Niliteseka na maumivu ya tumbo – ndipo nikagundua ni Ugonjwa wa amoeba
Maelezo kutoka kwa Dr.Ombeni wa Afyaclass:
Ugonjwa wa amoeba au amoebiasis ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea(parasite) kinachoitwa Entamoeba histolytica. Entamoeba histolytica ni kimelea kwenye kundi la anaerobic parasite na kwa mara ya kwanza hupatikana kwenye Utumbo mpana(colon);
Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha ugonjwa wa amoeba kwa mtu yeyote anayekula au kunywa kitu kilichoambukizwa na kimelea hiki.
Dalili Kubwa za Ugonjwa huu wa Amoeba ni pamoja na;
- Mgonjwa kujisaidia kinyesi chenye vitu kama makamasi
- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota
- Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana
- Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa
- Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu
- Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)
- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili
- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa
- Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu
- Kupoteza appetite ya chakula kabsa
- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika
- Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda
NB:Hizi ni Miongoni mwa Dalili kubwa ambazo tunaziona kwa Wagonjwa wenye Vimelea hivi vya Amoeba, Na Ukifuatilia historia ya Ugonjwa wao(Patient history) ulivyoanza asilimia 88% wanaishi kwenye mazingira ambayo maji sio Salama,wala mazingira ya maandalizi ya Vyakula Sio Masafi Pia.
Ushauri wangu kwako,hakikisha Unakunywa maji Safi,Chakula kiwe Safi,Vyoo Safi utakuwa Salama....
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.





.webp)



image quote pre code