Daktari anayefanya mafunzo kwa vitendo (intern), Amit Yadav, amefariki dunia leo Jumapili asubuhi baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya tano ya Hospitali ya Nobel Medical College iliyopo Biratnagar.
Kwa mujibu wa Polisi, tukio hilo lilitokea majira ya saa 12:30 asubuhi, ambapo Yadav alipelekwa hospitalini kwa matibabu lakini baadaye alifariki dunia. Marehemu alikuwa mkazi wa Jagdari, Manispaa ya Rajbiraj, wilaya ya Saptari, na alikuwa amehitimu masomo ya Shahada ya Udaktari (MBBS), akifanya mafunzo ya kazi katika hospitali hiyo kwa miezi kadhaa.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Naibu Kamishna wa Polisi Kopila Chundal, msemaji wa Polisi wa Wilaya ya Morang, alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
“Uchunguzi unaendelea na kwa sasa bado ni mapema kubaini chanzo halisi cha tukio hilo,” alisema Chundal.
Polisi wamesema taarifa za awali zinafanyiwa uchambuzi, huku wakisisitiza kuwa hakuna hitimisho rasmi lililofikiwa iwapo tukio hilo lilikuwa la bahati mbaya au vinginevyo. Matokeo ya uchunguzi yatatangazwa baada ya kukamilika.
Uongozi wa hospitali umetoa pole kwa familia, ndugu na wafanyakazi wenzake, ukimtaja marehemu kuwa daktari mwenye bidii na nidhamu.









image quote pre code