Madhara ya p2,haya ni madhara ya matumizi ya Vidonge vya P2Afyaclass Bongo Social •

Madhara ya p2,haya ni madhara ya matumizi ya Vidonge vya P2


Madhara baada ya kutumia p2,Fahamu hapa

Fahamu P2 ni dawa ya dharura yaani kwa kitaalam hujulikana kama emergency contraceptive pill, dawa hii inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya mapenzi pasipo kupanga na upo siku za hatari,au umelazimishwa kufanya mapenzi au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazima Kunywa hizi dawa.

Ukweli ni kwamba dose ya hormones ndani ya p2 ni kubwa kuliko vidonge vya kawaida vya Uzazi(birth control pills) kitu ambacho kinaifanya isifae kwa Matumizi ya kila siku,

Hii husababisha madhara Zaidi kwa Mtu mwenye mazoea ya kuzitumia mara kwa mara. Na moja ya madhara ni mzunguko wako wa hedhi kuathiriwa sana – Periods yako inaweza isitoke kama kawaida, inaweza kuwa nyingi,zito sana,isiyoeleweka(Irregular bleeding) n.k.

Pia baadhi ya Wanawake huongezeka uzito, Hivo basi P2 haishauriwi kabsa kwa matumizi ya kila siku au kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Madhara baada ya kutumia p2,

Haya ni baadhi ya Madhara au matokeo baada ya kutumia p2(emergency contraceptive pills):

  • Kupata kichefuchefu
  • Kutapika
  • Mwili kuchoka Sana
  • Kupata kizunguzungu
  • Kupata maumivu ya kichwa
  • Kupata maunivu ya tumbo
  • Maziwa kuuma au kuvuta zaidi
  • Kubadilika kwa hedhi yako ya kawaida,ikiwemo kuvuja damu nyingi au kwa muda mrefu,au kuvuja katikati ya mzunguko n.k

Kutokwa na Vitone vya damu mara kwa mara(spotting) – Unaweza kupata vitone vya damu ndani ya wiki ijayo baada ya kumeza kidonge cha dharura cha kuzuia mimba yaani P2,

Pia, hedhi yako inayofuata inaweza kuwa nyepesi au nzito, ikawahi kutoka mapema au kuchelewa kuliko kawaida. Hakikisha unapata Msaada wa Tiba ikiwa unakutana na changamoto hizi.

Mzunguko wa hedhi usio wa kawaida(Irregular menstrual cycle) – Kwa sababu ya tembe za dharura za kuzuia mimba(p2), kipindi chako cha hedhi kinaweza kufika mapema au kuchelewa, jambo ambalo hutokea sana kwa wanawake wanaotumia vidonge hivi. Hata hivyo, unapaswa kufanya kipimo cha ujauzito ikiwa hupati kipindi chako cha hedhi ndani ya wiki mbili za tarehe inayotarajiwa.

MADHARA YA KUTUMIA P2

P2 Ni Dawa iliyotengenezwa kutumiwa mara chache tu,inapokulazimu.Sio dawa unayotakiwa kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu. Kuna wanawake humeza p2 kila mwezi,hii haitakiwi. Katika mazingira ya kawaida,haipaswi kumezwa zaidi ya mara 3 kwa mwaka. Kuendekeza kila mwezi kunywa hizi p2 sio sahihi,Unatakiwa ende hospitali ili upate njia sahihi ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

Baadhi ya Side effects/madhara ni ya matumizi holela ya dawa hizi ni

1.Unaweza kujisikia kichefuchefu au kutapika baada ya kumeza,

2.Maumivu ya tumbo

3.Matiti kuuma na kujaa

4.Pia hedhi zako zinazofuata zinaweza zikawahi au zikachelewa au zikatoka nyingi sana( ukiona zimezidi siku 8 fika muone daktari) au ukawa unapata hedhi nyepesi sana,au pia haupati hedhi kabisa (amenorhoea)

5.Kichwa kuuma na kizunguzungu

6.Mabadiliko ya Ute ukeni (change in cervical secretion,hapa unakuta Ute wa ovulation mtu hapati).

7.Kupata maambukizi ukeni,vaginal infections

8.Hatari ya kupata PID

9.Maumivu wakati wa sex(dyspareunia)

10.Mama anakuwa hatarini kutungisha mimba nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.

11.Lakini pia kuna wanawake hupata Ovarian cyst,vivimbe kwenye mfuko wa mayai.

Kuna sababu hapo juu kama PID,kutopata UTE,infections kwenye uke hizi zinakuja athiri mwanamke anakuwa anapata taabu kwenye Kupata mimba

Kama hujapanga kupata mimba,tafadhari fuata njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu inayokufaa,achana na kumeza p2 kila mwezi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Hali ya Wastara ya Kiafya yazidi kuwa mbaya,tumbo limevimba zaidiAfyaclass Bongo Social •

Hali ya Wastara ya Kiafya yazidi kuwa mbaya,tumbo limevimba zaidi



Msanii maarufu wa filamu nchini Tanzania, Wastara Juma, ameibuka kwa mara nyingine akisimulia kwa uchungu mkasa unaoendelea kuutikisa moyo wa mashabiki wake – akidai kuwekwa sumu kwenye soda na mtu anayemhisi ni rafiki wa mdogo wake.

Akiwa kitandani, akiwa na uso wa uchungu na machozi yakimtiririka, Wastara amesema hali yake ya kiafya inazidi kuwa mbaya huku tumbo lake likiwa limevimba vibaya kiasi kwamba linahisi “linataka kupasuka.”

Katika mahojiano yaliyofanyika nyumbani kwake na kusambaa mitandaoni kupitia chaneli ya Bint Kigoma, Wastara alieleza kuwa mashaka yake makubwa ni kuwa sumu hiyo iliwekwa kimakusudi kwenye soda aliyokunywa, na kwamba mtu aliyefanya hivyo alilenga kumdhuru au hata kumuua.

“Sikutegemea, mtu ambaye nilimwamini kama familia, rafiki wa mdogo wangu, ndiye anayehusishwa na tukio hili. Mange Kimambi anasema watu wanataka nife – mimi sijui kwa nini wanichukie kiasi hiki,” alisema kwa uchungu.

Kwa mujibu wa Wastara, baada ya tukio hilo alianza kuhisi maumivu makali tumboni, hali iliyoambatana na kuvimba kwa tumbo, maumivu ya viungo, na hatimaye kushindwa kabisa kusimama au kufanya kazi zake kama kawaida.

Amewataka Watanzania kumuombea lakini pia kuungana naye katika kutafuta haki kwa kuwa sasa anahitaji msaada mkubwa wa kifedha na matibabu ili kunusuru maisha yake.

“Nimekuwa nikipitia mateso makubwa, nimevumilia kwa muda mrefu lakini sasa naomba msaada. Naomba Serikali, taasisi za haki za binadamu na mashirika ya kupambana na ukatili wanishike mkono. Ninateseka kwa sababu ya wivu wa watu,” alisema kwa sauti ya masikitiko.

Kauli hiyo imeamsha hisia kali mitandaoni ambapo mashabiki, wasanii wenzake, na Watanzania kwa ujumla wameonesha mshikamano mkubwa kwa kumtakia nafuu na kutaka uchunguzi wa kina kufanyika kuhusu madai hayo.

Wapo pia waliotaka jina la mtuhumiwa litajwe hadharani ili sheria ichukue mkondo wake, huku wengine wakitaka vyombo vya usalama kuchunguza tukio hilo ambalo limeonekana kuibua taharuki kubwa katika tasnia ya burudani.

Wastara ameendelea kuwa mmoja wa wasanii waliopitia changamoto nyingi za kiafya na bado kuendelea kuwa na matumaini. Lakini safari hii hali inaonekana kuwa mbaya zaidi, na ujumbe wake kwa taifa ni mmoja tu: “Sitaki huruma, nataka haki.”

0 Comment

Mtazamo hasi dhidi ya Waaguzi kutoka kwa Jamii wawavunja MoyoAfyaclass Bongo Social •

Mtazamo hasi dhidi ya Waaguzi kutoka kwa Jamii wawavunja Moyo



Mwenyekiti wa Chama cha Wauguzi Tanzania Tawi la Muhimbili , Ramadhan Mwita akizungumza na wauguzi

WAUGUZI wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wameeleza kusikitishwa na mtazamo hasi wa jamii dhidi yao, wakisema jamii inawadhalilisha na kushindwa kutambua mchango wao mkubwa katika utoaji wa huduma za afya.

Licha ya jukumu lao kubwa la kuokoa maisha ya wananchi, wamesema  jamii inapaswa kutambua kuwawana fanya kwa upendo, huruma na weledi, badala ya kuendelea kuwahukumu kwa mitazamo hasi. Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyoadhimishwa Mei 30, 2025, Mwenyekiti wa Chama cha Wakunga (TANNA) Tawi la Muhimbili, Ramadhan Mwita, amesema wauguzi wamekuwa mstari wa mbele katika kumhudumia mgonjwa kuanzia anapowasili hospitalini hadi kuruhusiwa.

 “Jamii inapaswa kutambua kuwa sisi ni binadamu kama wao, tumeapa kuwatumikia kwa moyo, lakini bado tunadhalilishwa na kukatishwa tamaa,” amesema Mwita. Mwita amesisitiza kuwa licha ya changamoto hizo, uongozi wa hospitali yao inaendelea kuboresha mazingira yao ya kazi ikiwemo maslahi ambayo wanayapata kwa wakati.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Dk. Faraja Chiwanga ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba, akimwakilisha Prof. Mohammed Janabi, amesema serikali itaendelea kushughulikia changamoto zinazowakabili wauguzi sambamba na kuboresha maslahi yao. Amesisitiza kuwa maadhimisho hayo ni fursa ya kuwakumbusha wauguzi wajibu wao kwa kuzingatia  viapo vya taaluma yao.

Kaulimbiu ya mwaka huu  ni “Wauguzi Nguvu ya Mabadiliko Duniani”, mnaweka  matumaini na uzima kwa wagonjwa, endeleeni  kuwa nguzo ya matumani na kujitolea kwa kuzingatia utu na ubinadamu,” alisema Dk Chiwanga.

Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga hospitalini hapo,   Redemptha Matindi  amesisitiza umuhimu wa huduma za kuvutia zinazomjali mgonjwa kama njia moja wapo ya kuleta mageuzi  katika sekta ya afya.

Amesema wauguzi  wanayo nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko Chanya kwa kuonyesha upendo, huruma  na uadilifu katika kazi zao kila siku, maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo Mei 12.

0 Comment

Marufuku yatolewa kwa bidhaa za tumbaku na nikotiki zilizotiwa Ladha:WHOAfyaclass Bongo Social •

Marufuku yatolewa kwa bidhaa za tumbaku na nikotiki zilizotiwa Ladha:WHO



Nchi nyingi zimeona viwango vya kutisha vya matumizi ya sigara za kielektroniki miongoni mwa vijana.

Leo ni siku ya kimataifa ya kupiga marufuku matumizi ya tumbaku na bidhaa zake ambapo shirika la Afya duniani(WHO) limetoa wito kwa serikali zote duniani kupiga marufuku ladha zote katika bidhaa za tumbaku na nikotini ikiwemo sigara, shisha, na sigara za kielektroniki ili kuwalinda vijana dhidi ya uraibu na magonjwa hatari.

Kupitia chapisho jipya lililotolewa leo Geneva, Uswisi, WHO inasema ladha kama vile mentha, ubani na sukari pamba, huficha ukali wa bidhaa za tumbaku na kuzifanya zivutie vijana.” Ladha hizi si tu kwamba hufanya kuwa vigumu kuacha matumizi, bali pia zimehusishwa na magonjwa makubwa ya mapafu,” imesema WHO.

Nafasi ya ladha katika kuongeza mvutowa tumbaku na bidhaa zinazohusiana nazo.

Ladha katika tumbaku, nikotini na bidhaa zinazohusiana nazo huongeza mvuto hasa kwa watoto na vijana, na kuchangia kujaribu matumizi, kuanza kutumia na kuendelea kutumia kwa muda mrefu. Ladha zinageuzwa kuwa  mitego inayowavutia vijana.

Sigara, ambazo bado huwaua hadi nusu ya watumiaji wake, pia huuzwa zikiwa na ladha au huongezewa ladha

Ladha hizi zipo katika aina zote za bidhaa hizo na hutangazwa kwa nguvu, hasa kwa vijana. Pia, ladha hufanya kuwa vigumu kwa watumiaji kuacha.

Zaidi ya hayo, hakuna ushahidi kuwa ladha hizi ni salama kuvutwa, na zinaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja na yasiyo ya moja kwa moja kiafya.

“Ladha hizi zinaendeleza wimbi jipya la uraibu na zinapaswa kupigwa marufuku,”amesema Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Kuelewa vipengele vya muundo wa bidhaa za tumbaku pamoja na athari zake zinazowezekana

Bidhaa za tumbaku, nikotini na zinazohusiana nazo hutengenezwa kwa makusudi ili kuwavutia watumiaji wapya hasa watoto na vijana na kuwafanya watumiaji waliopo waendelee kuzitumia.

Bidhaa hizi huundwa kuwa na mvuto wa macho, rahisi kutumia na kuvutia kihisia, huku zikificha madhara yake halisi. Viwanda vya tumbaku na nikotini hutumia vipengele kama vichujio, miundo midogo, rangi angavu na miundo ya kuvutia ili kupotosha mtazamo wa hatari na kuongeza uraibu.

Halikadhalika, baadhi ya bidhaa pia hutengenezwa ili zitumike kwa kificho, hali inayohujumu sera za maeneo yasiyo na moshi.

Zaidi ya nchi 50 zimepiga marufuku tumbaku zenye ladha.

Nchi kama Ubelgiji, Denmark na Lithuania zimeanza kuchukua hatua, na WHO inazitaka nchi nyingine kuiga mfano huo.Ladha ni mojawapo ya sababu kuu zinazowafanya vijana kujaribu kutumia bidhaa za tumbaku na nikotini.

Zikiwa zimeambatana na vifungashio vya kuvutia na matangazo kupitia mitandao ya kijamii, ladha zimeongeza mvuto bidhaa za tumbaku na nikotini.

“Tunaona kizazi kizima kikitekwa na uraibu wa nikotini kupitia bidhaa zenye ladha ya pipi na zile zisizotoa moshi zenye rangi kama upinde wa mvua,” amesema Dkt. Rüdiger Krech, Mkurugenzi wa Uhamasishaji Afya katika WHO.  “Hii si ubunifu ni udanganyifu. Na lazima tukomeshe.”

Kamoeni ya Siku ya kutotumia Tumbaku mwaka 2025  inataka serikali, wanaharakati vijana na mashirika ya kiraia kuzuia harakati za kuimarisha matumizi ya tumbaku ambapo Dkt. Krech anasema “Hatua zenu zinabadilisha sera na kuokoa maisha.”

WHO inasema kwa kuwa vifo vya watu milioni 8 kila mwaka vinahusiana na matumizi ya tumbaku, wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Ladha, na viwanda vinavyozitumia,havina nafasi katika mustakabali wenye afya. 

0 Comment

Dalili za tatizo la mzio,au Allergy hizi hapaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za tatizo la mzio,au Allergy hizi hapa

Mzio (au "allergy" kwa Kiingereza) ni hali ambayo mfumo wa kinga ya mwili hujibu kwa kupita kiasi dhidi ya vitu ambavyo kwa kawaida si hatari kwa watu wengi. Vitu hivyo vinaweza kuwa vumbi, poleni, baadhi ya vyakula, dawa, au sumu za wadudu.

Dalili za mzio (allergy) hutegemea aina ya mzio, lakini kwa ujumla zinaweza kujumuisha:

1. Dalili za mzio wa hewani (airborne allergies)

Hizi ni mzio wa vitu vinavyopumulika kama poleni, vumbi, manyoya ya wanyama, na ukungu:

  • Kukohoa au kikohozi kisichoisha
  • Pua kuziba au kutoka makamasi (kama mafua sugu)
  • Kuwashwa puani, kooni au machoni
  • Macho kuwa mekundu, kuvimba au kutoa machozi
  • Kupiga chafya mara kwa mara
  • Kizunguzungu au kichwa kuuma kwa sababu ya msongamano wa pua

2. Dalili za mzio wa vyakula (food allergies)

Mzio wa vyakula kama karanga, mayai, maziwa, samaki, nk. unaweza kuwa hatari zaidi:

  • Kichefuchefu, kutapika au kuharisha
  • Tumbo kuuma au kujaa gesi
  • Midomo, ulimi au koo kuvimba (hii ni hatari sana)
  • Upele au vipele mwilini (rash)
  • Kuvimba uso au macho
  • Kizunguzungu au kupoteza fahamu (anafilaksisi – hali ya dharura ya mzio)

3. Dalili za mzio wa ngozi (skin allergies)

Kama vile mzio wa vipodozi, sabuni, au kemikali nyingine:

  • Upele mkali au ngozi kuvimba
  • Ngozi kuwa nyekundu au kuwasha sana
  • Malengelenge au ngozi kupasuka
  • Ngozi kukauka na kupasuka

4. Dalili za mzio wa dawa (drug allergies)

Kwa baadhi ya watu, dawa kama penicillin, sulfa, au aspirini huweza kusababisha:

  • Upele au vipele mwilini
  • Kuvimba midomo, uso au koo
  • Kupumua kwa shida
  • Anafilaksisi (kupoteza fahamu, kushuka kwa presha ya damu, nk.)

5. Anaphylaxis – hali hatari ya mzio mkubwa

Hii ni hali ya dharura ya mzio inayohitaji matibabu ya haraka:

  • Kupumua kwa shida sana
  • Koo au ulimi kuvimba ghafla
  • Mapigo ya moyo kwenda kasi au kupungua
  • Kushuka kwa presha ya damu (hypotension)
  • Kupoteza fahamu au kuchanganyikiwa

Vitu vya kawaida vinavyosababisha mzio:

  • Poleni kutoka kwenye maua
  • Vumbi la nyumba
  • Manyoya ya wanyama
  • Vyakula kama karanga, maziwa, samaki
  • Dawa kama penicillin
  • Sumu za wadudu kama nyuki au siafu

Unatakiwa kufanya nini ukihisi una mzio?

  • Muone daktari kwa uchunguzi na vipimo (kama vile skin test au blood test)
  • Epuka chanzo cha mzio
  • Tumia dawa za antihistamine au corticosteroids
  • Kwa mzio mkali, daktari anaweza kupendekeza utembee na sindano ya dharura ya epinephrine (Epipen)

Ikiwa una dalili zinazojirudia kama mafua yasiyoisha, kuwashwa mara kwa mara, au vipele vya ajabu — huenda ni mzio. 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Watu 115 wamefariki dunia kwa Mafuriko nchini NigeriaAfyaclass Bongo Social •

Watu 115 wamefariki dunia kwa Mafuriko nchini Nigeria



Watu 115 wamefariki dunia baada ya mafuriko kuukumba mji wa kibiashara wa Mokwa katika jimbo la Niger huko Nigeria.

Mkuu wa ofisi ya operesheni huko Minna, Husseini Isah, amesema watu wengi zaidi bado wako kwenye hatari huku juhudi za uokoaji zikiendelea Ijumaa.

Ripoti za awali zilikuwa zimesema kuwa watu 20 ndio waliofariki ila Isah amedai kuwa idadi inazidi kuongezeka.

Chanzo cha mafuriko hayo ni mvua kubwa iliyonyesha kwa masaa kadhaa na kulingana na ripoti, kuvunjika kwa bwawa moja katika eneo jirani ndiko kulikopelekea hali kuwa mbaya zaidi.

Mji wa Mokwa ni makutano ya wafanyabiashara kutoka kusini mwa Nigeria na wakulima wa kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwaka 2024 kulikuwa na tukio kama hilo ambapo mvua kubwa na kuvunjika kwa bwawa kulisababisha vifo vya angalau watu 30 huko Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

0 Comment

WHO yaitambua Novemba 17 Siku ya Watoto Njiti DunianiAfyaclass Bongo Social •

WHO yaitambua Novemba 17 Siku ya Watoto Njiti Duniani



Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza rasmi kuijumuisha tarehe 17 Novemba katika kalenda yake ya kimataifa kama Siku ya Watoto Njiti Duniani, ikiwa ni hatua muhimu ya kutambua na kuhamasisha jitihada za kulinda maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda kamili wa ujauzito.

Hatua hii ni ushindi mkubwa kwa sekta ya afya ya uzazi duniani, na hasa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania, ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kupigania uboreshaji wa huduma kwa watoto wachanga, hususan wale njiti. WHO imesisitiza kuwa kuwepo kwa siku hiyo kutasaidia kuongeza uelewa, kuimarisha sera za afya na kuvutia uwekezaji zaidi katika huduma za watoto wachanga.

Tanzania yaandika historia kupitia juhudi za Doris Mollel

Tanzania imechukua nafasi ya kipekee katika mafanikio hayo kupitia juhudi za muda mrefu za Doris Mollel, mwanzilishi wa Doris Mollel Foundation (DMF). Doris, ambaye alizaliwa njiti, amegeuza simulizi yake kuwa chachu ya mabadiliko kwa watoto wengine waliopitia changamoto kama alizopitia yeye.

Kwa zaidi ya miaka saba, taasisi yake imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali ya kutoa elimu kwa jamii kuhusu watoto njiti, kuchangisha na kusambaza vifaa tiba kwa hospitali nchini, na kuwajengea uwezo wahudumu wa afya wanaohudumia watoto hao. Zaidi ya hospitali 20 zimepata msaada wa incubator, mashine za oksijeni, vifaa vya kupima joto, na usaidizi wa mafunzo kwa wauguzi kupitia DMF.

Akizungumzia uamuzi huo wa WHO, Doris amesema:

"Kupitishwa kwa Novemba 17 na WHO ni heshima kubwa kwa watoto njiti duniani. Kwa upande wangu binafsi na kwa Tanzania, hii ni zawadi ya juhudi za miaka mingi. Ninaamini sasa dunia itasikia kilio cha watoto hawa na kuchukua hatua madhubuti.

"What a Proud Moment! Ahsante sana Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Rais Dr @samia_suluhu_hassan huu ni ushindi mwingine wa ushawishi kutoka Tanzania.
Nashukuru sana @wizara_afyatz pamoja na @wizara_mambo_ya_nje_tz kwa kufanya kazi nasi kwenye hili muhimu kwa Taifa na Dunia kiujumla. @dorismollelfoundation ilikutana na @drtedros kujadiliana nae juu ya Siku hii muhimu na hili ni moja kati ya matokeo mazuri ya kazi yetu. Huu ni Mfano Mzuri wa namna Serikali yetu inafanya kazi na Mashirika yasio ya kiserikali.

Kipekee nakushukuru sana Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani @who @drtedros kwa uongozi na support kubwa uliyotupa wewe pamoja na ofisi yako, Ubalozi wetu Geneva @ubalozigeneva Mhe Balozi @hoycetemu

Ahsante nchi wanachama wote kwa kuunga mkono na kubariki Siku hii iwepo kwenye Kalenda ya Shirika la Afya Duniani, naamini uwepo wa siku hii na kutambulika kimataifa utazidi kuongeza chachu ya maboresho ya huduma za afya kwa Mama na Mtoto pamoja na vijana. Nina Tarajia tutafanya kazi kubwa ya kuhamasisha mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa ujauzito ili kupunguza watoto Njiti kuzaliwa lakini pia hata wakizaliwa kuendelea kuboresha huduma za watoto wachanga Duniani.

I am proud !

Serikali ya Tanzania yapongezwa kwa ushirikiano na dhamira ya dhati

Mbali na jitihada za DMF, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya imetajwa kuwa miongoni mwa wadau waliounga mkono mchakato wa kuidhinisha siku hiyo. Serikali imekuwa ikitekeleza mikakati mbalimbali ya kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa kuboresha huduma za afya ya uzazi, kujenga vitengo maalum kwa watoto njiti katika hospitali za umma na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya, Tanzania imeongeza idadi ya vitengo vya kuhudumia watoto njiti katika hospitali za mikoa na wilaya, sambamba na kusambaza vifaa tiba vya msingi vinavyohitajika katika huduma hizo.

Msemaji wa Wizara hiyo amesema:

"Tunatambua umuhimu wa kuwalinda watoto wachanga, hususan wale njiti. Ushirikiano wetu na wadau kama Doris Mollel Foundation umesaidia sana kuongeza uelewa, kupunguza unyanyapaa na kuimarisha huduma hizi katika maeneo mengi ya nchi."

Takwimu zasema yote – na changamoto bado zipo

Kwa mujibu wa WHO, kila mwaka zaidi ya watoto milioni 15 huzaliwa njiti duniani, na kati yao, takriban milioni moja hufariki dunia kutokana na matatizo yanayohusiana na kuzaliwa kabla ya wakati. Afrika, ikiwemo Tanzania, inaongoza kwa idadi ya watoto njiti huku ikikumbwa na changamoto ya upungufu wa vifaa tiba, rasilimali watu na elimu ya jamii kuhusu mahitaji ya watoto hao.

Hata hivyo, hatua ya WHO kuutambua rasmi Novemba 17 kama siku maalum inaonekana kama fursa adhimu ya kuongeza ushirikiano wa kimataifa, kushirikisha sekta binafsi, na kuhakikisha kuwa kila mtoto anapewa nafasi ya kuishi na kufikia ndoto zake.

0 Comment

Vyakula Vitano(5) vinavyosaidia mmeng'enyo wako wa chakulaAfyaclass Bongo Social •

Vyakula Vitano(5) vinavyosaidia mmeng'enyo wako wa chakula

Matatizo ya mmeng'enyo wa chakula, kama vile gesi, kuvimbiwa na kuhara, huathiri mamilioni ya watu kote duniani. Ili kukabiliana na tatizo hili ulimwengu hauna budi kuzingatia afya ya mmeng'enyo au usagaji chakula.

Kabla kuangazia ni vyakula gani vinaweza kudhibiti matatizo ya mmeng'enyo wa chakula, kwanza ni vyema kuelewa kwa nini afya ya mmeng'enyo wa chakula ni muhimu?

Afya ya mmeng'enyo wa chakula ni muhimu kwa ustawi wa jumla, inayoathiri kila kitu kutoka kwa viwango vya nishati yetu hadi utendaji wetu wa kinga. Mfumo wa mmeng'enyo au usagaji chakula unasaidia kuvunja chakula tunachokula kuwa virutubishi, ambavyo mwili hutumia kwa nishati, ukuaji na ukarabati wa seli.

Mfumo wa usagaji chakula wenye afya huhakikisha kwamba mwili unafyonza virutubisho hivi kwa ufanisi, huku mfumo usio na afya unaweza kusababisha masuala mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuvimbiwa, kuhara, na hali ikiwa mbaya zaidi unapata ugonjwa wa utumbo mwembamba au ugonjwa wa matumbo kwa ujumla.

Usagaji chakula vizuri huruhusu ufyonzaji wa vitamini, madini, na virutubisho vingine muhimu. Utaratibu huu ni muhimu kwa kudumisha viwango vya nishati, kusaidia kazi ya kinga, na kukuza afya kwa ujumla. Vifuatavyo ni aina ya vyakula muhimu kusaidia mmeng'enyo. Ni vyakula vinavyosaidia sana afya ya utumbo.

1. Vyakula vya nyuzinyuzi

Lishe yenye nyuzinyuzi ni muhimu kwa mfumo wa utumbo wenye afya. Vyakula vya aina hii husaidia usagaji chakula na kuzuia kuvimbiwa.

Mchele mweupe au kahawia? Ngano nzima au mkate mweupe? Wataalamu wa afya wanapendekeza watu wazima kula walau gramu 25 ya nyuzi kwa siku.

Madaktari pia wanasema kwamba ikiwa unataka utumbo wako ufanye kazi vizuri, chagua nafaka nzima, kwani utumbo unahitaji angalau gramu 25 za nyuzi kila siku ili kufanya kazi iivizuri.

Jitahidi kula mikate ya unga au punje badala ya nyeupe. Pia unaweza kula wali wa kahawia au pasta ya ngano ili kuongeza ulaji wako wa nyuzi.

Chanzo kingine cha nyuzinyuzi ni pamoja na viazi ambavyo havijamenywa (kama vile viazi vilivyookwa) na kunde kama maharagwe, pojo au mbaazi, ambazo zinaweza kutumiwa kama kitoweo mbali na mchuzi wa nyama na saladi.

2. Vyakula vilivyochachushwa

Vyakula vilivyochachushwa ni chanzo kikuu cha bakteria yenye manufaa ambayo inakuza microbiome ya utumbo yenye afya. Microbiome iliyosawazishwa ya utumbo husaidia usagaji chakula, huongeza ufyonzaji wa virutubishi, na kuimarisha mfumo wa kinga. Vyakula vilivyochachushwa ni pamoja na:

Sauerkraut na kimchi: Mboga iliyochachushwa ambayo ni matajiri katika probiotics na nyuzinyuzi, kukuza afya ya utumbo na harakati za kawaida za matumbo.

Kefir: Kinywaji cha maziwa kilichochachushwa ambacho kina probiotics nyingi na kinaweza kusaidia kudumisha afya ya mimea ya utumbo.

Kombucha: Chai iliyochacha ambayo ina probiotics na inaweza kusaidia kuboresha usagaji chakula na kupunguza uvimbe kwenye utumbo

3. Matunda na mbogamboga

Matunda na mboga zimejaa vitamini, madini, na nyuzinyuzi ambazo zinasaidia usagaji wa chakula kwa ujumla.

Iwe wewe ni mlaji wa lishe inayotokana na mimea au mboga mboga na matunda muda mrefu au ndio mwanzo unaanza lishe ya aina hii, kupata mlo kamili ni jambo ambalo linaweza kufikiwa kwa kupanga vizuri bila ujuzi mkubwa.

Lishe itokanayo na mimea ina liyopangwa ipasavyo inaweza kuwa na faida kadhaa za kiafya lakini hakikisha inajumuisha virutubishi muhimu kama vile vitamini B12 na D, madini ya kalsiamu ya kujenga mifupa, pamoja na chuma, zinki na asidi ya mafuta ya omega-3.

Mlo wa mboga mboga, unaojumuisha vyakula vilivyoimarishwa, huhusishwa na afya bora kwa sababu zina nyuzinyuzi nyingi za lishe, hujumuisha ugavi mwingi wa vyakula vyenye folate, vitamini C na E na madini, potasiamu na magnesiamu.

Ulaji mwingi wa matunda na mboga mboga, viwango vya chini vya sodiamu (chumvi) na mafuta yaliyojaa, yote haya yanamaanisha kuwa vyakula vya mboga mboga huwa na faida nyingi za kiafya.

4. Vyakula vya Protini

Protini ni muhimu kwa ajili ya kurekebisha na kujenga tishu, ikiwa ni pamoja na zile za njia ya utumbo. Unashauriwa kuzingatia vyanzo vya protini konda ambavyo ni rahisi kwenye mfumo wa usagaji chakula.

Mayai- Ni chanzo muhimu cha protini kwasababu yana amino acids muhimu kwa chakula bora. Pia yana kiwango cha juu cha mafuta ya omega-3 pamoja na vitamini A na E.

Samaki- ina mafuta ya omega-3, ambayo ina mali ya kuzuia uchochezi na inaweza kunufaisha afya ya utumbo

5. Mafuta yenye Afya

Mafuta yenye afya ni muhimu kwa ufyonzaji wa virutubisho na afya ya usagaji chakula kwa ujumla. Vyanzo hivi vya mlo ulio na mafuta asili vinasaidia mwili kunyonya vitamini A, D, E, na K, ambazo ni muhimu kwa kazi mbalimbali za mwili.

Mafuta ya Mzaituni: Haya mafuta yenye afya ambayo yanaweza kusaidia kupunguza uvimbe kwenye njia ya utumbo na kuboresha ufyonzaji wa virutubisho.

Parachichi: Tunda hili lina kiwango kikubwa cha mafuta na nyuzinyuzi zenye afya, huchochea usagaji chakula vizuri na ufyonzaji wa virutubisho.

0 Comment

Afungwa maisha kwa kumuuza Mtoto wake huko Afrika KusiniAfyaclass Bongo Social •

Afungwa maisha kwa kumuuza Mtoto wake huko Afrika Kusini



Mtoto huyo wa kike Joshlin Smith, aliye na miaka 6 aliripotiwa kutoweka mwezi Februari mwaka jana katika eneo la Saldanha Bay, Afrika Kusini. 

Mama yake Racquel "Kelly" Smith, alipatikana na hatia ya kumteka nyara na kumuuza mtoto wake kwa dola 1,100 za kimarekani. Jaji Nathan Erasmus alitoa hukumu kwamba Racquel aliye na miaka 35, na mpenzi wake aliyeshitakiwa nae pamoja na rafiki yao watumikie kifungo cha maisha kwa kufanya biashara haramu ya kuuza watu. 

Jaji aliyetoa hukumu hiyo alisema mama huyo wa watoto watatu hakuonesha dalili yoyote ya kujitia matendo yake. 

Kesi hiyo imegusa hisia za wengi nchini humo, huku picha za mtoto Joshlin zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na ahadi ya zawadi ya randi milioni 1 kwa atakayemrudisha salama. Polisi bado inaendelea na uchunguzi ndani na nje ya Afrika kusini.

0 Comment

Huduma za Dialysis zafika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa ManyaraAfyaclass Bongo Social •

Huduma za Dialysis zafika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara



Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga, amezindua rasmi huduma ya kusafisha damu (Dialysis) pamoja na huduma ya kipimo cha mfumo wa chakula katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, hatua inayolenga kupunguza gharama na usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakilazimika kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Sendiga alisema kuwa mpango huu ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya na kuzisogeza karibu na wananchi.

"Huduma hii ni ya kisasa na muhimu sana kwa wakati huu, hasa ikizingatiwa kuwa magonjwa ya figo yanaongezeka kwa kasi duniani," alisema Sendiga.

Awali, wagonjwa waliokuwa wakihitaji huduma za kusafisha damu walilazimika kwenda Hospitali ya Rufaa ya Haydom au hospitali nyingine zilizoko mbali, jambo lililoongeza gharama na usumbufu mkubwa kwao na familia zao. 

Kwa sasa, huduma hiyo inapatikana mkoani Manyara, na hivyo kuondoa adha ya safari ndefu.

Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, Dkt. Yesige Mutajwaa, hospitali imeshatoa jumla ya rufaa 22 kwa wagonjwa waliokuwa wakihitaji huduma ya Dialysis kuanzia Julai 2024 hadi sasa. 



Amesema baadhi ya wagonjwa walilazimika kuhamia kabisa mikoa yenye huduma hiyo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kugharamia safari mbili hadi tatu kwa wiki.

Mradi huo mkubwa umegharimu kiasi cha Shilingi milioni 522.5, ambazo zilitumika kununua mashine sita za kusafisha damu, mashine ya kupima mfumo wa chakula, na kufanya ukarabati wa jengo litakalotumika kutoa huduma hizo. 

Aidha, kiasi cha Shilingi milioni 29.8 zilitumika kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi wanaotoa huduma hizo maalum.

Dkt. Mutajwaa alisisitiza kuwa vifaa hivyo vya kisasa vitunzwe ipasavyo ili huduma iwe endelevu na wananchi waendelee kupata huduma bora kama ilivyokusudiwa na Serikali. 

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha huduma hizi muhimu kuwafikia wananchi wa Manyara,” aliongeza.

Huduma hii mpya ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Manyara na mikoa jirani, kwani sasa wanaweza kupata matibabu ya uhakika bila usumbufu wa safari ndefu na gharama kubwa.

0 Comment

Ugonjwa wa Bawasiri,Dalili,Chanzo cha TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Bawasiri,Dalili,Chanzo cha Tiba

Ugonjwa wa Bawasiri kwa kitaalam Hemorrhoids ni ugonjwa unaohusisha kuvimba na kutuna kwa mishipa kwenye mfereji wa Njia ya haja kubwa, ambapo Mishipa hii husaidia wakati wa utoaji wa kinyesi.

Kwa Lugha nyingine, Bawasiri huhusisha kuvimba kwa mishipa inayojulikana kama Veins kwenye eneo la haja kubwa yaani anus, pamoja na Sehemu ya ndani ya rectum yaani Lower rectum.

Tumezungumzia kuhusu kutanuka na kuvimba kwa mishipa ya Veins, na tumezungumzia habari ya Rectum.

Veins ni nini?

Veins ni mishipa ya damu iliyo katika mwili wako wote ikiwemo eneo hili la Haja kubwa ambayo hukusanya damu isiyo na oksijeni na kuirudisha kwenye moyo.

Je, Rectum ni nini?

Rectum ni sehemu ya chini ya Utumbo mpana au Utumbo mkubwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Colon au Large intenstine, Sehemu hii ina Karibu Cm15 Sawa na Ichi 6 kwa Urefu. Hapa ndipo Uchafu hupokelewa kutoka kwenye Utumbo mpana kisha kuhifadhiwa mpaka hapo ambapo utatolewa nje ya mwili wako kupitia Sehemu ya haja kubwa au Anus.

AINA ZA BAWASIRI(HEMORRHOIDS)

Kulingana na asili ya Bawasiri au hemorrhoids tunaweza kupata aina kuu Mbili za bawasiri
  1. Bawasiri ya ndani
  2. Na Bawasiri ya nje
Bawasiri au Hemorrhoids ikitokea ndani ya rectum hujulikana kama bawasiri ya ndani au kwa kitaalam Internal hemorrhoids

Lakini endapo bawasiri imetokea chini ya ngozi inayozunguka eneo la haja kubwa au Anus hujulikana kama bawasiri ya Nje au kwa kitaalam external hemorrhoids.

Hivo basi, Tunaweza kujua aina za bawasiri uliyonayo kulingana na eneo ilipotokea pamoja na Dalili ulizonazo kwa wakati husika.

DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI NA BAWASIRI YA NJE

Watu wengi hawajui kwamba bawasiri zipo za aina kuu mbili,kuna bawasiri ya ndani na kuna bawasiri ya nje.

Na dalili pia za bawasiri hutegemea ni bawasiri ya Nje au ya ndani.

Tuanze na dalili za bawasiri ya nje

1.DALILI ZA BAWASIRI YA NJE(External hemorrhoids)

Aina hii ya bawasiri huhusisha eneo la kuzunguka sehemu ya haja kubwa au Anus. Na dalili zake ni pamoja na;

- Kutokea kwa kinyama au uvimbe eneo la haja kubwa ambacho huonekana kabsa kwa nje,

kinyama hiki unaweza kukishika kabsa na kujua sehemu ya haja kubwa ina kitu

- Mtu kuhisi hali ya miwasho kwenye eneo la haja kubwa

- Mtu kupata maumivu hasa wakati wa kujisaidia haja kubwa

- Mtu kuhisi hali ya kutekenywa au kukereka eneo la haja kubwa

- Kuanza kuvuja damu(Bleeding) au kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu n.k

Baada ya kuangalia dalili za bawasiri ya Nje, twende moja kwa moja kutazama Dalili za bawasiri ya Ndani kama aina nyingine ya bawasiri

2.DALILI ZA BAWASIRI YA NDANI(Internal hemorrhoids)

Aina hii ya bawasiri hutokea kwenye eneo la ndani la Rectum,

- Na kwa kawaida huwezi kuona au kufeel chochote kwa nje

- Na ni mara chache huweza kuleta kero au usumbufu wowote kwa nje

- Lakini mtu huanza kuhisi hali ya mkazo usio wa kawaida(straining) au Irritation wakati kinyesi kikipita anapojisaidia, na hii ndyo huweza kusababisha;

• Kujisaidia kinyesi chenye damu au kuvuja damu wakati wa kujisaidia pasipo kupata maumivu ya aina yoyote,

• Unaweza kushangaa kuna vidamu damu ambavyo ni Bright red blood kwenye toilet tissue au ndani ya kinyesi

Je,unasumbuliwa na aina yoyote ya bawasiri kati ya hizi?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Hakikisha Unaongea na Wataalam wa Afya

Ikiwa unatokwa na damu wakati wa kwenda haja kubwa au una bawasiri ambazo haziishi baada ya wiki, licha ya kuzingatia kanuni za utunzaji wake ukiwa nyumbani, zungumza na mtoa huduma wako wa afya.

Sio kila kutokwa na damu kwenye njia ya haja kubwa ni kwa sababu ya bawasiri, haswa ikiwa una mabadiliko katika tabia ya kinyesi chako au ikiwa kinyesi chako kinabadilika rangi au hali yake ya kawaida ya kutoka kila siku. 

Kutokwa na damu kwenye eneo la Haja kubwa kunaweza kutokea kwa sababu ya magonjwa mengine, Ikiwemo saratani ya utumbo mpana na saratani ya Sehemu ya haja kubwa.

Tafuta huduma ya dharura ikiwa unatokwa na damu nyingi kwenye eneo la haja kubwa, au una dalili zingine kama vile; maumivu makali ya kichwa,kichwa kuwa kizito, maumivu makali ya tumbo,kupata hali ya kizunguzungu au kuzirai.n.k

SABABU ZA UGONJWA WA BAWASIRI

Mishipa ya Veins inayozunguka njia ya haja kubwa hutanuka kutokana na shinikizo inayopata na inaweza kujitokeza au kuvimba.  Bawasiri au Hemorrhoids inaweza kuendelea kutokana na kuongezeka kwa shinikizo kwenye eneo la rectum kwa sababu mbali mbali Zikiwemo:

  • Hali ya mkazo wakati wa kujisaidia ambayo hutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo ya kujisaidia choo kigumu sana.
  • Kukaa kwa muda mrefu hasa wakati wa kujisaidia
  • Kuwa na tatizo la kuharisha kwa muda mrefu yaani chronic diarrhea 
  • Kujisaidia choo kigumu sana au kupata tatizo la constipation.
  • Kuwa na Uzito kupita kiasi au Unene(overweight and Obesity)
  • Kuwa Mjamzito, Wajawazito wengi pia hupata shida hii ya bawasiri hasa kutokana na kuongezeka kwa mgandamizo au shinikizo kwenye eneo hili
  • Kufanya Mapenzi kinyume na maumbile(anal sexual intercourse)
  • Kula vyakula vyenye kiwango kidogo cha nyuzinyuzi yaani low-fiber diet.
  • Kunyanyua Vitu vizito mara kwa mara n.k

Wakati mwingine hakuna Sababu ya moja kwa moja ambayo hujulikana kama chanzo cha bawasiri, lakini mara nyingi Wataalam wa afya huzungumzia sababu kuu kadhaa. Sababu hizi ni pamoja na;

 1. Kupata choo kwa shida au Kupata Choo Kigumu

2. Tatizo la kuharisha kwa muda mrefu, 

3. Kukaa kwa muda mrefu hasa wakati wa kujisaidia

4. Bawasiri au Hemorrhoids pia inaweza kuonekana kwa sababu ya michezo ambayo watu hucheza mfano; kunyanyua Vyuma au vitu vizito,

Wakati kitu kizito kinapoinuliwa, shinikizo la ziada linatumika kwenye eneo hilo hivo kuweza kuchangia tatizo hili.

5. Wanawake wako katika hatari ya kuwa na bawasiri wakati wa ujauzito.

Hii pia hutokea kwa sababu ya kuongezeka kwa shinikizo la kutoka kwa mtoto.  Bawasiri ina uwezekano mkubwa wa kuongezeka kwa sababu tishu zinakuwa dhaifu.

Watu ambao wapo kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa bawasiri

- kuwa kwenye Familia yenye Tatizo hili(Genetics)

Unaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata bawasiri ikiwa wanafamilia wengine, kama wazazi wako, walikuwa nayo.

- Wazee

Wazee wanaweza kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata bawasiri kwa sababu tishu katika eneo la Haja kubwa huwa dhaifu kadri unavyozeeka.

- Wajawazito

Mimba huongeza hatari ya kupata bawasiri kwa njia kadhaa.  Uzito wa Mtoto aliye tumboni huweka shinikizo la ziada kwenye puru yako.  Pia una uwezekano mkubwa wa kupata bawasiri kwa Sababu ya kupata tatizo la Kujisaidia Choo Kigumu.

- Wanaokaa kwa Muda mrefu

Mtindo wa maisha wa kukaa tu, au kazi ambayo lazima ukae kwa muda mrefu, pia huongeza hatari ya kupata bawasiri.  Usipozunguka sana au kufanya mazoezi ya mwili,damu inaweza kujikusanya kwenye eneo lako la Haja kubwa na kuweka shinikizo kwenye mishipa ya damu hapo, Hali hii huongeza hatari ya wewe kupata bawasiri.

Madhara ya Ugonjwa wa bawasiri

Bawasiri inaweza kuleta wasiwasi na maumivu, lakini mara nyingi haisababishi matatizo makubwa.  Mara chache, watu walio na Bawasiri hupata madhara haya:

• Upungufu wa damu; Unaweza kupoteza damu nyingi ikiwa una bawasiri ambayo hudumu kwa muda mrefu na inayosababisha kutoka kwa damu nyingi. Hali hii huweza kusababisha upungufu wa damu mwilini

• Kuganda kwa damu; Hali ya kuganda kwa damu(Blood clots) huweza kutokea hasa kwa mtu mwenye bawasiri ya nje.

 • Maambukizi; Baadhi ya bawasiri kama bawasiri ya nje huweza kusababisha vidonda ambavyo huwa rahisi kuambukizwa.

• Tatizo la Skin tags(kitambaa cha tishu zinazoning'inia kwenye ngozi); Tone la damu kwenye bawasiri yenye mvilio linapoyeyuka, linaweza kuacha sehemu ya ngozi, na eneo hili linaweza kuwasha.

 • Bawasiri zilizofungwa(Strangulated hemorrhoids);

Misuli inaweza kuzuia mtiririko wa damu hadi kwenye bawasiri iliyozidi,prolapsed hemorrhoid. Hii inaweza kusababisha maumivu makali na inahitaji upasuaji.

🔺UTAMBUZI WA UGONJWA WA BAWASIRI

 Bawasiri au Hemorrhoids hugunduliwa na daktari au wataalam wa afya,

Daktari wako atakuuliza kuhusu historia ya Ugonjwa wako, matibabu na dalili ulizo nazo.

Vipimo mbali mbali vitafanyika ikiwemo; kufanya

  • Physical examination; Ambapo daktari huweza kukuangalia eneo la Haja kubwa pamoja na rectum, ili kuona kama kuna uvimbe wowote, au tatizo lingine lolote.
  • Kipimo cha Digital rectal exams;

Hapa Daktari wako atavaa gloves, atapaka mafuta, na kuingiza kidole kwenye puru yako ili kuangalia sauti ya misuli na kuhisi hali yoyote ya uvimbe, au matatizo mengine.

 Uchunguzi wa kuona sehemu na Njia ya haja kubwa kwa undani lazima ufanyike.  katika kufanya uchunguzi wa rectal ambao utasaidia kugundua bawasiri ya ndani, uvimbe, polyps, au jipu,

Uchunguzi huu wa kuona kawaida huhitaji kifaa maalum, kinachoitwa Anoscopy kuingizwa kwenye eneo la haja kubwa.  Utaratibu huu hauna maumivu isipokuwa ugonjwa mwingine umewasilishwa.

 🔴 MATIBABU YA UGONJWA WA BAWASIRI

 Matibabu ya bawasiri au hemorrhoids yanaweza kufanyika kuanzia nyumbani au hospitalini.  Kawaida, chaguo bora ni kuzuia kuipata.  Moja ya vitu Muhimu ni pamoja na kuongeza unywaji wa Maji mengi na ulaji wa vyakula au matunda yenye asili ya nyuzi nyuzi. 

👉 Hii inamaanisha kula matunda zaidi, mboga mboga, na nafaka nzima.  Watu wengi hawapati Fiber au nyuzi za kutosha katika lishe yao.  Katika hali kama hiyo, virutubisho vya nyuzi, kama vile psyllium au methylcellulose, vinaweza kuwa na faida.

👉 Pia ni muhimu kuongeza unywaji wa maji ya kutosha na kudumisha unyevu.  Inashauriwa kunywa glasi sita hadi nane za maji kwa siku ili kusaidia katika hali hii.

👉 Njia nyingine ya kupunguza hali hii;

  • Loweka eneo lako la haja kubwa katika maji ya Moto ya kawaida ambayo hayatakuunguza kwa dakika 10 hadi 15 mara mbili au tatu kwa siku.  Hii huweza kukusaidia pia.

Matibabu ya Bawasiri

Mbali na vitu vya kula,kufanya na kuzingatia ukiwa nyumbani,Zipo njia mbali mbali ambazo hutumika kama Tiba kwa Mgonjwa wa bawasiri ikiwemo;

  • Matumizi ya dawa mbali mbali za Kupaka(Cream), Na za kuweka Sehemu ya Haja kubwa(suppository)
  • Kutumia dawa za kutuliza maumivu
  • Pamoja na Huduma ya Upasuaji

Jinsi ya Kuzuia Bawasiri(Prevention)

Njia bora ya kuzuia bawasiri ni kuhakikisha kinyesi chako kinakuwa laini ili kipite kwa urahisi.  Ili kuzuia hemorrhoids na kupunguza dalili za hemorrhoids, fuata vidokezo hivi:

 ✓ Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi.

 Kula matunda zaidi kama papai,parachichi,embe,n.k. Pia kula mboga mboga na nafaka nzima.  Kufanya hivyo kunapunguza kinyesi kuwa kigumu na kuongeza wingi wake.  Hii itakusaidia kuepuka matatizo ambayo yanaweza kusababisha hemorrhoids.  Ongeza nyuzinyuzi kwenye mlo wako polepole ili kuepuka matatizo na gesi.

 ✓ Kunywa maji mengi. 

 Kunywa glasi 6 hadi 8 za maji na vinywaji vingine kila siku ili kusaidia kuweka kinyesi kuwa laini.  Kuepuka pombe pia kunaweza kusaidia.

 ✓ Fikiria virutubisho vya nyuzinyuzi.

  Watu wengi hawapati nyuzinyuzi za kutosha katika mlo wao.  Uchunguzi umeonyesha kuwa virutubisho vya nyuzi, kama vile psyllium au methylcellulose (Citrucel), vinaweza kupunguza dalili na hali ya kutokwa na damu kutokana na bawasiri.

 Ikiwa unatumia virutubisho vya nyuzinyuzi, hakikisha unakunywa angalau glasi nane za maji au vinywaji vingine kila siku.  Vinginevyo, virutubisho vinaweza kusababisha kuvimbiwa au kuifanya hali hii kuwa mbaya zaidi.

 ✓ Usijikaze sana wakati wa Kujisaidia. 

 Kujikaza sana na kushikilia pumzi yako wakati wa kujaribu kupitisha kinyesi husababisha shinikizo kubwa kwenye mishipa ya puru ya chini. Hii huweza kuongeza hatari ya wewe kupata bawasiri

 ✓ Fanya MaZoezi ya Mwili.

 Endelea kufanya kazi na mazoezi ili kusaidia kuzuia tatizo la kupata choo kigumu au constipation na kupunguza shinikizo kwenye mishipa.  Mazoezi pia yanaweza kukusaidia kupunguza uzito kupita kiasi ambapo hali hii inaweza kusababisha bawasiri au kuifanya kuwa mbaya zaidi.

Pamoja na Mazoezi unayofanya,epuka kunyanyua vitu vizito sana,na fanya mazoezi kwa kiasi.

✓ Epuka kukaa kwa muda mrefu.  

Kukaa kwa muda mrefu, haswa kwenye choo, kunaweza kuongeza shinikizo kwenye mishipa kwenye njia ya haja kubwa, hali hii inaweza kusababisha bawasiri au kuifanya kuwa mbaya zaidi.

Hitimisho

Ugonjwa wa Bawasiri kwa kitaalam Hemorrhoids ni ugonjwa unaohusisha kuvimba na kutuna kwa mishipa kwenye mfereji wa Njia ya haja kubwa, ambapo Mishipa hii husaidia wakati wa utoaji wa kinyesi.

Kwa Lugha nyingine, Bawasiri huhusisha kuvimba kwa mishipa inayojulikana kama Veins kwenye eneo la haja kubwa yaani anus, pamoja na Sehemu ya ndani ya rectum yaani Lower rectum.

DALILI ZA KUWEPO KWA UGONJWA WA BAWASIRI KWA UJUMLA

 ➖ Dalili za bawasiri ni pamoja na hali ya kuwashwa, kutokwa na damu, uvimbe,hisia ya kuchoma au kuwaka sehemu ya haja kubwa, na kuhisi kama mchanga sehemu ya Haja kubwa.

➖ Wagonjwa pia wanalalamika juu ya usumbufu wa jumla wakiwa wamekaa, kuhisi uwepo kitu ndani ya njia ya haja kubwa.

➖  Bawasiri au  Hemorrhoids inaweza kusababisha kutokwa na damu kwa njia ya haja kubwa

➖ Kupata maumivu sehemu ya haja kubwa

➖ Uwepo wa kitu kama donge la hudhurungi sehemu ya Haja kubwa.Lakini wakati mwingine hemorrhoids za ndani pia zinaweza kuwa chungu sana.  Hii hufanyika kwa sababu hua na kitu kama kitambaa. 

 ➖ Kumbuka maumivu katika eneo karibu na njia ya haja kumbwa yanaweza kuwa ni kwa sababu ya tatizo Lingine, kama michubuko au kuchanika njia ya haja kubwa, tatizo la fistula ya njia ya haja kubwa n.k

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!

0 Comment

Majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga JKTAfyaclass Bongo Social •

Haya hapa majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga JKT







JKT yatoa majina ya wanafunzi waliohitimu kidato cha sita watakaopaswa kujiunga na mafunzo ya kijeshi mwaka 2025.

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limetoa orodha ya wanafunzi waliomaliza kidato cha sita mwaka 2025 watakaotakiwa kujiunga na mafunzo ya lazima ya kijeshi kwa mujibu wa sheria, huku vijana hao wakipangiwa kambi mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na JKT, vijana kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wamepangiwa katika kambi tofauti ikiwemo Bulombora, Rwamkoma, Msange, Kanembwa, Makutopora, Mpwapwa, Ruvu, Nachingwea, Oljoro, Kibiti na Maramba.

>>Fungua hapa kusoma orodha kamili ya ya vijana waliochaguliwa kujiunga JKT

0 Comment

TANZIA: Ngugi wa Thiong’o afariki dunia,Mwandishi gwiji wa FasihiAfyaclass Bongo Social •

TANZIA: Ngugi wa Thiong’o afariki dunia,Mwandishi gwiji wa Fasihi



Ngugi wa Thiong’o Mwandishi gwiji wa fasihi kutoka Kenya, ameripotiwa kufariki dunia leo Mei 28, 2025, akiwa na umri wa miaka 87 ambapo taarifa rasmi zinaeleza kuwa Mwandishi huyo mashuhuri amefariki akiwa Marekani ambako amekuwa akiishi na kufundisha kwa miaka mingi.

Ngugi alitambulika kwa kazi zake mashuhuri kama Weep Not, Child, The River Between, na Petals of Blood, pamoja na maandiko ya kiitikadi kama Decolonising the Mind vilevile alikuwa mtetezi thabiti wa matumizi ya lugha za Kiafrika katika elimu na fasihi na alihamasisha uhuru wa kiakili kupitia maandiko yake yenye nguvu ya kisiasa na kijamii.

Mbali na kuwa mwandishi, Ngugi pia alikuwa Mwalimu na Mwanafikra ambaye alitoa mchango mkubwa katika vyuo vikuu mbalimbali, hasa Chuo Kikuu cha California, Irvine.

0 Comment

Tatizo la busha,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la busha,chanzo,dalili na Tiba

Busha ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa eneo la korodani au uvimbe ndani ya vifuko vya korodani(Scrotum) unaosababishwa na kujaa maji.

Tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama hydrocele

Tatizo la busha au hydrocele ni aina ya uvimbe kwenye korodani, au mfuko wa ngozi unaoshikilia korodani. Uvimbe huu hutokea wakati majimaji yanapojikusanya kwenye kifuko chembamba kinachozunguka korodani. Hydroceles ni kawaida pia kwa watoto wachanga”

Dalili za Tatizo la Busha

Mara nyingi ishara pekee ya busha ni uvimbe usio na uchungu au maumivu kwenye korodani moja au zote mbili.

Uvimbe huo unaweza kufanya korodani ya mtu mzima kuhisi nzito. Kwa ujumla, maumivu yanaongezeka wakati uvimbe unaongezeka. Wakati mwingine, eneo lenye kuvimba linaweza kuwa dogo asubuhi na kubwa baadaye mchana.

Vitu hivi huongeza hatari ya Kupata tatizo la busha

Busha nyingi zipo wakati wa kuzaliwa. Tafiti zinaonyesha Angalau asilimia 5% ya wanaume waliozaliwa wana busha,

Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati, ambao huzaliwa zaidi ya wiki tatu kabla ya tarehe zao za kuzaliwa, wana hatari kubwa ya kuwa na busha pia.

Sababu za hatari za kupata Tatizo la busha baadaye maishani ni pamoja na:

  • Kupata Jeraha au kuvimba ndani ya korodani.
  • Maambukizi, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya zinaa.n.k

Madhara ya Tatizo la busha ni yapi?

Mara nyingi si tatizo lenye hatari kubwa au madhara zaidi ni la kawaida, Na pia haliathiri uwezo wa kupata mtoto kama baadhi ya watu wanavyosema.

Ingawa pia busha linaweza kuhusishwa na shida za kiafya ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa. Kuna uhusiano wa hydrocele na Matatizo haya:

• Maambukizi au tumor.

Na matokeo yake inaweza kusababisha korodani kutengeneza kiwango kidogo cha manii au zisifanye kazi vizuri kama kawaida.

• Hernia ya inguinal.

Hii inaweza kusababisha matatizo ya kiafya ambayo huweza kutishia maisha.

Chanzo cha tatizo la busha

Tatizo la hydrocele au Busha ni tatizo la kujaa kwa maji kwenye mfuko wa korodani za mwanaume.

SABABU AU CHANZO CHA TATIZO LA BUSHA NI NINI?

Tatizo la Busha au hydrocele huweza kusababishwa na vitu mbali mbali ikiwemo;

– hali ya eneo la Kuzunguka Korodani kuwa na Maji mengi kuliko ilivyokawaida,

– Mirija ya Lymph kwenye Korodani au mishipa ya Damu inayosafirisha damu kutoka kwenye korodani kwenda maeneo mengine ikiwa Imeziba kabsa,

Vyote hivi hupelekea kupungua kwa ufyonzwaji wa maji yanayozunguka eneo la korodani. Hali ambayo hupelekea maji kujikusanya kwenye vifuko vya Korodani.

HIZI NI BAADHI YA SABABU ZA MAJI KUWA MENGI KWENYE ENEO LA KORODANI

• Mtu kupata Majeraha au kuumia kwenye Korodani(Injury)

• Mtu kupata Maambukizi ya magonjwa kwenye eneo la Korodani

• Mtu kupata Maambukizi kwenye mshipa wa-epididymis

• Mtu kupata Maambukizi yanayo sababishwa na vimelea wa filaria (filariasis) wanao sababishwa na kuumwa na mbu aina ya Culex.

• Mtu kupata tatizo la Korodani Kujisokota ambapo kwa kitaalam hujulikana kama testicular torsion

• Mtu kupata Uvimbe kwenye korodani yaani testicular tumors,

Hii pia huweza kuchangia uzalishwaji wa maji mengi kwenye korodani.

• Mtu Kufanyiwa upasuaji ambao huweza kuathiri ufyozwaji wa maji kwenye korodani

• Mtu kupata Tiba ya mionzi kipindi cha nyuma. n.k

KUMBUKA; Watu ambao wapo maeneo ya Pwani, wapo kwenye hatari zaidi ya kupata tatizo la Busha,

Hui ni kutokana na kuwa kwenye hatari zaidi ya kung’atwa na mbu aina ya Culex anayeeneza vimelea vya filaria.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

0 Comment

Daktari atupwa jela kwa kuwabaka mamia ya watotoAfyaclass Bongo Social •

Daktari atupwa jela kwa kuwabaka mamia ya watoto



Mahakama ya Ufaransa imetoa kifungo cha juu cha miaka 20 jela kwa daktari bingwa wa upasuaji ambaye alikiri kuwadhulumu kingono mamia ya wagonjwa, wengi wao wakiwa watoto, kwa zaidi ya miongo miwili.

Kesi hiyo iliyodumu kwa miezi mitatu ya Joel Le Scouarnec, mwenye umri wa miaka 74, imefichua ukubwa wa uhalifu wake na mateso ya waathiriwa lakini pia imezusha maswali kwa nini juhudi zaidi hazikufanywa mapema ili kumzuia. Amepatikana na hatia ya kuwadhulumu kingono na kuwabaka wagonjwa 229 katika kliniki yake mjini Vannes. 

Le Scouarnec, mmoja wa wanyanyasaji wakubwa wa kingono waliopatikana na hatia katika historia ya Ufaransa, alikuwa tayari gerezani baada ya kuhukumiwa mwaka 2020 adhabu ya miaka 15 kwa kuwabaka na kuwadhalilisha kingono watoto wanne, wakiwemo wapwa zake wawili.

Hukumu ya miaka 20 jela kwa uhalifu mkubwa wa ubakaji iliyotolewa na hakimu mfawidhi Aude Buresi ndiyo ya juu zaidi ambayo inaweza kutolewa nchini Ufaransa kwa shtaka la ubakaji uliokithiri, ambapo hukumu hazijumuishwi pamoja kwa kila kosa alilofanya. Le Scouarnec hatakuwa na haki ya kuomba kuondoka jela kabla ya kifungo chake kukamilika, hadi atakapotumikia theluthi mbili ya hukumu yake ambayo ni sawa na miaka 13.

0 Comment

Wanafunzi 10,300 waliopata mimba warejeshwa shuleniAfyaclass Bongo Social •

Wanafunzi 10,300 waliopata mimba warejeshwa shuleni



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, jumla ya wanafunzi 10,300 waliopata ujauzito wamerudishwa shule na kuendelea na masomo yao.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amesema hayo leo Mei 27, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo.

“Hadi sasa kwa mujibu wa takwimu ni wanafunzi 10,300 ambao ndio wamerejeshwa shule baada kupata mimba na kuendelea na masomo yao na wengine wamefanya vizuri sana, kumekuwepo na changamoto kadhaa lakini zinaendelea kushughulikiwa lengo letu ni kuona hakuna mtoto anayepata mimba akiwa shule lakini pia hatupaswi kuzuia aliyepata mimba kupata haki yake ya kusoma,”amesema 

0 Comment

Ifahamu nchi inayohesabu umri wa mtoto tangu akiwa tumboniAfyaclass Bongo Social •

Ifahamu nchi inayohesabu umri wa mtoto tangu akiwa tumboni



Nchi ambayo mtoto anapozaliwa alikuwa anahesabiwa kuwa na mwaka mmoja ni Korea Kusini (na zamani Korea Kaskazini pia ilifuata utaratibu huu). Mfumo huu wa kihistoria unaitwa “Korean age system”, ambapo mtu huhesabiwa kuwa na umri wa mwaka mmoja punde tu anapozaliwa, na kila mtu huongezewa mwaka mmoja tarehe 1 Januari, bila kujali tarehe yao ya kuzaliwa halisi.

Mtoto akizaliwa tarehe 31 Desemba 2024, siku inayofuata (1 Januari 2025), atahesabika kuwa na miaka miwili kwa mujibu wa mfumo huo, ingawa kwa umri wa kimataifa atakuwa na siku moja tu.

Mnamo mwaka 2023, Korea Kusini ilianza kutumia rasmi mfumo wa umri wa kimataifa (ambapo mtu anahesabiwa kuwa na umri wa miaka 0 anapozaliwa na huongezewa mwaka mmoja kila baada ya mwaka mmoja wa kuzaliwa kwake). Hii ni sehemu ya jitihada za kupunguza mkanganyiko wa kimataifa.

Kwa hiyo, kihistoria Korea Kusini ilikuwa inatumia mfumo huo, lakini sasa wamehamia kwenye mfumo wa kimataifa ambao ni wa kawaida duniani kote baada ya kupitishwa sheria kufuta utamaduni huo.
Sheria hiyo imefuta mfumo ule wa jadi uliokuwa ukimhesabu Mkorea kuwa na umri wa mwaka mmoja pindi anapozaliwa, kwa kujumlisha muda aliokaa tumboni mwa mama.

Mabadiliko haya, ambayo sasa yanahesabu umri wa mtu kwa kuzingatia tarehe halisi ya kuzaliwa, yalianza kutekelezwa mwaka 2021.

Rais Yoon Suk Yeol alihamasisha sana mabadiliko haya alipokuwa akiwania urais. Alisema kuwa mbinu hizo za jadi za kuhesabu umri zilileta “gharama zisizo za lazima kijamii na kiuchumi”.

Kwa mfano, migogoro iliibuka kuhusu ulipaji wa bima na uamuzi wa kustahiki kwa baadhi ya programu za msaada wa serikali.
Hapo awali, mfumo uliotumika sana nchini Korea ulikuwa ni ule wa “umri wa Kikorea” ambao umekuwa ukitumika kwa karne nyingi, ambapo mtu huhesabiwa kuwa na mwaka mmoja pindi tu anapozaliwa, na huongezewa mwaka mmoja kila tarehe 1 Januari. 

Hii inamaanisha kuwa mtoto aliyezaliwa tarehe 31 Desemba atakuwa na umri wa miaka miwili siku inayofuata.
Wabunge walipiga kura kuondoa tamaduni hiyo ya jadi mnamo Desemba mwaka 2023.
Utafiti uliofanywa na kampuni ya ndani ya Hankook Research mwezi Januari 2022 ulionyesha kuwa watu watatu kati ya wanne wa Korea Kusini waliunga mkono uamuzi huo wa kuoanisha mfumo huo na wa kimataifa.

Mbinu hizi za jadi za kuhesabu umri ziliwahi pia kutumika katika nchi nyingine za Asia Mashariki, lakini nyingi imeziacha.
Japani ilikuwa na utamaduni huo lakini ilianza kutumia kiwango cha kimataifa mwaka 1950, huku Korea Kaskazini ikifuata katika miaka ya 1980.

0 Comment

Madhara ya Vumbi la kongo,Fahamu hapa kila kituAfyaclass Bongo Social •

Madhara ya Vumbi la kongo,Fahamu hapa kila kitu

Vumbi la kongo ni jina ambalo ni maarufu sana na linatumika kwa dawa ambayo hutumiwa sana na wanaume kwa lengo la kuwaridhisha wapenzi wao au wake zao.

Dawa hii ya vumbi la kongo hupakwa kwenye uume nusu saa kabla ya Mwanaume kushiriki tendo la Ndoa ili ifanye kazi vizuri, 

Kinachotokea ni kwamba, ndani ya dawa hii kuna kemikali ambazo zimeweka kwa lengo la kutia ganzi uume hivo kumfanya mwanaume ashiriki tendo la ndoa kwa muda mrefu zaidi.

MADHARA YA KUTUMIA VUMBI LA KONGO

Madhara ya kutumia vumbi la kongo kwa wanaume ni pamoja na;

- Mwanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa kama hajatumia dawa hii ya vumbi la kongo

- Kuathiri mishipa ya uume na kusababisha  uume wa mwanaume kushindwa kusimama moja kwa moja kutokana na athari za kutiwa ganzi, hivo ikabaki kazi moja tu ya kukoja na sio kufanya mapenzi

- Uume kusinyaa kabsa na kulegea hata wakati wa kushiriki tendo la ndoa

- Kukosa hamu ya kufanya mapenzi na kufurahia tendo

- Pia matumizi ya dawa kama hizi za kupaka kwenye uume huweza kusababisha fangasi wa sehemu za siri kwa mwanamke endapo mmeshiriki tendo la ndoa bila kutumia kinga au Condom

- Mwanaume kupoteza kabsa uwezo wa kurudia tendo la Ndoa mara ya pili

Epuka matumizi ya vitu hivi ni hatari kwa afya yako, kama una tatizo la kukosa nguvu za kiume kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya matibabu sahihi.

SWALI: Uume wangu umelegea baada ya Kutumia Vumbi la Congo

Ni kweli kuna Madhara ya kutumia vitu kama Vumbi la Kongo?

Madhara ya kutumia vumbi la kongo kwa wanaume ni pamoja na;

- Mwanaume kushindwa kushiriki tendo la ndoa kama hajatumia dawa hii ya vumbi la kongo

- Kuathiri mishipa ya uume na kusababisha  uume wa mwanaume kushindwa kusimama moja kwa moja kutokana na athari za kutiwa ganzi, hivo ikabaki kazi moja tu ya kukoja na sio kufanya mapenzi

- Uume kusinyaa kabsa na kulegea hata wakati wa kushiriki tendo la ndoa n.k

VITU AMBAVYO HUWEZA KUATHIRI AFYA YA UZAZI KWA MWANAUME

1. Matumizi ya baadhi ya dawa za kutibu magonjwa mbali mbali

2. Ulevyi au unywaji wa pombe kupita kiasi

3. Mlo au lishe yake ya kila siku

4. Tabia ya uvutaji wa sigara

5. Tabia ya upigaji wa punyeto (Soma zaidi hapa...!!!)

6. Kazi anayofanya kila siku

7. Magonjwa shambulizi kama fangasi, Uti n.k

8. Tatizo la Tezi dume pamoja na kansa zingine kama kansa ya korodani n.k

9. Tatizo la uzito pamoja na unene kupita piasi

10. Matumizi ya dawa za asili kwa lengo la kuongeza uwezo wa kufanya tendo la ndoa, kama vile; dawa maarufu kwa jina la Vumbi la Kongo n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figoAfyaclass Bongo Social •

Ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameshuhudia utiaji saini wa hati ya makubaliano ya ujenzi wa kituo kikubwa cha kupandikiza figo pamoja na utoaji mafunzo kwa Madaktari bingwa ambacho kitakuwa ni kikubwa katika ukanda wa Jangwa la Sahara.

Kituo hicho ambacho kitajengwa kwenye Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma ni ushirikiano kati ya Shirika la Tiba la TOKUSHUKAI, Hospitali ya Benjamin Mkapa na Chuo Kikuu cha Dodoma na kinatarajia kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 28 ikiwa ni msaada usiokuwa na masharti yoyote.

Utiaji saini huo umefanyika May 26, 2025 wakati Kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililowakutanisha Wafanyabiashara wa Tanzania na Wawekezaji wa Japan, Osaka, Japan, ikiwa ni sehemu ya  ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025, kongamano hilo lilifunguliwa na PM Majaliwa.



Akiongea baada ya utiaji saini huo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa, Profesa Abel Makubi amesema wamesaini makubaliano na shirika hilo linaloundwa na kundi la madaktari Wakijapan ambao wamekuwa wakisaidia utoaji na uboreshaji huduma za afya “Hawa ni Wadau wetu wa muda mrefu na walikuwa watu wa kwanza kusaidia utoaji wa huduma Dialysis katika Hospitali ya Benjamin Mkapa”

0 Comment

Ushindi wa Liverpool waleta balaa,Ajali mbaya yatokeaAfyaclass Bongo Social •

Ushindi wa Liverpool waleta balaa,Ajali mbaya yatokea



Ushindi wa Liverpool waleta balaa nchini Uingereza Jeshi la Polisi Merseyside limesema mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 53 amekamatwa baada ya gari kugonga watembea kwa miguu wakati wa gwaride la ushindi wa Kombe la Ligi Kuu ya England la Liverpool, na kusababisha watu wawili kujeruhiwa vibaya.

Watu 27 walikimbizwa hospitalini kwa gari la wagonjwa. Wawili kati yao — mmoja akiwa ni mtoto — walipata majeraha makubwa. Jumla ya watoto wanne walijeruhiwa.

Watu wengine 20 walitibiwa eneo la tukio na hawakuhitaji kupelekwa hospitalini. Mtaalamu wa huduma ya kwanza aliyekuwa kwenye baiskeli aligongwa na gari hilo lakini hakujeruhiwa.

Kulingana na Nick Searle, Afisa Mkuu wa Zimamoto na Uokoaji wa Merseyside, wazima moto waliwaokoa watu wanne — wakiwemo mtoto mmoja — waliokuwa wamenaswa chini ya gari hilo.

Huduma za dharura ziliwasili haraka Water Street baada ya Polisi wa Merseyside kupokea taarifa kuhusu tukio hilo muda mfupi baada ya saa 12 jioni siku ya Jumatatu.

Gari hilo lilikomea eneo la tukio, na mwanaume kutoka eneo la Liverpool — anayeaminika kuwa dereva — alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi.

Naibu Kamishna Mkuu wa Polisi wa Merseyside, Jenny Sims, alisema tukio hilo halichukuliwi kama tendo la kigaidi.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu jioni, alisema polisi wanaamini ni tukio la kipekee na kwa sasa hawamtafuti mtu mwingine yeyote kuhusiana nalo.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD