TANZIA:Watu Wawili waliofariki katika ajali ya Bondia Anthony Joshua watambuliwa
Maelezo ya picha,Sina Ghami (kushoto) na Latif "Latz" Ayodele
Wanaume wawili waliofariki katika ajali iliyomuhusisha mwanamisumbwi raia wa Uingereza, Anthony Joshua huko Lagos Nigeri wametambuliwa.
Wanaume hao ambao ni marafiki na wanachama wa timu ya Joshua, ni Sina Ghami na Latif Ayodele, kwa mujibu wa kampuni ya kuandaa michezo ya Joshua ya Matchroom Boxing.
Taarifa hiyo inasema, wawili hao walifanya kazi kwa karibu na Anthony Joshua, na wote walikuwa marafiki wazuri.
Sina Ghami alikuwa kocha wa viungo wa Joshua kwa zaidi ya miaka 10. Pia ni mmiliki wa ukumbi wa michezo wa Evolve Gym jijini London.
Kwa mujibu tovuti hiyo Ghami ni mtaalamu wa michezo na mazoezi aliyebobea katika mazoezi ya misuli.
Mwingine ni Latif "Latz" Ayodele alikuwa mkufunzi binafsi wa Joshua. Mapenzi yake kwa mazoezi yapo wazi kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Matchroom Boxing imesema Joshua alipelekwa hospitalini kwa ajili ya "uchunguzi na matibabu" na yuko katika "hali imara na atabaki hapo kwa uchunguzi."
Maafisa huko Nigeria wanasema gari la Joshua liligonga lori wakati wakiendesha kwa kasi.
Joshua - bingwa wa dunia mara mbili wa uzito wa juu – familia yake ina asili ya Sagamu, mji ulioko katika Jimbo la Ogun, Nigeria.









image quote pre code