Rais Paul Biya wa Cameroon ametangaza rasmi kuwa atawania tena kiti cha Urais wa Nchi hiyo kwa muhula wa nane (8) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Tangazo la uamuzi huo amelitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X akisema atakuwa Mgombea katika uchaguzi wa Oktoba 12 kupitia Chama chake cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM) ambacho yeye ndiye Mwenyekiti wake.
Biya ambaye kwa sasa ana umri miaka 92, ameitawala Cameroon kwa miaka 43 ambapo hata hivyo kwenye miaka ya hivi karibuni hali dhaifu ya afya yake imekuwa chanzo cha mjadala Nchini humo.
Washirika wake wawili wa zamani wamejitenga naye na sasa wanawania pia kiti cha Urais ikiwemo Waziri Mkuu wa zamani Bello Bouba Maigari atakayekuwa Mgombea wa Chama cha NUDP.
REPLY HAPA
image quote pre code