Je,Unaogopa Kula Nyanya? unajua una hali gani ya kiafya? Food phobia
Dunia ina mambo… kuna watu wanaogopa kula kama vile ni sumu!
Hii si utani—kuna hali ya kisaikolojia inaitwa food phobia, ambapo mtu anaweza kuogopa chakula fulani bila sababu ya moja kwa moja. Wapo watu ambao hata wakiona nyanya tu wanahisi kichefuchefu, hofu au mapigo ya moyo kwenda kasi.
Kinachoshangaza zaidi, zamani sana nyanya zilikuwa zinaitwa “tunda la sumu” katika baadhi ya maeneo ya dunia, watu waliamini zinaweza kuua. Ilichukua miaka mingi kwa watu kuanza kuziamini na kuzila kama chakula salama.
Leo hii, wakati wengine wanazila kila siku kwa afya, bado kuna watu wachache duniani wanazikwepa kabisa kwa hofu isiyoelezeka.
Kweli dunia ina mambo… chakula unachokiona cha kawaida kwako, kwa mwingine kinaweza kuwa chanzo cha hofu kabisa!





Post a Comment
Related Discussions...