Head

Papai linaweza kusaidia kwa Maumivu ya hedhi kwa Mwanamke

Papai lina vimeng'enya asilia(natural enzymes) kama vile papain ambavyo vinaweza kusaidia kudhibiti mtiririko wa damu wakati wa hedhi na kupunguza usumbufu unaohusiana na maumivu ya tumbo au mizunguko isiyo ya kawaida.

Linapotumiwa kwa kiasi, mara nyingi hujumuishwa katika lishe za asili kwa ajili ya kuleta ahueni kwa usumbufu unaohusiana na hedhi.

Tunda hili pia husaidia usawa wa estrojeni, ambapo ni muhimu katika udhibiti wa tatizo la homoni Imbalance na kusaidia mzunguko wa hedhi kuwa Sawa.

Utafiti wa Indonesian Journal of Obstetrics and Gynecology ulionyesha kuwa matumizi ya papai yalihusishwa na maboresho ya mzunguko wa hedhi kwa baadhi ya wanawake waliokuwa wakitumia DMPA(Depot Medroxyprogesterone Acetate),Au kwa Kifupi Depo Injection, Sindano za uzazi wa mpango.

Chanzo;

https://inajog.com/index.php/journal/article/view/2303

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584