Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke chanzo na Tiba

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke chanzo na Tiba

#1

Maumivu wakati wa tendo la ndoa kwa mwanamke (yanayojulikana kitaalamu kama dyspareunia) ni tatizo la kawaida linaloweza kusababishwa na mambo mengi ya kimwili au kisaikolojia. Hebu tuchambue kwa undani:

Sababu Kuu za Maumivu Wakati wa Tendo la Ndoa

1. Ukavu wa uke (Vaginal dryness)

Sababu: kukosa ute wa asili unaolainisha uke. Hii Hutokea zaidi kwa: 

  • Wanawake baada ya kujifungua au wanaonyonyesha.
  • Wanaotumia dawa fulani (mfano antihistamines, antidepressants).
  • Wanawake waliokaribia au walio katika kipindi cha kukoma hedhi.

Lakini pia huweza kusababishwa na sababu mbali mbali ikiwemo; mabadiliko ya Vichocheo mwilini,maambukizi ya magonjwa n.k.

2. Maambukizi ya uke (Vaginitis)

Dalili: harufu mbaya, kutokwa na uchafu, kuwasha, au kuchoma,Ukavu ukeni n.k.

Yapo maambukizi ya magonjwa kama vile: fangasi (candida), bakteria, au magonjwa ya zinaa. Haya huweza kusababisha tatizo hili.

Tiba hutegemea na chanzo: ila dawa kama jamii ya antifungal, antibiotic, au dawa za STI, huweza kutumika kutibu hali hii.

3. Maambukizi ya bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke (Pelvic Inflammatory Disease – PID)

Maambukizi ya kizazi, mirija ya uzazi, au ovari.

Dalili huweza kuwa: maumivu chini ya tumbo, homa, uchovu, maumivu wakati wa tendo.n.k

4. Kuwa na michubuko au Vidonda kwenye mlango wa kizazi au kuvimba (Cervical inflammation / erosion)

Hali hii Huleta maumivu ya ndani zaidi (deep pain) wakati wa tendo.

Kuvimba pamoja na Michubuko pia huweza kuwepo kwenye eneo la ukeni,hali hii inachangia maumivu pia wakati wa tendo.

5. Matatizo ya kihisia au kisaikolojia

Msongo wa mawazo, hofu, kutopata raha au mapenzi kwa mwenza, au uzoefu mbaya wa nyuma. n.k.

Suluhisho juu ya hili: 

  • Mazungumzo ya wazi na mwenza.
  • Ushauri wa kisaikolojia au sex therapy.

6. Tatizo la Uvimbe kwenye kizazi,Endometriosis au Fibroids

Haya ni magonjwa ya mfumo wa uzazi yanayosababisha maumivu ya kina ndani ya Uke

Dalili huweza kuwa: maumivu wakati wa hedhi, tendo, au wakati wa haja kubwa.

Suluhisho: uchunguzi wa kitaalamu (ultrasound / laparoscopy) na tiba maalum.

Zingatia Mambo haya ya Kufanya Nyumbani Kabla ya Kuenda Hospitali

•Hakikisha unapata muda wa kutosha wa maandalizi “foreplay” ili uke uwe na unyevunyevu wa kutosha.

•Epuka tendo kama una maumivu makali au uchafu usio wa kawaida.

•Kunywa maji mengi na kula matunda (hasa yenye vitamin C na E).

•Vaa nguo za ndani zisizobana, zenye material ya pamba sio mpira.

Wakati wa Kumwona Daktari kwa haraka

Ongea na daktari au Nenda hospitali ukiona mojawapo ya haya:

-Maumivu makali kila mara unapofanya tendo.

-Kutokwa na uchafu, damu, au harufu isiyo ya kawaida.

-Maumivu ya tumbo la chini yanayoendelea.

-Homa au uchovu unaoambatana na maumivu hayo. n.k..

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code