Madhara ya kuinama kwa mjamzito(dalili za hatari kwa mwanamke mjamzito)Afyaclass Bongo Social •

Madhara ya kuinama kwa mjamzito(dalili za hatari kwa mwanamke mjamzito)

FAHAMU:

Kunyanyua vitu vizito sana, Kusimama kwa muda mrefu sana, Kujikunja sana,kutikiswa sana ikiwa ni pamoja na kuinama sana na kwa Muda mrefu,

huongeza uwezekano wa kutoka kwa ujauzito yaani Miscarriage, mwanamke mjamzito kujifungua kabla ya wakati yaani Preterm birth, Au kupata majeraha n.k

Bonus tips; Kabla ya kuendelea nimekuchambulia baadhi ya Dalili za hatari unazotakiwa kuzijuia ukiwa mjamzito

DALILI ZA HATARI KWA MWANAMKE MJAMZITO

Mwanamke mjamzito hushauriwa kuwahi haraka hospital endapo atapata dalili hizi hapa chini;

- Kuvuja damu sehemu zake za siri

- Kutoa maji sehemu za siri

- Kutoa uchafu wenye harufu mbaya sana ukeni

- Kutokumsikia mtoto akicheza tumboni zaidi ya masaa 24 kwa wale ambao mtoto kafikia umri wa kucheza tumboni

- Mwanamke mjamzito Kuona marue rue

- Kuvimba kupita kiasi miguuni,kwenye mikono,usoni n.k

- Joto la mwili kupanda au mama mjamzito kuwa na  Homa

- Mwanamke mjamzito kupata kizunguzungu

- Kuanza kuwa na mawazo ya kutaka kujiua mwenyewe au kuuwa kiumbe kilichopo tumboni

- Kupata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu

- Kupata maumivu makali sana ya kichwa

n.k

Mjamzito anaweza kuinama kwa urahisi katika kipindi chote cha ujauzito, lakini mbinu bora za kuinama zinahitajika ili kuepuka usumbufu na maumivu.

Katika miezi mitatu ya mwanzoni mwa ujauzito, mjamzito anaweza kuinama kama kawaida bila shida kubwa, kwa kutumia mbinu za kawaida kama kukunja kiuno na shingo. 

Katika miezi 4 hadi 6, mjamzito anaweza kukumbana na changamoto kulingana na hali ya tumboni. Kwa mjamzito mwenye tumbo dogo, kuinama kwa taratibu kama vile kuchuchumaa bila kukunja kiuno kunaweza kuwa rahisi na salama. Hata hivyo, kwa wale wenye tumbo kubwa au hali maalum, changamoto zinaweza kutokea, kama vile:

  • Mjamzito mwenye mtoto mkubwa tumboni.
  • Mjamzito mwenye maumivu makali ya kiuno na nyonga.
  • Mjamzito mwenye maji mengi yanayomzunguka mtoto.
  • Mjamzito mwenye mimba ya watoto zaidi ya mmoja, kama mapacha au watoto watatu.
  • Mjamzito mwenye tumbo kubwa kutokana na uzito mkubwa au kitambi.n.k.

Katika hatua hii, ni muhimu kutumia mbinu za kuzingatia ili kuepuka maumivu na hatari zinazoweza kutokea wakati wa kuinama.

Njia bora ya kuinama kwa Mama Mjamzito

Kwa mjamzito, njia bora ya kuinama inategemea kipindi cha ujauzito na hali ya tumboni. Hapa kuna mbinu nzuri za kuinama katika hatua tofauti za ujauzito:

1. Miezi Mitatu ya Mwanzoni;

 Katika hatua hii, mjamzito anaweza kuinama kwa urahisi kama ilivyo kawaida. Hata hivyo, ni bora kufuata mbinu nzuri, kama kuinama taratibu ili kuepuka mshtuko mkubwa kwa mwili.

2. Miezi Mitatu ya Kati (4-6):

   - Kwa Mjamzito Aliye na Tumbo Dogo:

 Mjamzito anaweza kuinama kwa kufuata mbinu ya kuchuchumaa badala ya kukunja kiuno, kwani hali hii ni rahisi kwa tumbo dogo.

   - Kwa Mjamzito Aliye na Maumivu au Tumbo Kubwa:

 Ikiwa mjamzito ana maumivu makali au tumbo kubwa, ni muhimu kuinama kwa taratibu na kwa msaada wa kitu chochote kinachoweza kutoa msaada, kama viti vya kuinamia au kutumia ukuta au meza kwa msaada.

3. Miezi Mitatu ya Mwishoni:

   - Kufanya Shughuli za Kila Siku: Katika hatua hii, mjamzito anapaswa kuwa mwangalifu sana. Ni bora kutumia mbinu za kuinama kwa upole, kama kujichuchumaa kwa kutumia mikono kwa msaada wa samani au kutumia viti vya kuzunguka kwa msaada.

   - Kuosha Vyombo na Kufanya Shughuli Nyingine: 

Kwa shughuli za kila siku kama kuosha vyombo au kufua, mjamzito anaweza kujaribu kutumia vifaa vya msaada kama viti vya kupumzika au kufuata mbinu ya kuinama kwa kutumia mikono ili kuepuka maumivu au kuanguka.

Mbinu za Kufuata:

- Tumia Msaada wa Mikono: 

Kuelekea chini kwa kutumia mikono kuunga mkono uzito wa mwili wako.

- Chuchumaa Polepole:

 Badala ya kuinama kwa ghafla, chuchumaa polepole ili kupunguza mzigo kwenye kiuno na nyonga.

- Tumia Samani au Viti vya Kuinamia:

 Vitu vya msaada vinaweza kupunguza hatari ya kuanguka na kufanya shughuli ziwe rahisi.

Kwa umakini na kujua mbinu sahihi, mjamzito anaweza kupunguza hatari na kuboresha faraja wakati wa shughuli za kila siku.

Miezi Mitatu ya Kuanza, Kati, na Mwishoni: Namna Bora ya Kuinama kwa Wajawazito

Miezi ya ujauzito inakubadilisha mwili wako kwa kiwango kikubwa, na kila hatua ya ujauzito ina mahitaji maalum kuhusu jinsi ya kutunza mwili wako. Katika makala hii, tutaangazia jinsi ya kuinama kwa usalama na kwa njia bora katika miezi mitatu ya mwanzo, katikati, na mwishoni mwa ujauzito.

Miezi Mitatu ya Mwanzo

Katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito, mabadiliko katika mwili yako bado hayajaathiriwa sana. Hii ni hatua rahisi ambapo unaweza kuinama kama kawaida, kwa kutegemea miguu yako na kutumia mikono kwa usaidizi. Kwa ujumla, unaruhusiwa kuinama kwa kukunja kiuno, kwani tumbo lako bado halijakua kwa kiasi kikubwa.

Miezi Mitatu ya Katikati

Hapa, ujauzito wako unaendelea kukua na unaweza kuanza kugundua mabadiliko katika mwili wako. Katika miezi hii, tumbo lako linaweza kuwa dogo au kubwa kulingana na maendeleo ya ujauzito. Ikiwa unapohisi maumivu au usumbufu wakati wa kuinama, kuna njia maalum za kufanya hivyo kwa usalama. 

Namna Bora ya Kuinama:

1. Kuwa na Mpangilio wa Mwili: 

Badala ya kukunja kiuno, jaribu kuinama kwa kutegemea misuli ya mapaja (hamstring muscles). Hii inasaidia kuepuka maumivu ya kiuno na huongeza usalama wa mwili wako.

2. Kutanguliza Mguu Mmoja Mbele:

 Ikiwa unahitaji kuinama, pandisha mguu mmoja kidogo mbele ili kupunguza mzigo kwenye tumbo lako. Kasha, shuka chini bila kukunja kiuno na tumia mikono yako kwa usaidizi.

Miezi Mitatu ya Mwishoni

Katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito, tumbo lako linakuwa kubwa sana na hali ya mwili wako inabadilika. Hii inafanya kuwa vigumu zaidi kuinama, na inaweza kuwa na hatari kama haifanywi kwa uangalifu. 

Changamoto na Hatari:

- Kupata Kizunguzungu:

 Kuinama kwa mtindo wa zamani kunaweza kuongeza mtiririko wa damu kwenye ubongo na kusababisha kizunguzungu.

- Hatari ya Kuanguka: Kwa kuwa tumbo lako limekua, unapoinama unaweza kuangukia mbele kutokana na uzito wa tumbo.

- Kiungulia au Tindikali: Kuinama kwa kutegemea kiuno kunaweza kuongeza hatari ya tindikali kurudi kwenye koo la chakula, kuleta maumivu ya kiungulia.

Namna Bora ya Kuinama:

1. Kuweka Mwili Wima: Jaribu kuinama ukiwa na mwili wima na miguu yako ya pembeni, badala ya kukunja kiuno. Hii inasaidia kupunguza msukumo kwenye tumbo.

2. Tumia Msaada wa Mikono: Tumia mikono yako kwa msaada unapoinama na kupanda, ili kupunguza mzigo kwenye kiuno na tumbo.

 Hitimisho

Kuinama kwa usalama wakati wa ujauzito ni muhimu kwa afya yako na ya mtoto wako. Katika kila hatua ya ujauzito, ni vema kutumia mbinu ambazo zitakusaidia kuepuka maumivu na hatari. Kumbuka, kama una maswali au unahitaji ushauri wa ziada, usisite kuwasiliana na daktari wako. 

Kwa kuwa na mbinu hizi kwa njia bora, utaweza kusimamia shughuli zako za kila siku kwa urahisi na usalama.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)Afyaclass Bongo Social •

 PID

• • • • •

PID NI NINI? Na Dalili zake ni Zipi?(magonjwa ya Wanawake)


PID NI NINI? 


PID ni maambukizi ya Bacteria kwenye via vya Uzazi vya mwanamke, ambapo hicho ni kifupi cha Maneno haya"Pelvic inflammatory Disease"


TATIZO HILI LINA DALILI ZIPI?


Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Ugonjwa wa PID kwa Wanawake;


- Mwanamke Kupata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu


- Mwanamke kutoa damu wakati na baada ya tendo la Ndoa


- Mwanamke kutoa uchafu wenye rangi kama ya njano n.k


- Mwanamke kutoa uchafu wenye harufu mbaya ukeni


- Kutoa maji maji sehemu za siri mara kwa mara


- Mwanamke kublid katikati ya mwezi


- Mwanamke kupata maumivu  makali wakati wa tendo la Ndoa


- Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa


- Pia kwa baadhi ya wanawake hupata maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, na kupata shida ya kutoa mkojo

N.k


CHANZO CHA TATIZO LA PID


Ugonjwa wa PID husababishwa na BACTERIA ila magonjwa kama Gonorrhea pamoja na Chlamydia huchangia sana uwepo wa Tatizo hili


MATIBABU YA UGONJWA WA PID


- Ugonjwa huu au tatizo hili la PID hutibiwa kwa dawa mbali mbali kama vile; Doxcycline n.k


Na matibabu haya ni vizuri kufanyika kwa mwanamke pamoja na mwanaume ambaye anashiriki naye tendo la ndoa,ili kuepusha tatizo kujirudia tena.


mwanamke mwenye tatizo la PID hushauriwa kutokufanya mapenzi mpaka apone.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MJAMZITO KUFANYA VIPIMO kama Ultrasound(Vipimo Muhimu)Afyaclass Bongo Social •

 ULTRASOUND

• • • • •

MJAMZITO KUFANYA VIPIMO kama Ultrasound(Vipimo Muhimu)


Mama mjamzito hutakiwa kufanya vipimo mbali mbali kwa ajali ya maendeleo salama ya ujauzito wake pamoja na Kujifungua vizuri.


Hivi hapa ni baadhi ya vipimo ambavyo ni muhimu sana kwa mama mjamzito


✓ Kupima kundi la Damu yaani Blood group, na kupata msaada kama mama ana Blood group rhesus factor NEGATIVE Halafu Baba ni Positive


✓ Kupima malaria kwa kutumia kipimo cha MRDT


✓ Kupima ugonjwa wa Kaswende yaani VDRL test


✓ Mama mjamzito kufanya kipimo cha Ultrasound


✓ Mama mjazito kupima Uzito wa mwili kwa ajili ya afya yake na pia kwa ajili ya kufwatilia ukuaji wa mtoto tumboni


✓ Mama mjamzito kupima presha au shinikizo la Damu


✓ Mama mjamzito kupima urefu siku anaanza Kliniki

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAMBO AMBAYO SIO YA KWELI KUHUSU UTIAfyaclass Bongo Social •

 UTI

• • • • 

MAMBO AMBAYO SIO YA KWELI KUHUSU UTI


Ugonjwa wa UTI umekuwa ukiwasumbua watu wengi sana mara kwa mara, huku wengine wakianza kueleweshana vitu visivyo sahihi kuhusu shida hii.


MAMBO AMBAYO SIO YA KWELI KUHUSU UTI


• UTI husababishwa na Mtu kufanya mapenzi mara kwa mara


• UTI huweza kumpata mtu kupitia mdomoni


• UTI huweza kusababisha mwanaume kuwa na hamu ya kufanya mapenzi zaidi kuliko kawaida


• UTI ni ugonjwa wa Wanawake tu


• UTI haiwezi kutokea kwa Mwanamke baada ya kujifungua


• Mwanaume huweza kumuambukiza mwenzake baada ya kuvaa nguo moja au kushare


• Hakuna uhusinao kati ya ugonjwa wa UTI na maumivu makali ya Mkojo


• Mwanamke mwenye UTI za Mara kwa mara huweza kutolewa kizazi


FAHAMU BAADHI YA DALILI ZA UGONJWA WA UTI


- Mtu kukojoa mara kwa mara


- Mkojo kuchoma wakati wa kukojoa


- Mtu kupata maumivu ya tumbo hasa upande wa kushoto kwa chini


- Joto la mwili kuwa juu au mtu kuwa na homa


- Maumivu ya joints,viungo pamoja na Misuli

n.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MUDA SAHIHI WA MTU KUFANYA MAZOEZIAfyaclass Bongo Social •

 MAZOEZI

• • • • •

MUDA SAHIHI WA MTU KUFANYA MAZOEZI


Kwanza kabsa, kufanya mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako, na moja ya Faida kubwa za kufanya mazoezi ni pamoja na;


✓ Kuimarisha kinga ya mwili na kukukinga dhidi ya magonjwa ambukizi


✓ Kukuepusha na magonjwa sugu kama vile; Presha,kisukari,magonjwa ya moyo n.k


✓ Mazoezi huleta furaha na kukuepusha na msongo wa mawazo


✓ Mazoezi huimarisha mzunguko wa damu na kusababisha vidonda kupona kwa haraka zaidi


✓ mazoezi husaidia sana kwa watu wenye tatizo la uzito mkubwa au wanene kupita kiasi

N.k


MUDA SAHIHI WA MTU KUFANYA MAZOEZI


- Inashauriwa mtu kufanya mazoezi angalau kuanzia Muda wa Nusu Saa au dakika 30 Kila siku,


Na watu wengi hupenda kufanya mazoezi wakati wa Asubuhi au Jioni, vyovyote ni sawa tu kulingana na ratiba yako



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

UMUHIMU WA KUFANYA VIPIMO JUU YA MAGONJWA MBALI MBALIAfyaclass Bongo Social •

 VIPIMO

• • • • •

UMUHIMU WA KUFANYA VIPIMO JUU YA MAGONJWA MBALI MBALI


Kwa hivi sasa kuna magonjwa mengi, na ambayo huwa na dalili sawa au zinazoingiliana,


Hivo swala la kufanya vipimo kabla ya kuanza tiba ni muhimu sana,


Kumbuka; sio kila homa ni Malaria


fanya vipimo kwanza kujua tatizo linalokusumbua kutokana na dalili unazozipata kabla ya matumizi ya dawa,


epuka matumizi ya dawa hovio pasipo maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE kWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

Chanzo cha Mtu Kupiga CHAFYA,Tiba yake na Faida zakeAfyaclass Bongo Social •

 CHAFYA

• • • •

Chanzo cha Mtu Kupiga CHAFYA na Faida zake


Kwa namna moja au nyingine kupiga chafya huweza kuwa ni mojawapo ya Njia ya mwili kuondoa uchafu au kitu chochote ambacho kinajaribu kuingia kwenye njia ya hewa,


japo zipo sababu mbali mbali zinazochangia mtu Kupiga Chafya.


SABABU ZA MTU KUPIGA CHAFYA NI PAMOJA NA;


- Tatizo la allergy juu  ya vitu flani kama sabuni,mafuta,perfume n.k


- Tatizo la mashambulizi ya Virusi wanaosababisha mafua kama vile; maambukizi ya RHINOVIRUS n.k


- Kuingia kwa vitu vya kigeni kama Vumbi, Pilipili n.k ambavyo husababisha hali ya muwasho ndani ya pua


- Mtu kuacha gafla matumizi ya dawa kama vile; Opioid narcotics


- Kuvuta dawa puani jamii ya Corticosteroids


- Kuvuta hewa ya baridi sana


- Na mara chache sana kuumia ndani ya pua

n.k


MATIBABU


endapo kupiga chafya imekuwa tatizo la kila mara, ni muhimu kuepuka vitu ambavyo hukusababishia tatizo lako,


Au unaweza kuongea na wataalam wa afya kwa ajili ya msaada zaidi.


KUMBUKA; Kupiga chafya kuna Faida mwilini,lakini kunaweza kuwa ni ugonjwa pia ambao huhitaji tiba


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

DAWA ZA MINYOO KWA MWANAMKE/MAMA MJAMZITOAfyaclass Bongo Social •

 MJAMZITO

• • • • •

DAWA ZA MINYOO KWA MWANAMKE/MAMA MJAMZITO


Kama umewahi kwenda na kuhudhuria kliniki ukiwa mjamzito,utakubaliana na mimi kwamba wakina mama Wajawazito hupewa dawa zinazoitwa MEBENDAZOLE,


Je dawa hizi ni kwa ajili ya nini?


Wakina mama wajawazito hupewa Dawa za MEBENDAZOLE KWA AJILI YA TATIZO LA MINYOO


Je kwanini wanawake wajawazito Wasipewe ALBENDAZOLE ambazo watu wengi hutumia kwa ajili ya kutibu Minyoo?


UTAFITI: 


Baada ya utafiti kufanyika ambao ulihusisha panya pamoja na Sungura wajawazito,ulionyesha matumizi ya Albendazole huweza kuleta madhara kwa viumbe ambavyo vipo tumboni,


Japo hakuna ushahidi wa moja kwa moja kwa Binadamu.



Hivo basi, kutokana na utafiti huo ikaonekana chaguo bora zaidi kwa mama mjamzito iwe ni mebendazole badala ya Albendazole


KUJUA kuhusu MAHUDHURIO YA KLINIKI kwa Mama mjamzito,Soma hapa


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)Afyaclass Bongo Social •

 Q FEVER

• • • • •

UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)


CHANZO


Ugonjwa wa Q fever ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria wanaojulikana kwa jina la Bacterium Coxiella Burnetii,


Bacteria hawa husambazwa kwenda kwa binadamu kupitia wanyama kama vile; Mbuzi,kondoo n.k


DALILI ZA UGONJWA WA Q FEVER NI PAMOJA NA;


✓ Joto la mwili kuwa juu sana Mfano; 41 °C


✓ Mgonjwa kupata tatizo la kuharisha


✓ Kupata kichefuchefu pamoja na kutapika


✓ Mgonjwa kukohoa mara kwa mara


✓ Mwili kutetemeka


✓ Mwili kuchoka kupita kawaida


✓ Mgonjwa kupata maumivu makali ya Kichwa



MADHARA YA UGONJWA WA Q FEVER


- Ugonjwa huu huweza kuharibu Mapafu,Ubongo,Ini pamoja na Moyo


- Ugonjwa huu huweza kusababisha kuvimba kwa kuta za ndani ya moyo yaani kwa kitaalam Endocarditis


- Ugonjwa huu huweza kusababisha shida kwenye mapafu kama vile; Pneumonia n.k


- Ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye ujauzito kama vile;mimba kutoka zenyewe,mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(premature), mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,mtoto kuzaliwa mfu n.k


MATIBABU YA Q FEVER


• Ugonjwa huu huweza kutibiwa kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; Doxcycline n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

LIST YA MAGONJWA AMBAYO HUWEZA KUSABABISHA MTU KUKOSA HAMU YA CHAKULAAfyaclass Bongo Social •

 APPETITE

• • • • •

LIST YA MAGONJWA AMBAYO HUWEZA KUSABABISHA MTU KUKOSA HAMU YA CHAKULA


Magonjwa haya huweza kutokana na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; PARASITE,BACTERIA,FANGASI,VIRUSI N.K


LIST YA MAGONJWA AMBAYO HUWEZA KUSABABISHA MTU KUKOSA HAMU YA CHAKULA


1. Ugonjwa wa malaria


2. Maambukizi kwenye ngozi ya mwili


3. Maambukizi kwenye njia ya hewa yaani upper respiratory infection


4. Ugonjwa wa Pneumonia


5. Ugonjwa wa kuvimba kwa mfumo wa chakula yaani Gastroenteritis


6. Tatizo la kuvimba utumbo mkubwa yaani Colitis


7. Magonjwa ya kudumu au muda mrefu ya ini yaani Chronic liver disease


8. Tatizo la moyo kufeli na kushindwa kufanya kazi


9. Tatizo la figo kufeli


10. Ugonjwa wa homa ya Ini


11. Maambukizi ya virusi vya UKIMWI


12. Tatizo la tezi aina ya thyroid kuzalisha hormone chache yaani Hypothyroidism


13. Aina mbali mbali za kansa kama vile;


• Kansa ya kongosho(pancrease)


• Kansa ya utumbo mkubwa


• Kansa ya tumbo


• Kansa ya vifuko vya mayai n.k


14. Hali ya kuwa mjamzito, hasa katika miezi mitatu ya mwanzoni yaani First trimester


KUMBUKA; Kuna Matumizi ya baadhi ya dawa ambayo pia huweza kusababisha hamu ya chakula kupotea kama vile;


• Dawa za chemotherapy


• morphine


• codeine


• na baadhi ya antibiotics


N.K


KWA USHAURI ZAID,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

Tatizo la macho kuto kuona mbaliAfyaclass Bongo Social •

 MACHO

• • • • 

Tatizo la macho kuto kuona mbali


Tatizo hili huwapata watu wengi kwa hivi sasa, na zipo dalili mbali mbali ambazo huonekana kwa mtu mwenye tatizo hili na ndipo uchunguzi wa kina wa macho yake hufanyika


DALILI ZA Tatizo la macho kuto kuona mbali NI PAMOJA NA;


✓ Mtu kuona marue rue au kutokuona vizuri kwa vitu ambavyo vipo mbali, ila vitu vya karibu huviona vizuri


✓ Mtu ili aone vizuri kitu ni mpaka akonyeze macho yake ndyo huweza kuona


✓ Kupata maumivu ya kichwa


✓ Mtu kutokuona vizuri hasa wakati wa usiku akiwa anaendesha gari yaani night myopia

N.k


MATIBABU YA Tatizo la macho kuto kuona mbali


- Mgonjwa mwenye shida hii huweza kupewa miwani yenye lense sahihi kwake baada ya kupimwa macho


- Mtu kufanyiwa upasuaji wa macho ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Refractive Surgery


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

HALI YA MWANAMKE KUWA NA NYWELE NYINGI USONI(Hirsutism)Afyaclass Bongo Social •

 Hirsutism

• • • • •

HALI YA MWANAMKE KUWA NA NYWELE NYINGI USONI(Hirsutism)


Hirsutism hii ni hali ya mwanamke kuwa na nywele nyingi maeneo ya usoni,kifuani,mgongoni,tumboni chini,kwenye mapaja n.k


CHANZO CHA HALI HII;


- mwanamke kuwa na kiwango kikubwa cha hormone aina ya Androgen


- Tatizo la Polycystic ovary syndrome(PCOS)


- mwili kuwa katika mazingira ya kiwango kikubwa cha hormone ya Cortisol ambayo hutokana na;


• Tezi la andrenaline (andrenal gland) kuzalisha kiwango kikubwa sana cha Cortisol


• matumizi ya dawa kama prednisone kwa muda mrefu


- mwanamke kuzaliwa na tatizo kwenye tezi la adrenaline yaani congenital adrenal hyperplasia ambapo huhusisha uzalishaji wa kiwango kikubwa sana cha hormone jamii ya Steroids kama vile; androgen na Cortisol


- Uvimbe kwenye tezi la adrenaline


- Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile; Danazol, Minoxidil n.k


DALILI ZA HALI HII YA Hirsutism NI PAMOJA NA;


✓ mwanamke kuwa na nywele nyingi maeneo ya usoni,kifuani,mgongoni,tumboni chini,kwenye mapaja n.k


✓ wengine huanza kuwa na kipara


✓ Matiti kuwa madogo sana kupita kawaida


✓ kuongezeka kwa misuli ya mwili


✓ Kinembe yaani Clitoris kuwa kikubwa zaidi

N.k


MATIBABU YA HALI HII


- Hali hii  huhusisha matibabu ya aina mbali mbali kama vile; matumizi ya dawa


mfano; combined oral contraceptives(COC's), dawa zinazozuia uzalishwaji wa androgeni yaani Anti-androgen drugs, Topical cream kama Vaniqa n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA UPUNGUFU WA CALCIUM MWILINI pamoja na Vyakula Vyenye Kiwango Kikubwa cha CalciumAfyaclass Bongo Social •

 CALCIUM

• • • • •

MADHARA YA UPUNGUFU WA CALCIUM MWILINI pamoja na Vyakula Vyenye Kiwango Kikubwa cha Calcium


MADHARA YA UPUNGUFU WA CALCIUM MWILINI ni pamoja na;


- Upungufu wa Calcium mwilini husababisha mifupa ya mwili kudhoofika na mtu kuwa na magonjwa mbali mbali ya mifupa


- Upungufu wa Calcium mwilini huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na kansa ya utumbo mpana yaani Colon pamoja na kansa ya Rectum


- Upungufu wa Calcium mwilini huongeza uwezekano wa mtu kupata magonjwa mbali mbali ya Moyo, Stroke n.k



- Upungufu wa Calcium mwilini huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo la Presha au shinikizo la damu


- Upungufu wa Calcium mwilini huongeza uwezekano wa mama mjamzito kuwa na kifafa cha mimba


- Upungufu wa Calcium mwilini huongeza uwezekano kwa mama mjamzito kuwa na tatizo la Presha kipindi cha mimba yaani Pregnancy Induced hypertension(PIH)


- Upungufu wa Calcium mwilini huongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo la kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi


- N.k


VYAKULA VYENYE KIWANGO KIKUBWA CHA CALCIUM


✓ Maziwa pamoja na vitu vyote vyenye maziwa ndani yake kama vile; Yogurt,cheese n.k


✓ Samaki wakubwa pamoja na wadogo kama dagaa n.k


✓ Cabbage, Chinese,spinach, Broccoli na mboga za majani zingine


✓ Maharage ya kawaida,Soya beans n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAIDA ZA MBEGU NA MAJANI YA MLONGE MWILINIAfyaclass Bongo Social •

 MLONGE

• • • • •

FAIDA ZA MBEGU NA MAJANI YA MLONGE MWILINI


Bila shaka ulishawahi kusikia kuhusu mlonge kama basi hujawahi kuuona au kuutumia, 


Mti huu una faida nyingi sana kwenye mwili wa binadamu, na katika makala hii tutachambua baadhi ya faida chache kuhusu matumizi ya mbegu za Mlonge pamoja na Majani yake


FAIDA ZA MBEGU ZA MLONGE PAMOJA NA MAJANI YAKE MWILINI


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana katika kuupa mwili nguvu


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kuongeza hamu ya chakula kwa mtu mwenye shida ya kukosa hamu ya kula


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kuondoa tatizo la mtu kuwashwa kutokana na mchafuko wa kwenye damu


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kuongeza kiwango cha CD-4 hivo kuwa faida kubwa kwa wagonjwa wa Ukimwi


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kwa wagonjwa wa Kisukari


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kwa wagonjwa wa shinikizo la Damu au Presha


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana hata kwa mgonjwa wa Malaria


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kwa mtu ambaye hupatwa na uchovu wa mara kwa mara


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kwa mtu ambaye hupatwa na Homa za mara kwa mara


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kwa watu Wenye Kansa au Saratani ya Tumbo


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kuongeza virutubisho muhimu mwilini kama vile; Madini ya Potassium, Calcium pamoja Na vitamin A na C


- Matumizi ya majani ya Mlonge husaidia sana kwa watu wenye magonjwa mbali mbali ya Ngozi


- Matumizi ya Mlonge husaidia sana kwa watu wanaopatwa na majipu ya Mara kwa mara


- Lakini pia baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba matumizi ya mlonge huongeza kiu ya maji, na kumfanya mtumiaji kunywa maji mengi swala ambalo ni muhimu sana na lina faida kubwa kwenye afya ya mwili


- Mlonge husaidia sana kuimarisha umeng'enyaji wa chakula mwilini


- Matumizi ya mlonge husaidia kuimarisha kinga yako ya mwili

N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA MTOTO KUTEMBELEA VIDOLE(toe walking)Afyaclass Bongo Social •

 MTOTO

• • • • •

CHANZO CHA MTOTO KUTEMBELEA VIDOLE(toe walking)


Mtoto kutembelea vidole yaani toe walking, mara nyingi ni hali ambayo humtokea mtoto wakati anajifunza kutembea,


Kumbuka; Mtoto kutembelea vidole akiwa na umri wa zaidi ya Miaka 2 huweza kuwa ni tatizo,


Watu wengi hawajui pia kuna baadhi ya matatizo ambayo huweza kuchangia mtoto kutembelea vidole, na matatizo hayo ni kama vile;


✓ Mtoto kupatwa na tatizo la autism


✓ Mtoto kupatwa na matatizo kwenye misuli yake yaani Muscular Dystrophy


✓ Mtoto kuwa na matatizo kwenye ubongo yaani Cerebral palsy


✓ Mtoto kuwa na matatizo kwenye tendons n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Mtoto huweza kukutana na wataalam wa afya na kupatiwa tiba mbali mbali kama vile;


Tiba ya mazoezi yaani Physiotherapy pamoja na Upasuaji kama tatizo litahitaji huduma hii


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAMBO AMBAYO HUTOKEA KWA MWANAMKE BAADA YA KUPOTEZA BIKRAAfyaclass Bongo Social •

 BIKRA

• • • • 

MAMBO AMBAYO HUTOKEA KWA MWANAMKE BAADA YA KUPOTEZA BIKRA


Baada ya mwanamke kupoteza usichana wake yaani Bikra hupata mabadiliko mbali mbali kwenye mwili wake,


Fahamu kuhusu mwanamke kupoteza Bikra na matokeo yake


MAMBO AMBAYO HUTOKEA KWA MWANAMKE BAADA YA KUPOTEZA BIKRA


• Bikra hutoka baada ya mwanamke kuanza kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza


• Sio kila mwanamke Bikra yake ilitoka baada ya kufanya mapenzi,wengine Bikra hutoka kutokana na sababu mbali mbali kama vile; Kuingiza vidole ukeni mara kwa mara, kutumia sex toys, kuchomwa na kitu cha ncha kali n.k


• Sio kwa kila mwanamke lazima damu itoke wakati Bikra inatoka


• Hali ya kuvutika kwa uke yaani Vaginal elasticity hubadilika mara tu baada ya Bikra kutoka


• Mwanamke huweza kuanza kupata mabadiliko mbali mbali mwilini kama vile; matiti kuwa makubwa zaidi n.k


• Mwanamke kupata maumivu makali, damu kutoka n.k Hasa baada ya Hymenal tissues kuvutika sana na kuharibika


• Mwanamke kuingiwa na hofu pamoja na wasiwasi mkubwa kuhusu swala la kufanya mapenzi


• Mwanamke kuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya zinaa wakati Bikra inatoka au muda mfupi baada ya kutoka,


Magonjwa hayo ni kama vile; Maambukizi ya HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV), ugonjwa wa Pangusa au Chlamydia, Kisonono(Gonorhea), Genital herpes N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

Chanzo cha Maambukizi kwenye Sikio(Acute Otitis media),DALILI NA TIBAAfyaclass Bongo Social •

 SIKIO

• • • • •

Chanzo cha Maambukizi kwenye Sikio(Acute Otitis media),DALILI NA TIBA


Acute Otitis media, ni maambukizi ambayo hutokea sehemu ya ndani ya Sikio yaani Middle Ear, maambukizi haya huwapata watoto zaidi ya watu wazima


CHANZO CHA MAAMBUKIZI KWENYE SIKIO


• Tatizo hili husababishwa na vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile BACTERIA au VIRUSI, japo pia kuna baadhi ya sababu huongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo hili, na sababu hizo ni kama vile;


✓ Allergy


✓ Tatizo la mafua


✓ Maambukizi yaani Sinus infection


✓ Uvutaji wa Sigara

n.k


DALILI ZA MAAMBUKIZI KWENYE SIKIO


1. KWA WATOTO


- Mtoto kupata maumivu makali ya sikio hasa wakati akijaribu kulala


- Sikio kutoa maji maji,usaha au damu


- Mtoto kupata shida ya kukosa usingizi


- Mtoto kulia sana


- Mtoto kupata Maumivu makali ya kichwa


- Mtoto kupata tatizo la kutokusikia vizuri


- Joto la mwili kuwa juu au mtoto kuwa na Homa


- Kupoteza balance ya mwili


- Kukosa hamu ya kula chakula


- Mtoto kupata Maumivu makali ya shingo


- Mtoto kuhisi sikio kujaa na kuwa zito


- Mtoto kutapika na kuharisha

n.k


2. KWA WATU WAZIMA


- Kupata maumivu makali ya sikio


- Sikio kuvuja maji maji,usaha au Damu


- Kupata tatizo la kutokusikia vizuri

n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


- matibabu ya tatizo hili huhusisha dawa mbali mbali kama vile; Dawa jamii ya antibiotics, dawa za maumivu n.k, 


kulingana na chanzo chake, hivo ni vizuri mgonjwa kwenda hospital na kuchunguzwa vizuri kabla ya kuanza tiba



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

ZIFAHAMU AINA MBILI ZA KISUKARI yaani Diabetes Type 1 and Diabetes Type 2Afyaclass Bongo Social •

 KISUKARI

• • • • • •

ZIFAHAMU AINA MBILI ZA KISUKARI yaani Diabetes Type 1 and Diabetes Type 2


DIABETES TYPE 1


Hii ni aina ya kisukari ambayo hutokana na Kongosho au Pancrease kuzalisha kiwango kidogo sana cha INSULIN au kutokuzalisha kabsa.


- Aina hii ya kisukari kwa asilimia kubwa huwapata sana Watoto pamoja na Vijana


DALILI ZA AINA HII YA KISUKARI(DIABETES TYPE 1)


- Mgonjwa kuona marue rue


- Mwili kuchoka kupita kiasi na kuwa dhaifu sana


- Uzito wa mwili kupungua kwa kasi sana na mtu kukonda


- Mtu kuhisi njaa sana kila mara


- Mtoto kuanza kujikojolea kitandani wakati wa usiku wakati hakuwa na shida hyo hapo mwanzo kabla ya ugonjwa


- Kukojoa mara kwa mara


- Mtu kupata kiu sana ya maji



KUMBUKA; hakuna tiba ya aina hii ya kisukari bali kuna matibabu dhidi ya kudhibiti dalili zake pamoja na kiwango cha sukari kwenye damu


DIABETES TYPE 2


- Hii ni aina ya kisukari ambayo hutokea baada ya mwili kushindwa kudhibiti,kurekebisha na kutumia sukari iliyopo hali ambayo hupelekea kiwango kikubwa sana cha sukari kuwepo kwenye damu,


na shida hii hutokea pale ambapo, Kongosho au Pancrease haizalishi kiwango cha kutosha cha Insulin au Hormones ambazo hurekebisha kiwango cha sukari ndani ya seli kutokufanya kazi vizuri na Insulin hivo kupelekea kiwango kidogo sana cha Sukari kuchukuliwa na Seli.


- Aina hii ya kisukari huwapata sana Watu wazima kuliko watoto na vijana


KUMBUKA; hakuna tiba ya aina hii ya kisukari bali kuna matibabu dhidi ya kudhibiti dalili zake pamoja na kiwango cha sukari kwenye damu



DALILI ZA AINA HII YA KISUKARI(DIABETES TYPE 2)


✓ Vidonda kuchelewa sana Kupona


✓ Mtu kupata kiu sana


✓ Kukojoa mara kwa mara


✓ Kupata njaa sana kila mara


✓ Uzito wa mwili kushuka kwa kasi


✓ Mwili kuchoka kupita kawaida


✓ Kuona marue rue


✓ Kupata maambukizi ya magonjwa ya mara kwa mara


✓ Kuhisi hali ya kuchomwa chomwa kwenye miguu na mikono



ZINGATIA HAYA;


- Hakikisha unapata dawa kama Insulin therapy n.k


- Kufanya mazoezi kila siku angalau dakika 30 au nusu saa


- Kula vyakula ambavyo vina virutubisho vyote


-N.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAHAMU KUHUSU FAIDA ZA UYOGA MWEKUNDU MWILINI (GANODERMA) Afyaclass Bongo Social •

 UYOGA

• • • • •

FAHAMU KUHUSU FAIDA ZA UYOGA MWEKUNDU MWILINI (GANODERMA)


Uyoga huu mwekundu umekuwa ukitumika sana kama dawa maeneo mbali mbali duniani kama vile CHINA n.k


Je matumizi ya aina hii ya Uyoga mwekundu yana Faida gani mwilini?


FAHAMU KUHUSU FAIDA ZA UYOGA MWEKUNDU MWILINI


- Uyoga huu mwekundu husaidia kuimarisha kinga yako ya mwili


- Uyoga huu mwekundu husaidia kuondoa hali ya uchovu mwilini


- Uyoga huu mwekundu husaidia kwa watu wenye matatizo ya Shinikizo la Damu au Presha


- Uyoga huu mwekundu husaidia sana katika kupunguza kiwango cha LEHEMU(cholestrol) mwilini


- Uyoga huu mwekundu husaidia kwa watu wenye shida ya Allergy mbali mbali


- Uyoga huu mwekundu husaidia sana katika kuzuia kansa au aina mbali mbali za Saratani mwilini


- Matumizi ya Uyoga huu mwekundu mara kwa mara husaidia kuondoa sumu mbali mbali mwilini


- Uyoga huu mwekundu husaidia kuimarisha afya ya Seli hai za mwili


- Uyoga huu mwekundu huweza kusaidia sana kwa watu wanaopatwa na mashambulizi ya UTI za mara kwa mara


- Uyoga huu mwekundu ni chanzo kizuri sana cha virutubisho vingi mwilini kama vile PROTEINS n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA KUCHA KUWA NGUMU KAMA BATIAfyaclass Bongo Social •

 KUCHA

• • • • • 

CHANZO CHA KUCHA KUWA NGUMU KAMA BATI


Tatizo hili huhusisha kucha kuwa nene na ngumu kupita kawaida, je chanzo chake ni nini?


CHANZO CHA KUCHA KUWA NGUMU KAMA BATI


- Moja ya sababu ya tatizo hili la kucha kuwa ngumu kupita kawaida ni pamoja na;

✓ Maambukizi ya Fangasi ambayo hujulikana kwa kitaalam kama ONYCHOMYCOSIS,


Maambukizi ya YEAST n.k


✓ Kuumia kwenye kucha mara kwa mara, tatizo ambalo huwapata sana watu wa michezo kama vile; Wachezaji wa mpira wa Miguu n.k


✓ Yellow nail syndrome, tatizo ambalo husababisha kucha kubadilika rangi na kuwa manjano na hatimaye kucha kuanza kujikunja na kuwa nene


✓ Matatizo kwenye mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune disorder kama vile PSORIASIS,

huweza kusababisha kucha kuwa na mikunjo pamoja na kuwa ngumu


✓ Tatizo la kwenye ngozi kama vile Paronychia ambalo husababisha wekundu kuzunguka kucha pamoja na Kuvimba


✓ Pia tatizo hili la kucha kuwa Ngumu huwapata sana watu ambao wana Umri mkubwa


MATIBABU YA TATIZO LA KUCHA KUWA NGUMU

- tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake,Mfano kama chanzo ni maambukizi ya fangasi,basi mgonjwa hupewa dawa za fangasi N.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

USHAURI KWA MWANAMKE BAADA YA MIMBA KUTOKA(miscarriage)Afyaclass Bongo Social •

 MIMBA

• • • • •

USHAURI KWA MWANAMKE BAADA YA MIMBA KUTOKA


Tatizo la mimba kutoka zenyewe yaani Miscarriage hutokea sana kwa wanawake wengi kwa hivi sasa,


Na asilimia kubwa ya mimba huharibika kwenye miezi mitatu(3) ya mwanzoni yaani First trimester


Je baada ya mimba kutoka,ni mambo gani mwanamke anatakiwa kuzingatia?


BAADHI YA MAMBO YA KUZINGATIA KWA MWANAMKE BAADA YA UJAUZITO KUHARIBIKA


- Hakikisha unapata muda wa kutosha wa kupumzika


- Epuka kufanya kazi nzito na za kunyanyua vitu vizito


- Hakikisha unapata vyakula ambavyo vinakiwango cha kutosha cha madini ya Chuma yaani Iron-rich foods


- Hakikisha unapata virutubisho vyenye aina zote za Vitamins kwa kiwango kikubwa Yaani Multivitamins


- Matumizi ya dawa ambazo umepewa hospital kwa ajili ya kukukinga na kupata maambukizi ya magonjwa mbali mbali ni muhimu sana Mfano; dawa jamii ya Antibiotics


- Ni vizuri kutokufanya mapenzi mpaka damu iache kutoka, ambapo kwa wataalam wa afya hushauri angalau ukae hata kipindi cha Wiki 6 bila kufanya mapenzi


- Kaa kwa muda mrefu kidogo kabla ya kubeba ujauzito mwingine, angalau kwa kipindi cha Miezi sita(6) na kuendelea


- Usitumie vitu mbali mbali wakati unaosha sehemu zako za siri, wala usiweke vidole sehemu zako za siri

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KUCHANGANYA DAWA NA MAZIWA,PAMOJA NA DAWA AMBAZO HURUHUSIWI KUNYWA NA MAZIWAAfyaclass Bongo Social •

 MAZIWA

• • • • • •

MADHARA YA KUCHANGANYA DAWA NA MAZIWA,PAMOJA NA DAWA AMBAZO HURUHUSIWI KUNYWA NA MAZIWA


Tukinzungumzia swala la kutokuchanganya dawa pamoja na maziwa, tunamaanisha MAZIWA yenyewe pamoja na kula vitu vyote ambavyo vina maziwa ndani yake kama Vile; YOGURT,CHEESE n.k


Kunywa dawa pamoja na maziwa hua sio salama kwani baadhi ya dawa huweza kuathiriwa katika uwezo wake wa Ufyonzwaji mwilini


Hapa tunaweza kusema "milk can interfere and affect some medications's absorption"


Je nini kinatokea?


Baadhi ya dawa hujishikiza kwenye Calcium(Ca) iliyopo kwenye maziwa na kutengeneza kitu tumboni au sehemu ya juu ya utumbo mdogo ambacho hakiwezi kufyozwa kabsa mwilini.


HIZI HAPA NI BAADHI YA DAWA AMBAZO HURUHUSIWI KUNYWA PAMOJA NA MAZIWA


✓ Tetracycline


✓ Doxycycline


✓ Ciproflaxin


✓ Quinolones


✓ Propranolol


✓ Mercaptopurine


✓ Non-steroidal anti-inflammatory drugs


✓ Digitalis


✓ Amiloride


✓ Omeprazole


✓ Spironolactone


✓ Ranitidine

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA MAZIWA YA KOPO YA FORMULA KWA WATOTOAfyaclass Bongo Social •

 MAZIWA

• • • • •

MADHARA YA MAZIWA YA KOPO YA FORMULA KWA WATOTO


Katika hali ya kawaida,mtoto baada ya kuzaliwa anatakiwa anyonye maziwa ya mama peke yake bila kupewa kitu kingine chochote kwa kipindi cha Miezi sita(6),


ambapo kwa kitaalam tunaita EXCLUSIVE BREASTFEEDING,


Lakini kuna baadhi ya wakina mama baada ya kuzaa watoto hupata changamoto ya maziwa kutokutoka, hivo kuwalazimu wengine kutumia maziwa ya Kopo,


Hata hivo wataalam wa afya huendelea kuwaelimisha na kuwasisitiza wakina mama wenye changamoto hii ya maziwa kutokutoka baada ya kujifungua, kwamba hali hii huisha na maziwa ya mama hutoka kwa kadri mtoto anavyojitahidi kunyonya,


Hivo maziwa ya kopo huwa ni ya dharura tu lakini sio ya kuyategemea kwa ajili ya kumlisha mtoto wako.


MADHARA YA MAZIWA YA KOPO YA FORMULA KWA WATOTO


- watalaam wa Afya na baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba,maziwa haya ya Kopo au FORMULA sio salama kwa watoto wadogo endapo yatakuwa ndyo Tegemezi lao, Hasa pale mama akiacha kabsa kumnyonyesha mtoto na kumpa maziwa ya kopo.


Baadhi ya madhara ambayo huweza kutokea endapo mtoto hutumia maziwa ya Kopo ni pamoja na;


1. Mtoto kushambuliwa kwa urahisi na magonjwa kwenye mfumo wa chakula na kuleta madhara mbali mbali kama vile; Gastroenteritis


2. Mtoto kupatwa na tatizo la kuharisha mara kwa mara


3. Mtoto kuwa katika hatari ya kupatwa na Kisukari hasa TYPE 1 Diabetes


4. Tatizo la Asthma


5. Vifo vya gafla kwa watoto yaani Sudden Infant Death syndrome


6. Mtoto kupatwa na maambukizi kwenye mfumo wa hewa yaani Lower respiratory tract Infection


7. Mtoto kupatwa na magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile; Atopic Dermatitis

N.K


KWA UJUMLA ni kwamba,maziwa ya mama humpa mtoto kinga ya kutosha dhidi ya Magonjwa mbali mbali hasa ile miezi mitatu(3) ya mwanzoni,ambapo bado mtoto hana kinga tegemezi inayotokana na mwili wake.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAHAMU KUHUSU AINA ZA MAKUNDI YA DAMU(BLOOD GROUPS) PAMOJA NA UCHANGIAJI WA DAMUAfyaclass Bongo Social •

BLOOD GROUPS

• • • • • 

FAHAMU KUHUSU AINA ZA MAKUNDI YA DAMU(BLOOD GROUPS) KWENYE MWILI WA BINADAMU PAMOJA NA UCHANGIAJI WA DAMU

AINA ZA MAKUNDI YA DAMU(BLOOD GROUPS)

Kuna aina kuu NNE(4) za makundi ya Damu ambayo ni;

1. Blood group A

2. Blood group B

3. Blood group AB

4. Blood group O

Lakini kwa kuongezea,bila shaka utaona kila kundi la damu ambalo mtu kapimwa,Huandikiwa alama mbili POSITIVE au NEGATIVE mfano;

Blood group A+, A-, B+,B-, AB+, AB-, O+, O- Je Hizi positive na Negative ni kitu gani?

Hizi Humaanisha Rhesus factor ambapo Kundi lolote la damu lazima liwe POSITIVE- ikiwa na maana kwamba lina Rhesus Factor au NEGATIVE ikiwa na maana kwamba,halina Rhesus factor.

UCHANGIAJI WA DAMU

- Hapana tuna watu wa aina mbili ambao ni MCHANGIAJI WA DAMU yaani DONOR pamoja na anayechangiwa damu au mpokeaji wa damu yaani RECIPIENT

- Tuanze na Maelezo kuhusu Mchangiaji wa Damu yaani donor

1. MCHANGIAJI WA DAMU(DONOR)

(i) Blood group A

- Mtu mwenye Blood group A+, hutoa damu kwa watu wenye Blood group A+ na AB+.

- Mtu mwenye Blood group A-, hutoa damu kwa watu wenye Blood group A-,A+,AB- na AB+.

(ii)  Blood group B

- Mtu mwenye Blood group B+ hutoa damu kwa watu wenye Blood group B+ na AB+.

- Mtu mwenye Blood group B- hutoa damu kwa watu wenye Blood group B-,B+,AB- na AB+.

(iii) Blood group AB

- Mtu mwenye Blood group AB+ hutoa damu kwa watu wenye  Blood group AB+ peke yake.

- Mtu mwenye Blood group AB- hutoa damu kwa watu wenye Blood group AB- na AB+.

(iv) Blood group O

- Mtu mwenye Blood group O+ hutoa damu kwa watu wenye Blood group O+,A+,B+ na AB+.

- Na Mtu mwenye Blood group O- huyu ni UNIVERSAL DONOR, yaani hutoa damu kwa watu wenye makundi yote ya damu, A+,A-,B+,B-,AB+,AB-,O+ na O-.

2. MPOKEAJI WA DAMU(RECIPIENT)

(i) Blood group A

- Mtu mwenye Blood group A+, hupokea damu kwa watu wenye Blood group A+,A-,O+ na O-.

- Mtu mwenye Blood group A-, hupokea damu kwa watu wenye Blood group A- na O-.

(ii) Blood group B

-- Mtu mwenye Blood group B+ hupokea damu kwa watu wenye Blood group B+,B-,O+ na O-.

- Mtu mwenye Blood group B- hupokea damu kwa watu wenye Blood group B- na O-.

(iii) Blood group AB

- Mtu mwenye Blood group AB+ hupokea damu kwa watu wote yaani ni UNIVERSAL RECIPIENT ,hivo hupokea damu kutoka kwa makundi yote ya damu yaani Blood group A+,A-,B+,B-, AB+,AB-,O+ na O-

- Mtu mwenye Blood group AB- hupokea damu kwa watu wenye Blood group A-,B-,AB- na O-.

(iv) Blood group O

- Mtu mwenye Blood group O+ hupokea damu kwa watu wenye Blood group O+ na O-

- Na Mtu mwenye Blood group O- hupokea damu kwa watu wenye Blood group O-.

KUFAHAMU ZAIDI kuhusu Madhara ya Baadhi ya makundi ya Damu Soma hapa..!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD