Muigizaji wa The Wire James Ransone afariki akiwa na umri wa miaka 46 kutokana na kujiua
James Ransone, mwigizaji wa Marekani anayejulikana zaidi kwa kucheza Ziggy Sobotka katika mfululizo wa filamu maarufu ya HBO The Wire, amefariki akiwa na umri wa miaka 46.
Kulingana na taarifa rasmi za kitabibu muigizaji huyo alifariki Ijumaa huko Los Angeles. Mamlaka iliorodhesha chanzo cha kifo hicho kama kujiua. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa.
Ransone ameacha mke wake, Jamie McPhee, na watoto wao wawili. Siku zilizofuata kabla ya kifo chake, McPhee aliongeza mchango wa kuchangisha fedha unaonufaisha Muungano wa Kitaifa wa Magonjwa ya Akili (NAMI) kwenye wasifu wake wa mitandao ya kijamii, Daily Mail iliripoti.









image quote pre code