Head

✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass
Daktari amfanyia Upasuaji Mama kumtoa Mtoto ili kumfanyia upasuaji wa Uvimbe Kisha Kumrudisha tena tumboni
Tukio hili lilitokea nchini Marekani, katika jimbo la Texas, katika hospital ya Texas Children's Hospital huko Houston. Na kwenye Picha hizi zinamhusisha daktari Oluyinka Olutoye, ambaye alikuwa sehemu ya timu iliyofanya upasuaji huo. 

Katika wiki 23 tu za ujauzito, Wadaktari walifanya upasuaji wa kijusi ambao ni nadra na maalum sana kutokea, ili kuondoa uvimbe unaohatarisha maisha kutoka kwa mtoto ambaye hajazaliwa. Wakati wa upasuaji huo, kijusi(fetus) kilitolewa kwa uangalifu kutoka kwenye uterasi huku kikiwa kimeunganishwa na kondo la nyuma(Placenta), na kuruhusu madaktari wa upasuaji kuondoa uvimbe kabla ya kumrudisha mtoto tumboni taratibu ili ujauzito uendelee.

Upasuaji wa kijusi hufanywa tu katika visa vya kipekee ambapo hali mbaya inatishia maisha au afya ya muda mrefu ya mtoto au mama. Operesheni hizi zinahitaji timu ya wataalamu mbalimbali ikiwemo wataalamu wa uzazi, madaktari wa upasuaji wa kijusi, wataalamu wa ganzi, wataalamu wa watoto wachanga, na wataalamu wengine wanaofanya kazi pamoja ili kuwalinda wagonjwa wote wawili katika utaratibu wote.

Kufuatia upasuaji uliofanikiwa, ujauzito uliendelea hadi wiki 36, wakati mtoto wa kike alizaliwa akiwa na afya njema, bila matatizo yoyote.

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584