Mfahamu Papa Mpya,Leo XIV,jina la kuzaliwa Robert Francis Prevost
Papa Leo XIV – Maelezo na Wasifu
Jina la kuzaliwa: Robert Francis Prevost
Tarehe ya kuzaliwa: 14 Septemba 1955, Chicago, Marekani
Rai: Marekani na Peru
Elimu na Lugha:
- Shahada ya Hisabati – Chuo Kikuu cha Villanova (1977)
- Mafunzo ya teolojia na falsafa
- Anazungumza Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kiitaliano, Kireno; anasoma Kilatini na Kijerumani
Huduma ya Kiroho:
- Aliwekwa wakfu kuwa padre (1982) katika Shirika la Mtakatifu Augustino
- Mmisionari nchini Peru kwa miaka mingi
- Askofu wa Chiclayo, Peru (2015–2023)
- Mkuu wa Shirika la Augustino (2001–2013)
- Mkuu wa Idara ya Maaskofu, Vatican (2023–2025)
Uchaguzi wa Kipapa:
- Papa Francis alifariki 21 Aprili 2025
- Mkutano wa makardinali (Conclave) ulifanyika 7–8 Mei 2025
- Alichaguliwa Papa katika duru ya nne ya upigaji kura
- Alichukua jina la Leo XIV, Papa wa kwanza kutoka Marekani katika historia
Maono na Msimamo:
- Kipaumbele: amani, mshikamano, huduma kwa waliotengwa
- Kuendeleza mageuzi ya uwazi na uwajibikaji n.k.
Hotuba ya Kwanza:
Alianza kwa kusema: “Amani iwe nanyi,” akisisitiza matumaini mapya kwa Kanisa Katoliki duniani.
Reply
image quote pre code