Hapa ni orodha ya magonjwa na matatizo ya kiafya yaliyosumbua sana dunia mwaka 2025, ikijumuisha magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na milipuko mikubwa iliyoripotiwa na Shirika La afya duniani: Katika Orodha hii namba si chochote,Wala haya sio magonjwa yote ni baadhi tu;
Magonjwa ya Kuambukiza (Infectious Diseases)
1. Ugonjwa wa kifua kikuu-Tuberculosis(TB)
Bakteria wanaosababisha ugonjwa wa mapafu,Kifua kikuu au TB bado ni tishio kubwa na inasababisha maelfu ya vifo kila mwaka.
2. COVID-19 na Mawimbi ya Virusi Vipya
Ingawa si Ugonjwa mpya kama awamu ya 2020, bado COVID-19 na mabadiliko ya virusi vyake yanachangia vifo na ugonjwa huu kuenea kote duniani.
3. Ugonjwa wa Surua (Measles)
Kupungua kwa chanjo kumeleta kuongezeka kwa kesi za Ugonjwa wa Surua, hasa miongoni mwa watoto.
4. Ugonjwa wa Kipindupindu(Cholera)
Milipuko mikubwa ya Ugonjwa wa Kipindupindu imeendelea katika nchi nyingi, ikisababisha maambukizi na vifo vingi, hasa maeneo yenye maji na usafi duni.
5. Ugonjwa wa Homa ya Dengue
Dengue bado inasababisha maambukizi makubwa katika nchi 90 na inaripotiwa visa vingi zaidi ya milioni kadhaa.
6. Ugonjwa wa Homa ya Nyani-Mpox (Monkeypox)
Milipuko ya mpox (pia inajulikana kama monkeypox) imeendelea kufuatilia dunia tangu 2023–2025 kama janga la kiafya la kimataifa.
7. Ugonjwa wa Malaria
Ingawa kuna mafanikio ya kudhibiti malaria, milipuko bado inatokea na inasababisha vifo hasa kwa watoto.
Magonjwa Makubwa Yasiyo ya Kuambukiza (Non-Communicable Diseases, NCDs)
Magonjwa haya ndio yanayosababisha vifo vingi zaidi duniani, mara nyingi kutokana na mtindo wa maisha, lishe mbaya, Uvutaji wa sigara, na uchafuzi wa hewa:
1. Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (Cardiovascular Diseases)
Mfano wa magonjwa hayo yanayoathiri moyo ni pamoja na;
- Shambulio la Moyo(Heart attack):Ugonjwa wa moyo kama vile mshtuko wa moyo(Heart attack) ni chanzo kikuu cha vifo duniani.
- Ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu ndani ya moyo mfano; Coronary artery diseases.
- Tatizo la mapigo ya moyo kutokueleweka-Irregular heartbeats (arrhythmias)
- Tatizo kwenye muundo wa moyo ambapo unazaliwa nalo (congenital heart defects)
- Tatizo la moyo kutanuka
- Tatizo la Moyo kujaa maji
- Ugonjwa wa kwenye misuli ya Moyo
- Ugonjwa wa kwenye Valve za moyo
- Ugonjwa wa kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo n.k
2. Saratani mbali mbali (Cancers)
Saratani ni mojawapo ya ugonjwa mbaya unaoongoza kwa vifo duniani.
Saratani Zinazoongoza kwa Vifo Duniani:
(i). Saratani ya Mapafu: (1.8 million deaths, 18.7% of the total cancer deaths)
Sababu kuu ya vifo vya saratani duniani kote, kwa jinsia zote mbili kwa pamoja
(ii). Saratani ya utumbo mpana:(colorectal cancer (900 000 deaths, 9.3%)
Sababu kuu ya vifo vya saratani.
(iii). Saratani ya Ini: liver cancer (760 000 deaths, 7.8%)
Muuaji mkuu, haswa katika sehemu za Asia.
(iv). Saratani ya Matiti:breast cancer (670 000 deaths, 6.9%)
Sababu kuu ya vifo vya saratani kwa wanawake.
(v). Saratani ya Tumbo:stomach cancer (660 000 deaths, 6.8%).Sababu nyingine kuu ya vifo vya Saratani.
3. Ugonjwa wa Kisukari (Diabetes)
Ambapo ugonjwa huu pia huweza Kusababisha matatizo mengine ya kiafya kama vile:
- Tatizo la figo,
- matatizo ya macho
- na mishipa ya damu. n.k
4. Magonjwa ya kudumu ya mfumo wa Upumuaji
Mfano wa magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji(Common Types of Respiratory Diseases)
- Ugonjwa wa asthma ni miongoni mwa magonjwa mengine makubwa yasiyo ya kuambukiza.
- Chronic Obstructive Pulmonary Disease (COPD):
- Ugonjwa wa Pneumonia
- Saratani ya Mapafu(Lung Cancer):
- Cystic Fibrosis (CF)
- Ugonjwa wa Tuberculosis (TB)
- Bronchitis & Bronchiolitis n.k...
5. Matatizo ya Afya ya Akili (Mental Health Conditions)
Matatizo ya Afya ya akili yamekuwa chanzo kikuu cha Ulemavu na Vifo Duniani,Zaidi ya mamilioni ya watu duniani wanaishi na shida za afya ya akili kama vile:
- Msongo wa mawazo(Stress)
- na wasiwasi(Anxiety disorders)
- Huzuni na Mfadhaiko(depression)
- Bipolar disorder.
- Post-Traumatic Stress Disorder (PTSD)
- Schizophrenia.
- Eating disorders.n.k....
Muhtasari
Mwaka 2025, dunia ilikumbana na magonjwa makubwa ya kuambukiza pamoja na kuendelea kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ndio chanzo kikuu cha vifo duniani. Kupunguza mzigo wa magonjwa haya kunahitaji chanjo, maji safi na usafi kwa ujumla, lishe nzuri, utunzaji bora wa afya ya akili, na sera madhubuti za afya ya umma.
Verified Sources Used:
- Shirika la Afya Duniani(WHO),
- Afyaclass disease List,
- Health and Me,
- Wikipedia,





.jpeg)
.jpeg)



image quote pre code