MJAMZITO
• • • •
Madhara ya kuinama kwa mjamzito(dalili za hatari kwa mwanamke mjamzito)
FAHAMU:
Kunyanyua vitu vizito sana, Kusimama kwa muda mrefu sana, Kujikunja sana,kutikiswa sana ikiwa ni pamoja na kuinama sana na kwa Muda mrefu,
huongeza uwezekano wa kutoka kwa ujauzito yaani Miscarriage, mwanamke mjamzito kujifungua kabla ya wakati yaani Preterm birth, Au kupata majeraha.
DALILI ZA HATARI KWA MWANAMKE MJAMZITO
Mwanamke mjamzito hushauriwa kuwahi haraka hospital endapo atapata dalili hizi hapa chini;
- Kuvuja damu sehemu zake za siri
- Kutoa maji sehemu za siri
- Kutoa uchafu wenye harufu mbaya sana ukeni
- Kutokumsikia mtoto akicheza tumboni zaidi ya masaa 24 kwa wale ambao mtoto kafikia umri wa kucheza tumboni
- Mwanamke mjamzito Kuona marue rue
- Kuvimba kupita kiasi miguuni,kwenye mikono,usoni n.k
- Joto la mwili kupanda au mama mjamzito kuwa na Homa
- Mwanamke mjamzito kupata kizunguzungu
- Kuanza kuwa na mawazo ya kutaka kujiua mwenyewe au kuuwa kiumbe kilichopo tumboni
- Kupata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu
- Kupata maumivu makali sana ya kichwa
n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comments