Familia kutoa ubongo wake kwa ajili ya utafiti

Familia kutoa ubongo wake kwa ajili ya utafiti

#1

Familia ya muigizaji wa Hollywood, Bruce Willis, imetangaza uamuzi wa kugusa Kwa kutoa ubongo wake kwa ajili ya utafiti wa kisayansi baada ya kifo chake. Willis alilazimika kustaafu kazi ya uigizaji baada ya kugunduliwa na ugonjwa wa frontotemporal dementia (FTD), unaoathiri lugha, tabia na uwezo wa kufikiri.

Mke wake, Emma Heming-Willis, amesema uamuzi huo haukuwa rahisi kihisia, lakini ni muhimu kwa maendeleo ya tafiti zitakazosaidia wanasayansi kuelewa ugonjwa huo kwa undani zaidi.

Familia ina matumaini kuwa mchango huo utasaidia wagonjwa wengine na familia zinazopitia changamoto kama zao.

Hatua hii imepokelewa kama ishara ya matumaini na mshikamano, ikionyesha namna maumivu binafsi yanavyoweza kubadilishwa kuwa mchango wenye manufaa kwa jamii na sayansi.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code