VIDEO; FAHAMU KUHUSU MATUMIZI YASIO SAHIHI YA BARAKOA(MASK)Afyaclass Bongo Social •

 BARAKOA

• • • •

VIDEO; FAHAMU KUHUSU MATUMIZI YASIO SAHIHI YA BARAKOA(MASK)




Cr: @Elimu_ya_afya

Bonyeza video hapa Chini ..




0 Comment

MATUMIZI YA PILIPILI KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBOAfyaclass Bongo Social •

 VIDONDA VYA TUMBO

• • • • • •

MATUMIZI YA PILIPILI KWA MTU MWENYE VIDONDA VYA TUMBO


Kuna makala nyingi zinaelezea matumizi ya pilipili kwa Mtu mwenye vidonda vya tumbo,


Na baadhi ya makala hizo huelezea kwamba pilipili huweza kuwa ni dawa ya vidonda vya tumbo


FAHAMU hili kuhusu pilipili na Mtu mwenye vidonda vya Tumbo;


Matumizi ya pilipili kwa mtu mwenye vidonda vya tumbo husababisha hali ya maumivu kuzidi sana,


Baadhi ya watu wenye vidonda vya tumbo wakila vyakula ambavyo vina pilipili hali huzidi kuwa mbaya zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

USUBIRI MUDA GANI KUPATA MAJIBU BAADA YA KUPIMA UKIMWI?Afyaclass Bongo Social •

 UKIMWI

• • • • •

USUBIRI MUDA GANI KUPATA MAJIBU BAADA YA KUPIMA UKIMWI?


Je majibu ya Ukimwi hutoka baada ya muda gani baada ya wewe kupimwa?


majibu ya Kipimo cha ukimwi hayakai muda mrefu ili kutoka, hata dakika 15 Haziwezi kuisha tayari utakuwa umeshajua majibu yako,


Swala la kupima tena ili kupata majibu sahihi ndiyo huchukua muda wa angalau Miezi mitatu.


Hii ni kwa sababu,kwa maambukizi mapya ya Ukimwi kwa Asilimia 98% ya watu huonekana baada ya miezi mitatu.


PIMA NA JITAMBUE AFYA YAKO SASA


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KUTOKUMALIZA DOSE ZA DAWA MARA KWA MARAAfyaclass Bongo Social •

 DAWA

• • • •

MADHARA YA KUTOKUMALIZA DOSE ZA DAWA MARA KWA MARA


Watu wengi hawamalizi dose za dawa kama walivyoelekezwa na wataalam wa Afya, hasa baada ya kupata nafuu au kupona ugonjwa ambao unawasumbua,


Ukweli ni kwamba tabia hii ina madhara, na moja ya madhara yake ni pamoja na;


✓ Kusababisha ugonjwa kurudi tena ndani ya muda mfupi


✓ Dawa ulizotumia kutokufanya kazi mwilini


✓ Kusababisha hali ya usugu wa mwili kwenye dawa flani, hivo kupelekea dawa hiyo kushindwa kutibu tatizo kila mara unavyoitumia


Epuka tabia ya kuachia dose za dawa Njiani,Maliza dawa hata baada ya kupata nafuu au kupona


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

SEHEMU ZA SIRI ZA MJAMZITO KUKOSA UTE UTE(chanzo)Afyaclass Bongo Social •

 MJAMZITO

• • • • •

SEHEMU ZA SIRI ZA MJAMZITO KUKOSA UTE UTE(chanzo)


Tatizo la kukosa ute ute na kuwa mkavu ukeni kwa mama mjamzito huweza kutokea, Na sababu kubwa ni kutokana na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini ambayo hufanyika kipindi cha ujauzito.


Katika sehemu za siri za mwanamke yaani ukeni kuna tezi ambalo huhakikisha ukeni kunakuwa na hali ya unyevu unyevu pamoja na ute ute, mabadiliko ya vichocheo mwilini huweza kusababisha tezi hili lishindwe kufanya kazi vizuri.


Mbali na hivo, kuna sababu nyingine kama maambukizi ya magonjwa mbali mbali kipindi cha ujauzito kama vile; UTI, Fangasi sehemu za siri au Maambukizi katika via vya uzazi yaani PID,


mama mjamzito ni rahisi kushambuliwa na magonjwa mbali mbali kama UTI kutoka na hali ya ujauzito ambayo hupelekea kushuka kwa kinga ya mwili


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MAMBO YA KUFANYA KAMA UMEATHIRIWA NA TABIA YA KUPIGA PUNYETOAfyaclass Bongo Social •

 PUCHU

• • • • • 

MAMBO YA KUFANYA KAMA UMEATHIRIWA NA TABIA YA KUPIGA PUNYETO


Fanya mambo haya kama umeathiriwa na kupiga punyeto


- Epuka kuangalia picha au video za ngono


- Epuka kukaa na watu ambao wana tabia hii


- Fanya mazoezi ya mwili kama kucheza mpira n.k


- Epuka tabia ya kupenda kuingiza mikono sehemu za siri


- Kama tatizo limekuathiri sana kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya ushauri,elimu au tiba


Pia tunaweza kuwasiliana kwa namba +255758286584.




0 Comment

JE MWANAMKE ANAWEZA KUPATA MIMBA AKIWA ANATUMIA VIZUIZI VYA MIMBA?Afyaclass Bongo Social •

 MIMBA

• • • 

JE MWANAMKE ANAWEZA KUPATA MIMBA AKIWA ANATUMIA VIZUIZI VYA MIMBA?


Hili ni swali ambalo wanawake wengi hujiuliza,


Hapa nazungumzia vizuizi mimba kama vile; sindano,vidonge,vipandikizi pamoja na Lupu au Kitanzi.


Sinzungumzii njia kama kalenda.


Ukweli ni kwamba,Mwanamke hawezi kubeba mimba akiwa anatumia njia hizi kwa usahihi wake.


✓ Kesi nyingi za wanawake ambao wanamimba lakini wanatumia vizuizi mimba, Ujue walibeba ujauzito kabla ya kuanza kutumia, na walipofika kwa watoa huduma wa afya, hawakupimwa mimba wakaanzishiwa njia ya uzazi wa mpango,


Matokeo yake wanatumia njia flani ya uzazi wa mpango lakini wanaona kadri siku zinavyokwenda mimba huendelea kukua.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KULALA NA JIKO LA MKAA NDANIAfyaclass Bongo Social •

 JIKO LA MKAA

• • • • •

MADHARA YA KULALA NA JIKO LA MKAA NDANI


Moja ya madhara makubwa ambayo hutokana na mtu kulala na jiko la Mkaa ndani ni Kifo,


Kwanini jiko la mkaa huweza kusababisha kifo?


SOMA HAPA; Jiko la mkaa hutoa hewa ya Carbondioxide kwa kiwango kikubwa, Na mtu hutakiwa kuvuta hewa safi ya Oxygen,


Hivo basi, Endapo utalala na jiko la mkaa ndani ya chumba halafu umefunga milango pamoja na madirisha yote, itasababisha jiko lizalishe kiwango kikubwa cha Carbondioxide na kujikusanya ndani ya chumba,


Hali ambayo husababisha mtu kukosa kabsa hewa safi ya Oxygen, matokeo yake ni mtu kukosa pumzi, kushindwa kupumua na kufariki.


Epuka Tabia ya kulala na Jiko la mkaa ndani kwani ni hatari sana kwa Afya yako.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

FAHAMU MAMBO 8 KUHUSU UKE WA MWANAMKEAfyaclass Bongo Social •

AFYA TIPS
• • • • •
FAHAMU MAMBO 8 KUHUSU UKE WA MWANAMKE


1. Unajisafisha wenyewe kwa ndani


2.Una idadi kubwa ya Bacteria wazuri au wema


3. Huweza kutoa uchafu na harufu mbaya pale tu umeshambuliwa na vimelea vya magonjwa kama fangasi,n.k


4. Unahitaji hewa pia


5. Huweza kukupa taarifa pindi ukiwa kwenye siku za hatari kama unajua kujichunguza vizuri


6. Hushambuliwa na magonjwa kwa Urahisi zaidi


7. Ni kawaida kuwa na hali ya unyevu unyevu


8. Ndyo sehemu pekee ambayo mtoto hupita wakati wa kuzaliwa


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

SWALI; JE KUNA MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA?Afyaclass Bongo Social •

 KLINIKI

• • • • •

SWALI; JE KUNA MAHUDHURIO YA KLINIKI KWA MAMA BAADA YA KUJIFUNGUA?


Wanawake wengi hawajui kwamba, mama baada ya kujifungua kuna kliniki yake kabsa,


Wengi wao wanajua kuna Kliniki ya mtoto tu basi,hivo hata hawazingatii


Kuna mahudhurio ya Kliniki kwa mama baada ya Kujifungua mbali na mahudhurio ya Kliniki kwa mtoto,


Mahudhurio ya Kliniki kwa mama baada ya kujifungua huwa hivi;


- Hudhurio la kwanza ni mama akishamaliza siku 7


- Hudhurio la pili ni siku 28


- Na hudhurio la tatu ni baada ya siku 42.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comment

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUSAGA MENOAfyaclass Bongo Social •

 MTOTO

• • • • •

CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUSAGA MENO


Tatizo la mtoto kusaga au kusigina meno ni tatizo ambalo huwapata baadhi ya watoto, na Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 20% ya watoto kati ya mwaka Mmoja na miaka Kumi na moja hupatwa na tatizo hili la kusigina meno.


CHANZO CHA TATIZO LA MTOTO KUSAGA MENO


Zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii kama vile;


- Mihemko ya usiku pamoja na tatizo la mtoto kukosa usingizi


- Mtoto ambaye anapata shida wakati wa kupumua hali ambayo husababisha mtoto apumue kwa mdomo


- Mtoto kuwa na tatizo la kuvimba kwenye tezi


- Mtoto kupatwa na tatizo la kufunga njia ya hewa wakati akiwa amelala


- Mtoto kuwa na meno ambayo yameota kwa mpangilio mbaya


- Mtoto kuwa na matatizo ya akili,mtindio wa ubongo n.k


- Mtoto kuwa na shida kwenye ungamo la taya na fuvu la kichwa


- Pia hali ya mama kuwa na msongo mkubwa wa mawazo wakati wa ujauzito huweza kupelekea kumzaa mtoto mwenye shida hii


- Hali ya mtoto kuwa na wasiwasi  sana na hofu kubwa kila mara

n.k


MATIBABU YA TATIZO HILI


Tatizo hili la mtoto kusaga meno hupona lenyewe bila matibabu, lakini endapo hali imekuwa mbaya zaidi kutana na wataalam wa Afya hasa wanaohusiana na magonjwa ya watoto pamoja na meno.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

TATIZO LA KUWASHWA KWENYE NGOZI WAKATI WA USIKUAfyaclass Bongo Social •

 NGOZI

• • • • • •

TATIZO LA KUWASHWA KWENYE NGOZI WAKATI WA USIKU


Kuna baadhi ya watu husumbuliwa na tatizo la kuwashwa kwenye ngozi mwili mzima hasa wakati wa usku,


Baadhi yao huwashwa wakiwa wamelala, na wengine huanza kuwashwa baada ya kuamka tu


Je hali hii hutokana na nini?


Kwa asilimia kubwa chanzo cha tatizo hili ni Allergy, mwili wa mtu una mfumo wa kinga mwili ambao hupambana na kitu chochote anbacho utaona ni kigeni kinachoingia mwilini


Kuna watu hupata allergy ya vitu mbali mbali kama vile; vyakula,nyama,maji n.k


Endapo unatatizo hili kutana na wataalam wa afya ili upate msaada wa kimatibabu zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

KUTEMA MATE CHINI SIO DAWA YA HARUFU MBAYA MDOMONI(soma)Afyaclass Bongo Social •

 HARUFU MDOMONI

• • • • • •

KUTEMA MATE CHINI SIO DAWA YA HARUFU MBAYA MDOMONI(soma)


Kuna baadhi ya watu wanaamini kwamba eti ukitema mate chini unaondoa tatizo la harufu mbaya mdomoni,


Hivo watu hawa hutema mate kila dakika ili kuondoa tatizo hili la harufu mbaya mdomoni


FAHAMU; Tatizo la harufu mbaya mdomoni huweza kuwa ni ugonjwa kabsa na ugonjwa huu huweza kusababishwa na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama FANGASI.


Watu ambao wana ugonjwa wa fangasi wa mdomoni hutoka harufu mbaya mdomoni


HIVO, acha tabia ya kutema mate chini kama una tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni,nenda hospital katibiwe 


Lakini pia mtu huweza kutoa harufu mbaya mdomoni kutokana na kutofanya usafi wa kinywa, piga mswaki,na safisha kinywa chako vizuri.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MUATHIRIKA WA UKIMWI?Afyaclass Bongo Social •

 UKIMWI

• • • • • 

NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MUATHIRIKA WA UKIMWI?


Wapo baadhi ya watu,wanaume kwa wanawake huingiwa na wasi wasi mkubwa baada ya kugundua kwamba watu ambao wameshiriki nao tendo la Ndoa ni Waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.


Hofu hii huja baada ya kushiriki tendo la ndoa,ndipo baadae Mmoja wa washiriki hawa agundue mwenzake ameathirika.


NINI CHA KUFANYA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MUATHIRIKA WA UKIMWI?


Fanya mambo haya yafuatayo baada ya kugundua kwamba, uliye fanya naye mapenzi ni muathirika wa ukimwi;


- Nenda hospital kafanye vipimo vya awali kwanza


- Hakikisha unarudia kupima tena baada ya Miezi mitatu


Kumbuka; Hata kama umepata maambukizi ya Virusi vya ukimwi leo, vipimo haviwezi kuonyesha kwa muda huu huu


Asilimia 98% ya maambukizi ya virusi vya ukimwi huonekana kwenye kipimo baada ya miezi mitatu.


Hivo ni lazima kuridia tena vipimo,ili kujua kama upo salama au umeambukizwa.


KUMBUKA; Sio kila aliyefanya mapenzi na muathirika wa ukimwi tayari ana ukimwi


- Zingatia kinga wakati wa kufanya mapenzi(Condom)


- epuka kuwa na wapenzi wengi


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

UNYWE DAWA MUDA GANI BAADA YA KUTAPIKA?Afyaclass Bongo Social •

 DAWA

• • • • •

UNYWE DAWA MUDA GANI BAADA YA KUTAPIKA?


Kwa namna moja au nyingine mtu huweza kutapika baada ya kunywa dawa, 


Sasa anajiuliza anywe dawa tena au afanyeje?


Fahamu hili; Kama umetumia dawa halafu ukatapika kabla ya Nusu saa kuisha yaani dakika 30, unaweza kutumia tena dawa hiyo


Lakini endapo umetapika baada ya nusu saa kuisha hutakiwi kunywa dawa tena.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

AFYACLASS INAPATIKANA KWENYE MITANDAO GANI?Afyaclass Bongo Social •

 AFYACLASS

• • • •

AFYACLASS INAPATIKANA KWENYE MITANDAO GANI?


Afyaclass inatoa elimu,ushauri na Tiba kuhusu ;


1. Afya ya Uzazi


2. Magonjwa ya wanawake


3. Magonjwa ya wanaume


4. Magonjwa ya Watoto


5. Matatizo sugu kama presha,kisukari,vidonda vya tumbo n.k


AFYACLASS INAPATIKANA KWENYE MITANDAO GANI?


• Tumapatikana GOOGLE kwa jina la Afyaclass


• Tunapatikana INSTAGRAM kwa jina la Afyaclass


• Tunapatikana FACEBOOK kwa jina la Afyaclass Group


PIA MAWASILIANO YETU NI;


- Namba ya Simu; +255758286584, Tuma meseg,Piga Simu, Au Whasap


- Email yetu ni; afyacheck26@gmail.com




0 Comment

TATIZO LA KUOTA VIPELE PEMBENI YA UUME(chanzo)Afyaclass Bongo Social •

 AFYA KWA WANAUME

• • • • •

TATIZO LA KUOTA VIPELE PEMBENI YA UUME(chanzo)


Baadhi ya wanaume hutokewa na tatizo la kuwa na vipele sehemu zao za siri hasa maeneo ya pembeni na uume.


Je chanzo chake ni nini?


Tatiz hili huweza kuwatokea watu ambao wamepatwa na mashambulizi ya kirusi aina ya HUMAN PAPPILOMA VIRUS au kwa kifupi HPV.


Na mashambulizi haya kwa Kitalaam hujulikana kama Genital warts.


Kirusi cha HPV husambaa kwa njia ya Kujamiiana hivo basi, tatizo hili ni miongoni mwa magonjwa ya zinaaa ambayo huweza kumtokea mtu wa jinsia yoyote (wanawake na wanaume).


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KUSHIRIKIANA TAULO LA KUOGEAAfyaclass Bongo Social •

 TAULO

• • • • •

MADHARA YA KUSHIRIKIANA TAULO LA KUOGEA


Baadhi ya watu bado wana tabia hii ya kushirikiana Taulo la kuogea hasa Kwa wanafunzi ambao wapo boding School.


Tabia hii sio nzuri kiafya kwani unaweza kukaribisha magonjwa wewe mwenyewe.


MADHARA YA KUSHIRIKIANA TAULO LA KUOGEA


- Madhara ambayo huweza kutokana na watu kushirikiana taulo la Kuogea ni pamoja na kupata maambukizi ya;


• Magonjwa ya ngozi endapo ukishirikiana taulo na mtu mwenye tatizo hili


• Lakini pia unajiweka katika hatari ya kupata mashambulizi ya Fangasi wa kwenye ngozi na Fangasi wa Sehemu za siri, 


hasa pale utakapotumia taulo ambalo lina unyevu unyevu baada ya kutumiwa na mwenzako


Kinga ni Bora kuliko Tiba, Epuka tabia hii ya kushirikiana Taulo la kuogea.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

JE MWANAUME KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA NI TATIZO?Afyaclass Bongo Social •

 AFYA YA UZAZI

• • • • •

JE MWANAUME KUFANYA MAPENZI MARA KWA MARA NI TATIZO?


Moja ya changamoto kubwa kwa hivi sasa ni swala la kutafta watoto, watu wengi baada ya kuoana au hata kabla ya kuoana ila wana nia ya kuwa na mtoto imekuwa vigumu sana kuwapata.


Lakini pia watu huuliza je kufanya mapenzi mara kwa mara kuna madhara?


Utakutana na makala nyingi zikielezea faida za mtu kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara, ila katika makala hii nazungumzia wale ambao wana shida ya kutafta watoto.


Tafiti zinaonyesha kwamba, mwanaume kufanya mapenzi mara kwa mara hupunguza uwezo,ubora na hata wingi wa mbegu za kiume,


Hivo unashauriwa kushiriki tendo la ndoa na mwenzi wako siku za hatari tu,ili kukusaidia kuwa na mda wa kutosha wa mbegu za kiume kutengezwa zikiwa za kutosha,zikiwa na nguvu pamoja na ubora mkubwa.


Tabia hii huongeza uwezekano wa mbegu za kiume kulirutubisha yai la mwanamke na kupata mimba


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA KULALA NA WANYAMA KAMA MBWA NA PAKAAfyaclass Bongo Social •

 WANYAMA

• • • • 

MADHARA YA KULALA NA WANYAMA KAMA MBWA NA PAKA


Kuna wanyama mbali mbali ambao tunaishi nao maeneo ya nyumbani kama vile paka,Mbwa n.k


Wanayama hawa tunaweza kuwapenda mpaka kuwa na tabia ya kulala nao usiku,


Je kuna madhara yoyote kwa kufanya hivo? Soma hapa.!


- Wanyama hawa huweza kuwa ni chanzo cha kutuletea magonjwa mbali mbali bila hata sisi kujua.


Wanyama hawa huweza kubeba wadudu mbali mbali kama vile; chawa,kunguni,viroboto n.k


ANGALIZO;


✓ Usilale na mnyama kama paka au mbwa ambaye ana shida ya kuharisha


✓ Usilale na Mnyama ambaye hachanjwi


✓ Usilale na mnyama ambae ana vidonda mbali mbali au michubuko


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA MWANAUME KUMWAGA NJE WAKATI WA KUFANYA MAPENZI(withdrawal method)Afyaclass Bongo Social •

 UZAZI

• • • • •

MADHARA YA MWANAUME KUMWAGA NJE WAKATI WA KUFANYA MAPENZI(withdrawal method)


Je Njia hii ya mwanaume kumwaga Nje wakati wa kufanya mapenzi ili asimpe mwanamke mimba ni salama?


Njia hii kwa kitaalam hujulikana kama Withdrawal method, na huweza kuwa miongoni mwa njia za uzazi wa mpango ambazo mtu huweza kutumia.


Njia hii haina madhara yoyote kiafya, Japokuwa kuna hasara za kutumia njia hii ili mwanamke asipate mimba


HASARA HIZO NI PAMOJA NA;


- Njia hii haiwezi kuzuia mimba kwa Asilimia 100%, Huhitaji umakini wa hali ya juu na ni ngumu pia kutumia


- Njia hii haiwezi kukukinga na magonjwa mbali mbali ya zinaa kama vile; Kisonono,kaswende,Chlamydia,  au Ukimwi


- Njia hii huweza kuathiriwa na vitu kama kujisahau,kunogewa, hasira,msongo wa mawazo n.k


- Mtumiaji huwa katika hatari ya kusababisha mimba ambazo hazijatarajiwa muda wowote


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

TATIZO LA MWANAMKE KUPATA HEDHI MFULULIZO BILA KUKATAAfyaclass Bongo Social •

 HEDHI

• • • • •

TATIZO LA MWANAMKE KUPATA HEDHI MFULULIZO BILA KUKATA


Mwanamke huweza kupata hedhi mfululizo bila kukata,tatizo ambalo huwapata wanawake wengi kwa hivi sasa,


Mwanamke ambaye anapata hedhi mfululizo kwa zaidi ya wiki moja Au Siku saba, sio dalili nzuri ni ishara kwamba kuna kitu hakipo sawa.


BAADHI YA SABABU ZA TATIZO HILI LA MWANAMKE KUPATA HEDHI MFULULIZO BILA KUKATA NI PAMOJA NA;


-  Tatizo la mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani kwa kitaalam hormone imbalance ambalo huchangiwa na vitu mbali mbali kama vile;


matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama vile; sindano, vipandikizi n.k


Tatizo hili la mvurugiko wa vichocheo mwilini ndyo sababu kubwa kwa wanawake wengi wenye shida ya kuvuja damu mfululizo bila kukata


- Sababu nyingine ni Mwanamke kupatwa na Tatizo la damu kushindwa kuganda, hali ambalo humpelekea mwanamke aendelee kuvuja damu mfululizo baada ya kuanza period.


Matatizo yote haya yanatibika kabsa na mwanamke kurudi katika hali yake ya kawaida.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

TATIZO LA MWANAMKE KUCHUBUKA UKENI WAKATI WA TENDO LA NDOAAfyaclass Bongo Social •

 MWANAMKE

• • • • •

TATIZO LA MWANAMKE KUCHUBUKA UKENI WAKATI WA TENDO LA NDOA


Tatizo la mwanamke kuchubuka ukeni wakati wa kufanya mapenzi huweza kuchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;


- Mabadiliko ya vichocheo mwilini yaani hormone imbalance hali ambayo inapelekea ukavu ukeni kutokana na kuathiriwa kwa tezi linalozalisha unyevu unyevu,ute ute na kuleta hali ya utelezi ukeni,


Tezi hili hufanya kazi chini ya udhibiti wa vichocheo vya mwili yaani Hormones.


Katika hali ya kawaida mazingira ya ukeni hutakiwa kuwa na unyevu unyevu sio kukauka.


- Sababu nyingine ni maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile UTI,FANGASI UKENI, au Maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani PID


- Kufanya mapenzi ukiwa huna hisia ya kufanya mapenzi na bila kufanyiwa maandalizi ya kutosha kabla ya kufanya mapenzi


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI NDANI YA MWEZI MMOJA SIO KAWAIDAAfyaclass Bongo Social •

 HEDHI

• • • • •

MWANAMKE KUPATA HEDHI MARA MBILI NDANI YA MWEZI MMOJA SIO KAWAIDA



Hali ya mwanamke kupata hedhi mara mbili ndani ya mwezi mmoja huweza kuwa kiashiria cha tatizo flani kwenye mwili wake, na tatizo hilo huweza kuwa;


- Tatizo la Mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani kwa kitaalam tunaita Hormone Imbalance 


- Au Dalili za magonjwa mengine kama UVIMBE kwenye kizazi, uvimbe kwenye Vifuko vya mayai,Saratani N.k


Ukiona tatizo hili kutana na wataalam wa afya kwa Ajili ya vipimo pamoja na Tiba


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA(Spinal cord compression)Afyaclass Bongo Social •

 UTI WA MGONGO

• • • • • • •

TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA

Tatizo hili la pingili za Uti wa Mgongo kubanana huweza kutokea kutokana na mgandamizo mkubwa pamoja na presha kwenye pingili hizi za Uti wa mgongo,

Ndipo tatizo hili hutokea na kwa baadhi ya watu mgandamizo huu hufikia hatua yakusababisha msuguano mkali,

 mpasuko kwenye pingili na hali ya maumivu makali ya Uti wa mgongo.

CHANZO CHA TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA

Tatizo hili huweza kuchangiwa na sababu mbali mbali kama vile;

- Pingili za Uti wa mgongo kujipanga vibaya, tatizo ambalo hutokea kwa watu wenye umri mkubwa mfano miaka 60 nakuendelea

- Kubanana kwa pingili za uti wa mgongo kutokana na mgandamizo mkubwa ndani ya uti wa mgongo unaotokana na sababu mbali mbali kama vile; kubeba vitu vizito sana mgongoni

- Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye pingili za uti wa mgongo kama vile; Bacteria,Virusi na Fangasi

- Kuumia sehemu ya mgongoni kwa kudondoka au ajali yoyote ile

- Kupatwa na tatizo la Kansa ya uti wa mgongo iliyoathiri mpaka kwenye pingili za uti wa mgongo

- Pamoja na magonjwa mengine ya mifupa ya uti wa mgongo

DALILI ZA TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA

✓ Mgonjwa kuanza kupata maumivu makali ambayo huweza kuanzia shingoni,sehemu ya juu ya mgongo na sehemu ya chini ya mgongo

✓ Maumivu makali ya mgongo wakati wa kushiriki tendo la ndoa

✓ Kushindwa kabsa kushiriki tendo la ndoa

✓ Shingo kupatwa na hali ya kukakamaa

✓ Mtu kupatwa na hali ya kuchomwa au kuhisi kuungua moto maeneo mbali mbali kama vile; miguuni na mikononi

✓ Mtu kushindwa kudhibiti utokaji wa mkojo hivo kuweza kupatwa na shida ya kujikojolea

✓ Mtu kupoteza hisia kabsa hasa maeneo ya miguuni

✓ Miguu kuwa dhaifu sana na kushindwa kutembea

✓ Mtu kutembea kwa kuinama

N.k


MATIBABU YA TATIZO LA PINGILI ZA UTI WA MGONGO KUBANANA

- Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake, kama nilovyoeleza hapo juu, hivo basi kama shida ni magonjwa ya mifupa, 

mtu atapata tiba ya mifupa, kama ni maambukizi ya Bacteria atapata dawa za kutibu mashambulizi haya n.k

Hivo kwa ujumla wake, matibabu ya tatizo la pingili za uti wa mgongo kubanana (Spinal cord compression) huweza kuhusisha matumizi ya Dawa mbali mbali, huduma ya Mionzi(Radiation) Upasuaji N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

MADHARA YA SUMUKUVU MWILINIAfyaclass Bongo Social •

 SUMUKUVU

• • • • •

MADHARA YA SUMUKUVU MWILINI


Je Sumukuvu ni nini?


Sumukuvu ni aina ya Kemikali ambayo huzalishwa na Jamii ya Fangasi, Na fangasi hawa hupenda kuwepo kwenye mazao mbali mbali kama vile; Kwenye punje za Mahindi, karanga,kunde,mbegu za mafuta n.k


kemikali hii huweza kuleta athari kubwa kwa Binadamu pamoja na mifugo ambayo itakula mimea yenye Sumukuvu.


RIPOTI ya Wizara ya Afya Mwaka 2016, ilisema kwamba " Kati ya kipindi cha Juni  mpaka Agosti 2016, Watu 68 waliathiriwa na Sumukuvu ambapo vifo 19 viliripotiwa katika mikoa ya DODOMA na MANYARA"


MADHARA YA SUMU KUVU MWILINI NI PAMOJA NA; 


✓ Kusababisha vifo kwa binadamu pamoja na Mifugo


✓ Kuleta athari kubwa kwenye Ini


✓ Kusababisha maumivu makali ya Tumbo


✓ Kusababisha hali ya kutapika


✓ Kusababisha mtu kuharisha damu


✓ Kusababisha tatizo la kuvimba tumbo


✓ Kusababisha tatizo la kuvimba Miguu


✓ Kusababisha joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na Homa


✓ Kusababisha rangi ya ngozi,macho,viganja vya mikono kuwa na rangi ya Manjano


✓ Kusababisha tatizo la Degedege

n.k


KWA USHAURI ZAIDI AU ELIMU TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

USHAURI,ELIMU NA TIBA JUU YA MAGONJWA MBALI MBALIAfyaclass Bongo Social •

 AFYA YAKO

• • • •

USHAURI,ELIMU NA TIBA JUU YA MAGONJWA MBALI MBALI


Kama unasumbuliwa na magonjwa yoyote kati ya haya hapa chini,kwa Ushauri,elimu au Tiba tunaweza kuwasiliana popote Ulipo


1. Ugonjwa wa UTI kwa wanawake na Wanaume


2. Ugonjwa wa Fangasi Kwa wanawake na wanaume


3. Tatizo la uvimbe kwenye kizazi, kuziba mirija ya Uzazi N.k


4. Matatizo yote ya Hedhi; Mfano kukaa kwa muda mrefu bila kuona siku za hedhi, kublid damu nyingi na kwa muda mrefu, hedhi inayobadilika badilika,maumivu makali ya tumbo wakati wa hedhi n.k


5. Tatizo la maambukizi kwenye via vya Uzazi vya mwanamke yaani PID


6. Tatizo la Mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani Hormone Imbalance


7. Magonjwa sugu kama vile, Presha, Kisukari, Vidonda vya tumbo n.k


8. Magonjwa yote ya wanaume kama vile; upungufu wa nguvu za kiume, tatizo la mwanaume kuzalisha kiwango kidogo sana cha mbegu za kiume yaani Low sperm count, tatizo la ngiri, mabusha n.k


9. Magonjwa yote ya watoto, kama vile; Mtoto kuharisha,kutapika, kukosa hamu ya kula, kukonda sana n.k


10. Matatizo ya uzazi na mwanamke kutokupata mimba


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MTOTO KUOTA VIPELE KWENYE NGOZI NA KUJIKUNAAfyaclass Bongo Social •

 AFYA KWA MTOTO

• • • • • •

MTOTO KUOTA VIPELE KWENYE NGOZI NA KUJIKUNA


Tatizo hili la mtoto kuota vipele vingi kwenye ngozi pamoja na kujikuna sana hutokea kwa watoto wengi, huku wengine hadi kufikia hatua ya Ngozi ya mwili kubadilika rangi na kuwa na mabaka mabaka mekundu kila mahali.


Je tatizo hili hutokana na nini? na je nini kifanyike kwa watoto wenye matatizo kama haya? soma hapa..!!


CHANZO CHA TATIZO HILI


- Kuna sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia tatizo hili la mtoto kupata vipele kwenye ngozi pamoja na kujikuna sana, na baadhi ya sababu hizo ni kama vile;


• Kuna vipele ambavyo hutokana na hali ya joto kali


• Kuna vipele ambavyo hutokana na Allergy ya vitu mbali mbali kama vile mafuta ya Kupaka n.k


• Kuna vipele ambavyo hutokana na reaction ya mfumo wa kinga ya mwili kwa mtoto mwenyewe


• Kuna vipele pamoja na miwasho kwenye ngozi kutokana na maambukizi ya Fangasi wa Ngozi


• Pia magonjwa mbali mbali ya ngozi huweza kusababisha tatizo hili


ANGALIZO; Mama au mlezi unaweza kumchunguza mtoto wako na kuwa muangalifu kwa sababu, kuna hali ya mikwaruzo,ngozi ya mtoto kubadilika rangi na kuwa nyekundu kutokana na mtoto mwenyewe kujiparua kila mara.


MATIBABU YA TATIZO HILI


- Tiba sahihi ya tatizo hili huanza na kujua chanzo chake. Hivo mpeleke mtoto hospital ili akutane na wataalam wa afya kwa Watoto,wamchunguze mtoto kisha kuanza matibabu kama ni tatizo ambalo huhitaji matibabu.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

JE UPANDIKIZAJI WA VIJITI HUWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA MAPENZI?Afyaclass Bongo Social •

 UZAZI

• • • •

JE UPANDIKIZAJI WA VIJITI HUWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA MAPENZI?


Hili ni swali ambalo baadhi ya Watu hujiuliza sana, Hapa kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyafahamu vizuri kabla ya kupata majibu ya Swali hili.


Kijiti ni njia ya Uzazi wa mpango ambayo ina uwezo wa kuzuia mimba kwa kipindi cha Miaka mitatu Pamoja na Miaka mitano.


Ndani ya kijiti hiki kuna vichocheo au Hormones, sasa endapo mtumiaji katumia mpaka hali ya vichocheo vyake vya mwili kuvurugika tatizo ambalo hujulikana kama Hormone Imbalance, hapa ndipo matatizo mengi huanza.


Na kumbuka Moja ya Sababu kubwa ya Mwanamke kukosa hisia za kimapenzi pamoja na Hamu ya tendo la Ndoa ni pamoja na hii ya; Mvurugiko wa vichocheo vyake vya mwili yaani Hormone imbalance


Hivo basi kwa maelezo hayo,tunaweza kusema matumizi ya baadhi ya Njia za uzazi wa mpango kama sindano,vijiti n.k huweza kuchangia mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa ingawaje hii haiwezi kuwa sababu ya kutosha kusababisha tatizo hili, Zipo sababu zingine nyingi kama vile;


- Uhusiano mbaya kati ya mwanamke na mwanaume huweza kupelekea mwanamke kukosa kabsa hamu ya mapenzi


- Magonjwa mbali mbali kama vile; ugonjwa wa Saratani ya shingo ya kizazi,shinikizo la Damu, maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani PID n.k


- Mwanamke kuwa na shida ya kupata maumivu makali kila akishiriki tendo la ndoa, hali ambayo humsababishia hofu, kutokufurahia mapenzi na hata kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa.


- Matatizo ya Kisaikolojia au Mwanamke kuathirika kisaikolojia


- Mwanamke kuwa na tatizo la msongo wa mawazo


- Mwanamke kupata majeraha yoyote yale sehemu za siri yanayotokana na sababu mbali mbali kama vile kubakwa n.k


- Matumizi ya baadhi ya Dawa

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





0 Comment

DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO(tatizo la mtoto kukosa choo)Afyaclass Bongo Social •

 AFYA KWA MTOTO

• • • • • •

DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO(tatizo la mtoto kukosa choo)


Baada ya  mtoto kuzaliwa huanza kunyonya maziwa ya mama yake, na baada ya muda huanza kujisaidia haja ndogo na haja kubwa pia. Lakini kukaa kwa muda mrefu bila mtoto kupata choo huweza kuleta mashaka hata kwa mama wa mtoto pia.


Swala la mtoto kukosa choo kwa muda mrefu huweza kusababisha mtoto kulia lia mara kwa mara, Mtoto kupata maumivu ya tumbo,tumbo kujaa n.k


Wengine tatizo la kukosa choo kabsa, huanza na haja kubwa kuwa ngumu sana wakati wa kujisaidia, Kujisaidia kinyesi kama cha mbuzi na baadae hali ya kukosa choo kabsa hujitokeza.


Watoto wadogo sana huweza kupatwa na shida hii, Watoto ambao ni kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka mitano pia huweza kusumbuliwa na shida hii.


DAWA GANI ITAMSAIDIA MTOTO KUPATA CHOO(tatizo la mtoto kukosa choo)


- Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kutatua tatizo hili kulingana na Umri wa mtoto, Mfano;

Kwa watoto ambao tayari wanakula vyakula vingine tofauti na maziwa ya mama pekee, hushauriwa ;

• kula matunda ambayo yana nyuzi nyuzi kama maembe,machungwa na matunda yenye kiwango kikubwa cha maji kama matikiti maji,

• Watoto kunywa kiwango kikubwa cha maji kwa siku

• Watoto kuepuka kubana kinyesi kila mara wanapohisi haja kubwa

• Lakini pia kuna njia ya kumassage tumbo la mtoto, hali ambayo itamsaidia mtoto kujisaidia kwa haraka zaidi.


Lakini pia unaweza kuonana na wataalam wa afya hasa wa mambo ya Watoto kwa ajili ya Msaada zaidi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI(hyperhidrosis),chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

 AFYA YA MWILI

• • • • •

TATIZO LA KUVUJA JASHO KUPITA KIASI(hyperhidrosis)


Tatizo hili la mtu kuvuja jasho kupita kiasi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hyperhidrosis, hutokea pale ambapo hakuna vyanzo vyovyote ambavyo huweza kusababisha jasho, Mfano mtu kuchomwa na jua sana, Kufanya mazoezi n.k


Hali hii hutokea mtu akiwa katulia kabsa, kitu ambacho huwa ni kero kubwa kwake pamoja na kwa watu wengine ambao wapo karibu na yeye,


Mtu huyu huweza kuloa sana jasho mwili mzima ikiwa ni pamoja na maeneo mbali mbali kama vile; Usoni, Miguuni, Kwapani na Kwenye Mikono yake.


CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?


• Chanzo cha kwanza cha tatizo hili, ni mfumo wa nerves mwilini kutuma taarifa kupita kiasi kwenda kwa tezi la Jasho yaani Sweat gland, hali ambayo hupelekea tezi hili kufanya kazi kupita kawaida,


Hasa hasa kukiwa hakuna mazingira yoyote ya joto,jua, au kitu chochote ambacho huweza kupasha mwili joto


• Mtu kuwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali,ambayo huweza kuupasha mwili joto kama vile Malaria n.k


• Kuwa na  tatizo la Kisukari


• Kuwa na matatizo kwenye mfumo wa Fahamu au Nerves mwilini


• Mtu kupata shambulio la Moyo yaani Heart attack


• Kuwa na matatizo kwenye tezi la Thyroid


• Kuwa na tatizo la Saratani


• Hali hii pia huweza kutokea kwa wanawake ambayo wamefika ukomo wa hedhi yaani Menopause hot Flashes


DALILI ZA TATIZO HILI LA HYPERHIDROSIS


- Dalili kubwa ni mtu kutoa jasho kupita kawaida pasipo na chanzo chochote cha jasho kama vile jua,mazoezi n.k


- Mtu kutoa jasho kupita kiasi hadi kufikia hatua ya kukosa nguvu na kuishiwa maji ya mwilini


- Nguo kuloa sana wakati mtu akiwa kavaa, kama vile; Shati n.k


- Mtu kuvuja jasho sana wakati wa Usiku akiwa amelala


MATIBABU YA TATIZO HILI


✓ Matibabu ya tatizo hili hutegemea na chanzo chake, ila kwa ujumla kuna aina mbali mbali za dawa ambazo huweza kutumika kama vile; Antidepressants, antiperspirant dawa za magonjwa kama Malaria N.k


Epuka kukaa kwenye mazingira yoyote ambayo huweza kupasha mwili joto kama vile; Kukaa kwenye jua sana, kukaa karibu na Moto n.k


Hivo kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya kupata msaada kama una tatizo hili.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA ULIMIAfyaclass Bongo Social •

 ULIMI

• • • • 

CHANZO CHA MAUMIVU MAKALI YA ULIMI


Kwa namna moja au nyingine mtu huweza kupata maumivu makali kwenye ulimi wake bila kujua sababu hasa ni nini, hali hii huweza kumsababisha ashindwe kula chakula, kukosa furaha n..k


SABABU AMBAZO HUWEZA KUWA CHANZO CHA MAUMIVU YA KWENYE ULIMI


Baadhi ya sababu katika makala hii kwa namna moja au nyingine huweza kuwa chanzo cha maumivu ya Ulimi wako


• Tatizo la maambukizi ya Fangasi, hapa nazungumzia fangasi wa Ulimi. Hali hii huweza kuwa chanzo cha ulimi kuchubuka,kuwa na vidonda pamoja na maumivu makali ya Ulimi.


• Maumivu ya Ulimi huweza kuchangiwa na ajali mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mtu kung'atwa ulimi au kujing'ata mwenyewe,kuchomwa na kitu cha ncha kali n.k


• Mtu kuwa na tatizo la Kansa ya kwenye Ulimi


• Urembo mbali mbali kama vile urembo wa kuvaa vidani kwenye ulimi n.k


• Mtu kushambuliwa na virusi jamii ya Herpes


• Kuwa na shida kwenye mfumo wa fahamu au Nerves


• N.k


Endapo una tatizo hili kutana na wataalam wa afya kwa Ajili ya uchunguzi zaidi na kupata tiba sahihi


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

SABABU ZA MTU KUKONDAAfyaclass Bongo Social •

 KUKONDA

• • • • • •

SABABU ZA MTU KUKONDA


sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa moja au mwingine huweza kukonda bila kujua sababu hasa ni nini.


Katika makala hii tunachambua baadhi ya sababu ambazo huweza kusababisha mtu kukonda sana.


SABABU ZA MTU KUKONDA NI PAMOJA NA;


✓ Mtu kufanyiwa operation ya kukata utumbo, Operation hii husababisha mtu kula chakula kidogo sana na kuhisi kushiba kwa haraka au kutokula kabsa hali ambayo hupelekea matatizo mbali mbali mwilini kama Utapiamlo,uzito kupungua sana na mtu kukonda sana.


✓ Mashambulizi ya magonjwa mbali mbali kama vile ugonjwa Wa Kisukari n.k


✓ Kupata lishe duni sana, Moja ya sababu kubwa ya mtu kukonda ni kula vyakula ambavyo havina kabsa virutubisho vya kujenga mwili kama proteins za kutosha n.k


✓ Mtu Kuwa na tatizo la kutapika kupita kiasi kila anapokula chakula, hali hii huweza kumsababisha mtu kukonda kupita kiasi ndani ya muda mfupi tu


✓ Mtu kupata tatizo la kuharisha mfululilo kwa muda mrefu


✓ Kuwa na Tatizo la minyoo iliyokithiri


✓ Mtu mwenye tatizo la upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI


✓ Mtu kukosa muda wa kulala kabsa na kupumzika kutokana na kazi nyingi anazofanya,mara nyingi afya yake hudhorota sana


✓ Kuwa na Tatizo la Msongo wa mawazo ambao hauishi


✓ Kuwa na hofu na wasiwasi wa maisha, mbali na kwamba hofu huweza kushusha kinga yako ya mwili, hata kukonda pia unaweza kukonda.


✓ Kukaa na Njaa kwa muda mrefu, Huku wengine wakiacha kula baadhi ya milo kwa siku.


✓ Matumizi ya baadhi ya Dawa

n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

NINI KINASABABISHA MATITI YA MWANAMKE KUANGUKAAfyaclass Bongo Social •

 MATITI

• • • • •

NINI KINASABABISHA MATITI YA MWANAMKE KUANGUKA


Kwa hivi sasa, kuna wakina dada wengi hawataki matiti yao kushuka kabsa au kulegea na hata wengine hadi kufikia hatua ya kutumia dawa na kufanya mazoezi maalumu  ili matiti yawe vizuri.


Je Nini kinasababisha matiti ya mwanamke kuanguka?


Soma baadhi ya sababu mbali mbali hizi hapa chini;


• Mabadiliko ya vichocheo mwilini kama vile Estrogen


• Kupenda kutokuvaa sidiria kwa muda mrefu, hivo matiti kukaa bila balance mara nyingi zaidi hali ambayo huweza kupelekea kulegea na kuanguka


• Hali ya mtu kuzeeka hupelekea misuli pamoja na ngozi ya titi kuchoka pia


• Mtu kuwa na uhaba mkubwa wa Collagen


• Mtu kuwa na matiti makubwa zaidi


• Hali ya unene kupita kiasi


• Mwanamke kufikia ukomo wa hedhi yaani Menopause


• Mwanamke kukonda kwa gafla sana


• Mwanamke kuvutwa sana matiti mda mrefu kwa sababu mbali mbali kama vile; Unyonyeshaji n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.






0 Comment

CHANJO YA KICHAA CHA MBWA HUTOLEWA MDA GANI?(Rabies vaccine)Afyaclass Bongo Social •

 KICHAA CHA MBWA

• • • • •

CHANJO YA KICHAA CHA MBWA HUTOLEWA MDA GANI?(Rabies vaccine)


Bila shaka umewahi kusikia kwamba,Mbwa mwenye kichaa akikung'ata ni hatari sana hivo lazima upate tiba ya haraka.


Je chanzo hii ya kuzuia kichaa cha Mbwa hutakiwa kutolewa muda gani?


UTANGULIZI; Ukisikia mbwa ana Kichaa maana yake ni kwamba, Mba huyo amebeba Virusi vya Kichaa ambavyo kwa kitaalam Hujulikana kama RABIES VIRUS,


Hivo basi endapo mbwa huyu akikung'ata, Moja kwa moja anahamisha virusi hawa na kuwapeleka kwenye mwili wako, hapo ndyo madhara huanza kutokea.


CHANJO YA KICHAA CHA MBWA HUTOLEWA MDA GANI?(Rabies vaccine)


Chanzo ya kuzuia virusi hawa Maarufu kama Rabies huweza kutolewa kabla ya mtu kung'atwa na Mbwa au kutolewa mda mfupi tu baada ya kung'atwa na Mbwa huyu mwenye Kichaa.


DALILI ZA MTU AMBAYE TAYARI VIRUSI HAWA WA RABIES WAMEANZA KUMLETEA MADHARA MWILINI


✓ Kuanza kupa maumivu makali ya kichwa


✓ Mwili kukosa nguvu kabsa


✓ Kujawa na hofu na wasi wasi mkubwa


✓ Mtu kupatwa na hali ya kuyaogopa maji yaani Hydrophobia


✓ Joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na homa


✓ Mtu kupooza au paralysis

n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD