Afyaclass Bongo Social HALI YA MWANAMKE KUWA NA NYWELE NYINGI USONI(Hirsutism)

 Hirsutism

• • • • •

HALI YA MWANAMKE KUWA NA NYWELE NYINGI USONI(Hirsutism)


Hirsutism hii ni hali ya mwanamke kuwa na nywele nyingi maeneo ya usoni,kifuani,mgongoni,tumboni chini,kwenye mapaja n.k


CHANZO CHA HALI HII;


- mwanamke kuwa na kiwango kikubwa cha hormone aina ya Androgen


- Tatizo la Polycystic ovary syndrome(PCOS)


- mwili kuwa katika mazingira ya kiwango kikubwa cha hormone ya Cortisol ambayo hutokana na;


• Tezi la andrenaline (andrenal gland) kuzalisha kiwango kikubwa sana cha Cortisol


• matumizi ya dawa kama prednisone kwa muda mrefu


- mwanamke kuzaliwa na tatizo kwenye tezi la adrenaline yaani congenital adrenal hyperplasia ambapo huhusisha uzalishaji wa kiwango kikubwa sana cha hormone jamii ya Steroids kama vile; androgen na Cortisol


- Uvimbe kwenye tezi la adrenaline


- Matumizi ya baadhi ya dawa kama vile; Danazol, Minoxidil n.k


DALILI ZA HALI HII YA Hirsutism NI PAMOJA NA;


✓ mwanamke kuwa na nywele nyingi maeneo ya usoni,kifuani,mgongoni,tumboni chini,kwenye mapaja n.k


✓ wengine huanza kuwa na kipara


✓ Matiti kuwa madogo sana kupita kawaida


✓ kuongezeka kwa misuli ya mwili


✓ Kinembe yaani Clitoris kuwa kikubwa zaidi

N.k


MATIBABU YA HALI HII


- Hali hii  huhusisha matibabu ya aina mbali mbali kama vile; matumizi ya dawa


mfano; combined oral contraceptives(COC's), dawa zinazozuia uzalishwaji wa androgeni yaani Anti-androgen drugs, Topical cream kama Vaniqa n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD