Showing posts with label Shirika la Afya Duniani (WHO). Show all posts
Showing posts with label Shirika la Afya Duniani (WHO). Show all posts

New:Afyaclass Disease List 2025,Orodha ya Magonjwa Yaliyosumbua sana Dunia 2025Afyaclass Forum •

Hapa ni orodha ya magonjwa na matatizo ya kiafya yaliyosumbua sana dunia mwaka 2025, ikijumuisha magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na milipuko mikubwa iliyoripotiwa na Shirika La afya duniani: Katika Orodha hii namba si chochote,Wala haya sio magonjwa yote ni baadhi tu;


Magonjwa ya Kuambukiza (Infectious Diseases)

1. Ugonjwa wa kifua kikuu-Tuberculosis(TB)

Bakteria wanaosababisha ugonjwa wa mapafu,Kifua kikuu au TB bado ni tishio kubwa na inasababisha maelfu ya vifo kila mwaka.

2. COVID-19 na Mawimbi ya Virusi Vipya

Ingawa si Ugonjwa mpya kama awamu ya 2020, bado COVID-19 na mabadiliko ya virusi vyake yanachangia vifo na ugonjwa huu kuenea kote duniani.

3. Ugonjwa wa Surua (Measles)

Kupungua kwa chanjo kumeleta kuongezeka kwa kesi za Ugonjwa wa Surua, hasa miongoni mwa watoto.

4. Ugonjwa wa Kipindupindu(Cholera)

Milipuko mikubwa ya Ugonjwa wa Kipindupindu imeendelea katika nchi nyingi, ikisababisha maambukizi na vifo vingi, hasa maeneo yenye maji na usafi duni.

5. Ugonjwa wa Homa ya Dengue

Dengue bado inasababisha maambukizi makubwa katika nchi 90 na inaripotiwa visa vingi zaidi ya milioni kadhaa.

6. Ugonjwa wa Homa ya Nyani-Mpox (Monkeypox)

Milipuko ya mpox (pia inajulikana kama monkeypox) imeendelea kufuatilia dunia tangu 2023–2025 kama janga la kiafya la kimataifa.

7. Ugonjwa wa Malaria

Ingawa kuna mafanikio ya kudhibiti malaria, milipuko bado inatokea na inasababisha vifo hasa kwa watoto.

Magonjwa Makubwa Yasiyo ya Kuambukiza (Non-Communicable Diseases, NCDs)

Magonjwa haya ndio yanayosababisha vifo vingi zaidi duniani, mara nyingi kutokana na mtindo wa maisha, lishe mbaya, Uvutaji wa sigara, na uchafuzi wa hewa:

1. Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (Cardiovascular Diseases)

Mfano wa magonjwa hayo yanayoathiri moyo ni pamoja na;

  • Shambulio la Moyo(Heart attack):Ugonjwa wa moyo kama vile mshtuko wa moyo(Heart attack) ni chanzo kikuu cha vifo duniani.
  • Ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu ndani ya moyo mfano; Coronary artery diseases.
  • Tatizo la mapigo ya moyo kutokueleweka-Irregular heartbeats (arrhythmias)
  • Tatizo kwenye muundo wa moyo ambapo unazaliwa nalo (congenital heart defects)
  • Tatizo la moyo kutanuka
  • Tatizo la Moyo kujaa maji
  • Ugonjwa wa kwenye misuli ya Moyo
  • Ugonjwa wa kwenye Valve za moyo
  • Ugonjwa wa kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo n.k

2. Saratani mbali mbali (Cancers)

Saratani ni mojawapo ya ugonjwa mbaya unaoongoza kwa vifo duniani.

Saratani zilizoongoza kutokea

Saratani Zinazoongoza kwa Vifo Duniani:

(i). Saratani ya Mapafu: (1.8 million deaths, 18.7% of the total cancer deaths)

Sababu kuu ya vifo vya saratani duniani kote, kwa jinsia zote mbili kwa pamoja

(ii). Saratani ya utumbo mpana:(colorectal cancer (900 000 deaths, 9.3%)

Sababu kuu ya vifo vya saratani.

(iii). Saratani ya Ini: liver cancer (760 000 deaths, 7.8%)

Muuaji mkuu, haswa katika sehemu za Asia.

(iv). Saratani ya Matiti:breast cancer (670 000 deaths, 6.9%)

Sababu kuu ya vifo vya saratani kwa wanawake.

(v). Saratani ya Tumbo:stomach cancer (660 000 deaths, 6.8%).Sababu nyingine kuu ya vifo vya Saratani.

3. Ugonjwa wa Kisukari (Diabetes)

Ambapo ugonjwa huu pia huweza Kusababisha matatizo mengine ya kiafya kama vile:

  • Tatizo la figo, 
  • matatizo ya macho 
  • na mishipa ya damu. n.k

4. Magonjwa ya kudumu ya mfumo wa Upumuaji

Mfano wa magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji(Common Types of Respiratory Diseases)

  • Ugonjwa wa asthma ni miongoni mwa magonjwa mengine makubwa yasiyo ya kuambukiza.
  • Chronic Obstructive Pulmonary Disease (COPD):
  • Ugonjwa wa Pneumonia
  • Saratani ya Mapafu(Lung Cancer):
  • Cystic Fibrosis (CF)
  • Ugonjwa wa Tuberculosis (TB)
  • Bronchitis & Bronchiolitis n.k...

5. Matatizo ya Afya ya Akili (Mental Health Conditions)

Matatizo ya Afya ya akili yamekuwa chanzo kikuu cha Ulemavu na Vifo Duniani,Zaidi ya mamilioni ya watu duniani wanaishi na shida za afya ya akili kama vile: 

  • Msongo wa mawazo(Stress)
  • na wasiwasi(Anxiety disorders)
  • Huzuni na Mfadhaiko(depression)
  • Bipolar disorder.
  • Post-Traumatic Stress Disorder (PTSD)
  • Schizophrenia. 
  • Eating disorders.n.k....

Muhtasari

Mwaka 2025, dunia ilikumbana na magonjwa makubwa ya kuambukiza pamoja na kuendelea kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ndio chanzo kikuu cha vifo duniani. Kupunguza mzigo wa magonjwa haya kunahitaji chanjo, maji safi na usafi kwa ujumla, lishe nzuri, utunzaji bora wa afya ya akili, na sera madhubuti za afya ya umma.

Verified Sources Used: 

  • Shirika la Afya Duniani(WHO),
  • Afyaclass disease List,
  • Health and Me,
  • Wikipedia,

0 Comment

WHO:Aina mpya ya homa ya mafua inaongezeka kwa kasiAfyaclass Forum •

WHO:Aina mpya ya homa ya mafua inaongezeka kwa kasi, lakini chanjo bado ni kinga bora

Muguzi mwenye tabasamu na mama aliye na mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minane kwenye kituo cha afya huko Kyiv, Ukrainia, akijitayarisha kwa ajili ya chanjo.

Wakati msimu wa homa ya mafua katika Ulimwengu wa Kaskazini ukianza mapema, aina mpya ya virusi inaenea kwa kasi hata hivyo, chanjo bado ndio “ulinzi wenye ufanisi zaidi”, limesema leo Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO.

Homa ya mafua na virusi vingine vya mfumo wa kupumua vinaongezeka, amesema Dkt. Wenqing Zhang, Mkuu wa Kitengo cha Vitisho vya Kimataifa vya Magonjwa ya Njia ya mfumo wa Hewa katika Idara ya Usimamizi wa tishio la Magonjwa ya milipuko na majanga wa WHO, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo.

Amesema “Mwaka huu umebainishwa na kuibuka na kuenea kwa kasi kwa aina mpya ya virusi vya AH3N2”.

Aina hiyo mpya inayoitwa J.2.4.1 au subkladi K amesema iligunduliwa kwa mara ya kwanza mwezi Agosti nchini Australia na New Zealand, na tangu wakati huo imebainika katika zaidi ya nchi 30.

Mabadiliko ya kijenetiki ya virusi

Dkt. Zhang amesema “Takwimu za sasa za kitabibu hazioneshi kuongezeka kwa ukali wa ugonjwa, ingawa mabadiliko haya ya kijenetiki yanaashiria mageuzi muhimu ya virusi.”

Ameeleza kuwa virusi vya homa ya mafua hubadilika kila wakati, ndio sababu muundo wa chanjo ya mafua husahihishwa mara kwa mara.

“WHO hufuatilia mabadiliko haya, hutathmini hatari zinazohusiana na afya ya umma na kutoa mapendekezo ya muundo wa chanjo mara mbili kwa mwaka, kupitia mfumo wa kimataifa wa muda mrefu, Mfumo wa Ufuatiliaji na Hatua ya Mafua Duniani (GISRS) kwa kushirikiana na wataalamu wengine wa kimataifa,” amesema Dkt. Zhang.

Mtaalamu huyo wa WHO amefafanua kwamba Aina hiyo mpya haijajumuishwa katika muundo wa chanjo za hivi karibuni zilizotengenezwa kwa msimu wa mafua wa Ulimwengu wa Kaskazini,

Hata hivyo amesema “ushahidi wa awali unaonesha kuwa chanjo za msimu wa sasa bado zinatoa kinga dhidi ya magonjwa makali na hupunguza hatari ya kulazwa hospitalini.”

WHO inakadiria kuwa kuna takribani visa bilioni moja vya homa ya mafua ya msimu kila mwaka, vikiwemo hadi visa milioni tano vya ugonjwa mkali wa mfumo wa kupumua.

Kwa mujibu wa WHO Hadi vifo 650,000 kila mwaka vinahusishwa na magonjwa ya mfumo wa kupumua yanayotokana na mafua ya msimu.

Ushauri wa kupunguza hatari

“Chanjo bado ndio ulinzi wetu wenye ufanisi zaidi, ikiwemo dhidi ya aina zilizobadilika, hasa kwa makundi yaliyo katika hatari kubwa na wale wanaowahudumia,” amesisitiza Dkt. Zhang.

Mtaalamu huyo wa WHO amebainisha matokeo ya makadirio ya awali ya ufanisi wa chanjo dhidi ya aina mpya, yaliyochapishwa nchini Uingereza wiki chache zilizopita.

“Ni ya kutia matumaini,” amesema, akirejelea takwimu zilizoonesha kuwa chanjo ina ufanisi wa takribani asilimia 75 dhidi ya ugonjwa mkali na kulazwa hospitalini kwa watoto, na karibu asilimia 35 miongoni mwa watu wazima.

Dkt. Zhang ameonya kuwa msimu ujao wa sikukuu unaweza kuleta ongezeko zaidi la magonjwa ya njia ya upumuaji.

“Mipango ya mapema na juhudi za maandalizi, ikiwemo kuhamasisha upokeaji wa chanjo na kuimarisha utayari wa mifumo ya afya, zinapendekezwa kwa dhati,” amesema.

Ameshauri nchi kuimarisha uchunguzi wa kimaabara na ufuatiliaji wa magonjwa mwaka mzima, na kushiriki katika mtandao wa ufuatiliaji wa WHO wa GISRS.

Ufuatiliaji wa kimataifa bado ni muhimu

Mtandao huo unajumuisha vituo vya mafua katika nchi 130 pamoja na maabara kumi na mbili za marejeleo.

Alipoulizwa iwapo Marekani itaendelea kuwa mwanachama wa mtandao huo mwaka ujao licha ya uamuzi wa nchi hiyo kujiondoa WHO kuanzia tarehe 22 Januari 2026, Dkt. Zhang amesema kuwa, “kwa mtazamo wa mafua, ufuatiliaji wa magonjwa ya njia yamfumo wa hewa na maandalizi, bila shaka tunahitaji nchi zote duniani kushiriki katika ufuatiliaji, maandalizi na hatua kwa mafua na virusi vingine vya njia ya mfumo wa kupumuai, kwa sababu hatujui aina inayofuata ya janga, itajitokeza lini na wapi”.

Amehitimisha kwa kusema kuwa “Na muda kati ya kuibuka kwake na kugunduliwa, kuchambuliwa na kujumuishwa kwenye chanjo unaweza kuleta tofauti kubwa katika idadi ya maisha yanayoweza kuokolewa”.

♦ UN Source.

0 Comment

Ugonjwa wa Malaria wazidi kuua Watoto duniani,WHOAfyaclass Forum •

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema Alhamisi kuwa watu takribani 610,000—wengi wao wakiwa watoto—wamefariki dunia mwaka 2024 kutokana na ugonjwa wa malaria.

Mbu ndio chanzo kikuu cha malaria ambayo inachangia ongezeko la vifo kote ulimwenguni

WHO imeonya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa maambukizi kutokana na kuenea kwa dawa zisizo na ufanisi, mabadiliko ya tabianchi na kupunguzwa kwa ufadhili kwa nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ongezeko la visa na vifo limeripotiwa zaidi katika Ethiopia, Madagascar na Yemen, wakati nchi 47 zimetajwa kuwa hazikuwa na maambukizi ya malaria mwaka 2024. Idadi hiyo ya vifo imeongezeka kidogo ikilinganishwa na mwaka 2023, huku maambukizi mapya yakipanda kutoka milioni 273 hadi milioni 282 ndani ya mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Malaria wa WHO, Daniel Ngamije Madandi, amesema kuongezeka kwa usugu dhidi ya dawa za malaria, kupungua kwa ufanisi wa viuatilifu vinavyotumika kwenye vyandarua, mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro isiyomalizika vyote vimechangia kuongezeka kwa maambukizi katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Vifo vitokanavyo na malaria pia vimeongezeka

Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa kuongezeka kwa vifo katika kipindi cha 2015 hadi 2024 kunahusishwa na ongezeko la idadi ya watu, ambapo visa vya vifo vimepanda kutoka 59 hadi 64 kwa kila watu 100,000 waliokuwa katika hatari ya kuambukizwa. Hata hivyo, kiwango cha vifo kilipungua kidogo mwaka uliopita, kutoka 14.9 hadi 13.8 kwa kila watu 100,000.

Kwa upande wa ufadhili, WHO imesema uwekezaji katika kudhibiti malaria ulikuwa dola bilioni 3.9 mwaka 2024—chini sana ya lengo la zaidi ya dola bilioni 9 zinazohitajika.

"Ufadhili mdogo wa kukabiliana na malaria unaleta hatari ya kurejea kwa kasi kubwa kwa ugonjwa huu,” alisema Ngamije.

Ameongeza kuwa zana mpya na bora zaidi—ikiwemo matibabu, vipimo na chanjo—ni muhimu ili kuokoa maisha, na akazitaka serikali za nchi zilizoathirika kuchukua jukumu la kuhakikisha vinawafikia wananchi.

Mwezi Januari mwaka huu, Marekani ilitangaza kupunguza ufadhili wa misaada ya kimataifa, hatua ambayo WHO imeonya kuwa imeathiri kwa kiasi kikubwa mapambano dhidi ya malaria na juhudi za kuokoa maisha.

0 Comment

Wagonjwa wa Malaria waliongezeka duniani 2024,WHOAfyaclass Forum •

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema ugonjwa wa malaria uliwaua takribani watu 610,000 duniani kote mwaka 2024.


Ripoti ya mwaka ya WHO kuhusu malaria iliyotolewa Alhamisi, imeeleza kuwa visa vya ugonjwa huo vimeongezeka zaidi nchini Ethiopia, Madagascar na Yemen.

Idadi hiyo ni juu kidogo ikilinganishwa na vifo vya 2023, huku maambukizi mapya yakipanda kutoka milioni 273 hadi takribani milioni 282.

Baada ya hatua kubwa kupigwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, mapambano dhidi ya malaria yamekuwa yakisuasua katika muongo mmoja uliopita.

Nchi kadhaa hazina malaria

Hata hivyo, nchi 47 zimethibitishwa kutokuwa na malaria.

Daniel Ngamije Madandi, Mkurugenzi wa Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Malaria wa WHO, amesema watu wengi bado wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa ambao unaweza kuzuilika na kutibika.

WHO imesema kuongezeka kwa maambukizi kunachangiwa na ongezeko la dawa zisizo na ubora wa kutibu malaria, mabadiliko ya tabianchi na kupungua kwa ufadhili.

0 Comment

WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya LenacapavirAfyaclass Forum •

WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya Lenacapavir

Shirika la Afya Duniani, WHO linatoa wito kwa serikali na washirika kutanua upatikanaji wa tiba mpya zilizoidhinishwa ikiwa ni pamoja na tiba mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV kupitia dawa ya Lenacapavir.

UN yasema kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa kumetatiza juhudi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya HIV.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema wanakabiliwa na changamoto kubwa, kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa, pamoja na kukwama kwa juhudi za kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Wakati huo huo, amesema kuna fursa kubwa muhimu na tiba mpya zenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa janga la Virusi Vya Ukimwi.

Ghebreyesus ameongeza kusema kupanua ufikiaji wa tiba kwa watu wanaokabiliwa na hatari zaidi ya maambukizi ya VVU kote duniani lazima liwe suala la kipaumbele kwa serikali zote na washirika.

WHO yahimiza mwelekeo wa pande mbili kukabiliana na VVU

Kwa kuadhimisha Siku hii ya UKIMWI Duniani chini ya kaulimbiu ''Kutokomeza janga, kubadilisha hatua dhidi ya UKIMWI"  WHO inahimiza mwelekeo wa pande mbili wa mshikamano na uwekezaji katika uvumbuzi ili kulinda na kuhamasisha jamii zilizo hatarini zaidi.

Shirika hilo limesema baada ya miongo kadhaa ya mafanikio, muitikio wa kukabiliana na VVU bado uko katika njia panda.

Afrika Kusini, Cape Town 2024 | Kuzuia VVU na Lenacapavir katika Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu Afrika Kusini, Cape Town 2024 | Kuzuia VVU na Lenacapavir katika Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu 

Tiba mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV, dawa ya Lenacapavir (LEN).Picha: Nardus Engelbrecht/AP Photo/picture alliance

Katika hatua nyingine, Shirika la UNAIDS limetahadharisha kwamba tangu Marekani na washirika wengine walipopunguza ufadhili wa ghafla mwaka huu, mfumo wa ikolojia unaoendeleza tiba na juhudi ya kuzuia maambukizi ya VVU katika nchi nyingi umetikiswa .

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi Winnie Byanyima, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva nchini Uswisi kwamba kiliniki zimefungwa ghafla na maelfu ya wafanyakazi wa afya wamepoteza kazi zao ama mishahara huku huduma za kuokoa maisha, upimaji, matibabu na kinga zikiendelea kutatizwa.

Takwimu za UNAIDS kuhusiana na maambuziki ya VVU

Byanyima amesema katika nchi 13, idadi ya watu wanaoanza matibabu imepungua ikilinganishwa na mwaka 2024. Amesema Uhaba wa vifaa vya kupimia VVU na madawa umeripotiwa katika nchi zikiwemo Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ameongeza kuwa huduma za kinga ambazo tayari zilikuwa zinakabiliwa na matatizo kabla ya mgogoro ndizo zilizoathirika zaidi.

Akiwasilisha ripoti mpya ya shirika hilo la UNAIDS, Byanyima aliitaja kuwa yenye changamoto kubwa. Katika ripoti hiyo, UNAIDS imesema mnamo mwaka 2024 takriban watu milioni 1.3 waliambukizwa HIV

UNAIDS | Winnie Byanyima UNAIDS | Winnie Byanyima 

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi Winnie ByanyimaPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Idadi hiyo ilikuwa asilimia 40 chini ya ile ya mwaka 2010, lakini ni zaidi ya mara tatu ya inavyohitajika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kumaliza janga la UKIMWI  kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo pia imesema mwaka jana, takriban watu 630,000 walikufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI, hili likiwa punguzo la asilimia 54 tangu 2010, na asilimia 15 tangu 2020.

Pia imebainisha kuwa mwaka jana, tayari watu milioni 9.2 kati ya zaidi ya milioni 40 wanaoishi na VVU duniani kote walikuwa hawapati matibabu. Byanyima ameonya ikiwa hali hiyo haitashughulikiwa, inaweza kusababisha maambukizi mapya milioni 3.3 kufikia mwaka 2030.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD