Niliteseka na maumivu ya tumbo – ndipo nikagundua ni Ugonjwa wa amoebaAfyaclass Bongo Social •

Niliteseka na maumivu ya tumbo – ndipo nikagundua ni Ugonjwa wa amoeba

Mimi naitwa Amani kutoka Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania,Katika Hali ambayo haikuwa ya kawaida,nilianza kupata maumivu ya Tumbo hali ambayo ilinisumbua kwa muda wa Zaidi ya wiki 2,

Maumivu haya ya tumbo yaliambatana na kuharisha choo kama cha Makamasi,hali ambayo ilishtua sana.

Baada ya kuona hali hii,nilianza kufuatilia ni kitu gani hiki kinaendelea kwenye Mwili wangu? Nikakutana na Mtu mmoja "rafiki yangu",akaniambia tunajaribu kuangalia Mtandaoni hizi ni dalili za Kitu gani? tukiangia mtandao wa Google, ndipo nilipokutana na Makala kutoka Afyaclass ikielezea Dalili hizi kwa Kina, ndipo nikaamua kutafuta Msaada kwao na kupata Ushauri na kupona kabsa tatizo Langu.

Kwa Idhini ya Mgonjwa,aliomba Ujumbe huu uandikwe ili kusaidia wengine kujifunza na kupata msaada wa kupona ikiwa wana tatizo kama lake Amani lililompata.

Maelezo kutoka kwa Dr.Ombeni wa Afyaclass: 

Zipo Cases nyingi za Aina hii ambazo tunazipata kila Siku, Lakini kwa Uzoefu niloupata asilimia 80% ya Wagonjwa wa amoeba ambao nilikutana nao;Wengi wao walikuwa na Dalili hizi;

Maumivu ya tumbo,Kuharisha,Choo kuwa kama chenye Makamasi, Kukosa hamu ya kula,na baadhi yao kupata Kichefuchefu na kutapika. Sasa, Je Ugonjwa wa Ameoba ni Ugonjwa gani?

Ugonjwa wa amoeba au amoebiasis ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea(parasite) kinachoitwa Entamoeba histolytica. Entamoeba histolytica  ni kimelea kwenye kundi la anaerobic parasite na kwa mara ya kwanza hupatikana kwenye Utumbo mpana(colon);

Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha ugonjwa wa amoeba kwa mtu yeyote anayekula au kunywa kitu kilichoambukizwa na kimelea hiki.

Dalili Kubwa za Ugonjwa huu wa Amoeba ni pamoja na;

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi chenye vitu kama makamasi

- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota

- Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana

- Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

- Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)

- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili

- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa

- Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu 

- Kupoteza appetite ya chakula kabsa

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

- Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda

NB:Hizi ni Miongoni mwa Dalili kubwa ambazo tunaziona kwa Wagonjwa wenye Vimelea hivi vya Amoeba, Na Ukifuatilia historia ya Ugonjwa wao(Patient history) ulivyoanza asilimia 88% wanaishi kwenye mazingira ambayo maji sio Salama,wala mazingira ya maandalizi ya Vyakula Sio Masafi Pia.

Ushauri wangu kwako,hakikisha Unakunywa maji Safi,Chakula kiwe Safi,Vyoo Safi utakuwa Salama....

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

TANZIA:Watu Wawili waliofariki katika ajali ya Bondia Anthony Joshua watambuliwaAfyaclass Bongo Social •

TANZIA:Watu Wawili waliofariki katika ajali ya Bondia Anthony Joshua watambuliwa

Maelezo ya picha,Sina Ghami (kushoto) na Latif "Latz" Ayodele

Wanaume wawili waliofariki katika ajali iliyomuhusisha mwanamisumbwi raia wa Uingereza, Anthony Joshua huko Lagos Nigeri wametambuliwa.

Wanaume hao ambao ni marafiki na wanachama wa timu ya Joshua, ni Sina Ghami na Latif Ayodele, kwa mujibu wa kampuni ya kuandaa michezo ya Joshua ya Matchroom Boxing.

Taarifa hiyo inasema, wawili hao walifanya kazi kwa karibu na Anthony Joshua, na wote walikuwa marafiki wazuri.

Sina Ghami alikuwa kocha wa viungo wa Joshua kwa zaidi ya miaka 10. Pia ni mmiliki wa ukumbi wa michezo wa Evolve Gym jijini London.

Kwa mujibu tovuti hiyo Ghami ni mtaalamu wa michezo na mazoezi aliyebobea katika mazoezi ya misuli.

Mwingine ni Latif "Latz" Ayodele alikuwa mkufunzi binafsi wa Joshua. Mapenzi yake kwa mazoezi yapo wazi kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Matchroom Boxing imesema Joshua alipelekwa hospitalini kwa ajili ya "uchunguzi na matibabu" na yuko katika "hali imara na atabaki hapo kwa uchunguzi."

Maafisa huko Nigeria wanasema gari la Joshua liligonga lori wakati wakiendesha kwa kasi.

Joshua - bingwa wa dunia mara mbili wa uzito wa juu – familia yake ina asili ya Sagamu, mji ulioko katika Jimbo la Ogun, Nigeria.

0 Comment

Fahamu Nchi sita zimeyaaga mashindano ya Afcon 2025Afyaclass Bongo Social •

Fahamu Nchi sita zimeyaaga mashindano ya Afcon 2025

Nchi sita zimeondolewa kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika la 2025 nchini Morocco huku mashindano hayo yakiingia katika mechi za mwisho za makundi.

Comoros, Zambia na Zimbabwe zimekuwa timu za hivi karibuni kuondolewa, zikijiunga na Botswana, Gabon na Equatorial Guinea, ambazo tayari ziliondoka baada ya kushindwa kukusanya pointi katika raundi za awali.

Timu ya kwanza kuondolewa katika AFCON 2025 ilikuwa Botswana. Equatorial Guinea na Gabon zilifuata.

Comoro ni timu ya kwanza iliyoshika nafasi ya tatu kuondolewa, kwani walimaliza mechi yao ya tatu tayari wakiwa chini ya timu nne kati ya tano zilizoshika nafasi ya tat.

Ushindi wa Afrika Kusini wa mabao 3-2 dhidi ya Zimbabwe ulimaliza safari ya majirani zao. Zimbabwe ilimaliza ikiwa ya mwisho na pointi moja, ikithibitisha kuondolewa kwao.

Mashindano hayo yanayoendelea Morocco, yataendelea leo kwa Uganda kukutana na Nigeria, Tanzania dhidi ya Tunisia, Bostwana kukipiga na DR Congo na Benin kuchuana na Senegal.

0 Comment

Kuhisi kitu kooni kimekwama,unahisi kama kuna kitu kimekwama kooni? Sababu hizi hapaAfyaclass Bongo Social •

Kuhisi kama kuna kitu kimekwama kooni (hujulikana kama globus sensation) kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa.

Hizi ndyo Sababu Kuu za kuhisi hali hii kwenye Koo Lako;

1. Tatuzo la Acid Reflux:Asidi ya tumboni kupanda kooni

– Asidi inapopanda huleta hali ya kero kooni, na kuhisi kama kuna kitu kimekwama

– Huambatana na kiungulia, ladha chungu mdomoni, au maumivu kifua

2. Maambukizi ya koo (tonsillitis, pharyngitis)

Maambukizi haya huweza kuhusisha kuvimba kwa tonses pia,

– Koo huvimba au kuwa na vidonda

– Huambatana na maumivu, homa, au ugumu wa kumeza kitu chochote.

3. Tezi la thyroid kuvimba

– Tatizo hilo huweza kusababisha hali ya kubana koo na kuhisi kama kitu kimekwama kooni

– Na mtu mwenye tatizo hili huonekana zaidi kama shingo imevimba

4. Misuli ya koo kujikaza bila wewe kujua

Ambapo hii huwapata watu wengi wakiwa kwenye Msongo mkali wa mawazo au wasiwasi (stress/anxiety) ndipo tatizo hili huanza.

– Mara nyingi huja bila maumivu, lakini hisia huendelea

5. Sababu Zingine ni pamoja na:

Kuwa na Kamasi nyingi eneo la ndani ya pua kushuka kooni (post-nasal drip) ambapo husababishwa na;

  • Mafua, 
  • Tatizo la sinusitis, 
  • au Tatizo la Mzio au allergy

– Hii huleta hisia ya kitu kinashuka au kimeshika kooni

Dalili hatarishi Zaidi (muone daktari haraka)

Nenda hospitali au tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass ikiwa una:

-Ugumu mkubwa wa kumeza

-Maumivu makali kooni au kifuani

-Kupungua uzito bila sababu

-Kikohozi chenye damu

-Hisia inaendelea zaidi ya wiki 2–3

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mnunuzi maarufu kwenye X, Shangazi Esther, aliyegunduliwa na saratani na 'kukataa' kuongezewa damu afarikiAfyaclass Bongo Social •

Mnunuzi maarufu kwenye mtandao wa X, Shangazi Esther, ambaye inasemekana aligunduliwa na saratani na 'alikataa' kuongezewa damu amefariki dunia.


Marehemu alijizolea umaarufu mapema mwezi huu baada ya updates mpya kufichua kwamba anadaiwa kukataa kuongezewa damu iliyopendekezwa na madaktari wake. Hapo awali alikuwa amewaarifu wafuasi wake kwamba matokeo yake ya vipimo yalikuwa nje, yakithibitisha saratani kwenye matiti yake na kwapa. Pia aliwashukuru kila mtu aliyechangia kifedha kwa matibabu yake.

Hata hivyo, mmoja wa waratibu wanaoshughulikia michango, Sir Dickson, alitangaza kwamba yeye na Aliyejitolea mwingine kwenye matibabu wamejiondoa katika kesi yake.

Kulingana naye, madaktari walimshauri kwamba alihitaji kuongezewa damu kabla ya kuanza tiba ya chemotherapy, lakini alikataa kutokana na imani yake ya Mashahidi wa Yehova.

Kulingana na Dickson, kanisa lake linadaiwa kuonya kwamba angetengwa na kanisa ikiwa angekubali damu, na baadhi ya wanafamilia walisisitiza kwamba "chochote kitakachotokea ni mapenzi ya Mungu."

0 Comment

Faida Usizozijua kabsa kuhusu Maji ya Limao,Soma makala hiiAfyaclass Bongo Social •

Maji ya limao ni kinywaji rahisi kinachotengenezwa kwa kuchanganya maji na juisi ya limao mbichi. Kunywa maji ya limao kila siku kunaweza kusaidia kuboresha afya kwa ujumla kwa kutoa virutubisho muhimu, kuimarisha kinga ya mwili na kusaidia kazi mbalimbali za mwili.

Kwa mujibu wa tovuti ya afya ya Healthline, glasi ya juisi iliyokamuliwa kutoka gramu 48 za limao ina takribani kalori 10.6 na virutubisho vifuatavyo:

  • 21% ya kiwango cha kila siku cha vitamini C
  • 2% folate
  • 1% potasiamu
  • 1% vitamini B1
  • 1% vitamini B5
  • 0.5% vitamini B2

Vitamini C husaidia kuimarisha kinga ya mwili na kulinda mwili dhidi ya magonjwa.

Kuchanganya juisi ya limao na maji ni njia rahisi na yenye afya ya kudumisha unyevunyevu mwilini. Maji ya limao pia yana faida nyingi kiafya kutokana na virutubisho vyao.

1. Huongeza Kiasi cha Vitamini C

Limao lina vitamini C nyingi, antioxidant inayolinda seli dhidi ya free radicals zinazoweza kusababisha uvimbe na magonjwa mbalimbali. Vitamini C pia husaidia:

Uzalishaji wa collagen na L-carnitine

Metabolism ya protini

Urejeshaji wa antioxidants

Usogeaji wa chuma mwilini

Uzalishaji wa homoni

Kupunguza hatari ya baadhi ya saratani na magonjwa ya moyo

Ukikosa vitamini C mwilini unaweza kupata: kuongezeka kwa hatari ya maambukizi, ngozi kavu, macho kavu, kinywa kavu, uchovu, usingizi mdogo, na upotevu wa meno.

2. Husaidia Kupunguza Uzito

Kunywa maji ya limao kunasaidia kuongeza unywaji wa maji kwa ujumla, kuchochea hisia ya utoshelevu, na kuongeza kiwango cha metabolism. Maji ya limao ni yenye kalori chache, rahisi kutengeneza, na yanaweza kuchukua nafasi ya vinywaji vyenye kalori nyingi, hivyo kusaidia kudhibiti uzito.

3. Badilisha Vinywaji Vyenye Sukari

Maji ya limao ni mbadala wa asili na wenye afya kwa vinywaji vyenye sukari. Kunywa vinywaji vyenye sukari mara kwa mara husababisha kuongezeka kwa uzito, unene wa kupita kiasi, kisukari aina ya 2, magonjwa ya moyo, figo, ini, kuoza kwa meno, na gout.

4. Kuzuia Mawe ya Figo

Asidi ya citric iliyopo kwenye maji ya limao inaweza kusaidia kuzuia mawe ya figo kwa kuongeza kiwango cha mkojo na kuongeza pH, hali inayofanya mazingira ya figo kuwa yasiyofaa kwa uundaji wa mawe. Watu waliokuwa na mawe ya figo wanaweza kuchanganya ml 113 ya juisi ya limao na maji pamoja na dawa zao ili kuzuia kurudiwa kwa mawe. Citrate, sehemu ya asidi ya citric, inaweza kupunguza asidi ya mkojo na kusaidia kuvunja mawe madogo.

5. Kusaidia Utumbo na Usagaji Chakula

Kunywa maji ya limao kabla ya mlo kunaweza kuboresha usagaji chakula. Asidi ya citric inachochea uzalishaji wa asidi tumboni, ambayo husaidia kuvunja chakula. Watu wenye matatizo ya tumbo wanapaswa kuwa makini kunywa maji ya limao kwa tumbo tupu.

Jinsi ya Kutengeneza Maji ya Limao

-Kamulia nusu limao ndani ya ml 230 ya maji ya moto au baridi.

-Maji ya limao yanaweza kunywewa kama yalivyo au kuongeza: majani ya mint, kijiko kimoja cha syrup ya maple au asali safi, kipande cha tangawizi au tango, tone la mdalasini, au kiasi kidogo cha manjano (turmeric).

-Anza asubuhi yako kwa glasi ya maji ya limao ya moto na weka chupa tayari kwenye friji ili kunywa kidogo kidogo siku nzima.

Kupunguza Madhara ya Maji ya Limao

Maji ya limao kwa kawaida ni salama, lakini asidi yake inaweza kuharibu enamel ya meno kwa muda. Ili kupunguza hatari:

Kunywa kwa kutumia straw (kijiko cha kunywa).

Kumbuka kunawa kinywa kwa maji safi baada ya kunywa.

0 Comment

Tanzania na Uganda wamelazimika kugawana alama baada ya kutoka sare ya 1–1Afyaclass Bongo Social •

Tanzania na Uganda wamelazimika kugawana alama baada ya kutoka sare ya 1–1 katika dabi ya Afrika Mashariki ya kwenye michuano ya AFCON 2025, matokeo ambayo yanaacha hatima ya timu zote mbili ikining'inia kuelekea michezo ya mwisho ya kundi.

Kipindi cha kwanza kilikuwa chini ya udhibiti wa Uganda, waliocheza kwa kujiamini na kuwabana Tanzania katika nusu yao ya uwanja. Cranes walionekana kuwa na mpango mzuri wa kumiliki mpira na kushambulia kupitia mipira ya juu, lakini walikosa umakini katika eneo la mwisho.

Kipindi cha pili kilipoanza, Tanzania walibadilika. Ndani ya dakika 10 za mwanzo, Taifa Stars waliongeza kasi na kuanza kuucheza mpira kwenye nusu ya Uganda, shinikizo lililozaa penati ambayo Simon Msuva aliitumia vyema kuiweka Tanzania mbele.

Hata hivyo, dakika 15 za mwisho waganda waliongeza nguvu na kuanza kuingia kwa kasi katika eneo la Tanzania, hali iliyowalipa walipopata bao la kusawazisha kupitia Uche Ikpeazu.

0 Comment

Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, amchakaza mpinzani wake kutoka Nigeria, EriboAfyaclass Bongo Social •

Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameendeleza ubabe baada ya kushinda kwa knockout (KO) dhidi ya mpinzani wake kutoka Nigeria, Eribo, katika pambano lililofanyika usiku wa leo kwenye Ukumbi wa Warehouse, Masaki — Dar es Salaam.

Mwakinyo alimaliza kazi ndani ya mizunguko miwili tu, akitumia umakini na kasi kubwa, jambo lililowafanya mashabiki waliokuwa ukumbini kusimama kwa shangwe.

Ushindi huo umeonekana kama faraja kwa Watanzania wengi, hususani baada ya timu ya taifa, Taifa Stars, kupata matokeo mabaya dhidi ya Nigeria kwenye michuano ya AFCON 2025.

Mwakinyo ameahidi kuendelea kupambana na kuipa heshima Tanzania kimataifa kupitia ndondi

0 Comment

Super Eagles ya Nigeria imeishinda Tunisia 3-2 na kufuzu kwa Raundi ya 16 ya AFCONAfyaclass Bongo Social •

Super Eagles ya Nigeria iliishinda Tunisia 3-2 na kufuzu kwa Raundi ya 16 ya AFCON

Super Eagles ya Nigeria imefuzu kwa raundi ya 16 ya Kombe la Mataifa ya Afrika linaloendelea nchini Morocco.

Nyota hao wa Nigeria waliishinda Tunisia 3-2 Jumamosi usiku katika Uwanja wa Fez kwa mabao kutoka kwa Victor Osimhen, Wilfried Ndidi, na Ademola Lookman, na kuhakikisha timu hiyo inafuzu kutoka kundi lao.

Victor Osimhen alifungua bao dakika ya 44 kupitia krosi kutoka kwa Ademola Lookman kabla ya mapumziko. Katika dakika ya 50, nahodha wa timu hiyo, Widfred Ndidi alifunga bao la pili dakika ya 50, akisaidiwa tena na Lookman.

Lookman aliongeza bao la tatu dakika ya 70, kufuatia pasi ya Osimhen.

 Wakati huo huo, Tunisia ilifanikiwa kupata bao moja kupitia Montassar Talbi, kabla ya penalti ya dakika za mwisho kufungwa na Ali Al-Abdi.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Nigeria ina pointi sita kutokana na mechi mbili, huku Tunisia ikibaki ya pili ikiwa na pointi tatu.

0 Comment

TMA yatoa tahadhari mvua kubwa mikoa 19 LeoAfyaclass Bongo Social •

Mvua hizo zinatarajiwa kunyesha Leo Jumapili, Desemba 28, 2025.

Zinaweza kusababisha mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii. 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi kuchukua tahadhari ya kujikinga na madhara ya mvua kubwa inayotarajia kunyesha katika mikoa 19 nchini ikiwemo Dar es Salaam. 

TMA imesema mvua hizo zinatarajiwa kunyesha kesho Jumapili, Desemba 28, 2025, na huenda zikasababisha madhara mbalimbali ikiwamo mafuriko, maporomoko ya udongo na usumbufu wa shughuli za kiuchumi na kijamii. 

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Desemba 27, 2025 imeeleza kuwa mvua hiyo itanyesha katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Kigoma, Katavi, Singida, Dodoma, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa.

Mikoa mingine ni Njombe, Morogoro, Ruvuma, Tanga, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia.

Wananchi wanaoishi katika maeneo tajwa, hususan walioko mabondeni na maeneo hatarishi, kuchukua tahadhari za mapema ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.

TMA imewasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na utabiri wa hali ya hewa unaotolewa mara kwa mara ili kupata taarifa sahihi na za wakati.

0 Comment

Mbegu kutoka ukeni baada ya tendo chanzo chake na TibaAfyaclass Bongo Social •

Mbegu kutoka ukeni baada ya tendo chanzo chake na Tiba

Tatizo la mbegu kutoka nje ya Uke baada ya tendo la ndoa chanzo kikubwa ni nini



Tatizo la mbegu kutoka nje baada ya tendo la ndoa ni jambo linalowahusu wanandoa au wapenzi wengi, hasa wale wanaojaribu kupata mtoto. Kwa kawaida, baada ya mwanaume kumwaga mbegu ndani ya uke, ni kawaida kiasi kidogo cha shahawa kurudi nje. Hata hivyo, ikitokea kiasi kikubwa kinatoka mara kwa mara, inaweza kuwa sababu ya kushindwa kupata mimba, japo si mara zote.

Sababu Zinazowezekana za Mbegu kutoka Nje:

  1. Mwili wa mwanamke kuwa wima haraka baada ya tendo
    – Kusimama au kwenda bafuni mara moja baada ya tendo kunaweza kusababisha mbegu kutoka kabla hazijaingia ndani vizuri.

  2. Shughuli ya misuli ya uke
    – Misuli ya uke inaweza kushindwa kuzuia mbegu ndani, hasa kama hakuna mshikamano mzuri wa misuli ya nyonga.

  3. Wingi wa shahawa
    – Wakati mwingine, kama mwanaume anatoa shahawa nyingi kupita kiasi, ni kawaida nyingine kutoka nje kwa sababu nafasi ya uke haitoshi kuziweka zote mara moja.

  4. Kutoingia kwa uume vizuri
    – Ikiwa uume haujaingia vizuri au tendo limefanyika kwa haraka sana, mbegu huweza kumwagwa karibu na mlango wa uke na kutoka kirahisi.

  5. Uwezekano wa matatizo ya mlango wa kizazi
    – Kama mlango wa kizazi (cervix) hauko katika nafasi nzuri ya kupokea mbegu (mfano mwanamke akiwa juu), mbegu haziwezi kuelekezwa vizuri ndani.

Je, hali hii ni tatizo kubwa?

Kwa kawaida, si tatizo kubwa na haitoshi peke yake kueleza kuwa Sababu ya Mwanamke kutokubeba mimba ingawa inaweza kuchangia pia. Kwa Wanawake wengi, kiasi cha mbegu kinachobaki ndani kinatosha kabisa kwa ajili ya kurutubisha yai. Kwa hiyo, ikiwa mnaendelea kufanya tendo mara kwa mara katika kipindi cha ovulation, kuna uwezekano mkubwa wa kushika mimba.

Njia za kusaidia kupunguza tatizo hili:

  1. Kubadilisha mikao ya tendo la ndoa:
    – Mikao kama mwanamke akiwa chini (missionary style) inasaidia mbegu kuingia zaidi na kukaa kwa muda mrefu.

  2. Kubaki umelala kwa mgongo baada ya tendo:
    – Mwanamke abaki amelala dakika 15–30 baada ya tendo, akiegesha mto chini ya nyonga ili mbegu ziende juu kuelekea kwenye kizazi.

  3. Epuka kusimama au kuoga haraka baada ya tendo

  4. Tumia mazoezi ya nyonga (Kegel exercises)
    – Husaidia kuimarisha misuli ya uke na kuzuia mbegu kutoka kwa haraka.

Wakati wa Kumwona Daktari:

Fikirieni kuonana na daktari au mtaalamu wa afya ya uzazi iwapo:

  • Mmejaribu kupata mimba kwa zaidi ya miezi 12 bila mafanikio.
  • Kuna dalili nyingine kama maumivu wakati wa tendo, kutokwa na uchafu usio wa kawaida, au hedhi isiyo ya kawaida.
  • Unashuku tatizo la uzazi kwa mmoja wenu.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Dawa ya gonorrhea,Dawa ya gono,Dawa ya Kutibu Kisonono Afyaclass Bongo Social •

Dawa ya Kutibu Kisonono Kabsa,Wengi Mnaita Gono

Je, ni Ipi dawa sahihi ya kutibu Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)?

Kisonono ni ugonjwa wa Zinaa ambao husabababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae,

Ugonjwa huu wa kisonono ndyo hujulikana kama Gonorrhea au kwa kifupi wengi hupenda kuita “Gono”, Soma Zaidi hapa;

Dalili za Ugonjwa wa Kisonono au Gono

Kwa Wanawake:

1. Kutokwa na Usaha au uchafu usio wa kawaida kwenye uke (unaoweza kuwa na rangi ya njano au kijani).

2. Kupata Maumivu au kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa.

3. Kupata Maumivu chini ya tumbo

4. Kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi au baada ya tendo la ndoa.

5. Kupata Maumivu kwenye sehemu ya haja kubwa (ikiwa eneo hilo limeathiriwa). n.k

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;

- Kutokwa na usaha kwenye Uume

- Uchafu wa majimaji meupe, ya njano, au ya kijani kutoka kwenye uume.

- Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita

- Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation

- Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko

- Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu

- Kupata maumivu kwenye korodani.

- Kupata Maumivu au uvimbe katika sehemu ya haja kubwa (ikiwa maambukizi yameathiri eneo hilo).

- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa n.k.

Dawa ya Kutibu Kisonono

Dawa za kisonono au Gono huweza kutibu kabsa tatizo hili likaisha ikiwa umepata tiba Sahihi na hujakutana na mazingira hatarishi ya kupata maambukizi haya tena baada ya Tiba.

Ni muhimu sana kupata Maelekezo kamili kutoka kwa Wataalam wa afya Wakati wa Kutumia Dawa za kutibu kisonono kwani badala ya kutibu Kisonono unaweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama “Usugu wa Dawa” ambapo vimelea hivi vya bacteria hutengeneza usugu kwenye dawa-Antimicrobial resistance”

Kwa hivi Sasa,Ukinzani huu kwenye Ugonjwa wa kisonono unazidi Kuongezeka, Hali ambayo hupelekea dawa ya Kutibu kwa mafanikio Ugonjwa wa Gono au kisonono Kuzidi kuwa Ngumu kuipata.

Hivo ni muhimu sana baada ya kupata dalili za gono au kugundulika una ugonjwa wa Kisonono, hakikisha unapata dawa ya Kisonono ambayo ni sahihi kwa tatizo lako, Usijaribu kila aina ya Dawa.

Hauhitaji Jaribio la kutibu ugonjwa wa Kisonono – ufuatiliaji wa dawa ya Kisonono au matibabu Sahihi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametibiwa kwa ufanisi – Ni muhimu Zaidi.

Ikiwa dalili za mtu zinaendelea kwa zaidi ya siku chache baada ya kupokea matibabu, anapaswa kurudi kwa mtoa huduma wa afya ili kutathminiwa upya,

Kuhusu Kipindi cha Matibabu:

Wagonjwa wanaotibiwa maambukizi ya koo wanashauriwa kufanyiwa kipimo cha uhakiki wa tiba (test of cure) siku 7–14 baada ya matibabu, kwa sababu koo ni eneo gumu zaidi kuponya maambukizi.

Kwa wagonjwa wengine (wasio na maambukizi ya koo), matibabu kwa dozi moja ya sindano mara nyingi hutosha, na hakuna haja ya kipimo cha uhakiki wa tiba isipokuwa dalili zitaendelea au maambukizi yawe sugu.

wanaume na wanawake walio na ugonjwa wa gono au kisonono wanapaswa kupimwa tena miezi mitatu baada ya matibabu ya maambukizi ya awali, bila kujali kama wanaamini kwamba wenzi wao walitibiwa kwa mafanikio.

Dawa ya gono;

Kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa “The Centers for diseases control and Prevention- CDC”

Wanashauri kwenye matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono au Gono; dawa ambapo huweza kutumika ni pamoja na;

  • Sindano
  • Na Vidonge

Ingawa dawa hizi Zitazuia maambukizi ya Gono hazitaweza kurudisha madhara yoyote yaliyosababishwa na Ugonjwa huu wa Kisonono au Gono.

NB: Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwa kina kabla ya kutumia dawa yoyote ya Gono ili kupata maelekzo sahihi kulingana na hali yako.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Imani Dia Smith Muigizaji wa Disney The Lion King afariki dunia nyumbani kwakeAfyaclass Bongo Social •

Imani Dia Smith, anayejulikana zaidi kwa kuigiza nafasi ya Young Nala kwenye filamu ya Disney The Lion King, amefariki dunia katika tukio linalochunguzwa kama mauaji.

Kwa mujibu wa polisi, mwili wake ulipatikana Desemba 21, 2025 nyumbani kwake mjini Edison, New Jersey, baada ya mamlaka kuitikia wito wa dharura. Alikimbizwa hospitalini lakini alithibitishwa kufariki dunia muda mfupi baadaye. Wakati wa kifo chake, Smith alikuwa na miaka 25.

Polisi wamemtaja mpenzi wake, Jordan D. Jackson-Small (miaka 35), kama mshukiwa mkuu katika tukio hilo, na tayari amekamatwa kwa ajili ya hatua za kisheria huku uchunguzi ukiendelea.

Kifo cha Imani Dia Smith kimeacha majonzi makubwa kwa familia, mashabiki na jamii, wengi wakimkumbuka kama msanii mwenye kipaji kikubwa, mwenye ndoto na maono muhimu aliyoanza tangu akiwa mtoto jukwaani Broadway.

0 Comment

Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutokaAfyaclass Bongo Social •

Ongeza kumtafuta Mungu 2026,hii ndyo akili ya kutoka

Mtu anayemtafuta Mungu ndye mwenye akili kuliko wote, Lakini Shetani hupofusha Fikra za Watu kwa nguvu Zote ili waone kumtafuta Mungu ni kupoteza muda,Kukosa cha kufanya,Kuwa Maskini n.k..

"Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu(Zaburi 14:2)".

Fikra Zako zifunguke Katika Jina la Yesu,Uuone Ukuu wa MUNGU kuliko ngome za mawazo anazojenga adui kwenye fikra zako, angusha ngome hizo,Na Mungu aweke Kiu ndani yako ya kumtafuta kwenye Kila Jambo.

Aweke Kiu kama ya Daudi,anasema katika Zaburi 27:4 "Neno Moja nimelitaka kwa Bwana, Nalo ndilo nitakalolitafuta, Nikae nyumbani mwa Bwana Siku zote za maisha yangu, Niutazame uzuri wa Bwana, Na kutafakari hekaluni mwake".

0 Comment

Mimba kuharibika husababishwa na nini Afyaclass Bongo Social •

Tatizo la mimba kuharibika,Sababu kubwa ni hizi hapa



Zifuatazo ni Baadhi ya Sababu Zinazochangia Kutokea kwa Tatizo hili la Mimba kuharibika au kutoka Zenyewe;

1. Matatizo yanayotokana na Mfumo mzima wa Kijenetiki ambapo kitaalam hujulikana kama-Genetics Abnormalities,tatizo hili huchangia mimba kuharibika hasa hasa katika kipindi cha Miezi mitatu(3) ya Mwanzoni.

2. Matatizo katika Via vya Uzazi vya Mwanamke kama Vile;

  • Kulegea kwa shingo ya kizazi hivo kushindwa kuhimili kushikilia ujauzito hatimaye ujauzito kutoka wenyewe, 
  • Matizo kama Vile Uvimbe kwenye kizazi n.k

3. Tatizo la Mvurugiko wa Vichocheo vyako vya Mwili ambapo kitaalam hujulikana kama Hormone Imbalance

4. Uwepo wa Magonjwa mbali mbali kipindi cha Ujauzito kama vile; 

  • Ugonjwa wa kisukari, 
  • Kifafa cha Mimba,
  • Shinikizo la Damu,
  • Ugonjwa wa Goita
  • Pamoja na maambukizi mengine kama vile ya Rubella.

5. Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo ni hatari kipindi cha Ujauzito kama vile,

  • matumizi ya dawa za Msongo wa mawazo mfano; paroxetine au venlafaxine

TABIA HATARISHI ZA KUPATA TATIZO LA MIMBA KUTOKA ZENYEWE

- Matumizi ya vilevi kama vile Pombe

- Uvutaji wa Sigara

- Matumizi ya vinywaji venywe Caffeine Nyingi

- Matumizi ya Dawa kiholela au Ovio bila kupewa maelekezo na wataalam wa afya n.k.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Video ya safina iliyojengwa na Mchungaji wa Ghana anayedai Mungu anataka kuiharibu dunia kwa mafuriko kama vile siku za NuhuAfyaclass Bongo Social •

Video ya safina iliyojengwa na Mchungaji wa Ghana anayedai Mungu anataka kuiharibu dunia kwa mafuriko kama vile siku za Nuhu

Video ya safina iliyojengwa na Mchungaji wa Ghana anayedai Mungu anataka kuiharibu dunia kwa mafuriko kama vile siku za Nuhu

Tamthilia inajitokeza nchini Ghana kufuatia kusambazwa kwa video inayoonyesha safina inayodaiwa kujengwa na mchungaji wa Ghana anayedai Mungu amefichua kwamba dunia itaharibiwa na mafuriko, sawa na simulizi ya kibiblia ya Nuhu.

Mchungaji huyo, anayetambuliwa kama Nabii Eboh Noah, ameripotiwa kujenga safina nane na kuonya kwamba ni wale tu walio ndani yake ndio watakaookolewa wakati mafuriko yanayotarajiwa yatakapotokea. Unabii huo, ambao anasema utatimizwa Desemba 25, umesababisha hofu, udadisi, na athari kubwa mtandaoni na nje ya mtandao.

Ripoti zinaonyesha kwamba idadi kubwa ya Waghana wamekuwa wakimiminika kwenye eneo hilo katika juhudi za kupata nafasi ndani ya safina kabla ya "hukumu duniani" iliyotabiriwa. Video na picha zilizoshirikiwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha umati wa watu ukikusanyika kuzunguka majengo hayo, na kuchochea mjadala na wasiwasi kote nchini.

0 Comment

New:Afyaclass Disease List 2025,Orodha ya Magonjwa Yaliyosumbua sana Dunia 2025Afyaclass Bongo Social •

Hapa ni orodha ya magonjwa na matatizo ya kiafya yaliyosumbua sana dunia mwaka 2025, ikijumuisha magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza pamoja na milipuko mikubwa iliyoripotiwa na Shirika La afya duniani: Katika Orodha hii namba si chochote,Wala haya sio magonjwa yote ni baadhi tu;


Magonjwa ya Kuambukiza (Infectious Diseases)

1. Ugonjwa wa kifua kikuu-Tuberculosis(TB)

Bakteria wanaosababisha ugonjwa wa mapafu,Kifua kikuu au TB bado ni tishio kubwa na inasababisha maelfu ya vifo kila mwaka.

2. COVID-19 na Mawimbi ya Virusi Vipya

Ingawa si Ugonjwa mpya kama awamu ya 2020, bado COVID-19 na mabadiliko ya virusi vyake yanachangia vifo na ugonjwa huu kuenea kote duniani.

3. Ugonjwa wa Surua (Measles)

Kupungua kwa chanjo kumeleta kuongezeka kwa kesi za Ugonjwa wa Surua, hasa miongoni mwa watoto.

4. Ugonjwa wa Kipindupindu(Cholera)

Milipuko mikubwa ya Ugonjwa wa Kipindupindu imeendelea katika nchi nyingi, ikisababisha maambukizi na vifo vingi, hasa maeneo yenye maji na usafi duni.

5. Ugonjwa wa Homa ya Dengue

Dengue bado inasababisha maambukizi makubwa katika nchi 90 na inaripotiwa visa vingi zaidi ya milioni kadhaa.

6. Ugonjwa wa Homa ya Nyani-Mpox (Monkeypox)

Milipuko ya mpox (pia inajulikana kama monkeypox) imeendelea kufuatilia dunia tangu 2023–2025 kama janga la kiafya la kimataifa.

7. Ugonjwa wa Malaria

Ingawa kuna mafanikio ya kudhibiti malaria, milipuko bado inatokea na inasababisha vifo hasa kwa watoto.

Magonjwa Makubwa Yasiyo ya Kuambukiza (Non-Communicable Diseases, NCDs)

Magonjwa haya ndio yanayosababisha vifo vingi zaidi duniani, mara nyingi kutokana na mtindo wa maisha, lishe mbaya, Uvutaji wa sigara, na uchafuzi wa hewa:

1. Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu (Cardiovascular Diseases)

Mfano wa magonjwa hayo yanayoathiri moyo ni pamoja na;

  • Shambulio la Moyo(Heart attack):Ugonjwa wa moyo kama vile mshtuko wa moyo(Heart attack) ni chanzo kikuu cha vifo duniani.
  • Ugonjwa unaoathiri mishipa ya damu ndani ya moyo mfano; Coronary artery diseases.
  • Tatizo la mapigo ya moyo kutokueleweka-Irregular heartbeats (arrhythmias)
  • Tatizo kwenye muundo wa moyo ambapo unazaliwa nalo (congenital heart defects)
  • Tatizo la moyo kutanuka
  • Tatizo la Moyo kujaa maji
  • Ugonjwa wa kwenye misuli ya Moyo
  • Ugonjwa wa kwenye Valve za moyo
  • Ugonjwa wa kwenye mfumo wa umeme ndani ya moyo n.k

2. Saratani mbali mbali (Cancers)

Saratani ni mojawapo ya ugonjwa mbaya unaoongoza kwa vifo duniani.

Saratani zilizoongoza kutokea

Saratani Zinazoongoza kwa Vifo Duniani:

(i). Saratani ya Mapafu: (1.8 million deaths, 18.7% of the total cancer deaths)

Sababu kuu ya vifo vya saratani duniani kote, kwa jinsia zote mbili kwa pamoja

(ii). Saratani ya utumbo mpana:(colorectal cancer (900 000 deaths, 9.3%)

Sababu kuu ya vifo vya saratani.

(iii). Saratani ya Ini: liver cancer (760 000 deaths, 7.8%)

Muuaji mkuu, haswa katika sehemu za Asia.

(iv). Saratani ya Matiti:breast cancer (670 000 deaths, 6.9%)

Sababu kuu ya vifo vya saratani kwa wanawake.

(v). Saratani ya Tumbo:stomach cancer (660 000 deaths, 6.8%).Sababu nyingine kuu ya vifo vya Saratani.

3. Ugonjwa wa Kisukari (Diabetes)

Ambapo ugonjwa huu pia huweza Kusababisha matatizo mengine ya kiafya kama vile:

  • Tatizo la figo, 
  • matatizo ya macho 
  • na mishipa ya damu. n.k

4. Magonjwa ya kudumu ya mfumo wa Upumuaji

Mfano wa magonjwa ya Mfumo wa Upumuaji(Common Types of Respiratory Diseases)

  • Ugonjwa wa asthma ni miongoni mwa magonjwa mengine makubwa yasiyo ya kuambukiza.
  • Chronic Obstructive Pulmonary Disease (COPD):
  • Ugonjwa wa Pneumonia
  • Saratani ya Mapafu(Lung Cancer):
  • Cystic Fibrosis (CF)
  • Ugonjwa wa Tuberculosis (TB)
  • Bronchitis & Bronchiolitis n.k...

5. Matatizo ya Afya ya Akili (Mental Health Conditions)

Matatizo ya Afya ya akili yamekuwa chanzo kikuu cha Ulemavu na Vifo Duniani,Zaidi ya mamilioni ya watu duniani wanaishi na shida za afya ya akili kama vile: 

  • Msongo wa mawazo(Stress)
  • na wasiwasi(Anxiety disorders)
  • Huzuni na Mfadhaiko(depression)
  • Bipolar disorder.
  • Post-Traumatic Stress Disorder (PTSD)
  • Schizophrenia. 
  • Eating disorders.n.k....

Muhtasari

Mwaka 2025, dunia ilikumbana na magonjwa makubwa ya kuambukiza pamoja na kuendelea kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo ndio chanzo kikuu cha vifo duniani. Kupunguza mzigo wa magonjwa haya kunahitaji chanjo, maji safi na usafi kwa ujumla, lishe nzuri, utunzaji bora wa afya ya akili, na sera madhubuti za afya ya umma.

Verified Sources Used: 

  • Shirika la Afya Duniani(WHO),
  • Afyaclass disease List,
  • Health and Me,
  • Wikipedia,

0 Comment

Hii ni Orodha ya Mitandao ya kijamii iliyotumiwa zaidi Tanzania 2025Afyaclass Bongo Social •

Kufikia Septemba 2025, Watanzania milioni 56.3 wameunganishwa na huduma ya intaneti huku takriban Watanzania milioni 26.9 wakirekodiwa kutumia simu janja.

Dar es Salaam. Mitandao ya kijamii ni miongoni mwa nyenzo za mawasiliano zinazotumiwa zaidi siku za hivi karibuni, ikisaidia kuwaunganisha watu kutoka maeneo mbalimbali, kubadilishana mawazo, taarifa na uzoefu kwa haraka na kwa urahisi.

Pamoja na kuwaungaisha watu, mitandao hiyo imekuwa fursa kwa vijana kujiajiri na kutunisha mifuko yao kiasi cha kufanya baadhi zao kutumia muda mwingi zaidi katika mitandao hiiyo na kusahau kujichanganya na wanajamii.

Ripoti ya takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) za robo ya tatu (Juni -Septemba)  ya mwaka 2025 inabainisha kuwa Watanzania milioni 56.3 wameunganishwa na huduma ya intaneti kufikia Septemba mwaka huu.

Kati ya watumiaji hao, milioni 26.9 waliunganishwa kupitia simu janja (Simu a rununu 58,850,493), (Modemu 743,376), (vishkwambi 544,888) pamoja na magari (8,539).

Facebook kinara wa matumizi

Kwa vijana wa zamani watakumbuka kuwa facebook ilikuwa mtandao wa kwanza maarufu kutumiwa zaidi nchini Tanzania ukijizolea umaarufu hata kwa watu ambao taratibu wanaanza kukaribia ‘kula chumvi nyingi’.

Hata hivyo, bado Facebook imeendelea kushika kinara ikiwa na watumiaji milioni 6.79 ikiwaacha nyuma washindani wake ambao wanaaminika kupendwa zaidi na kizazi kipya yaani Gen Z.

Idadi hiyo ya watumiaji wa Facebook ni sawa na kusema asilimia 9.7 ya Watanzania wote waliopo nchini kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Watumiaji hao wa Facebook waliongezeka kwa asilimia 19.5 kati ya mwaka 2024 na mwanzoni mwa mwaka 2025. 

Instagram 

Instagram ni mtandao wa kijamii unaolenga zaidi matumizi ya picha na video, na umekuwa chaguo maarufu sana miongoni mwa Watanzania. Watumiaji wengi huutumia kuonyesha maisha yao ya kila siku, kushirikisha matukio muhimu.

Takwimu za DataReportal zinabainisha kuwa mtandao huo kwa mwaka 2025 uliuwa na watumiaji milioni 3.7 wakiongezeka kwa asilimia 5.7 kutoka idadi ya watumiaji iliyorekodiwa mwaka uliopita.

Mbali na mtandao huo kutumiwa kwa ajili ya mawasiliano, umekuwa ukitumiwa pia kukuza biashara kama anavyobainisha Cletus Mboya (20) anayejihusisha na uuzaji wa simu kariakoo, Dar es Salaam. 

“Kwa siku, wateja ninaopata (kupitia mtandao wa instagram)  ni wengi zaidi kuliko wale wanaoniona kwa macho wakipita dukani,” anaeleza Mboya.

Linkedin

Kwa wamiliki wa kampuni, wajasiriamali na wanaotafuta ajira huenda wakawa wameutumia zaidi mtandao wa Linkedin na kuufanya kuwa miongoni mwa mitandao yenye idadi kubwa ya watumiaji mwaka 2025.

Meta inabainisha kuwa watu milioni 1.5 sawa na asilimia 2.2 ya Watanzania walitumia Linkedin mwanzoni mwa mwaka 2025, idadi inayodhihirisha ongezeko la uelewa wa matumizi ya mitandao huo kitaaluma. 

Messenger

Messenger, jukwaa hili linaendelea kutumika zaidi kama chombo cha mawasiliano ya haraka kati ya watu binafsi, familia na wafanyabiashara.

Takwimu zinaonyesha kuwa Messenger ilikuwa na watumiaji takribani milioni 1.3 nchini. Kati ya watumiaji hao, wanawake walikuwa asilimia 37.1 na wanaume asilimia 62.9.

Watumiaji wengi hutumia Messenger kubadilishana ujumbe wa maandishi, sauti na picha kwa wakati halisi, kurahisisha mawasiliano ya kila siku bila hitaji la kupiga simu. 

X jukwaa la mijadala 

Licha ya kuwa na idadi ndogo ya watumiaji ikilinganishwa na mitandao mingine, mtandao wa X (zamani Twitter) umeendelea kuwa jukwaa lenye ushawishi mkubwa Tanzania katika uundaji wa hoja na mjadala wa umma, hasa miongoni mwa wanahabari, wanasiasa, wachambuzi na watumiaji wanaopenda maudhui ya habari na hoja.

Mpaka kufikia mwanzoni mwa mwaka 2025, X ilikuwa na watumiaji 666,000, ikiongezeka kwa 7.2, wanaume wakiwa ni  asilimia 87.7 ya na wanawake asilimia 12.3.

0 Comment

Mgongo Kuwaka Moto,chanzo Na Matibabu YakeAfyaclass Bongo Social •

Tatizo hili la mgongo kuwaka moto hutokea kwa watu wengi na sio waafrika tu peke yake hata wazungu wengi husumbuliwa na shida hii ya mgongo kuwaka moto, soma hapa chini;

Kutokana na takwimu za Taasisi ya "National institute of Neurological disorders and strokes" huko marekani inasema kwamba,Asilimia 80% ya Wamarekani husumbuliwa na shida hii ya mgongo kuwaka moto kwenye vipindi flani tofauti vya maisha kwa kila mtu,

Je shida hii ya mgongo kuwaka moto chanzo chake ni nini?, Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha mtu kupata shida hii ya mgongo kuwaka moto,

CHANZO CHA TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO NI PAMOJA NA;

1. Mtu kufanya kazi ambazo zinahusu kukaa kwenye vyanzo vya moto kwa muda mrefu,kama vile kazi za kupika,kuchomelea,au mtu kuchomwa na jua sana au kuunguzwa na moto

2. Ugonjwa unaotokea kwenye pingili za uti wa mgongo maarufu kama Degenerative Disc disease, kutokana na sababu mbali mbali kama vile: pingili kusagika, pingili za uti wa mgongo kuzeeka(aging) n.k

3. Shida ya Misuli kukaza kuliko kawaida yaani Muscle strains

4. Shida ya nerves eneo la uti wa mgongo kubanwa zaidi yaani Spinal cord nerves compression

5.Mtu kupata majeraha yoyote au kuumia kwenye uti wa mgongo

6. Mtu kupatwa na shida ya uvimbe unaotokea eneo la uti wa mgongo au spinal cord tumor

7. Uharibifu wa Mfumo wa Nerves kutokana na matumizi ya pombe kupita kiasi,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Alcohol Neuropathy

8. Uharibifu wa Mfumo wa Nerves kutokana na ugonjwa wa Kisukari,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Diabetic Neuropathy

9. Mtu kuwa na tatizo la upungufu wa vitaminis(Vitamin deficiency) ambapo huleta shida kwenye mgongo ikiwemo kwenye nerves pamoja na shida hii ya mgongo kuwaka moto

10. Mtu kupata shida ya mgongo kuwaka moto kutokana na mfupa wowote eneo la mgongoni kuvunjika

11. Uwepo wa Maambukizi kuzunguka eneo la uti wa mgongo nakusababisha shida kama vile Epidural abscess

12. Kuvimba kwa ubongo kutokana na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile Virusi, hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Encephalitis,au mtu kupatwa na mashambulizi ya herpes Zoster n.k

13. Uwepo wa magonjwa ambayo huathiri ubongo pamoja na uti wa mgongo kama vile Multiple Sclerosis n.k

14. Uwepo wa tatizo la Rheumatoid arthritis,ambapo huhusisha mashambulizi ya kinga yako ya mwili mwenyewe yaani Autoimmune disease na kusababisha matatizo kama vile joint kuvimba,mgongo kuwaka moto n.k

15. Shida ya mwili kuzishambulia seli pamoja na Tisu na kusababisha matatizo kama vile Systemic Lupus Erytheimatosus disorder

16. Tatizo la kwenye nerves ambalo huhusisha kuvimba kwa uti wa mgongo,shida hii kwa kitaalam hujulikana kama Transverse Myelitis(Neurological disorder)

MATIBABU YA TATIZO LA MGONGO KUWAKA MOTO

Kama nlivyokwisha kuelezea baadhi ya sababu za tatizo hili la mgongo kuwaka moto,Na matibabu yake hutegemea na chanzo husika, hivo kwa ujumla wake, Mfano;

kama mgonjwa anapata shida ya mgongo kuwaka moto kutokana na upungufu wa Vitamins(Vitamin deficiency) ambazo hupelekea shida kwenye nerves za uti wa mgongo,

Basi shida hii huweza kuhusisha matibabu ya matumizi ya dawa jamii ya Neuroton pamoja na Dawa zingine ambazo zitasaidia shida hii n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Familia kutoa ubongo wake kwa ajili ya utafitiAfyaclass Bongo Social •

Familia ya muigizaji wa Hollywood, Bruce Willis, imetangaza uamuzi wa kugusa Kwa kutoa ubongo wake kwa ajili ya utafiti wa kisayansi baada ya kifo chake. Willis alilazimika kustaafu kazi ya uigizaji baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa frontotemporal dementia (FTD), unaoathiri lugha, tabia na uwezo wa kufikiri.

Mke wake, Emma Heming-Willis, amesema uamuzi huo haukuwa rahisi kihisia, lakini ni muhimu kwa maendeleo ya tafiti zitakazosaidia wanasayansi kuelewa ugonjwa huo kwa undani zaidi.

Familia ina matumaini kuwa mchango huo utasaidia wagonjwa wengine na familia zinazopitia changamoto kama zao.

Hatua hii imepokelewa kama ishara ya matumaini na mshikamano, ikionyesha namna maumivu binafsi yanavyoweza kubadilishwa kuwa mchango wenye manufaa kwa jamii na sayansi.

0 Comment

Homa ya Ini ina Dalili Zipi? Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

 Ugonjwa Wa Homa Ya Ini(Hepatitis): Sababu, Dalili, Matibabu, na Kinga

Ugonjwa wa homa ya ini ni ugonjwa hatari wa ini ambao husababisha uvimbe na uharibifu wa ini. Ugonjwa huu husababishwa na virusi, kemikali, na magonjwa mengine. Katika makala hii, tutajifunza zaidi kuhusu sababu, dalili, matibabu, na kinga ya ugonjwa wa homa ya ini.

Wakati Ini linapovimba au kuharibiwa huathirika kiutandaji pia,hivo kazi zote zinazofanywa na kiungo hiki muhimu huathiriwa pia, Matumizi ya Pombe kupita kiasi,Sumu(toxins),baadhi ya dawa au matatizo kadhaa ya kiafya huweza kusababisha tatizo la Ini kuvimba(hepatitis).  Soma zaidi hapa.!!

Sababu ya Ugonjwa Wa Homa Ya Ini:

Ugonjwa wa homa ya ini husababishwa Zaidi na virusi wa aina tatu:

  1. virusi vya hepatitis A,
  2. hepatitis B,
  3. Pamoja na hepatitis C. Ingawa kuna aina nyingine kama vile
  4. hepatitis D
  5. na hepatitis E

Vilevile, kemikali, pombe, na baadhi ya dawa zinaweza kusababisha ugonjwa huu wa kuvimba kwa Ini(hepatitis).

Sababu nyingine ambazo huongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa homa ya Ini ni pamoja na:

  • Kuchora tatoo au kupasua mwili kwa vifaa visivyo visafi
  • Kupokea damu au viungo vya mwili visivyo safi
  • Kufanya mapenzi bila kinga/condom
  • Kugusana na damu,jasho au maji maji yoyote ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu
  • Kutumia sindano zisizo safi au vifaa vingine vyenye ncha kali n.k

Kwa Ujumla,Njia nyingi ambazo unaweza kupata ugonjwa wa homa ya Ini, zinafanana kabsa na njia ambazo unaweza kupata Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Dalili za Ugonjwa Wa Homa Ya Ini:

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na:

  1. Kupata Homa kali
  2. Kuhisi uchovu sana
  3. Kuhisi Kichefuchefu na kutapika
  4. Kupata Maumivu ya tumbo
  5. Viungo kuuma au kupata muwasho
  6. Kuharisha
  7. Kupoteza hamu ya kula
  8. Ngozi na macho kuwa na rangi ya njano
  9. Mkojo kuwa mweusi n.k

Matibabu ya Ugonjwa Wa Homa Ya Ini (Hepatitis):

Matibabu ya ugonjwa wa homa ya ini hutofautiana kulingana na aina ya virusi vya hepatitis.

• Kwa hepatitis A, hakuna tiba maalum, lakini dalili hupungua kwa muda wa wiki nne hadi sita.

• Kwa hepatitis B na hepatitis C, tiba inapatikana, lakini kadri unavyochelewa kupata Tiba ndivo inavyokuwa ngumu zaidi kupona.

Kinga ya Ugonjwa Wa Homa Ya Ini:

Kuna hatua kadhaa unazoweza kuchukua ili kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini, na hatua hizo ni pamoja na:

✓ kupata Chanjo ya Kuzuia ugonjwa wa homa ya Ini,

•Soma Zaidi hapa Kuhusu Chanjo ya ugonjwa wa Homa ya ini

✓ Kuepuka kugusana na damu,jasho,mate au maji maji yoyote ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu

✓ Kuepuka ngono isiyo salama au Kutumia kondomu wakati wa kufanya mapenzi

✓ Kupata chanjo ya hepatitis A na hepatitis B

✓ Kuhakikisha kwamba vifaa vya tiba na vipimo vya damu ni safi

✓ Kuepuka kutumia dawa bila ushauri wa daktari

✓ Kuepuka matumizi ya pombe kabsa au kutumia kwa kiasi kidogo

FAQs:

Je! Ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis) ni hatari kwa afya yangu?

Ndio, ugonjwa wa homa ya ini ni hatari kwa afya yako na unaweza kusababisha uharibifu mkubwa wa ini ikiwa haikutibiwa.

Je! Ni njia zipi za kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis)?

Kujikinga na ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na kupata chanjo, kuepuka kugusana na damu,jasho, mate au maji maji ya mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu, kutumia kondomu wakati wa tendo la ndoa, na kuepuka matumizi ya pombe au kutumia kwa kiasi kidogo.

Je! Ni dalili zipi za ugonjwa wa homa ya ini (hepatitis)?

Baadhi ya dalili za ugonjwa wa homa ya ini ni pamoja na homa kali, kuhisi uchovu sana, kichefuchefu na kutapika, maumivu ya tumbo,ngozi na macho kuwa na rangi ya njano,kukojoa mkojo mweusi n.k.

SOMA ZAIDI HAPA kuhusu Ugonjwa huu wa Homa ya Ini

Ugonjwa Wa Homa Ya Ini(Hepatitis)

Ugonjwa wa Homa ya Ini ni Ugonjwa unaoshambulia kiungo muhimu mwilini kinachojulikana kama INI, ambapo WANAWAKE wakiwa miongoni mwa kundi linaloshambuliwa sana na Ugonjwa huu. Ifahamike kwamba Ini linafanya kazi zaidi ya 500 katika miili yetu ikiwa ile ya kupambana na sumu yaani Untoxification,na kuchuja damu mwilini.

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kufanya ini lisifanye kazi vizuri,au livimbe ambapo hii ndyo huitwa Hepatitis kitaalam,Mfano; Unywaji wa pombe kupita kiasi,maambukizi ya magonjwa, VIRUSI au uwepo wa sumu kwenye damu,vitu hivi vinaweza kuathiri utendaji kazi wa Ini.

MAKUNDI YA VIRUSI VINAVYOLETA HOMA YA INI (HEPATITIS)

Tafiti zinaonyesha kwamba,kwa AFRIKA,Maambukizi ya Homa ya Ini,ndiyo shida kubwa inayosumbua ini kuliko matatizo mengine kwenye Ini.

Kuna Aina Tano;
(1) HEPATITIS A

(2) HEPATITIS B✔️

(3) HEPATITIS C

(4) HEPATITIS D

(5) HEPATITIS E

Ambapo hepatitis B na C zikiongoza kwa kuwa sababu kuu za kusambaa ugonjwa wa homa ya ini na husambaaa kwa njia kuu ya Damu pamoja na majimaji yanayotoka mwilini mwa mgonjwa, mfano jasho,mate,mkojo,machozi,Mbegu za kiume n.k

Hepatitis B peke yake,inakadiriwa kuwa, husababisha vifo kwa Takiribani watu 600,000 hivi kwa kila mwaka kutokana na Takwimu za Vifo DUNIANI. Na zaidi ya watu billion mbili sawa na asilimia 33% ya watu wote Duniani wameshaambukizwa virusi hivi vya Homa ya ini (Hepatitis B)

VIRUSI HIVI HUSAMBAA KWA NJIA GANI (HEPATITIS B NAC)?

Chanzo kikubwa cha kusambaa kwa maambukizi haya ni kwa Njia ya Damu,au majimaji kutoka kwa mgonjwa mfano; jasho lake,mate,mkojo,machozi,mbegu za kiume n.k na Hatari ya virusi hivi ni kwamba vina nguvu ya kuathiri au kushambulia mtu mara 100 zaidi ya virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI.

NJIA AMBAZO MTU ANAWEZA KUPATA VIRUSI HIVI

NB; Njia zote ambazo virusi vya ukimwi husambaa,ndyo njia hizo hizo virusi vya Homa ya Ini Husambaaa.

(1) Mama mwenye virusi hivi anaweza kuvisambaza kutoka kwake kwenda kwa mtoto wakati wa Kujifungua ambapo uwezekano ni mkubwa zaidi ya asilimia 90% kama kusipochukuliwa tahadhari thabiti

(2) Kushiriki tendo la Ndoa na Mtu mwenye virusi hivi vya Homa ya Ini

(3) Kushare vifaa vyenye ncha kali kama wembe,sindano,miswaki n.k

(4) Kuongezewa damu ya Mtu mwenye virusi vya Ugonjwa huu wa Homa ya Ini

MDA AMBAO VIRUSI VYA HOMA YA INI HUWEZA KUISHI VIKIWA NJE YA MWILI

Virusi vya Homa ya Ini vinauwezo wa kukaa Nje ya mwili hadi siku 7 na bado vikawa na uwezo wa kuangia kwa mtu na kumuambukiza ugonjwa huu.

KUNDI LA WATU AMBAO WAPO KATIKA HATARI YA KUPATA UGONJWA HUU

(1) Watu wanaofanya Ngono zembe na pia wanashiriki kitendo hiki na watu wengi

(2) Watoto wanaozaliwa na mama mwenye ugonjwa huu wa Homa ya Ini

(3) Watu wanaotumia madawa ya kulevyia hasa aina ya Sindano

(4) Watu wanaoshiriki mapenzi ya Jinsia moja hasa wanaume

(5) Mtu mwenye mpenzi au mke mwenye virusi hivi

(6) Wagonjwa wenye magonjwa ya vigo ambao wanapata huduma ya kusafisha damu au kitaalam Dialysis

(7) Watumishi wote wa Afya

DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA INI

✓ kukojoa mkojo wenye rangi kama ya COCACOLA

✓Kupata rangi ya manjano katika maeneo tofauti ya mwili kama macho,mikono au mwili mzima ngozi hubalika rangi na kuleta rangi ya manjano

✓Hali ya kichefuchefu,kutapika,mwili kuchoka sana, na kukosa hamu kabsa ya kula chakula

Kumbuka; Maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Ini,huweza kuwa chanzo kikubwa cha kuleta Ugonjwa wa Saratani ya Ini.

Ni muhimu sana kupima kwa Ugonjwa huu ili kuwa salama zaidi, hasa kwa makundi hatarishi niliyoyataja hapo juu.

Hitimisho:

Ugonjwa wa homa ya ini ni ugonjwa hatari wa ini ambao husababisha uvimbe na uharibifu wa ini,Ugonjwa huu husababishwa na virusi, kemikali, na magonjwa mengine.

Ni muhimu kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja na kupata chanjo, kuepuka kugusana na damu,mate,jasho au maji maji yoyote ya mwili kutoka kwa mtu aliyeambukizwa ugonjwa huu, na kutumia kondomu wakati wa tendo la ndoa.

Kwa wale walio na dalili za ugonjwa wa homa ya ini, ni muhimu kutafuta matibabu haraka ili kuzuia uharibifu mkubwa wa ini.

KWA USHAURI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KUPITIA NAMBA +255758286584

0 Comment

Muigizaji wa The Wire James Ransone afariki akiwa na umri wa miaka 46Afyaclass Bongo Social •

Muigizaji wa The Wire James Ransone afariki akiwa na umri wa miaka 46 kutokana na kujiua

James Ransone, mwigizaji wa Marekani anayejulikana zaidi kwa kucheza Ziggy Sobotka katika mfululizo wa filamu maarufu ya HBO The Wire, amefariki akiwa na umri wa miaka 46.

Kulingana na taarifa rasmi za kitabibu muigizaji huyo alifariki Ijumaa huko Los Angeles. Mamlaka iliorodhesha chanzo cha kifo hicho kama kujiua. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.

Ransone ameacha mke wake, Jamie McPhee, na watoto wao wawili. Siku zilizofuata kabla ya kifo chake, McPhee aliongeza mchango wa kuchangisha fedha unaonufaisha Muungano wa Kitaifa wa Magonjwa ya Akili (NAMI) kwenye wasifu wake wa mitandao ya kijamii, Daily Mail iliripoti.

0 Comment

Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Afyaclass Bongo Social •

Waandishi wa Habari Kupimwa Moyo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

DAR-ES-SALAAM : TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  inatarajia kufanya upimaji wa siku mbili wa  magonjwa ya moyo bure kwa waandishi wa habari na Wahariri wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kundi hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi  Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge amesema upimaji huo maalum utafanyika Disemba 23 hadi 24 katika tawi la JKCI lililopo Ostabey ikiwa ni  sehemu ya utekelezaji wa ahadi aliyotoa kwa waandishi wa habari. 

"Tumekuwa tukifata watu mbalimbali ,mashirika na wadau kama wadau wa michezo,wasanii,wanafunzi wa shule za msingi,tulikutana na wahariri walipimwa afya ya moyo ilikuwa ni ahadi yangu kuwafikia waandishi wa habari kabla ya mwaka huu kuisha katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani kesho na kesho kutwa kuaanzia saa nne asubuhi hadi saa 10 tutanaanza kutoa huduma ,"amesisitiza Dk Kisenge.

0 Comment

Wanafunzi waliokuwa bado wametekwa nyara Nigeria waachiwa huruAfyaclass Bongo Social •

Wanafunzi waliokuwa bado wametekwa nyara Nigeria waachiwa huru

Watoto 130 wa shule wa Nigeria waliokuwa bado wametekwa nyara kutokana na uvamizi wa mwezi Novemba kutoka shule ya Kikatoliki katika jimbo la Niger wameachiliwa huru, msemaji wa Rais Bola Tinubu alisema Jumapili, kufuatia moja ya utekaji nyara mkubwa zaidi nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.

"Watoto 130 waliokuwa bado wametekwa nyara na watekaji...sasa wameachiliwa huru. Wanatarajiwa kufika Minna Jumatatu na kuungana na wazazi wao kwa sherehe ya Krismasi," Bayo Onanuga alisema katika chapisho kwenye mtandao wa X.

"Kuachiliwa huru kwa watoto wa shule kumewezeshwa na operesheni iliyoendeshwa na ujasusi wa kijeshi."

Wanafunzi hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 300 na wafanyakazi 12 waliokamatwa na watu wenye silaha kutoka shule ya bweni ya St Mary's Catholic katika kijiji cha Papiri saa za mapema Novemba 21.

Watoto hamsini kati ya watoto hao walifanikiwa kutoroka wakati huo, Chama cha Wakristo cha Nigeria kilisema hapo awali, huku serikali ya Nigeria ikisema mnamo Desemba 8 kwamba ilifanikiwa kuwaokoa 100 kati ya waliotekwa nyara.

Onanuga alisema jumla ya wanafunzi walioachiliwa huru sasa ni 230.

Utekaji nyara huo ulisababisha hasira juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa usalama kaskazini mwa Nigeria, ambapo magenge yenye silaha mara nyingi hulenga shule kwa ajili ya kulipwa fidia. Utekaji nyara shuleni uliongezeka baada ya wanamgambo wa Boko Haram kuwateka nyara wasichana 276 kutoka Chibok mwaka wa 2014. BBC

0 Comment

Daktari Afariki Baada ya Kuanguka Kutoka Ghorofa ya Tano ya HospitaliAfyaclass Bongo Social •

Daktari anayefanya mafunzo kwa vitendo (intern), Amit Yadav, amefariki dunia leo Jumapili asubuhi baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tano ya Hospitali ya Nobel Medical College iliyopo Biratnagar.

Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:30 asubuhi, ambapo Yadav alipelekwa hospitalini kwa matibabu lakini baadaye alifariki dunia. Marehemu alikuwa mkazi wa Jagdari, Manispaa ya Rajbiraj, wilaya ya Saptari, na alikuwa amehitimu masomo ya Shahada ya Udaktari (MBBS), akifanya mafunzo ya kazi katika hospitali hiyo kwa miezi kadhaa.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Naibu Kamishna wa Polisi Kopila Chundal, msemaji wa Polisi wa Wilaya ya Morang, alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo.

“Uchunguzi unaendelea na kwa sasa bado ni mapema kubaini chanzo halisi cha tukio hilo,” alisema Chundal.

Polisi wamesema taarifa za awali zinafanyiwa uchambuzi, huku wakisisitiza kuwa hakuna hitimisho rasmi lililofikiwa iwapo tukio hilo lilikuwa la bahati mbaya au vinginevyo. Matokeo ya uchunguzi yatatangazwa baada ya kukamilika.

Uongozi wa hospitali umetoa pole kwa familia, ndugu na wafanyakazi wenzake, ukimtaja marehemu kuwa daktari mwenye bidii na nidhamu.

0 Comment

Teknolojia mpya ya “nyumba zinazoelea” Afyaclass Bongo Social •

Kampuni ya Air Danshin Systems nchini Japan imebuni teknolojia mpya ya “nyumba zinazoelea” inayolenga kulinda makazi dhidi ya athari za tetemeko la ardhi.

Teknolojia hiyo hufanya kazi kwa kutumia vihisi (sensors) vinapogundua mtikisiko wa ardhi. Mara moja, mifuko maalum ya hewa iliyobanwa hujaa na kuinua nyumba kwa sentimita chache kutoka ardhini. Hatua hii husaidia kupunguza mtikisiko mkali unaoweza kusababisha uharibifu mkubwa.

Baada ya tetemeko kupungua na ardhi kutulia, nyumba hurudi chini taratibu kwenye msingi wake bila madhara.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, mfumo huu umefanya kazi vizuri katika matetemeko madogo, na kwa sasa unaendelea kuboreshwa ili uweze kulinda nyumba hata wakati wa matetemeko makubwa zaidi.

Ubunifu huu unaonekana kuwa hatua muhimu katika kupunguza athari za majanga ya asili nchini Japan, ambayo ni moja ya nchi zinazokumbwa mara kwa mara na matetemeko ya ardhi.

0 Comment

Jake Paul afanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika taya kutokana na kipigo cha Anthony JoshuaAfyaclass Bongo Social •

Jake Paul afanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika taya kutokana na kipigo cha Anthony Joshua

Jake Paul afanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika taya kutokana na Anthony Joshua knockout

Jake Paul amethibitisha kuwa afanyiwa upasuaji kutokana na kuvunjika taya baada ya kupoteza dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu Anthony Joshua Ijumaa usiku huko Miami.

Pambano hilo lililokuwa likitangazwa sana, lililorushwa kwenye Netflix, lilimalizika katika raundi ya sita baada ya Joshua kumpiga mkono wa kulia uliomfanya Paul aanguke kwenye turubai katika Kituo cha Kaseya. Ngumi hiyo ilimaliza pambano hilo na, kama ilivyothibitishwa baadaye, ilivunja taya ya Paul, New York Post iliripoti.

0 Comment

Tatizo la kunuka mdomo,tatizo la mdomo kutoa harufu,chanzo na TibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la kunuka mdomo,tatizo la mdomo kutoa harufu,chanzo na Tiba

Shida hii ya kutoa harufu mbaya kinywani huwasumbua watu wengi, na wengine hushtuka baada ya kuambiwa kwamba Wakati wanaongea kuna harufu mbaya inatoka mdomoni,

Katika makala hii tumechambua zaidi kuhusu chanzo cha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni pamoja na Dawa nzuri ya kutoa harufu mbaya mdomoni.

Chanzo cha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni

Tatizo hili husababishwa na nini? zipo sababu mbali mbali ambazo huchangia kinywa kutoa harufu mbaya,

BAADHI YA SABABU HIZO NI PAMOJA NA;

- Baadhi ya vyakula, baada ya chakula kuvunjwa vunjwa na baadhi ya mabaki ya chakula kuganda kuzunguka meno huweza kupelekea mashambulizi ya bacteria pamoja na kinywa kuanza kutoa harufu mbaya,

Kula VITUNGUU MAJI, vitunguu saumu(garlic) au viungo vingine huweza kuongeza harufu mdomoni

- Uvutaji wa Sigara ikiwemo Tumbaku, mbali na kuwa kwenye hatari ya kupata magonjwa ya fizi(gum disease) na meno,wavutaji wa sigara ikiwemo tumbuku wapo kwenye hatari ya kupata shida ya kutoa harufu mbaya mdomoni

- kUtokusafisha kinywa vizuri(Poor oral and dental hygiene), Hii ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo hupekea kutoa harufu mbaya kinywani,

Mbali na kutoa harufu mbaya kinywani, kutokusafisha meno na kinywa vizuri hupelekea mabaki ya chakula kuganda kwenye meno, hali ambayo hupelekea watu wengi sana kuwa na matatizo ya Meno.

KUMBUKA; Wataalam wa meno na kinywa wanasema,miongoni mwa sababu kubwa za matatizo ya meno kwa wagonjwa wengi ambao wanawapata, ni kuganda kwa uchafu kwenye meno kutokana na meno kutokusafishwa vizuri.

- Shida ya mdomo kuwa mkavu(Dry mouth), Mate husaidia sana kusafisha mdomo na kuondoa mabaki ya chakula(Food particles) ambayo huweza kusababisha harufu mbaya mdomoni,

Tatizo hili la mdomo kuwa mkavu yaani Dry mouth or xerostomia huweza kusababisha harufu mbaya kutoka kinywani kwa sababu ya upungufu mkubwa wa mate mdomoni,

Hali hii ya mdomo kuwa mkavu mara nyingi hutokea usiku ukiwa umelala, ndyo maana ukiamka asubuh mdomo hutoa harufu zaidi, mbali na kuwa na mabaki ya chakula mdomoni na kwenye meno kama hukupiga mswaki.

Endapo shida hii ya mdomo kuwa mkavu(xerostomia) hutokea wakati wote bila kuondoka,inabidi upate matibabu ya tatizo hili.

- Matumizi ya dawa, baadhi ya dawa huweza kuchangia tatizo hili la kutoa haruf u mbaya kinywani kwa kukausha mdomo(dry mouth) au kwa kutoa chemicals baada ya uvunjwaji wake,ambazo huweza kuongeza harufu mdomoni.

- Maambukizi ya magonjwa kwenye meno,Fizi na kinywa, kuwa na shida ya fangasi mdomoni, maambukizi ya bacteria, kidonda baada ya kutoa jino au meno,meno kuoza,vidonda mdomoni,n.k vyote hivi huweza kusababisha tatizo la kutoa harufu mbaya mdomoni.

matatizo mengine kama vile; Kansa au saratani, metabolic disorders,(gastroesophageal reflux disease, or GERD),N.k, vyote hivi huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili.

MATIBABU YA TATIZO HILI LA KUTOA HARUFU MBAYA KINYWANI

Baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina pamoja na Vipimo,kisha wataalam wa afya kujua chanzo chake,ndipo tiba sahihi ya tatizo lako hufanyika.

Kama nilivyokwisha kueleza hapo juu baadhi ya sababu za tatizo hili, na matibabu yake yatahusu vyanzo vyake.

- Epuka uvutaji wa sigara ikiwemo tumbaku,

- Epuka matumizi ya Pombe,Ugoro n.k

- Hakikisha unasafisha kinywa na meno vizuri hasa baada ya kula

- Epuka kutafuna vitunguu maji,vitunguu saumu,kula viungo vingi n.k

- Hakikisha unakunywa maji ya kutosha

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Anthony Joshua amshinda Jake Paul kwa knockout katika raundi ya sita (Video)Afyaclass Bongo Social •

Anthony Joshua amshinda Jake Paul kwa knockout katika raundi ya sita (Video)

Anthony Joshua ameadhimisha kurudi kwake kwenye ndondi rasmi kwa ushindi wa knockout dhidi ya Jake Paul, na kumzuia bondia huyo aliyegeuka kuwa YouTuber katika raundi ya sita ya pambano lao lililorushwa moja kwa moja kwenye Netflix.

Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa juu aliingia kwenye pambano hilo,huku kitu kingine chochote isipokuwa knockout kikitarajiwa kuwa miongoni mwa matukio makubwa zaidi katika historia ya ndondi.

Huku Paul akiingia kwenye pambano hilo akiwa na ushindi mara 12 kutoka kwenye mapambano 13 aliyocheza, ikiwa ni pamoja na knockout saba.

0 Comment

Tambua Rehema na Neema za Mungu kwako,UtamshukuruAfyaclass Bongo Social •

Tambua Rehema na Neema za Mungu kwako,Utamshukuru

Rehema ni pale ambapo Mungu hakutuadhibu kwa Dhambi tulizostahili adhabu,

Neema ni pale ambapo Mungu anatubariki wakati hatukustahili.

Toba ya Kweli kutoka Moyoni huturidisha Kwa Mungu,

Yoeli 2:13 inasema "rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, mkamrudie Bwana, Mungu wenu; kwa maana yeye ndiye mwenye neema, amejaa huruma; si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya".

Kama Mungu hajakuadhibu Kwa Kosa Ulilostahili adhabu, tena kukubariki wakati hukustahili(Fikiria kwa Kina Utaona UPENDO mkuu wa MUNGU kwako,Nawe UTAMSHUKURU siku Zote).

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD