Showing posts with label Utafiti. Show all posts
Showing posts with label Utafiti. Show all posts

Vijana barubaru kukabiliwa Zaidi na changamoto ya Afya ya Akili - WHOAfyaclass Forum •

Vijana barubaru kukabiliwa Zaidi na changamoto ya Afya ya Akili - WHO

Kwa mujibu wa Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) uwekezaji wa haraka unahitajika ili kukabiliana na changamoto za kiafya zinazoongezeka kwa vijana barubaru ikiwemo kuhakikisha mahitaji ya afya ya akili pamoja na afya ya uzazi kwa vijana bilioni 1.3 duniani kote yanatimizwa. Kulingana na ripoti hiyo, ujana ni hatua ya kipekee na muhimu katika maendeleo ya binadamu, ambapo misingi ya afya bora ya muda mrefu huwekwa.

"Kuhamasisha na kulinda afya na haki za vijana ni muhimu kwa kujenga mustakabali bora kwa dunia yetu," amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesus huku akionya kuwa kushindwa kushughulikia vitisho vya kiafya vinavyowakabili vijana  baadhi vikiwa vimekuwepo kwa muda mrefu na vingine vikiwa vipya kutaleta athari kubwa kwa vijana wenyewe na kusababisha gharama kubwa kwa jamii. "Hii inafanya uwekezaji katika huduma na programu za afya ya vijana kuwa si tu jambo la kimaadili bali pia ni jambo lenye maana kiuchumi," ameongeza.

Ripoti hiyo Mpya imezinduliwa hivi karibuni ikiwa kuna mkutano wa mustakabali wa Umoja wa Mataifa na imebainisha uwepo wa wasiwasi kwenye afya ya vijana kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, ikionesha hitaji la hatua za haraka.

Takribani kijana mmoja kati ya vijana 7 duniani wanakabiliwa na matatizo ya afya ya akili kama vile unyogovu(depression) na wasiwasi(anxiety). Aidha, kiwango cha upungufu wa damu kwa wasichana vijana hakijabadilika tangu mwaka 2010, huku karibu kijana mmoja kati ya vijana 10 wakiwa wanakabiliwa na Unene kupita kiasi.

Maambukizi ya magonjwa ya zinaa (STIs), ikiwa ni pamoja na;

  • kaswende,
  • klamidia,
  • Pamoja na virusi vinavyosababisha malengelenge sehemu za siri,

yanazidi kuongezeka, hali ambayo inahitaji tiba mapema ili kuepusha athari za muda mrefu kwa afya.

Vile vile, ghasia, ikiwemo uonevu, huathiri mamilioni ya vijana kila mwaka, na kuwa na athari mbaya kwa afya zao za kimwili na kiakili.

Wasiwasi kuongezeka:

Wasiwasi umeongezeka zaidi, Kwani vizuizi vinavyosababisha vijana kutokupata huduma za afya ya uzazi vimeongezeka, huku Sera Zinazoboresha upatikanaji wa huduma za magonjwa ya zinaa na VVU kwa vijana zikiendelea kutelekezwa. Hatua hizi zinapunguza mwitikio wa vijana kutafuta huduma, hali inayosababisha athari za kiafya za muda mrefu.

Ripoti hiyo pia inasisitiza changamoto nyingine kubwa zinazokabili mustakabali wa vijana, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, migogoro, na ukosefu wa usawa. Hata hivyo, waandishi wa ripoti hiyo wamebainisha kuwa mafanikio yanawezekana kupitia uwekezaji sahihi na msaada.

Mafanikio kama vile kupungua kwa maambukizi ya VVU miongoni mwa vijana, kupungua kwa mimba za utotoni, na kupungua kwa vitendo vya ukatili kama vile ukeketaji na ndoa za mapema ni matokeo ya juhudi za pamoja. Aidha, ongezeko la wasichana wanaosalia shuleni limechangia katika kuboresha afya za vijana, na tangu mwaka 2000, idadi ya watoto wenye umri wa kwenda sekondari wasio shuleni imepungua kwa karibu asilimia 30.

Wito wa ripoti hiyo

Kwa kuzingatia changamoto hizi, ripoti hiyo inatoa wito wa uwekezaji zaidi katika afya na ustawi wa vijana, kwa kuzingatia masuala ya elimu, huduma za afya, na lishe bora. Waandishi wanasisitiza umuhimu wa kuweka sheria na sera zinazolinda haki za vijana, huku mifumo ya afya ikitakiwa kuwa rafiki kwa mahitaji yao maalumu.

"Vijana wana uwezo mkubwa wa ubunifu wanapopewa fursa ya kushiriki katika maamuzi kuhusu ustawi wao na mustakabali wao," amesema Rajat Khosla, Mkurugenzi Mtendaji wa Ushirikiano wa Afya ya Mama, Watoto wachanga, na Watoto (PMNCH) na kuongeza kuwa "Viongozi lazima wasikilize sauti za vijana na kuhakikisha wanakuwa washirika muhimu katika maamuzi."

Viongozi wa dunia, katika mkutano wa Afya Duniani mwaka huu, wameahidi kuongeza juhudi za kuboresha afya ya vijana, ikiwa ni sehemu ya ahadi zao katika mkataba wa mustakabali wa Umoja wa Mataifa. Utekelezaji wa ahadi hizi utakuwa muhimu katika kulinda na kuboresha afya na ustawi wa vizazi vya sasa na vijavyo.

Source Credits|Link; Via

United Nations(UN)

Shirika la Afya Duniani(WHO)

Afyaclass(Reviewed&edited)

0 Comment

Je! unajua kwamba Jua huweza kuimarisha afya yako ya akili? Afyaclass Forum •

 Je! unajua kwamba Jua huweza kuimarisha afya yako ya akili? 

Tafiti zinaonyesha Mwangaza wa jua husaidia kuongeza kemikali katika ubongo wako inayoitwa serotonin, ambayo inaweza kukupa nishati zaidi na kukusaidia kuwa mtulivu, kuwa chanya, na kuongeza umakini(focused).

Unapofikiria jua, wazo lako la kwanza linaweza kuwa juu ya uharibifu unaoweza kutokea, na ni kiasi gani inaweza kusababisha shida kubwa za kiafya.  

Lakini je, unajua kwamba kukaa kwa dakika 15 tu kwenye jua kila siku kunaweza kuongeza viwango vyako vya vitamini D, kukusaidia kulala vizuri na hata kukusaidia kudumisha Uzito wenye afya(kudhibiti Uzito mkubwa)?

0 Comment

WHO: Mtu mmoja hufa kwa kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sitaAfyaclass Forum •

WHO: Mtu mmoja hufa kutokana na kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sita

Shirika la Afya Duniani (WHO) siku ya Jumanne lilisema kuwa mtu mmoja hufa kutokana na kuumwa na nyoka kila baada ya dakika nne hadi sita, na zaidi ya theluthi moja ya waathiriwa wote wana umri wa chini ya miaka 20.

“Wakati nyoka wenye sumu husambaa kwa upana katika maeneo ya dunia ya kitropiki na baridi, na hatari kubwa zaidi kwa afya ya umma hutokea katika mataifa ya kipato cha chini na cha kati ‘ David Williams, mtaalamu wa WHO kuhusu nyoka na kuumwa na nyoka, aliambia mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Matamshi yake yalikuja kabla ya Siku ya Kimataifa ya Uhamasishaji kuhusu Kuumwa na Nyoka, ambayo huadhimishwa kila Septemba 19.

Kulingana na mtaalamu huyo, visa milioni 1.8-2.7 vya kuumwa na nyoka hutokea kila mwaka, na hivyo kusababisha vifo kati ya 81,000-138,000.

Wengi wa kuumwa na nyoka hutokea Asia, Afrika, Marekani Kusini, Williams alisema, wakati inakadiriwa watu milioni 1.2 walikufa kutokana na kuumwa na nyoka nchini India pekee mwaka 2000-2019 – wastani wa 58,000 kila mwaka.

Alisisitiza kuwa si kila mtu anayeumwa na nyoka husababisha vifo, lakini kwa kila anayefariki dunia, watatu zaidi hubaki na “ulemavu wa muda mrefu au wa kudumu” mfano kovu la mwili kudhoofika au hata kukatwa viungo.

Akizungumzia tishio hili, alisema maeneo yaliyoathiriwa zaidi na kuumwa na nyoka hayana uwezo wa kupata matibabu ya kutosha.

Makala Zaidi,Fahamu Kuhusu Kuumwa na Nyoka

KUUMWA NA NYOKA:

janga hili linazikumba jamii nyingi zilizo kwenye maeneo ya joto kote duniani.  Takribani visa milioni 1.8-2.7 vya kuumwa na nyoka hutokea kila mwaka, na hivyo kusababisha vifo kati ya 81,000-138,000.

WATU WALIOKATIKA HATARI

1. Wavuvi

2. Wawindaji

3. Wakulima vijijini

4. Watoto wadogo

5. Watu wanaoishi kwenye mazingira/nyumba duni na wasio na elimu ya kujikinga na wasio na huduma za afya katika maeneo yao. 

Nyoka wenye sumu huweza kugawanywa kwenye makundi makuu mawili nayo kitaalamu ni 

1. Crotalinae

2. Elapidae

Hii ni kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika hasa marekani. 

Tofauti za makundi haya ni, 

1. Crotalinae

Nyoka hawa sifa zao ni

- wana vichwa vya pembe tatu

- mboni za macho yao huwa mfano wa mviringo husio sawa

- wanavishimo joto usoni

- wana chonge/meno makubwa mfano wa msitatili kwa mbele. 

2. Elapidae

Nyoka hawa sifa zao ni

- wana vichwa vya duara

- mboni zao ni za mviringo

- hawana chonge

- wamegawanyika katika makundi makuu matatu. 

Ajari za kuumwa na nyoka hasa miguuni ni nyingi sana. 

NINI HUTOKEA UUMWAPO NA NYOKA

Nyoka katika kundi la crotalinae huweka sumu zao chini ya ngozi ya binadamu wamuumapo yaani katika ukanda/tishu wa mafuta.  Mara chache sumu huweza fika kwenye misuli na hivyo kupelekea kufa kwa seli na kuoza kwa eneo ilo na hata shida katika mfumo wa mzunguko wa damu. Sumu hizi zinamadhara katika damu. 

Iwapo sumu itapelekea kuharibika na kuvuja kwa mishipa midogo ya damu, hali hii huweza kupelekea kukusanyika kwa majimaji ktk mapafu na mfumo mzima wa upumuaji, shinikizo la chini la damu nk. Pia sumu hizi zinaweza pelekea kuharibika kwa mfumo mzima wa ugandaji wa damu na hivyo kupelekea kutokwa na damu nyingi. 

Sumu hizi zina vijenzi vya protini amino asidi,  mafuta wanga na madini mbalimbali yakiwemo zinc. Protein hizi hupelekea kuharibika kwa ukuta ulindao seli,  viunganishi vya seli na hivyo kuleta madhara makubwa mwilini. Madhara yanategemea wingi/kiwango na ubora wa sumu yenyewe. 

Sumu za elapidae zinavijenzi ambavyo hushambulia mfumo mzima wa fahamu na hivyo kusababisha madhara makubwa ndani ya muda mfupi ikiwemo kushindwa kupumua. 

KUUMWA NA NYOKA,DALILI ZAKE

crotalinae husababisha

1. Kuvimba

2. Maumivu makali mfanano wa kuungua na moto

3. Kuvilia damu

4. Malengelenge

5. Iwapo matibabu yatachelewa hupelekea kuoza kwa eneo husika

Dalili nyingine ni

6. Kichefu chefu na kutapika

7. Shida katika kuona

8. Ladha ya chuma mdomoni

9. Kukakamaa kwa misuli

Elapidae husababisha

1. Kushindwa kupumua

2. Kushindwa kufanya kazi kwa milango ya fahamu

3. Kupooza kwa sehemu mbalimbali za mwili

NINI KIFANYIKE BAADA YA KUUMWA NA NYOKA. 

Ziko njia mbalimbali za asili/ tiba mbadala ambazo zimekuwa zikitumika. Baadhi ya njia hizi zinapingwa kitaalamu na badhi zinafanyiwa uchunguzi.  Njia kama kuchana chana kidonda,  kuweka manyoya ya ndege au kutumia denge,  kunyonya sumu,  kufunga kamba na nyinginezo zimeonekana kuwa na madhara zaidi ya faida hivyo zinapingwa na wataalamu. 

Iwapo mtu ameumwa na nyoka haraka fanya yafuatayo. 

1. Toka/ mtoe eneo ambapo tukio imetokea

2. Ondoa kitu chochote kinachobana eneo hilo kuzuia madhara iwapo uvimbe utatokea.  Tambua nyoka wengi wenye sumu hawasababishi vifo. 

3. Epuka kutumia njia za asili 

4. Safisha kidonda kisha nyanyua eneo husika juu ya usawa wa moyo na kisha haraka muwaishe hospitali. Huko matibabu yatafanyika kama inavyostahiri. 

0 Comment

Takwimu Mpya;Watanzania asilimia 9% huishi na magonjwa ya kisukariAfyaclass Forum •

Takwimu Mpya;Watanzania asilimia 9% huishi na magonjwa ya kisukari

Takwimu za magonjwa yasiyoambukiza ya mwaka 2012 inaonesha watanzania asilimia 9 wanaishi na magonjwa ya kisukari huku asilimia 26 wana magonjwa ya moyo .

Hayo ameyasema Jana Jijini Dar es salaam Happy Nchimbi Meneja mradi Shirikisho la vyama vya magonjwa Yasiyoambukiza (TANCDA) kwenye semina ya iliyoandaniliwa na TANCDA baina ya waandishi wa habari na Wasanii yenye lengo la kuwapatia elimu juu ya maganjwa yasiyoambukiza

Happy amesema magonjwa hayo yasiyoambukiza kwenye takwimu hizo inaonesha watanzania wengi hawafanyi mazoezi , kutumia vitu vyenye mafuta na sukari pamoja na mtindo wa maisha.

Aidha Happy amesema magonjwa waliyagusia waandishi wa habari na wasanii yasiyoambukiza ni wagonjwa ya kisukari, saratani, magonjwa ya moyo, selimundu magonjwa ya mfumo wa hewa na afya ya akili ambapo amesema elimu hiyo waliyopewa itawasaidia jamii kwa kiasi kikubwa kuelewa magonjwa hayo yasiyoambukiza na kubadili mfumo wa maisha .

Kwa upande wake Dk.Ana Nswila Mshauri wa magonjwa yasiyoambukizwa Shirikisho ka vyama vya magonjwa yasiyoambukizwa (TANCDA)amesema magonjwa yasiyoambukizwa yamekuwa ni tatizo kubwa katika nchi hivyo kutokana na tatizo hilo kuna njia mbalimbali za kuweza kuzuia kwa kuwapa watu elimu juu ya magojwa hayo yasiyoambukizwa

Nae Prof.Andrew Swai Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambukiza (TANCDA) amewashauri wananchi kutokutumia vyakula vilivyosindikwa, kutokukoboa nafaka ,kutokuongeza sukari kwenye vyakula mbalimbalimbali.

Aidha miongoni mwa waandishi waliopata elimu hiyo ya magonjwa yasiyoambikiza Kissa Daniel amesema atakuwa mfano wa kuigwa kwa kutoa taarifa kwa jamii juu ya magonjwa yasiyoambukizwa.

0 Comment

Uhaba wa maji safi na Salama kuchangia kuongezeka kwa milipuko ya kipindupinduAfyaclass Forum •

Uhaba wa maji safi na Salama kuchangia kuongezeka kwa milipuko ya kipindupindu

Uhaba wa maji safi na salama na umaskini watajwa kuchangia kuongezeka kwa milipuko ya kipindupindu mwaka jana. 

Taarifa Mpya: Kwa Mujibu wa Takwimu za shirika la Afya Duniani(WHO)

Migogoro, mabadiliko ya tabianchi, uhaba wa maji safi na salama, umaskini,na watu kuhama makazi yao kutokana na kuibuka na kuzuka upya kwa migogoro na majanga ya asili - yote yalichangia kuongezeka kwa milipuko ya kipindupindu mwaka jana.

Rejea Link;

https://x.com/WHO/status/1831367936394645756?t=SXCeowMmpo6lBy5yiWV6Tg&s=19

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD