UVIMBE KWENYE KIZAZI(FIBROIDS),CHANZO CHAKE,DALILI ZAKE,MADHARA YAKE NA TIBA YAKE
➡️ Ombeni Mkumbwa
🔺SUMMARY
Utangulizi;
🔷 UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?
Uvimbe kwenye Kizazi ambapo kwa Kitaalam Hujulikana kama "FIBROIDS"- ni aiana ya Uvimbe ambao hutokea katika kuta za ndani za Mji wa mimba(Kizazi) au Uterus,au katikati ya kuta za Mji wa mimba,hivo kuleta madhara mengi. Kuta hizo za Mji wa mimba au Uterus zimegawanyika katika Maeneo au sehemu kuu Tatu.
- Kuna Submucosal Fibroids- ambayo hii ni Uvimbe wa Kizazi lakini unatokea sehemu ya Ndani ya Kizazi
- Intramural fibroids- hii ni aina ya Uvimbe wa Kizazi unaotokea sehemu ya katikati ya Kizazi
- Subserosal Fibroids-aina hii ya Uvimbe wa Kizazi hutokea sehemu ya Nje ya Kizazi
🔴Kumbuka; Uvimbe kwenye kizazi Huweza kutokea katika maeneo mbali mbali ya Kizazi Mfano;
Kuna Uvimbe wa vifuko vya mayai yaani kitaalam Hujulikana kama Ovarian Cysts
Kuna uvimbe kwenye kuta za Mji wa Uzazi kama nilivyoelezea hapo mwanzoni
Kuna uvimbe unaoweza kutokea kwenye Mirija ya Uzazi,na kuleta tatizo la kuziba kwa Mirija ya Uzazi
CHANZO CHA UVIMBE KWENYE KIZAZI AU FIBROIDS
- Matumizi ya dawa ambazo zina vichocheo vingi ndani yake,hasa vile vinavyohusika na Ukuaji wa seli hai za mwili kama vile progesterone,estrogen,n.k
- Tatizo la Unene pamoja na Uzito kupita kiasi
- Matumizi ya Njia mbalimbali za Uzazi wa Mpango
- Unywaji wa Pombe na matumizi ya vyakula vyenye sukari nyingi pamoja na Proteins
KUNDI LA WATU AMBAO WAPO KATIKA HATARI YA KUPATA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI
- Umri wa kuanzia kubalehe au kuvunja Ungo mpaka ukomo wa hedhi
- Mwanamke ambaye hajawahi kupata mtoto hadi kufikia umri mkubwa
- Watu wanene na wenye Uzito Kupita Kiasi
- Wanawake waliowahi kuingia hedhi
- Kuwa na historia ya Tatizo la Uvimbe wa Kizazi katika Familia yenu
DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI
🔻Uvimbe ukiwa Mkubwa sana huweza kuleta dalili kama hizi;
- Kukojoa mara kwa mara,kwani nafasi kubwa ya uvimbe husababisha mgandamizo wa kibofu cha Mkojo
- Mkojo kubakia kwenye kibofu mara baada ya kukojoa
- Kupata Choo kigumu sana,hata kukuletea maumivu makali sehemu ya Haja kubwa pamoja na Michubuko
MADHARA YA KUWA NA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI
- Maumivu makali wakati wa Hedhi na wakati wa Tendo la Ndoa
- Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wenye harufu mbaya
- kutolewa kizazi chote wakati wa matibabu kama uvimbe umeathiri sehemu kubwa ya Kizazi
- Tatizo la kushindwa kubeba Ujauzito
- Mvurugiko wa siku za Hedhi,ikiwemo kupata hedhi katikati ya mwezi



