nyumbani?
Nini unaweza kufanya Ukiwa nyumbani endapo unaona hali ya Usaha au Kamasi kwenye kinyesi chako?
1.Kunywa maji mengi Kila Siku
2.Kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi zaidi(Fibers)
3.Wasiliana na Mtoa huduma wako wa afya
Ongea na Mtoa huduma wa afya Mapema endapo;
-Unatokwa na Usaha au Vitu kama Kamasi na haviishi
-Unapata maumivu ya Tumbo au Misuli ya tumbo kuvuta au kukaza sana
-Unaona Damu kwenye choo
-Unapata hali ya Homa
-Unaharisha,hasa mfululizo kwa zaidi ya Siku 3
-Unapata hali ya kichefuchefu na Kutapika
-Unapungua Uzito bila kujua Sababu ni nini?
Je,Unachangamoto hii? na Unahitaji Msaada zaidi?
Kwa Ushauri zaidi na Tiba tuwasiliane kwa namba +255758286584.
Reference;
https://www.medicalnewstoday.com/articles/310101
https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/mucus-in-stool
Other Links;
Wikipedia – Mucus
https://en.wikipedia.org/wiki/Mucus
Wikipedia – Feces
https://en.wikipedia.org/wiki/Feces
Wikipedia – Ulcerative colitis
https://en.wikipedia.org/wiki/Ulcerative_colitis
Wikipedia – Crohn's disease
https://en.wikipedia.org/wiki/Crohn%27s_disease
Merck Manual Consumer Version – Mucus in Stool
https://www.merckmanuals.com/home
MSD Manual Professional Version
https://www.msdmanuals.com/professional
NCBI Bookshelf
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/
StatPearls (NCBI Bookshelf)
https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430892/


Post a Comment