Viwango vya kemikali zenye sumu katika mchele kuongezeka
Mchele ni chakula kikuu kwa zaidi ya nusu ya Idadi ya watu duniani. Hutumiwa kila siku na watu wengi zaidi kuliko ngano au mahindi.
Na tafiti za hivi karibuni zinaonyesha,kadiri uzalishaji wa kaboni unavyoongezeka, na joto kuongezeka duniani, viwango vya kemikali zenye sumu katika mchele huongezeka.
Uwepo wa kemikali hizi katika mchele umejulikana kwa muda mrefu kuwa tatizo.
Karibu mchele wote una kemikali yenye sumu. Kemikali hii inayotokea kiasili inaweza kujilimbikiza kwenye udongo wa mashamba ya mpunga, na kuchafua nafaka za mpunga zinazolimwa.
Lakini kiasi kinachopatikana katika nafaka za mchele kinaweza kutofautiana kwa kiasi kikubwa, kutoka chini ya mipaka inayopendekezwa na mashirika ya udhibiti hadi viwango vya juu zaidi.
Nchini Brazil,kwa kawaida uwepo wa kemikali za sumu katika mchele si tatizo.
Kemikali yenye sumu katika mchele husababisha hatari kiafya, hasa kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi.
Mamlaka ya Kitaifa ya Usimamizi wa Afya ya Umma ya Brazil (Anvisa) inaeleza kuwa kwa kuwa kemikali hizi hupatikana kwa asili katika ardhi, inaweza pia kuwepo kwenye maji na vyakula.
Kwa sababu hiyo, kuna kikomo cha juu kilichowekwa kisheria kuhusu kiasi cha sumu hiyo kinachokubalika kwenye chakula.
Kiwango cha juu cha kemikali hiyo kinachoruhusiwa nchini Brazil ni:
0.20 mg kwa kila kilo ya mchele mweupe
0.35 mg kwa kila kilo ya mchele wa brown (mchele wa maganda)
Bruno Lemos Batista, profesa wa kemia katika Chuo Kikuu cha Shirikisho cha ABC (UFABC), mmoja wa watafiti wa kwanza kuchunguza kuhusu kemikali hii katika vyakula nchini Brazil, anasema kuwa tafiti zake za hivi karibuni zinaonyesha kuwa viwango vya arseniki viko ndani ya mipaka ya kimataifa na ya sheria ya Brazil.
Tathmini ya mwisho ya Anvisa ilifanyika mwaka 2023, na pia ilibaini kuwa hali ilikuwa ya kawaida.
Hata hivyo, Lemos anaonya kwamba hata kiasi kidogo cha kemikali yenye sumu isiyo ya kikaboni kinachopatikana kupitia chakula au maji ya kunywa kinaweza kusababisha; Saratani,Magonjwa ya moyo na hata Kisukari.
Anasema pia kuwa, "kama tungeweka kiwango sifuri cha arseniki katika vyakula, huenda tusingekuwa na chakula kabisa cha kutufaa kula." Kwa sasa, viwango vilivyowekwa kwa mchele vinahusishwa na matukio machache sana ya magonjwa yanayosababishwa na kemikali hiyo.
"Hii hupunguza hatari na kuruhusu matumizi ya mchele, lakini hatari bado ipo," anaongeza Lemos.
Watafiti duniani kote wanaendelea kutafuta mbinu za kupunguza kemikali yenye sumu kwenye mchele.
Wakati huo huo, kuna njia za kupika mchele zinazoweza kusaidia kuondoa sehemu ya kemikali hiyo hatari kwenye nafaka.
Lakini tafiti mpya kuhusu mkusanyiko wa arseniki isiyo ya kikaboni zimeonesha kuwa tatizo linaweza kuongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi.
Watafiti walipanda aina 28 tofauti za mchele katika maeneo manne tofauti nchini China, chini ya hali ya majaribio kwa kipindi cha miaka 10.
Waligundua kuwa viwango viliongezeka kadri viwango vya hewa ya kaboni (CO₂) kwenye anga na joto la dunia vilivyoongezeka.
Baadaye, wataalamu wa magonjwa walichunguza mwenendo wa kisayansi kuonesha jinsi viwango hivyo vya kemikali yenye sumu vinavyoweza kuathiri afya ya watu kwa kuzingatia matumizi ya sasa ya mchele.
Walibaini kuwa ongezeko hilo la viwango vya kemikali yenye sumu linaweza kusababisha hadi kiasi cha watu milioni 19.3 kupata ugonjwa wa saratani nchini China pekee.
Reply
image quote pre code