Showing posts with label Ukanda wa Gaza. Show all posts
Showing posts with label Ukanda wa Gaza. Show all posts

Kampeni ya chanjo kwa watoto yazinduliwa Ukanda wa GazaAfyaclass Forum •

Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF, afya duniani WHO, linalohudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA na wizara ya afya ya Palestina wamezindua kampeni maalum ya chanjo, lishe na ufuatiliaji wa ukuaji wa watoto katika Ukanda wa Gaza, lengo likiwa ni kuwafikia watoto 44,000 waliokosa huduma muhimu za afya kutokana na vita vilivyodumu kwa miaka miwili.

Taarifa ya pamoja ya mashirika hayo imeeleza kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa awamu tatu, Kati ya mwezi huu wa Novemba 2025 mpaka mwezi Januari 2026 ikilenga kuwapatia watoto chanjo dhidi ya magonjwa hatari kama surua, rubella, kifaduro, dondakoo, pepopunda, homa ya ini, kifua kikuu, polio na nimonia.

Awamu ya kwanza itaanza tarehe 9 hadi 18 Novemba 2025. Awamu ya pili na ya tatu za kampeni zinatarajiwa kufanyika Desemba 2025 na Januari 2026, zikiwa na lengo la kurejesha kiwango cha chanjo kama kabla ya vita.

Kabla ya vita, Gaza ilikuwa na kiwango cha chanjo cha zaidi ya asilimia 98 kwa watoto, lakini sasa kiwango cha chanjo kimeshuka chini ya asilimia 70.

0 Comment

Kundi la Hamas lakubali kuwaachia mateka kumi wa IsraelAfyaclass Forum •

Hamas imesema iko tayari kuwaachilia mateka 10 kama sehemu ya mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza, baada ya Israel kutoa kauli ya matumaini kuhusu uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha vita Ukanda wa Gaza.



Taarifa ya Hamas ilitolewa baada ya siku nne za mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja yaliyosimamiwa na Qatar, huku Marekani ikionyesha imani kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku 60 yatafikiwa kabla ya mwisho wa juma hili.

Aidha Israel ikiongeza kwamba bado kuna vikwazo katika mazungumzo hayo ikiwemo suala la kuingia kwa misaada ndani ya Gaza, kuondoka kwa vikosi vya Israel katika eneo hilo na kile walichokiita 'dhamana halisi ya amani ya kudumu'.

"Licha ya ugumu wa mazungumzo juu ya masuala haya hadi sasa kutokana na ukaidi wa Israel, tunaendelea kushirikiana kwa dhati na kwa moyo na wapatanishi ili kushinda vikwazo hivyo, kumaliza mateso ya watu wetu, na kuhakikisha wanatimiza matarajio yao ya uhuru, usalama, na maisha yenye heshima,” sehemu ya taarifa ya Hamas ilisema.

Mapema, Israel ilionekana kuunga mkono matumaini ya Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kumalizika kwa vita hivyo, wakati mazungumzo mjini Doha yakiingia siku ya nne huku kukiwa na taarifa ya kutoridhika kuhusu msimamo wa Israel juu ya misaada ya kibinadamu.

Mkuu wa majeshi ya Israel, Eyal Zamir, amesema katika hotuba ya televisheni kuwa hatua za kijeshi zilizochukuliwa hadi sasa zimeandaa mazingira ya kufikiwa kwa makubaliano ambayo yenye matokeo ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel nyumbani.

Awali, afisa mwandamizi wa Israel akiwa katikati mwa ziara ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu huko Washington alisema, iwapo pande zote mbili zitakubaliana na pendekezo la kusitisha mapigano kwa siku 60, Israel itatumia muda huo kutoa pendekezo la kusitisha mapigano kabisa na Hamas kutakiwa kupokonywa silaha.

"Ikiwa Hamas itakataa, tutaendelea na operesheni za kijeshi huko Gaza." Alisema afisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Rais Donald Trump wa Marekani alikutana kwa mara ya pili na Waziri Mkuu Netanyahu kujadili hali ya Gaza, huku mjumbe wa rais wa Marekani Mashariki ya Kati akionyesha kuwa Israel na Hamas walikuwa karibu kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyopendekezwa na Marekani baada ya vita vya miezi 21.

Hapo awali Trump alitabiri huenda makubaliano yangelifikiwa ndani ya juma hili, hali iliyozua tetesi kuhusu uwezekano wa kutangazwa kabla ya Netanyahu kurejea Israel siku ya Alhamisi.

Mjumbe maalum wa Trump Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, aliwaambia waandishi wa habari siku ya Jumanne kuwa makubaliano yaliyotarajiwa yangelikuwa na kipengele cha kuachiliwa kwa mateka 10 walio hai na 9 waliokufa.

Israel yaendeleza mashambulizi ndani ya Gaza

Shirika la ulinzi wa raia la Gaza limesema kuwa watu 23, wakiwemo watoto wanane, wameuawa katika mashambulizi ya anga ya Israel usiku ya kuamkia leo.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD