Utajuaje unaugua Ugonjwa wa chikungunya?
Kulingana na WHO dalili kuu za Ugonjwa wa chikungunya ni homa ya ghafla ikiambatana na maumivu ya viungo.
Dalili nyingine za kawaida ni maumivu ya misuli, kuumwa na kichwa, kuhisi kichefuchefu na kutapika, kuhisi uchovu na kutokwaa vipele. Maumivu ya viungo yanachosha kwani hudumu kwa siku moja hadi wiki kadhaa.
Dalili za chikungunya huonekana kati ya siku 4 na 7 baada ya mgonjwa kung'atwa na mbu aliyebeba vimelea vya chikungunya. Kwa ujumla dalili nyingi hudumu kwa siku 2 hadi 3 na ni nadra sana mtu kufa kwa chikungunya.
Baadhi ya wagonjwa hupona baada ya siku chache lakini wakati mwingine maumivu ya viungo yanaweza kudumu kwa wiki, miezi au hata zaidi
Nani yuko hatarini kupata chikungunya?
Msafiri anakabiliwa na tishio la kupata virusi vya chikungunya ikiwa utazuru nchi au ameneo ambayo yana mlipuko wa ugonjwa huo.
Kabla ya kusafiri, unashauriwa kuwasiliana na mtoa huduma wako wa afya au kufuatilia taarifa za mashirika ya afya kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kubaini kama sehemu unayozuru inakabiliwa na mlipuko wa ugonjwa wa chikungunya.
Mama mjamzito aliye na virusi anaweza kumuambukiza mtoto aliye tumboni. Hata hivyo hakuna ushahidi unaoonyesha kwamba virusi vinaweza kueneakwa mtoto mchanga kupitia maziwa ya mama.
Lakini, wanawake ambao ni wajawazito wanaokaribia kujifungua wanashauriwa kusafiri kwenda maeneo yaliyo na mlipuko wa virusi vya chikungunya kwani zinaweza kupita kwa mtoto wao wakati wa kujifungua.
Athari za chikungunya ni zipi?
Baadhi ya wagonjwa hupona kikamilifu, lakini wakati mwingine maumivu ya viungo yanaweza kudumu kwa miezi kadhaa au hata miaka.
Matukio ya mara kwa mara ya matatizo ya jicho, mfumo wa mishipa ya fahamu na moyo yameripotiwa, pamoja na malalamiko ya utumbo.
Matatizo makubwa si ya kawaida, lakini ugonjwa huo unaweza kuchangia sababu ya kifo kwa wazee.
Mara nyingi dalili za watu walioambukizwa huwa hafifu na huenda maambukizi yasitambuliwe au kutambuliwa kimakosa katika maeneo ambayo homa ya dengue pia hutokea.
Chikungunya ina tiba?
Hakuna tiba mahususi dhidi ya virusi vya chikungunya na hakuna chanjo maalum ya kumkinga mtu dhidi ya chikungunya. Hata hivyo chanjo kadhaa zinatengenezwa kwa sasa ili kukabiliana na magonjwa yanayoenezwa na mbu.
Wataalamu wa afya wanasema kile ambacho mtu anapata iwapo amepatikana na chikungunya ni matibabu ya kudhibiti dalili zaidi na kupunguza maumivu.
Maumivu kwa kiasi kikubwa yanadhibitiwa kwa kutumia dawa za kupunguza homa na maumivu ya mwilini.
Anayeugia chikungunya pia anashauriwa kunywa maji kwa wingi na kupata wasaa wa kupumzika.
Aspirini na dawa zingine za kupunguza maumivu na uvimbe hazipaswi kutumiwa hadi pale itakapothibitishwa kuwa mgonjwa hana dengue, kwani akipatiwa bila taarifa mahsusi mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutokwa na damu.
REPLY HAPA
image quote pre code