Kuhisi kitu kooni kimekwama,unahisi kama kuna kitu kimekwama kooni? Sababu hizi hapa

Kuhisi kitu kooni kimekwama,unahisi kama kuna kitu kimekwama kooni? Sababu hizi hapa

#1

Kuhisi kama kuna kitu kimekwama kooni (hujulikana kama globus sensation) kunaweza kusababishwa na mambo kadhaa.

Hizi ndyo Sababu Kuu za kuhisi hali hii kwenye Koo Lako;

1. Tatuzo la Acid Reflux:Asidi ya tumboni kupanda kooni

– Asidi inapopanda huleta hali ya kero kooni, na kuhisi kama kuna kitu kimekwama

– Huambatana na kiungulia, ladha chungu mdomoni, au maumivu kifua

2. Maambukizi ya koo (tonsillitis, pharyngitis)

Maambukizi haya huweza kuhusisha kuvimba kwa tonses pia,

– Koo huvimba au kuwa na vidonda

– Huambatana na maumivu, homa, au ugumu wa kumeza kitu chochote.

3. Tezi la thyroid kuvimba

– Tatizo hilo huweza kusababisha hali ya kubana koo na kuhisi kama kitu kimekwama kooni

– Na mtu mwenye tatizo hili huonekana zaidi kama shingo imevimba

4. Misuli ya koo kujikaza bila wewe kujua

Ambapo hii huwapata watu wengi wakiwa kwenye Msongo mkali wa mawazo au wasiwasi (stress/anxiety) ndipo tatizo hili huanza.

– Mara nyingi huja bila maumivu, lakini hisia huendelea

5. Sababu Zingine ni pamoja na:

Kuwa na Kamasi nyingi eneo la ndani ya pua kushuka kooni (post-nasal drip) ambapo husababishwa na;

  • Mafua, 
  • Tatizo la sinusitis, 
  • au Tatizo la Mzio au allergy

– Hii huleta hisia ya kitu kinashuka au kimeshika kooni

Dalili hatarishi Zaidi (muone daktari haraka)

Nenda hospitali au tuwasiliane hapa hapa ndani ya afyaclass ikiwa una:

-Ugumu mkubwa wa kumeza

-Maumivu makali kooni au kifuani

-Kupungua uzito bila sababu

-Kikohozi chenye damu

-Hisia inaendelea zaidi ya wiki 2–3

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code