🔷UKWELI KUHUSU MTOTO KUBEMENDWA
Maneno yaliyopo (imani zilizojengeka) siku zote ni hizi
1. Wazazi wakishiriki tendo la ndoa baada ya mama kujifungua hata kama 40 imepita wanaweza kubemenda mtoto, kwa kuwa shahawa za mwanaume zinaenda kwenye maziwa ya mama zinadhoofisha afya ya mtoto
2. Mama akipata mimba,huku akiwa na mtoto mchanga wa Miezi kadhaa anabemenda mtoto
3. Mtoto Mchanga Akinyonya maziwa ya Mama ambae ni mjamzito atabemendwa
4. Mwanandoa Akitoka nje ya ndoa akazini huko, Akirudi kusex na Mwenzie Wanabemenda mtoto
5. Eti uki sex Ukamgusa mtoto anabemendwa👐
Hoja HIZO ZOTE SIO KWELI, kwani
-mbegu za mwanaume Haziwezi enda kwenye maziwa
-kufanya tendo la ndoa ndani au nje ya ndoa HAVIBEMENDI MTOTO.
-Ukipata MIMBA unaruhusiwa kuendelea kunyonyesha Mchanga wako(Nitaandaa SOMO)
MTOTO wanaesema KABEMENDWA,kitaalamu tunasema DELAYED DEVELOPMENTAL MILESTONES, yaani mtoto anakuwa HAKUI inavyotakiwa,unakuta mtoto ana MIEZI 9, shingo Hajakaza, Hakai, au mtoto wa Mwaka na Nusu hawezi hata kusimama..na Kilo zinakuwa wengi HAZIONGEZEKI ipasavyo(inability to gain Weight). Vyanzo vikubwa vya mtoto Kutokukua Inavyotakiwa ni
1. Mtoto kutokupata maziwa ya kutosha (mama hanyonyeshi au hana maziwa ya kutosha au mtoto hanyonyi)
2. Magonjwa kama Ukimwi,magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo,pneumonia...
3. Mtoto kukosa lishe inayofaa,yaani utapiamlo pia huwa unadhoofisha mtoto na kuleta shida kwenye Ukuaji.
Kitaalamu Mke na Mume wanaruhusiwa kufanya tendo la ndoa mara tu baada ya SIKU 42 KUPITA Tangu kujifungua.
Muhimu ni Haya
1. Mama Anyonyeshe Mtoto wake ipasavyo mara kwa mara(asipozingatia italeta shida kwenye ukuaji wa mtoto)
2. Mama mwanao anyonye miezi pasipo kumpa kitu kingine chochote, akifika Miezi 6 hakikisha unampa lishe Bora(lishe yenye makundi yote ya vyakula) ili asipate utapiamlo
3. Kutoka Nje ya ndoa yako ni Hatari maana unaweza pata magonjwa ya kuambukizwa kama Maambukizi ya VVU (iwe baba,iwe Mama,ni hatari,mwisho wa siku unaweza mwambukiza na mwanao maana ANANYONYA, na hii ikampa Afya dhoofu)
Muhimu:Unapoona Afya ya mwanao HAIPO SAWA,Nenda hospitali iliyokaribu .
.
(NA @lakadoctor wa @uzazipoint)
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY HAPA
image quote pre code