Afyaclass Bongo Social UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)

 Q FEVER

• • • • •

UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)


CHANZO


Ugonjwa wa Q fever ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria wanaojulikana kwa jina la Bacterium Coxiella Burnetii,


Bacteria hawa husambazwa kwenda kwa binadamu kupitia wanyama kama vile; Mbuzi,kondoo n.k


DALILI ZA UGONJWA WA Q FEVER NI PAMOJA NA;


✓ Joto la mwili kuwa juu sana Mfano; 41 °C


✓ Mgonjwa kupata tatizo la kuharisha


✓ Kupata kichefuchefu pamoja na kutapika


✓ Mgonjwa kukohoa mara kwa mara


✓ Mwili kutetemeka


✓ Mwili kuchoka kupita kawaida


✓ Mgonjwa kupata maumivu makali ya Kichwa



MADHARA YA UGONJWA WA Q FEVER


- Ugonjwa huu huweza kuharibu Mapafu,Ubongo,Ini pamoja na Moyo


- Ugonjwa huu huweza kusababisha kuvimba kwa kuta za ndani ya moyo yaani kwa kitaalam Endocarditis


- Ugonjwa huu huweza kusababisha shida kwenye mapafu kama vile; Pneumonia n.k


- Ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye ujauzito kama vile;mimba kutoka zenyewe,mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(premature), mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,mtoto kuzaliwa mfu n.k


MATIBABU YA Q FEVER


• Ugonjwa huu huweza kutibiwa kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; Doxcycline n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD