Head

✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass

 JE, POMBE hupunguza testosterone na Ubora wa mbegu za Kiume?

Ndiyo, pombe inaweza kuathiri viwango vya testosterone na Ubora wa mbegu za kiume,

Unywaji pombe huweza kuathiri vibaya ubora wa manii(Sperm quality), idadi ya mbegu(Count), na mwendo wake(motility). Pia,huweza kuvuruga usawa wa homoni, ambao unaweza kusababisha kasoro za kimuundo na kupungua kwa uzazi(Fertility). Hii inamana kama unakunywa pombe na unachangamoto ya kupata watoto,Fikiria pia jambo hili jinsi ya kulidhibiti.

Tafiti zinaonyesha kuwa unywaji wa pombe, hasa kwa kiasi kikubwa au mara kwa mara, unaweza:

1.Kupunguza uzalishaji wa testosterone kwa muda.

2.Kuongeza homoni ya mfadhaiko (cortisol), ambayo inaweza kuathiri utengenezaji wa testosterone.

3.Kupunguza ubora wa mbegu za kiume na kuathiri uwezo wa uzazi ikiwa unywaji ni wa muda mrefu na wa kupindukia.

Pia, usingizi wa kutosha, lishe bora, mazoezi ya mara kwa mara na uzito wa mwili unaotakiwa(Controlled body weight) vina mchango mkubwa katika kudumisha viwango vizuri vya vya hormone ya kiume(testosterone).

Na tafiti za hivi karibuni;"Shirika la Afya Duniani(WHO) Linasema matumizi ya kiwango chochote cha pombe yana madhara kwa Mtumiaji".

Vyanzo: World Health Organization (WHO), National Institutes of Health (NIH), na tafiti zilizochapishwa kwenye Alcohol and Alcoholism pamoja na Journal of Clinical Endocrinology & Metabolism.

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584