Showing posts with label ugonjwa wa kipindupindu. Show all posts
Showing posts with label ugonjwa wa kipindupindu. Show all posts

Maji machafu ni chanzo cha Ugonjwa wa KipindupinduAfyaclass Forum •

Maji machafu au yasiyochemshwa yanaweza kusababisha kipindupindu. Hii ni kwa sababu vimelea vya Vibrio cholerae (bakteria wanaosababisha kipindupindu) huishi na kusambaa kupitia maji na chakula kilichochafuliwa na kinyesi cha binadamu.

Maji machafu huleta kipindupindu kwa njia hizi:

-Kunywa maji machafu yenye vijidudu vya kipindupindu.

-Kutumia maji machafu kupikia au kuosha vyombo.

-Kuoga au kusafisha chakula kwa maji yasiyo safi.

-Kuchanganyika na kinyesi kilichoingia kwenye vyanzo vya maji.

Njia za kujikinga:

1. Chemsha maji kabla ya kunywa.

2. Tumia vidonge vya kutibu maji (water guard/chlorine).

3. Hifadhi maji kwenye chombo safi kilichofunikwa.

4. Osha mikono kwa sabuni kabla ya kula na baada ya choo.

5. Epuka kula chakula kilichoandaliwa sehemu zisizo safi.

0 Comment

Watu 40 wafariki kwa kipindupindu DarfurAfyaclass Forum •

Watu 40 wafariki kwa kipindupindu nchini Darfur



Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeripoti kwamba takriban watu 40 wamefariki katika eneo la Darfur nchini Sudan kutokana na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miaka mingi.

MSF ilieleza kuwa eneo hilo kubwa la magharibi, ambalo limekuwa uwanja wa mapambano makali kwa zaidi ya miaka miwili kati ya jeshi na kikosi cha wanamgambo cha RSF, ndilo  lililo athirika zaidi na mlipuko huo ambao umeendelea kwa mwaka mzima.

Taarifa ya MSF imedokeza kuwa katika wiki moja iliyopita, madaktari walio Darfur waliwahudumia wagonjwa zaidi ya 2,300 na kuripoti vifo 40.

Kwa jumla, MSF ilisema kufikia tarehe 11 Agosti, vifo 2,470 vilivyohusishwa na kipindupindu vimeripotiwa kati ya visa vinavyoshukiwa kufikia 99,700.

MSF ilieleza kuwa uhamishaji mkubwa wa raia kutokana na vita nchini Sudan umechochea mlipuko huo kwa kuwanyima watu maji safi kwa matumizi ya usafi wa msingi kama kuosha vyombo na chakula. Watu wanapata wastani wa lita tatu za maji kwa siku – chini ya nusu ya kiwango cha dharura cha lita 7.5 kwa mtu kwa siku kinachohitajika kwa kunywa, kupika, na usafi.

0 Comment

Ugonjwa wa Kipindupindu watesa Afrika Magharibi na Kati – DRC ikiwa Kitovu cha MlipukoAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa Kipindupindu watesa Afrika Magharibi na Kati – DRC ikiwa Kitovu cha Mlipuko



Wakati mvua zikiripotiwa kuanza kunyesha katika maeneo mbalimba ya Afrika Magharibi na Kati, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Watoto UNICEF limeripoti kuwa takribani watoto 80,000 wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu.

Taarifa iliyotolewa leo na shirika hilo kutoka Dakar Senegal imeripoti kuwa nchi 12 zimeathirika na mlipuko huu unaoenea kwa kasi, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo -DRC ikitajwa kuwa ndiyo iliyoathirika zaidi.

DRC hali ni mbaya

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya ya DRC, zaidi ya wagonjwa 38,000 wa kipindupindu na vifo 951 vimeripotiwa nchini humo mwezi huu wa Julai pekee. Takribani asilimia 25.6 ya wagonjwa wa kipindupindu ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Mkurugenzi wa UNICEF wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Gilles Fagninou amesema “Hii ni hali ya dharura inayohitaji hatua za haraka, ni suala la maisha na kifo.”

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na majimbo ya South Kivu, North Kivu, Haut Katanga, Tshopo, Haut Lomami, Tanganyika, na Maniema.

Jiji la Kinshasa limeingia kwenye hali ya dharura baada ya ongezeko kubwa la maambukizi ndani ya wiki nne zilizopita kufuatia mafuriko makubwa na mvua zinazoendelea, huku kiwango cha vifo kwa wagonjwa kikifikia asilimia 8, hiki ni kiwango cha kutisha kwa muktadha wa ugonjwa huu unaotibika haraka iwapo utagundulika mapema.

“Hali mbaya ya mvua, mafuriko na watu wengi waliolazimika kuhama makazi yao vinaongeza kasi ya kusambaa kwa kipindupindu na kuweka maisha ya watoto hatarini,” amesemaFagninou

UNICEF inaonya kuwa bila hatua madhubuti za kudhibiti mlipuko huu, DRC inaweza kukumbwa na janga la kipindupindu kubwa zaidi tangu mwaka 2017.

Hali ilivyo katika mataifa mengine

Nchi nyingine zilizoathirika ni Nigeria (wagonjwa 3,109 na vifo 86), Chad (wagonjwa 55 na vifo 4), Ghana (wagonjwa 612), Côte d’Ivoire (wagonjwa 322 na vifo 15), na Togo (wagonjwa 209 na vifo 5).

Nchi kama Niger, Benin, Liberia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Cameroon zinaendelea kufuatiliwa kwa karibu.

Mkuu huyo wa kanda wa UNICEF amesema “Tupo kwenye mbio dhidi ya wakati, tukishirikiana na serikali kutoa huduma muhimu kama maji safi na salama, lishe na huduma za afya kwa watoto walio katika hatari kubwa. Tunafanya kila jitihada kuhakikisha hakuna mtoto anayesahaulika.”

UNICEF imekuwa mstari wa mbele kusambaza huduma za afya, maji safi, vifaa vya usafi na katika utoaji wa chanjo, pamoja na kuelimisha jamii kuhusu kinga na tiba ya kipindupindu.

Hata hivyo, shirika hilo linahitaji dola milioni 20 ndani ya miezi mitatu ijayo ili kuongeza kasi ya msaada katika nchi zilizoathirika.

0 Comment

Mtu mmoja amefariki, Na 5 wamelazwa hospitalini huku Kipindupindu kikienea katika Jimbo la Ogun,NIGERIAAfyaclass Forum •

Kipindupindu kimegharimu maisha ya mwanamke mwenye umri wa miaka 62 huko Ijebu-Igbo, eneo la Serikali ya Mtaa ya Ijebu Kaskazini katika Jimbo la Ogun,Nchini Nigeria.

Mwanamke aliyefariki aliambukizwa ugonjwa huo alipokuwa akimhudumia mtoto wake aliyeambukizwa, ambaye sasa amelazwa hospitalini.

Tukio hilo lilisemekana kutokea siku tatu zilizopita.

Akithibitisha kuzuka kwa ugonjwa huo, Dk. Tomi Coker, Kamishna wa Afya, alisema: “Mwanamke mwenye umri wa miaka 62 alikufa na watu watano walilazwa hospitalini. Ilitokea Ijebu-Igbo katika eneo la serikali ya mitaa ya Ijebu-Kaskazini katika jimbo hilo.”

Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Nigeria, NMA, katika jimbo hilo, Dk. Kunle Ashimi, katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi, Juni 20, alikiri kuenea kwa athari za ugonjwa wa kipindupindu, ambao, kulingana naye, umeathiri majimbo 30 kote nchini, ikiwemo Ogun.

Alibainisha kuwa kesi zitatibiwa bila malipo katika vituo vilivyotengwa na kuwataka wananchi kuchukua hatua za kuzuia kuenea kwa kipindupindu.

Ashimi alisema: “Wagonjwa kama hao watasafirishwa na kutibiwa bure katika vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kudhibiti kesi za kipindupindu katika jimbo zima.

“Tunatumia fursa hii kuwaomba wananchi wetu kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na kujisaidia wazi, kuepuka kutupa taka ovyo, kunawa mikono mara kwa mara, kunawa matunda na mboga mboga vizuri kabla ya kula na kutibu maji kabla ya kuyanywa. ama kwa kuchemsha au kutibu kwa mawakala wa kusafisha kemikali.

“Tunatetea kwamba pale ambapo hakuna sababu ya kufanya hivyo, matone mawili ya bleach ya nyumbani katika lita 1 ya maji ni mbadala nzuri. Pia tunazisihi shule kufuatilia wachuuzi wa vyakula, matunda na vitafunwa karibu na shule ili kuhakikisha kuwa wanazingatia usafi. Vile vile, shule zinapaswa kuanzisha tena vituo vya kunawia mikono kama ilivyofanywa wakati wa COVID-19.”

Mtu mmoja amefariki, Na 5 wamelazwa hospitalini huku Kipindupindu
kikienea katika Jimbo la Ogun,NIGERIA
0 Comment

Watu 10 wafariki kwa kipindupindu KageraAfyaclass Forum •

Watu 10 wafariki kwa kipindupindu Kagera

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo leo Machi 6, 2024. Picha na Ananias Khalula

Ugonjwa wa Kipindupindu mkoani Kagera uligundulika Novemba 29, 2023 katika kata ya Bugorola kijiji cha Buchurago wilayani Misenyi, ambapo watu wanne walipoteza maisha, huku wengine watano wakiwahiwa matibabu.

Watu 10 wameripotiwa kupoteza maisha  kwa ugonjwa wa kipindupindu tangu Novemba, 2023 hadi Machi mwaka huu,  huku waliougua ugonjwa huo wakifikia 161 mkoani Kagera.

Akieleza mwenendo wa hali ya magonjwa ya mlipuko katika Mkoa wa Kagera kwenye kikao cha Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) leo Jumatano Machi 6, 2024, Mkuu wa Mkoa huo, Fatma Mwassa,  amesema kati ya wagonjwa wa kipindupindu 161 waliorpotiwa,  151 walipona huku 10 wakipoteza maisha.

”Kwa sasa tayari ugonjwa huu umeripotiwa katika halmashauri za Wilaya ya Missenyi, Bukoba DC na Bukoba Manispaa… mlipuko wa ugonjwa huu umeendelea kuwepo kwenye Kisiwa cha Goziba hadi tunapoongea muda huu kutokana na kuwepo kwa ugonjwa huo kwenye kisiwa hicho. Niendelee kuelekeza uongozi wa Wilaya ya Muleba kuendelea kudhibiti ugonjwa huo,”ameeleza Mwassa.

Akizungumza kwenye kikao hicho,  Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima ametaja mbinu walizozitumia kuhakikisha wanaudhibiti ugonjwa huo kwenye wilaya za Bukoba vijijini na Bukoba Manispaa kuwa ni kuhakikisha wanasimamia usafi kwenye mji mzima,  kwa kuhakikisha wanazoa takataka kwenye madampo yote na yale ambayo yalikuwa siyo rasmi, kuyafunga kama vile dampoo la Kashai na dampo la Omba Mungu.

Mbunge wa Muleba kasikazini, Charles Mwijage amesema kisiwa cha Goziba kipo kwenye hatari kubwa ya kuathirika, kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu mizuri ya maendeleo,  akidai watu wanaoishi ndani ya kisiwa ni wengi, wakati eneo ni dogo hivyo kukosa huduma muhimu na za msingi kwa wakati sahihi.

Ameiomba halmashauri hiyo iwe na mikakati ya kuwanasuru wananchi wanaoishi kisiwani humo, akisema kisiwa hicho ni kati ya vyanzo vya mapato muhimu kinachozalisha zaidi ya Sh100 milioni kwa mwaka.

Via:Mwananchi.

Soma hapa Zaidi: Dalili za Ugonjwa wa kipindupindu

Watu 10 wafariki kwa kipindupindu Kagera
0 Comment

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa mara ya pili watokea SIMIYUAfyaclass Forum •

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa mara ya pili watokea SIMIYU

SIMIYU; Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dk Yahaya Nawanda, amepiga marufuku watu kula kwenye misiba, kutokana na kuibuka tena kwa ugonjwa wa kipindupindu katika Wilaya za Meatu, Bariadi na Itilima.

Hiyo ni mara ya pili kwa mkoa huo kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambapo mara ya kwanza ilikuwa Desemba, 2023 hadi Januari, 2024 na kusababisha uwepo wa wagonjwa 273 huku vifo vikiwa vitatu.

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa huo, Dk Nawanda ameagiza kuanza kutekelezwa kwa mara nyingine marufuku ya watu kula misibani, kwani katika awamu ya pili ya mlipuko wa ugonjwa huo chanzo kikubwa imeonekana kuwa ni misiba.

“ Awamu ya kwanza tulipiga marufuku na tukafanikiwa kudhibiti ugonjwa huu, sasa umerudi tena, naagiza hapa tunasitisha tena watu kupika na kula misibani, imeonekana misiba imekuwa chanzo kikubwa cha ugonjwa huu,” amesema Dk Nawanda n kuongeza:

“ Tukimaliza kuzika kila mtu nyumbani, hakuna kupika wala kula kwenye misiba, awamu hii ya pili ugonjwa umekuja kwa kasi hasa Wilaya ya Meatu, na wote walipatwa na ugonjwa huu wameutoa misibani baada ya kula chakula.”

Mganga Mkuu wa Mkoa Dk Boniphace Marwa, amesema kuwa mlipuko wa awamu ya kwanza mkoa ulifanikiwa kuudhibiti, ambapo uwepo wa marufuku ya kula misibani na kufungwa kwa minada ilisaidia kwa kiasi kikubwa.

• Soma Zaidi hapa; kuhusu ugonjwa wa kipindupindu,chanzo,dalili na Tiba

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwa mara ya pili watokea SIMIYU
0 Comment

Upatikanaji wa maji safi na salama kupunguza magonjwa ya mlipukoAfyaclass Forum •

Upatikanaji wa maji safi na salama kupunguza magonjwa ya mlipuko

Na WAF – Simiyu

Wizara ya Afya, Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU), kwa pamoja kupitia mradi wa kupambana na Magonjwa ya Mlipuko wamewezesha vijiji vya Nyanguge na Bunamhala Wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu, kufikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Kupitia mradi huo Visima vimekarabatiwa na kuwekwa pampu za umeme na kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama mabadiliko ambayo yameleta furaha kwa wananchi kwa kuchochea ustawi wa afya na kupunguza hatari ya magonjwa ya mlipuko.

Mwenyekiti wa kamati ya maji katika Wilaya ya Bariadi, Swales Ngusa, amesema kuboreshwa kwa ubora wa maji kumechochewa na gharama za uendeshaji kupungua kufuatia upatikanaji wa umeme.

Kwa upande wake, Afisa Afya na Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma Mkoani Simiyu, Bashiri Salum, amethibitisha kuwa matumizi ya dawa ya Klorini yamekuwa muhimu katika kuhakikisha maji yanakuwa safi na salama.

Mradi huo unaotekelezwa katika wilaya kadhaa za Mkoa wa Simiyu unalenga kuhakikisha upatikanaji wa umeme vijijini na kuwezesha huduma za maji safi na salama, huku ikilenga kuboresha afya na ustawi wa jamii awali wananchi walikabiliwa na changamoto za kuchota maji katika vyanzo visivyokuwa salama, hali iliyosababisha kuongezeka kwa magonjwa ya mlipuko kama vile Kipindupindu.

Upatikanaji wa maji safi na salama kupunguza magonjwa ya mlipuko
0 Comment

Fahamu hapa,Masharti mapya ya kukabiliana na kipindupindu pamoja na ‘red eyes’Afyaclass Forum •

Fahamu hapa,Masharti mapya ya kukabiliana na kipindupindu pamoja na ‘red eyes’

Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Tumaini Nagu amezitaka nyumba za ibada kusitisha utaratibu wa waumini wake kushikana mikono, ikiwa ni sehemu ya kupambana na magonjwa ya mlipuko ya viral keratoconjunctivitis (red eyes) na kipindupindu.

Profesa Nagu alisema hayo jana, wakati akiongoza kikao cha 10 cha Bodi ya Ushauri wa Hospitali Binafsi.

Pia, alitoa rai ya matumizi ya majisafi tiririka na sabuni maeneo ya mikusanyiko, ofisi za umma na binafsi, nyumbani na sehemu za biashara, huku akiwahimiza wanaotumia vyombo vya usafiri kutumia vitakasa mikono.

Profesa Nagu alisema hayo baada ya kuwapo ongezeko la wagonjwa wa macho unaoambukizwa kwa kushikana mikono, kugusa sehemu aliyogusa mwenye maambukizo ambalo kwa sasa imefikia mikoa 17 na ugonjwa wa kipindupindu umesambaa katika mikoa 14.

“Muhimu kuzingatia usafi wa mtu binafsi na mazingira, tuepuke kushikana mikono, hasa katika nyumba za ibada sitisheni huu utaratibu kwa muda,” alisema Profesa Nagu.

“Maeneo ya mikusanyiko tusishikane mikono, wekeni miundombinu ya kunawa maji tiririka na sabuni, agizo hili ni kwa watu wote wa majumbani, sehemu za biashara, kwenye mikusanyiko, ofisi za umma na binafsi.”

Januari 29, Wizara ya Afya ilisema jumla ya mikoa 17 imeathirika na ugonjwa wa macho mekundu.

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Profesa Paschal Rugajjo alisema hadi kufikia Januari 26 mwaka huu, idadi ya waliofika kwenye vituo vya afya walikuwa 5,359 kutoka 1,109, Januari 19.

“Ugonjwa huu umesambaa zaidi, ingawa ni wachache ndio wanafika vituo vya huduma za afya, mpaka sasa ugonjwa huu umesambaa na kuongezeka katika mikoa 17, ikiwamo ya Singida, Katavi, Kilimanjaro, Mara, Iringa, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Mtwara, Lindi, Songwe, Rukwa na Mwanza,” alisema Profesa Rugajjo.

Akizungumza jana, Profesa Nagu alisema Serikali imechukua hatua nyingi, ikiwamo kuhakikisha kuna upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo yote yaliyoathirika na kushughulikia miundombinu ya majitaka ili kuhakikisha inakuwa vizuri.

“Kwa sababu ya mvua, miundombinu mingine ya maji taka inafunikwa, hivyo jitihada kubwa zimefanyika kuhakikisha inafukuliwa na timu ya wataalamu wa elimu ya afya kwa jamii wapo maeneo yote wakihimiza usafi wa mtu binafsi na mazingira,” alisema Profesa Nagu.

Alisisitiza watumiaji wa usafiri wa vyombo vya moto vya kuchangia, kutembea na vitakasa mikono, huku akihamasisha unywaji wa majisafi na salama pamoja na kuosha matunda na mbogamboga kuepuka maambukizi.

Profesa Nagu alisema mlipuko wa magonjwa hayo umetokana na mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa kuna mvua zilizozidi kiwango, miundombinu imebadilika na kutokea kwa milipuko ya magonjwa duniani kote.

Alisema kipindupindu si Tanzania pekee, bali kimeathiri nchi kadhaa, ikiwamo Zambia ambayo mpaka sasa shule zimeshindwa kufunguliwa.

“Baadhi ya mikoa tumefanikiwa kudhibiti ugonjwa huu, lakini bado tunapambana katika mikoa michache ya Mwanza, Katavi na Kagera, hatua zinapaswa kuchukuliwa na wananchi wenyewe kwa kujikinga, mvua bado zinakuja,” alisema.

Imani potofu

Chanzo cha kusambaa kwa kipindupindu wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza hadi kufika watu 61, imeelezwa ni kutokana na kuwepo kwa imani potofu kwa jamii kuwa wakitumia dawa za kienyeji kujikinga zitasaidia kupona ugonjwa huo.

Sakata hilo liliibuka jana, kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Sengerema, kilichokuwa kikijadili na kupitisha rasimu ya bajeti ya mwaka 2024/25.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Binuru Shekidele alisema timu ya wataalamu wa afya ilikwenda maeneo yaliyoathirika kwa ajili ya kutoa huduma za afya na kujikinga na baadaye ilibaini wananchi wakitumia njia isiyo sahihi kujitibu na kujikinga.

“Kusambaa kwa ugonjwa huu, kumetokana na imani potofu kwa wananchi kutumia dawa za kienyeji za kuvaa kiunoni na kushindwa kufuata kanuni za afya, wakisema zitawasaidia,” aliseme Shikidele.

Tangu kuibuka kwa kipindupindu, Wilaya ya Sengerema wameripotiwa wagonjwa 61 kutoka Januari 30 hadi Februari 2, mwaka huu.

Kati yao, 27 wamepona na kuruhusiwa, huku 34 wakiendelea kulazwa kwa matibabu kwenye vituo vya afya wilayani humo.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga amepiga marufuku uuzwaji wa vyakula holela shuleni, sambamba na mikusanyiko kwenye misiba.

Ugonjwa huo kwa sasa unasambaa kwa kasi kwenye maeneo yaliyopo pembezoni mwa Ziwa Victoria, yakiwamo ya Chifunfu, Kijiji cha Kiweni, Kata ya Kasenyi, Kijiji cha Lugongo na Mbalagane na Kata ya Katunguru.

Kisababishi kingine kilichotajwa ni wakazi wa mwambao wa ziwa kujisaidia hovyo.

Mmoja wa wananchi wa Kata ya Kasenyi, Anastazia John alisema ni kweli jamii ya wananchi wa kandokando mwa Ziwa Victoria wanaamini dawa za kienyeji zinatibu kuzuia magonjwa mbalimbali kuliko dawa zinazopatikana kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

“Elimu inahitajika kwa jamii kuachana na imani potofu na kufuata kanuni za afya ili kuepuka kupata magonjwa ya mlipuko,” alisema Annastazia.

Baadhi ya madiwani waliwaomba wataalamu wa afya kuweka nguvu kwenye maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Thomas Rutachunzibwa yuko Sengerema na timu ya afya ya mkoa, wakishirikiana na ya wilaya hiyo katika kata zilizoathirika.

Alipoulizwa hali ya kipindupindu mkoani Mwanza, Mratibu Elimu ya Afya wa Mkoa huo, Renard Mlyakado bila kutaja takwimu za mkoa mzima, alisema ugonjwa huo bado upo, akiwataka wananchi waendelee kuchukua tahadhari.

Aliwaomba wananchi kuacha utaratibu wa kusalimiana kwa kushikana mikono ili kuepuka kula bakteria, akidai hawawezi kujua wanaoshikana nao kama wana bakteria mikononi au la.

“Muhimu ni usafi wa mazingira na vyoo bora. Hata kama mtu ana choo cha shimo basi ahakikishe anakifunika ili inzi asitoe bakteria kwenye kinyesi na kusambaza kwa wakazi husika,” alisema Mlyakado.

Fahamu hapa,Masharti mapya ya kukabiliana na kipindupindu pamoja na
‘red eyes’
0 Comment

Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa kipindupinduAfyaclass Forum •

Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa kipindupindu.

Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo zitakazosaidia kupambana na ugonjwa wa kipindupindu uliolilikumba taifa hilo la Kusini mwa Afrika tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

Umoja wa Mataifa umeidhinisha hizo. Kulingana na data za hivi karibuni zilizotolewa na wizara ya afya mjini Lusaka, mpaka sasa zaidi ya watu 365 wamekufa kutokana na ugonjwa huo na watu 418 wameambukizwa ugonjwa huo.

Muda wa kufunguliwa shule na vyuo umesogezwa mbele kutoka tarehe 8 Januari hadi tarehe 29 wakati serikali ikiendelea na juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo.

Zambia imepokea dozi milioni 1.4 za chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa
kipindupindu
0 Comment

Mpaka Sasa Mikoa Sita ya Tanzania ina kipindupinduAfyaclass Forum •

Mpaka Sasa Mikoa Sita ya Tanzania ina kipindupindu.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini kwa mwaka 2023 katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema mpaka sasa kuna Mikoa sita ambayo inaendelea na mlipuko wa kipindupindu nchini.

Waziri Ummy amenukuliwa akisema “kwa mwaka jana 2023 mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ulitolewa taarifa katoka Mikoa 12 nchini ambapo Wagonjwa 927 na vifo 27 vilitolewa taarifa, Mkoa wa Arusha uliongoza kwa visa 214 lakini bahati nzuri hakukutokea kifo, katika Mkoa wa Mara jumla ya visa 193 na vifo vinane (8) vilitolewa taarifa, Mkoa wa Simiyu Visa 184 na vifo Viwili (2)”

“Mpaka sasa kuna Mikoa 6 ambayo inaendelea na mlipuko ambayo ni Shinyanga, Ruvuma, Tabora, Simiyu, Mwanza na Kagera”

Waziri Ummy amewapongeza Wakuu wa Mikoa pamoja na watendaji wa Sekta ya Afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri kwa kuendelea kuimarisha usimamizi ili ugonjwa huo udhibitiwe.

Mpaka Sasa Mikoa Sita ya Tanzania ina kipindupindu
0 Comment

Watu watano wabainika kuwa na vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu Kahama ShinyangaAfyaclass Forum •

Watu watano wabainika kuwa na vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu Kahama Shinyanga.

Watano wathibitika kuugua, 13 walazwa na 452 waliochangamana na wagonjwa wafuatiliwa na watalaamu wa afya

Shinyanga. Watu watano wamethibitika kuugua ugonjwa wa kipindupindi uliolipuka katika mji mdogo wa Kagonga, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Mlipuko wa ugonjwa huo umethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita leo Ijumaa, Januari 5, 2024 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Mkuu huyo wa wilaya amesema hadi leo jioni, watu 13 walikuwa wamelazwa kwa matibabu katika  kituo cha afya Mwendakulima na wataalamu wa afya wanaendelea kuwafuatilia watu wengine 452 wanaodaiwa kuchangamana na waliothibitika kuugua ugonjwa huo.

“Kituo cha afya Mwendakulima  kimetengwa maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaothibitika kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu,” amesema DC Mhita.

Amesema tayari Serikali imechukua hatua kadhaa kudhibiti ugonjwa huo ulioripotiwa kuibuka wilayani humo tangu Januari 2, 2024 ikiwemo kuwatenga wanaohisiwa kuambukizwa.

“Timu ya wataalamu tayari ipo Mji mdogo wa Kagongwa kutoa elimu kwa umma namna ya kuepuka maambukizi na kuhudumia wagonjwa ambao tayari wameambukizwa,” amesema Mhita.

Kutokana na ugonjwa huo, Serikali imepiga marufuku biashara ya kuuza pombe za kienyeji kwa kufunga vilabu vyote katika mji mdogo wa Kagonga ambako pia mikusanyiko isiyo ya lazima imezuiliwa.

Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya ya Kahama, Dk Shani Mdami amesema hadi sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kagongwa, Michael Shija amesema Desemba 25, 2023 kulitokea msiba wa mtoto ambaye kabla ya kufikwa umauti alikuwa akiharisha na kutapika.

“Baba mzazi wa mtoto yule naye alianza kuugua na kufariki dunia baada ya siku mbili.  Hali hiyo iliibua taharuki na sisi viongozi kuamua kutoa taarifa kwa mamlaka za juu Januari 2,2024 kwa msaada zaidi ya kiuchunguzi,” amesema Shija.

Watu watano wabainika kuwa na vimelea vya Ugonjwa wa kipindupindu
Kahama Shinyanga
0 Comment

Kesi za kipindupindu nchini Zambia zazidi 3,000Afyaclass Forum •

Kesi za kipindupindu nchini Zambia zazidi 3,000

Idadi ya kesi za kipindupindu nchini Zambia imeongezeka na kufikia 3,189 tangu mlipuko wa ugonjwa huo ulipotokea mwezi Januari mwaka jana 2023.

Mamlaka za afya nchini humo zimesema, ugonjwa huo uligunduliwa katika wilaya nne za mkoa wa Lusaka, na kuenea katika wilaya nyingine zilizo katikati ya nchi hiyo.

Jumatatu wiki hii, rais wa Zambia, Hakainde Hichilema alisema anajitahidi kuiwezesha Zambia kuwa kituo cha uzalishaji wa chanjo ya kipindupindu.

Kesi za kipindupindu nchini Zambia zazidi 3,000
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD