Rais wa Marekani, Donald Trump amesema amepata wa kuinunua kampuni ya TikTokAfyaclass Bongo Social •

NEWS: Kwenye Jukwaa la Teknolojia leo hii tuna habari kuhusu kampuni ya Tiktok.



Rais wa Marekani, Donald Trump amesema amepata wa kuinunua kampuni ya TikTok.

Kauli hiyo inakuja wakati ambapo kampuni ya ByteDance ya China inakabiliwa na shinikizo la kuiuza TikTok kwa Marekani, vinginevyo itazuiwa kutumika nchini humo.

1 Comment

Ester Bulaya achukua fomu ya Ubunge jimbo la BundaAfyaclass Bongo Social •

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalum Ester Bulaya amechukua fomu ya kuwania Ubunge wa jimbo la Bunda mkoani Mara kupitia Chama cha Mapinduzi CCM.



Ester Bulaya amechukua fomu hiyo leo June 30 2025, akilenga kuchuana na watia nia wengine akiwemo Mbunge wa jimbo hilo anayemaliza muda wake Robert Maboto.

Ester Bulaya kabla kurejea CCM amewahi kuwa Mbunge wa Vijana kupitia CCM Mwaka 2010, na baadae kwenda Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuwa Mbunge wa kuchaguliwa Mwaka 2010 -2015 jimbo hilo kupitia CHADEMA, Mwaka  2010 - 2020 Mbunge wa Viti Maalum. 

Leo Bulaya amekabidhiwa fomu ya kutia nia ya Ubunge ndani ya chama hicho na Katibu wa CCM Wilaya ya Bunda, Evodia Zumba.

0 Comment

Rais Mwinyi aizawadia Yanga Sc Million 100Afyaclass Bongo Social •

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Klabu ya Yanga SC shilingi milioni 100, kwa kutambua ushindi na mafanikio makubwa waliopata katika msimu wa mwaka 2024/2025.



Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 30 Juni 2025 alipokutana na viongozi pamoja na wachezaji wa Yanga waliofika Ikulu kwa ajili ya kumkabidhi makombe matano ya michuano mbalimbali waliyoyatwaa msimu huu.

Akizungumza nao, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza mafanikio hayo makubwa yaliyopatikana na klabu hiyo kongwe, akieleza kuwa yanajenga heshima na historia muhimu katika tasnia ya michezo nchini.

Aidha, ameishukuru Yanga kwa kuendelea kuitangaza Zanzibar ndani na nje ya nchi kupitia kampeni ya Visit Zanzibar, huku akieleza kuwa hatua ya klabu hiyo kucheza baadhi ya michezo yake Zanzibar kunachangia kukuza uchumi na sekta ya utalii kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wageni na wananchi kunufaika na fursa mbalimbali.

0 Comment

Ndege ya Abiria ya Batik Air yanusurika kuteleza,Sababu Hali Mbaya ya HewaAfyaclass Bongo Social •

Ndege ya abiria ya Batik Air ilinusurika kuteleza wakati wa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, kutokana na hali mbaya ya hewa. Tukio hilo lilinaswa kwenye video iliyorekodiwa na mmoja wa abiria na kusambaa kwa kasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii.



Katika video hiyo, ndege ilionekana ikitikisika kwa nguvu wakati wa kutua, ikionyesha hali ya hatari huku ikikaribia kutoka nje ya njia ya kurukia na kutua (runway).

Batik Air ilithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa hakuna abiria wala wahudumu walioumia.

0 Comment

Fahamu Ugonjwa wa baridi yabisi,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Baridi Yabisi ni ugonjwa unaoshambulia membreni za synovial katika viungo vya binadamu na mara zote hupenda kushambulia sana viungo vidogo na zaidi ya kiungo kimoja  na mara zote hupenda kushambulia viungo vya pande zote mbili kwa pamoja(symmetrical).



Ni ugonjwa unaosumbua sana na huweza kumletea mtu madhara makubwa  ikiwemo uharibifu wa viungo na ulemavu mkubwa kama hautatibiwa,

Baridi yabisi yaweza kumpata mtu yeyote katika umri wowote lakini kijinsia ugonjwa huu huwata sanasana wanawake na huanza kuonekana kuanzia miaka 40 na kuendelea kwa walio wengi.

KINACHOSABABISHA BARIDI YABISI

Hakuna Sababu ya moja kwa moja inayosababisha ugonjwa huu; ila zipo tu sababu za kimazingira,kimaumbile,kivinasaba,kifamilia na kijiografia ambazo zinaweza kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa huu.

WALIO KWENYE HATARI YA KUPATA BARIDI YABISI

1)Wanawake(kwa sababu ya vichocheo vya oestrogen)

2) Wenye Mimba

3) Wasionyonyesha kwa muda mrefu(chini ya mwaka 1)

4) Wanaume wenye upungufu wa kichocheo Testosterone

5) Unene ulopitiliza

6) Wanaovuta sigara

7) Kua kwenye familia yenye watu wenye baridi yabisi.

8) wanaofanya kazi migodini,sheli,wajenzi  na viwandani

DALILI ZA UGONJWA WA BARIDI YABISI

Dalili za ugonjwa huu huanza kidogokidogo na kama mtu hataenda kupimwa hospitali unaweza kusema ni mabadiliko ya kawaida,kama mnakumbuka huko juu nilisema matokeo ya ugonjwa huu yaweza kuchukua hadi miaka 20 kuja kukufanya ushindwe kufanya jambo lolote.

Mtu mwenye ugonjwa huu anaanza kupata shida kwenye viungo na baadae  mwili mzima hupata matokeo/madhara ya ugonjwa huu..Mgonjwa  wa ugonjwa huu anaweza kujikuta anashindwa kufanya yafuatayo bila ya hata yeye kujua ana shida gani;mambo hayo ni kushindwa kufanya shughuli zako za kila siku kama vile;

- KUVAA,

- KUFUNGUA MFUNIKO WA  CHUPA,

- KUJISAFISHA UKIWA CHOONI,

- KUTEMBEA,

- KUPANDA NGAZI,

- KUAMKA KUTOKA KWENYE KITI,

- KUFUNGUA MLANGO,

- KUANDIKA,KUCHAPA n.k

DALILI ZA BARIDI YABISI NI KAMA IFUATAVYO;

1. MAUMIVU YA VIUNGO; Mgonjwa wa rheumatoid atapata maumivu ya viungo na huanzia katika viungo vidogo vya mkononi(vidole) na mara zote hua ni mikono yote miwili.. hii yaweza kua ndo dalili ya mwanzo na pekee ya ugonjwa huu

2. VIUNGO KUKAKAMAA (STIFFNESS):Mgonjwa wa rheumatoid atapata ukakamavu wa viungo kushindwa kufanya kazi zake katika viungo vya mikono; mara zote mgonjwahupata hali hii lile lisaa la kwanza kabisa punde anapoamka na akishamaliza lisaa limoja na kadiri anaendelea kutembea tembea basi hali hio ya ukakamavu wa viungo hupungua.Mgonjwa anaweza kutumia lisaa au zaidi kutoka kitandani….hali hii huonekana katika ugonjwa wa baridi yabisi pekee

3. KUVIMBA VIUNGO; ; Mgonjwa wa rheumatoid  viungo  vyake vitavimba  na huanzia katika viungo vidogo vya mkononi(vidole) na mara zote hua ni mikono yote miwili.. hii yaweza kua ndo dalili ya mwanzo na pekee ya ugonjwa huu

4. Dalili Zingine ni pamoja na;

- Mwili Kupata Joto(fever)

- Kupungua Uzito(weight Loss)

- Kuchoka Mwili Mzima(chronic Fatigue) n.k

MATOKEO YA BARIDI YABISI KWA MWILI

Ugonjwa huu ni wa viungo lakini unaweza kuleta madhara katika mwili mzima (extra-articular),kwa maana ugonjwa unaweza kutoka nje ya viungo na kuleta madhara katika mfumo wowote katika mwili wa mgonjwa..Sio kila mgonjwa wa rheumatoid atapata madhara ya mwili mzima bali kuna baadhi ambao wapo kwenye uhatari zaidi wa kupata matokeo hayo,baadhi ya walio hatarini ni wenye umri mkubwa,wanaovuta sigara,mwanamke,wenye uharibifu wa viungo,wenye kipimo cha rheumatoid factor POSITIVE. .

Matokeo ama madhara ya rheumatoid katika mwili mzima ni kama ifuatavyo

• Udhaifu Wa Mifupa(osteopenia)

• Udhaifu Wa Misuli(muscle Weakness)

• Mwili Kujaa Mafuta(sarcopenia)

• Manundu Kwenye Ngozi(rheumatoid Nodules)

• Madonda Kwenye Ngozi(skin  Ulcers)

• Kua Na Macho Makavu(Keratoconjuctivitis Sicca)

• Matatizo Ya Kupumua

• Magonjwa Ya Moyo

• Matatizo Ya Mishipa Ya Damu(Vasculitis)

• Matatizo Ya Mafigo

• Kiharusi

• Upungufu Wa Damu

NAMNA UGONJWA HUU HUGUNDULIKA

Ugonjwa huu hugundulika tu kirahisi pale unapomuona mtaalam wa afya ,atrakusikiliza juu ya historia ya unavojisikia,atakuchunguza viungo vyako na utafanyiwa vipimo kadhaa vya kubaibini tatizopamoja na kujua kama kuna mdahara ya ugonjwa ulio nao.. Viko vipimo vya damu na vya mionzi katika uchunguzi wa tatizo hili

BARIDI YABISI KWA WAJAWAZITO

Ugonjwa huu kama nilivosema hapo awali huwapata sana wanawake na hasa walio katika umri wa kupata watoto, baridi yabisi kwa wajawazito imekua ni changamoto kwa wataalamu kimatibabu kutokana na hali ya ugonjwa wenyewe na adhari za madawa ya ugonjwa huu kwa wajawazito.

Habari Njema Ni Kwamba Wajawazito Walio Wengi Wenye Ugonjwa Huu Huanza Kujisikia Vizuri Na Hata Dalili Kupotea Zote Kipindi Cha Ujauzito Na Kuanza Kujitokeza Tena Baada Ya Kujifungua.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea SameAfyaclass Bongo Social •

 DAR ES SALAAM;RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea jana Same mkoani Kilimanjaro, huku akiwataka madereva waendelee kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya ndugu zetu 37 na majeruhi 30 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea jana jioni eneo la Sabasaba, Barabara Kuu ya Moshi - Tanga, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, kwa magari mawili kugongana na kuungua moto.

"Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka. Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Nurdin Babu, familia zote za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu.

“Kama ambavyo nilieleza Juni 27 katika hotuba yangu ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ajali za barabarani zimeendelea kugharimu maisha ya wapendwa wetu. Ninawasisitiza madereva kuendelea kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani, na Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria hizo," ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

0 Comment

Dr Ipyana – Nawezaje Kunyamaza|Audio|Mp3Afyaclass Bongo Social •



 Listen to “Dr Ipyana – Nawezaje Kunyamaza” Below

0 Comment

Aitishia AI nayo ikamtishia kufichua mahusiano yake ya nje ya ndoaAfyaclass Bongo Social •

Watafiti wametahadharisha kuwa baadhi ya programu za akili mnemba zenye ufanisi mkubwa zinaweza kuwa tishio kubwa kwa watumiaji.



Hayo ni baada ya kubainika kuwa baadhi ya programu hizo zenye ufanisi za (AI) ili kufikia malengo yake zinaweza kudanganya, kubuni njama na hata kutoa vitisho.

Katika mfano mmoja wa kutatanisha, mtumiaji mmoja alitishia kuizima programu ya AI inayofahamika kama "Anthropic Claude 4", na ndipo programu hiyo ikamtishia kufichua mahusiano yake ya nje ya ndoa.

Matukio kama haya yanatia wasiwasi baada ya programu ya akili mnemba ya ChatGPT kutikisa ulimwengu karibu miaka miwili iliyopita, lakini yanabainisha ukweli kwamba hata watafiti wa AI bado hawaelewi kikamilifu jinsi ubunifu wao wenyewe unavyofanya kazi.

0 Comment

TANZIA: Watu 36 wafariki dunia kwa ajali wilayani Same,Magari yawaka motoAfyaclass Bongo Social •

Ajali hiyo  imetokea leo Jumamosi  Juni 28,2025  ikihusisha basi la abiria kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na Toyota coaster lilikuwa likitokea Same kwenda Moshi.



Same. Wakati shughuli ya uokoaji na uondoshaji wa miili ikiendelea katika eneo ambalo ajali ya basi la abiria la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Toyota Coaster yaliyogongana uso kwa uso na kuwaka  moto, watu 36 wamethibitishwa kupoteza maisha huku 23 wakijeruhiwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi ambaye yupo eneo la tukio usiku huu amethibitisha huku akisema ni taarifa za awali.

"Miili iliyotolewa eneo la tukio mpaka sasa ni  36 na majeruhi 23 ambao wamekimbizwa hospitali na bado zoezi linaendelea,"amasema Kamanda Mkomagi 

Hata hivyo, taarifa kutoka eneo la tukio ni kwamba abiria waliokuwa wamepanda coaster kuja  Moshi mjini walikuwa wakienda kwenye sherehe ya harusi ambayo inafanyika katika ukumbi wa Kuringe hall, ambao upo Moshi mjini.



0 Comment

Jesca Magufuli achukua form ya Ubunge Viti MaalumAfyaclass Bongo Social •

Jesca Magufuli ambaye ni Mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr. John Pombe Magufuli, leo June 28 2025 amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa.

Jesca ni Binti ambaye amejipambanua kama sauti ya matumaini kwa Vijana na Wanawake wa Tanzania akisimamia maadili, haki na maendeleo jumuishi ambapo amelenga kupeleka nguvu mpya ya kijana Bungeni, kusimamia ajenda za maendeleo kwa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla huku akihakikisha UVCCM inasikika, inaonekana na inawakilishwa kwa heshima katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nipo tayari kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu, umoja na kwa kutanguliza maslahi ya Vijana na Wanawake, Geita inapeleka sauti ya mabadiliko chanya,” amesema Jesca Magufuli mara baada ya kuchukua fomu hiyo leo.

0 Comment

AJIRA MPYA:Serikali yamwaga ajira mpya bandariAfyaclass Bongo Social •

Dar es Salaam. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) imetangaza nafasi 184 za kazi.



Tangazo hilo la ajira limetolewa Juni 27, 2025 ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuongeza ufanisi ndani ya taasisi zake.

Kwa upande wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetangaza nafasi 176 kwa Watanzania wenye sifa stahiki na wanaojituma, kama iliyoorodheshwa hapa chini.

Miongoni mwa nafasi hizo ni pamoja na zimamoto, wataalamu wa mashine za ukaguzi, nahodha, nahonda wasaidizi, wakufunzi wa unahodha na nafasi nyinginezo.

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimetangaza nafasi nane zikiwemo za wakufunzi.

Katika masharti ya jumla ya kwa waombaji wanatakiwa wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.

Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba, maombi yaambatane na wasifu (CV) wa kisasa, wenye mawasiliano ya uhakika.

Wajaze taarifa kwa kuzingatia tangazo husika, wawasilishe vyeti vilivyothibitishwa, stashahada au shahada na transkripti za kidato cha nne na sita, vyeti vya usajili kitaaluma pamoja na cheti cha kuzaliwa.

Pia wanatakiwa waambatanishe picha ndogo (passport size) ya hivi karibuni.

Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba, wastaafu wa umma hawaruhusiwi kuomba, wataje watu watatu wanaowajua (referee), wenye mawasiliano ya uhakika, vyeti vya nje vya O/A-Level vithibitishwe na NECTA.

Vyeti vya taaluma vya nje vibatilishwe na TCU/NACTE, barua ya maombi isainiwe, iwe kwa Kiswahili au Kiingereza na ipelekwe kwa Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira, S.L.P 2320, Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi hayo ni Julai, 9, 2025 na waliochaguliwa kwa usaili watapewa taarifa na vyeti vya kughushi vitasababisha hatua za kisheria.

0 Comment

Baada ya Kuchanganya Ndizi na nyama kama Mlo wako unapata nini kiafya?Afyaclass Bongo Social •

Mchanganyiko wa ndizi na nyama unaweza kuwa na faida nyingi kiafya, hasa unapoliwa kwa uwiano sahihi. Kila moja kati ya hivi viwili ina virutubisho maalum ambavyo vinapochanganywa vinaweza kuimarisha afya ya mwili kwa njia mbalimbali:



Faida za kiafya za mchanganyiko wa ndizi na nyama:

1. Kutoa nguvu nyingi (High Energy)

Ndizi ni chanzo kizuri cha wanga (carbohydrates), hasa sukari asilia kama fructose, glucose, na sucrose, ambazo huupa mwili nguvu za haraka.

Nyama ina protini na mafuta ambayo hutoa nguvu kwa muda mrefu na kusaidia ukarabati wa seli za mwili.

2. Kujenga na kutengeneza misuli

Protini ya nyama husaidia kujenga misuli, hasa kwa watu wanaofanya mazoezi au wanaotaka kuongeza uzito wa afya.

Ndizi hutoa potasiamu, ambayo husaidia misuli kufanya kazi vizuri na kuzuia misuli kuchoka haraka.

3. Afya ya mfumo wa mmeng'enyo

Ndizi zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo huboresha mmeng'enyo wa chakula na kuzuia kuvimbiwa.

Mchanganyiko huu unaweza kusaidia usagaji bora wa protini inayopatikana kwenye nyama.

4. Utulivu wa moyo na mishipa ya damu

Potasiamu ya ndizi husaidia kudhibiti shinikizo la damu.

Wakati nyama (hasa isiyo na mafuta mengi) hutoa madini kama chuma, muhimu kwa usafirishaji wa oksijeni kwenye damu.

5. Kuongeza damu (hemoglobin)

Nyama ina kiwango kikubwa cha chuma heme ambacho ni rahisi kufyonzwa na mwili, muhimu kwa wale wenye upungufu wa damu.

Ndizi pia husaidia mwili kutumia vizuri chuma kutokana na viwango vyake vya vitamini C kidogo.

6. Kuongeza hamu ya kula kwa wagonjwa

Kwa wagonjwa au watu waliopoteza hamu ya kula, mchanganyiko huu unaweza kusaidia kurudisha nguvu kwa haraka kwa kuwa ni laini kuliwa na rahisi kumeng’enywa.

⚠️ Tahadhari

Usile nyama yenye mafuta mengi mara kwa mara, kwani inaweza kuongeza kolesteroli.

Kwa wenye matatizo ya figo, kula ndizi nyingi huenda si salama kutokana na potasiamu nyingi.

Mchanganyiko huu usiliwe mara kwa mara bila uwiano sahihi – unaweza kupelekea uzito mkubwa au matatizo ya mmeng’enyo kwa baadhi ya watu.

0 Comment

Kusikiliza Muziki unaoupenda huweza kuleta matokeo bora kwa afya ya akiliAfyaclass Bongo Social •

Tafiti zinaonyesha kwamba,Kusikiliza nyimbo unazozipenda sana huweza kusaidia kuwa na Mudi nzuri(music therapy can have a positive impact on your mood). 



Hali hii ya kusikiliza nyimbo hizo huweza kuchochea Ubongo wako kuzalisha zaidi kichocheo cha dopamine, ambacho husaidia kuleta zaidi hali ya kujisikia vizuri(the brain chemical that helps you feel pleasure). 

Tafiti hizi zinaonyesha;Kusikiliza Nyimbo unayoipenda husaidia kuondoa Hofu,Hali ya huzuni,Msongo wa mawazo,maumivu pamoja na kuleta Usingizi mzuri.⁠

0 Comment

Tatizo la uvimbe tumboni,chanzo,dalili na Tiba yakeAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la uvimbe tumboni bila kuhusisha mfumo wa uzazi. Katika makala hii tunazingatia uvimbe kwenye sehemu nyingine za tumbo kama ini, figo, utumbo, tumbo la chakula, au peritoneum.



CHANZO CHA UVIMBE TUMBONI (BILA KUHUSISHA MIFUMO YA UZAZI)

1. Saratani (Cancer)

Uvimbe unaweza kuwa dalili ya saratani katika maeneo ya tumbo, kama:

  • Saratani ya tumbo la chakula (gastric cancer)
  • Saratani ya ini (hepatocellular carcinoma)
  • Saratani ya kongosho (pancreatic cancer)
  • Saratani ya utumbo mpana au mdogo
  • Peritoneal cancer – saratani ya utando wa ndani wa tumbo

2. Kusanyiko la Maji Tumboni (Ascites)

  • Hutokea mara nyingi kutokana na ini kushindwa kufanya kazi (cirrhosis).
  • Maambukizi ya TB ya tumbo au saratani pia huleta maji tumboni.

3. Uvimbe wa Figo (Renal Masses)

  • Kama hydronephrosis (figo kujaa maji)
  • Renal cysts (uvimbe maji kwenye figo)
  • Saratani ya figo

4. Uvimbe wa Utumbo

  • Uvimbe wa saratani kwenye utumbo
  • Polyp au uvimbe wa kawaida unaokua ndani ya ukuta wa utumbo
  • Diverticulitis – uvimbe wa mifuko midogo kwenye utumbo mpana

5. Maambukizi na Kuvimba kwa Viungo vya Ndani

  • Kifua kikuu cha tumbo (Abdominal TB)
  • Appendicitis – kidole tumbo kuvimba
  • Pancreatitis – kongosho kuvimba kwa sababu ya pombe au mawe kwenye nyongo

6. Hernia (Ngiri ya Tumbo)

  • Sehemu ya utumbo au mafuta ya tumbo kusukumwa nje kupitia ukuta dhaifu wa tumbo

7. Gesi na Tatizo la Mmeng'enyo wa Chakula

  • IBS (Irritable Bowel Syndrome) – utumbo kujaa hewa au kuvimba
  • Indigestion – chakula kutoyeyuka vizuri
  • Constipation sugu – choo kigumu hushindwa kutoka na kuleta hali ya kujaa tumbo

DALILI ZA UVIMBE TUMBONI (ISIYOHUSIANA NA MIFUMO YA UZAZI)

  • Tumbo kuongezeka ukubwa au kujaa
  • Maumivu ya tumbo (ya kudumu au ya ghafla)
  • Kujisikia kushiba haraka
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kichefuchefu au kutapika
  • Kupungua uzito bila sababu
  • Kuvimba miguu (kama ini au figo zimeathirika)
  • Kukosa choo au kuharisha mara kwa mara
  • Mabadiliko ya rangi ya mkojo au kinyesi
  • Uchovu mwingi au dalili za upungufu wa damu mwilini

VIPIMO MUHIMU KUFANYIKA

  1. Ultrasound ya tumbo
  2. CT Scan au MRI – kuona uvimbe kwa undani
  3. Vipimo vya damu:
    • Liver Function Test (LFT)
    • Kidney Function Test (KFT)
    • Tumor markers kama CEA, AFP, CA19-9 (kwa saratani)
  4. Paracentesis – kuchukua maji tumboni kwa uchunguzi
  5. Endoscopy / Colonoscopy – kuangalia ndani ya tumbo au utumbo

MATIBABU YA UVIMBE TUMBONI

Matibabu hutegemea chanzo kilichosababisha uvimbe:

  • Maambukizi: Antibiotiki au dawa za TB
  • Mkusanyiko wa maji (ascites): Kudhibiti kwa dawa za kupunguza maji (diuretics) au kufyonza maji
  • Saratani: Chemotherapy, upasuaji, au radiotherapy
  • Gesi na kuvimbiwa: Dawa za mmeng'enyo, probiotics, mabadiliko ya lishe
  • Hernia: Upasuaji wa kuziba sehemu dhaifu ya tumbo
  • Figo au ini kushindwa kazi: Dialysis au matibabu ya kushughulikia kiini

USHAURI WA KISHAURI

  • Epuka kula vyakula vinavyoleta gesi sana (kama soda, maharage, kabichi)
  • Kula vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber) kusaidia choo
  • Epuka pombe (hasa kwa afya ya ini)
  • Fanya mazoezi mara kwa mara
  • Kunywa maji mengi kila siku
  • Usijitibu bila uchunguzi – uvimbe unaweza kuwa dalili ya tatizo kubwa

HITIMISHO

Uvimbe tumboni ni dalili muhimu inayohitaji kufuatiliwa kwa makini. Haipaswi kubezwa, hasa kama unaambatana na dalili nyingine kama maumivu, kichefuchefu, au kupungua uzito. Ni muhimu kumwona daktari kwa uchunguzi wa kina ili kupata tiba sahihi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Squid game season 3 tayari imetokaAfyaclass Bongo Social •

Fahamu,Squid game season 3 tayari imetoka




Ndiyo, msimu wa 3 wa Squid Game umetoka leo — tarehe 27 Juni 2025 — kwenye Netflix. Vipindi vyote sita vya msimu huu wa mwisho vimeachiwa kwa wakati mmoja leo asubuhi.

Msimu wa mwisho wa squid game waachiwa rasmi leo : huenda usiwe na mwisho wa furaha.

Leo Juni 27, 2025, ni siku ambayo Wapenzi wa filamu Duniani walikuwa wakiisubiri kwa hamu—filamu maarufu kutoka Korea Kusini, Squid Game, imeachiwa rasmi kwa msimu wake wa tatu, ambao pia unatajwa kuwa msimu wa mwisho wa mfululizo huo uliotikisa ulimwengu tangu 2021.

Filamu hiyo ambayo ilianzishwa na Hwang Dong-Hyuk, ilijizolea sifa na mafanikio makubwa Duniani kutokana na uhalisia wa kijamii uliowasilishwa kwa njia ya kipekee ya kisanaa. Tangu ilipoanza, Squid Game imekuwa gumzo kutokana na ujasiri wake wa kuonesha athari za ukosefu wa usawa wa kijamii, madeni, na tamaa ya fedha katika jamii ya kisasa.

Katika mahojiano na The Guardian, Mtayarishaji Hwang Dong-Hyuk alieleza kuwa wasitarajie mwisho wa furaha kama ilivyozoeleka:  

"Watu hupenda mwisho wa furaha. Mimi pia ni kama wao. Lakini baadhi ya hadithi, kwa asili, haziwezi kuwa na mwisho wa furaha. Ukijaribu kuubuni kwa nguvu, kiini cha hadithi kinaharibika. Kama hadithi inaakisi uhalisia, basi si kila mara huwa na mwisho wa furaha. Squid Game siyo tofauti," alisema Hwang.

Tayari mitandao ya kijamii imejaa mijadala kuhusu kile kinachotarajiwa kutokea kwenye msimu huu wa mwisho. Mashabiki wengi wanaelekeza macho yao kwenye njia ya kipekee ambayo Hwang ataikamilisha simulizi hii, huku wengi wakiamini kuwa hata kama mwisho hautakuwa wa furaha, utakuwa wa kukumbukwa sana.

Kwa mashabiki wa Squid Game, huu ni mwanzo wa mwisho unaohitaji kuangaliwa kwa makini.

Muhtasari wa Msimu wa 3:

  • Gi-hun anarudi: Baada ya vurugu za mwisho wa msimu wa pili, Gi-hun (mchezaji 456) anarudi kwa lengo la kusitisha kabisa michezo hiyo ya kifo.
  • Kurudi kwa Front Man: Lee Byung-hun anarudia nafasi yake kama kiongozi wa michezo hiyo ya kikatili, akiwa na mipango mipya na ya kutisha.
  • Michezo mipya hatari zaidi: Kuna changamoto mpya za kisaikolojia — zinazohusisha hofu, usaliti, na mashindano ya kuvunja moyo.
  • Hitimisho la hadithi: Msimu huu unafunga simulizi kuu ya Squid Game, ingawa kuna uwezekano wa kuwa na vipindi vya matawi (spin-offs) siku za baadaye.

Squid Game Season 3, the final season of the hit series, premiered today—June 27, 2025—on Netflix. All six episodes dropped simultaneously this morning.  

🎬 Summary of Season 3 Highlights:

Protagonist’s struggle: Gi‑hun (Player 456) returns with a mission to dismantle the deadly games after the rebellion’s collapse at the end of Season 2  .

The Front Man’s return: Lee Byung‑hun reprises his role as the ominous Front Man, escalating the stakes  .

Deadlier new games: Expect even more psychologically intense challenges—height-based fears, suspense, and betrayal woven through the storyline  .

Final chapter: This season wraps up the main narrative, though spin-offs remain a possibility.

0 Comment

Umri wa Wazee ni moja ya kihatarishi cha kupata magonjwa yasiyoambukizaAfyaclass Bongo Social •

Kwa Tanzania na nchi nyingine duniani umri wa uzee ni miaka 60 kuendelea. Kitabibu umri huu ni moja ya kihatarishi cha kupata magonjwa yasiyoambukiza.



Sababu ya kimsingi ni kutokana na mchanganyiko wa mambo kadhaa ya kibailojia kama vile kutumika na kulika hatimaye kuchakaa kwa viungo, mrundikano wa mambo hatarishi kiafya kadiri umri unavyoenda na uchaguzi usiofaa wa mitindo ya kimaisha.

Magonjwa yasiyoambukiza yanaweza kuathiri ubora wa maisha ya wazee, kuathiri ustawi wao wa kimwili na kiakili, uhuru na tija.

Ni Changamoto kutibu magonjwa haya kwasababu yanahitaji huduma ziinazoendelea kwa muda mrefu. Hivyo kusababisha kuongezeka kwa gharama kwa mzee binafsi, familia na mifumo ya huduma za afya.

Magonjwa yasiyoambukiza huwapata wazee na hatimaye kufariki au kupata ulemavu wa kudumu na maisha bora ya uzeeni.

Ni kweli umri wa uzee ni kihatarishi cha kupata magonjwa, lakini mzee mwenye mitindo mibaya kimaisha yupo katika hatari zaidi ya kupata magonjwa haya.

Mienendo na mitindo mibaya ya kimaisha ni pamoja unywaji pombe, uvutaji tumbaku, ulaji holela wa chumvi, sukari, wanga na mafuta na kutofanya mazoezi au kuushughulisha mwili na kazi.

Magonjwa hayo ni pamoja na shinikizo la juu la damu, unene, matatizo ya mishipa ya damu ya moyo, lehemu nyingi, kiharusi na kisukari.

Vile vile ugonjwa sugu wa figo, matatizo sugu mfumo wa hewa, saratani mbalimbali, matatizo ya viungo vya mwili ikiwamo mifupa na magonjwa ya akili.

Ni muhimu kutumia njia za kujikinga mapema kabla ya kupata magonjwa hayo, hasa kwa wale wanaoelekea uzeeni, ambao tayari ni wazee au tayari wanakabiliwa na magonjwa hayo.

Hatua muhimu kujua huduma za afya zilizopo jirani na anapoishi ili iwe rahisi kupata ushauri wa kiafya hata kabla ya kuugua.

Mazingira bora ya kuishi yasiyo katika mazingira yenye uchafuzi wa hewa na kelele nyingi, lishe bora iliyozingatia kanuni za afya na mazoezi mepesi ni muhimu kwa afya ya wazee.

Wazee walio katika hatari ya kupoteza maisha mapema wanapopata magonjwa hayo ni wale wa nchi za kipato cha chini mpaka kati. Wengi wao hawana uwezo wa kufanya kazi ngumu za kujiingizia kipato.

Vile vile tayari wameisha staafu kazi zile walizokuwa wameajiriwa na pengine alikuwa na bima kubwa ya afya lakini sasa huenda hana au anayo lakini ni ya kawaida.

Umri wa miaka 60+ wanatakiwa kupendelea zaidi kula mlo mboga mboga, matunda, protini itokanayo na mimea, kuepuka chumvi, sukari au wanga na mafuta mengi.

Vyema umri huo kuwaona wataalam lishe katika huduma za afya ili kukupa mwongozo mpana na ratiba ya vyakula.

Mzee kufanya mazoezi huwa ni vigumu, kwa yule anayeweza kutembea vyema kufanya zoezi la kutembea angalau hatua 10,000 kwa siku au umbali wa kilometa 2 kwa dakika 30 kwa siku katika siku 5 za wiki.

Au kujishughulisha na kazi za nyumbani kama kazi bustani au usafi wa nyumba na mazingira unaweza kutumia kama mazoezi au anayeishi mazingira rafiki kwa kutembea.

Kulala angalau saa 8 kwa usiku mmoja, kupata mapumziko na kupata burudisho ili kuepukana na matatizo ya akili.

Angalau kufanya uchunguzi wa afya wa jumla mara moja kwa miezi 6, hii inasaidia kubaini matatizo ya kiafya mapema kwa gharama ndogo.

Kuwepo kwa ongezeko la vihatarishi vinavyochangia kutokea kwa matatizo hayo, ni muhimu wazee kushikamana na njia za kujikinga mapema kabla ya kuugua.

Kwa wanaotarajia kuelekea umri wa uzeeni kuanza kuchukua hatua hizi mapema na pia kuwekeza katika afya zao ikiwamo kuwa na bima za afya.

 By DK. SHITA SAMWEL

0 Comment

Rwanda na Kongo Kusaini Mkataba wa Amani mjini WashingtonAfyaclass Bongo Social •

Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo leo wanatarajiwa kusaini mkataba muhimu mjini Washington wa kumaliza mzozo uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la mashariki mwa Kongo ambapo mzozo huo umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kusababisha mateso makubwa kwa raia wa kawaida katika maeneo yaliyoathirika.



Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa mstari wa mbele katika kusukuma juhudi za kidiplomasia ambazo hatimaye zimezaa matunda kwa kufikiwa kwa mkataba huu na uongozi wake umetoa nafasi kwa mazungumzo ya kina kati ya pande husika, huku akihakikisha kwamba Marekani inatoa msaada wa kutosha kuleta suluhisho la kudumu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Tommy Pigolt, mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na Kongo wameshawasili Washington tayari kwa hafla ya kusaini vilevile kkataba huo utatiwa saini mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio katika hafla maalum inayolenga kuonyesha mshikamano na dhamira ya kweli ya amani.

Aidha katika taarifa ya pamoja iliyotolewa kabla ya hafla hiyo, Mataifa hayo matatu yamesisitiza kuwa mkataba huo utaheshimu mipaka ya kimataifa utapiga marufuku machafuko ya aina yoyote na utaweka utaratibu wa kupokonya silaha makundi yote yasiyo ya kiserikali yaliyojihami huku lengo kuu ni kurejesha utulivu wa kudumu na amani kwa wakazi wa mashariki mwa Kongo.

VIA @dw_kiswahili

0 Comment

TAARIFA:Bunge la 12 kuhitimishwa Leo,DodomaAfyaclass Bongo Social •

DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan leo anatarajiwa kuhitimisha Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli alizindua bunge hilo Novemba 13, 2020 jijini Dodoma kwa kuzingatia Ibara ya 91 Ibara ndogo ya kwanza ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi alisema bungeni kuwa leo Rais Samia atahutubia bunge na kuhitimisha shughuli za Bunge la 12.

0 Comment

Magonjwa yasio ambukiza ni magonjwa ya aina ganiAfyaclass Bongo Social •

Ni moja kati ya magonjwa ambayo sio ambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine. Vilevile ni kati ya magonjwa ambayo ni endelevu.



Kuna magonjwa makuu manne yasiyo ambukizi

  1. Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu-shambulizi la moyo na kiharusi
  2. Kansa au saratani
  3. Kisukari
  4. Magonjwa sugu yasababishayo kuziba mfumo wa upumuaji kitaalamu COPD’s

Kulingana na taarifa za shirika la afya duniani

Watu milioni 36 kila mwaka huathiriwa na magonjwa yasiyo ambukizi

Karibu asilimia 80 sawa na watu milioni 29 hufa kutokana na magonjwa yasiyo ambukizi katika nchi za vipato vidogo na vya kati.

Magonjwa ya moyo na mishipa ya damu ndio husababisha vifo zaidi watu milioni 17 kwa mwaka, ikifuatiwa na kansa watu milioni 7, mfumo wa upumuaji watu milioni 4, na kisukari milioni 1.

Magonjwa haya yote huweza kusababishwa na vifuatavyo: utumiaji wa tumbaku, kutofanya mazoezi kabisa, utumiaji wa pombe kupita kiasi, utumiaji wa vyakula visivyo bora.

Je magonjwa haya yanaathari gani kijamii na kiiuchumi?

Magonjwa haya yanaelekea kukwamisha malengo ya umoja wa taifa ya maendeleo ya milenia. Na kwasasa kuna uhusiano wa karibu kati ya umaskini na magonjwa yasiyoambukizi. Kuna uzorotaji wa juhudi za kupunguza umaskini kwasababu ya ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizi .

Mazingira magumu husabisha watu wa kipato cha chini kuumwa zaidi na kufa mapema kuliko wa kipato cha juu, kwasababu hao ndio huweza kupelekea kuwa karibu  na bidhaa zenye madhara kama tumbaku, chakula kischo bora na kutoweza kumudu huduma za afya. Umaskini huweza kuingia haraka kama magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kansa, kisukari na Magonjwa sugu yasababishayo kuziba mfumo wa upumuaji kitaalamu COPD’s yakivamia familia zisizo na uwezo kwasababu ya kuwa na rasilimali chache kwa ajili ya gharama za huduma ya afya.

Jinsi ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasioambukizi

Hapa mbinu elekezi huitajika hasa kwa kushirikisha sekta mabalimbali zikiwemo ya afya, elimu, fedha, na mipango ilikuzuia na kudhibiti magonjwa haya.

Cha muhimu kingine ni kupunguza vihatarishi ambavyo hupelekea kwenye magonjwa haya:

  • Kupunguza matumizi ya tumbaku
  • Kula chakula bora
  • Kufanya mazoezi
  • Kupunguza kunywa pombe

Elimu ya afya ya msingi itasaidia kugundulika na kutibiwa mapema kwa magonjwa haya

Njia nyingine ni kukuza uelewa kuhusu kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukizi kwa kuanzisha sera ya afya ya umma.

Kwa ufupi kwasasa kuna mlipuko wa magonjwa yasiyoambukizi hata hapa Nchini kwetu Tanzania, ni muhimu kuzingatia : mazoezi japo nusu saa kwa siku, kula chakula bora, kupunguza matumizi ya tumbaku na unywaji wa pombe. 

0 Comment

Watanzania 42 warejeshwa kutoka nchini Israel na IranAfyaclass Bongo Social •

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwarejesha salama nchini Watanzania 42 kutoka nchini Israel na Iran kufuatia vita vilivyokuwa vikiendelea baina ya mataifa hayo mawili.



Akizungumza mara baada ya kuwapokea Watanzania hao kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema zoezi la kuwarejesha Watanzania wote salama nchini ni utekelezaji wa agizo maalumu la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kwamba Watanzania wote waliopo katika mataifa hayo mawili wanarejeshwa nchini salama.

Aidha Balozi Shelukindo amesema Juni 25, 2025 wameingia Watanzania makundi mawili, kundi moja liliwasili mchana wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kwamba gharama zote za kuwarejesha Watanzania hao zimegharamiwa na serikali na kuongeza kuwa Watanzania wengine kutokea nchini Iran wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Juni 26, 2025.



0 Comment

Dalili za uvimbe kwenye kizazi pamoja na Chanzo chakeAfyaclass Bongo Social •

UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Uvimbe kwenye Kizazi ambapo kwa Kitaalam Hujulikana kama "FIBROIDS"- ni aina ya Uvimbe ambao hutokea katika kuta za ndani za Mji wa mimba(Kizazi)au huweza kutokea katikati ya kuta za Mji wa mimba,hivo kuleta madhara mengi. 



Kuta hizo za Mji wa mimba au Uterus zimegawanyika katika Maeneo au sehemu kuu Tatu.

  1. Ukuta wa Ndani kabsa-ambao hujulikana kitaalam kama Endometrium
  2. Ukuta wa katikati-ambao kitaalam hujilikana kama Myometrium
  3. Na ukuta wa Nje ya Uzazi-ambao kitaalam hujulikana kama Perimetrium

Kumbuka; Uvimbe kwenye kizazi Huweza kutokea katika maeneo mbali mbali ya Kizazi Mfano;  

- Kuna Uvimbe unaoweza kutokea kwenye vifuko vya mayai

- Kuna uvimbe kwenye kuta za Mji wa Uzazi kama nilivyoelezea hapo mwanzoni

- Kuna uvimbe unaoweza kutokea kwenye Mirija ya Uzazi n.k.

CHANZO CHA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Hakuna sababu ya Moja kwa moja ya mtu kupata Tatizo hili la Uvimbe wa kizazi,Japo kuna vitu ambavyo huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Uvimbe huu wa kwenye Kizazi, Kama vile;

1. Mabadiliko ya Vichocheo muhimu mwilini,hasa vile vinavyohusika na Ukuaji wa seli hai za mwili kama vile progesterone,estrogen,n.k

2. Tatizo la Unene pamoja na Uzito kupita kiasi

3. Kuwa na historia ya Tatizo la Uvimbe wa Kizazi katika Familia yenu

4. Mabadiliko flani ya Kigenetic,Kitaalam hujulikana kama genetic mutations

5. Umri mkubwa, Mwanamke ambaye hajawahi kupata mtoto hadi kufikia umri mkubwa anaweza kuwa kwenye hatari hii pia

6. Mwanamke kuwahi Sana kupata Hedhi au tunasema Hedhi ya Mapema: Kuanza kupata hedhi katika umri mdogo kunaweza kuwa sababu ya hatari

7. Baadhi ya vyakula,Zipo tafiti mbali mbali ambazo huonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu na pombe unaweza kuongeza hatari hii, ilhali ulaji mwingi wa matunda, mboga mboga, na nyuzinyuzi unaweza kuwa kinga kwa tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili ambazo huweza Kujitokeza kwa mtu mwenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi;

  • Kutokwa na Damu nyingi ya Hedhi (Heavy menstrual bleeding)
  • Kupata period kwa muda mrefu bila kukata au kupata period katikati ya mwezi au mara kwa mara
  • Kupata Maumivu makali ya Tumbo wakati wa Hedhi
  • Kupata maumivu makali ya Tumbo na Kiuno hasa wakati wa Tendo la Ndoa
  • Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wakati mwingine huambatana na harufu kali sehemu za Siri,hasa hasa kama uvimbe umeziba mirija ya Uzazi(fallopian Tubes)
  • Kutokwa na Damu wakati wa tendo la Ndoa
  • mvurugiko wa Mpangilio wa siku za Hedhi.
  • Lakini pia Uvimbe ukiwa Mkubwa sana huweza kuleta dalili kama;Kukojoa mara kwa mara,kwani nafasi kubwa ya uvimbe husababisha mgandamizo wa kibofu cha Mkojo, Kupata Choo kigumu sana,hata kukuletea maumivu makali sehemu ya Haja kubwa pamoja na Michubuko

MADHARA YA KUWA NA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI 

1. Maumivu makali wakati wa Hedhi na wakati wa Tendo la Ndoa

2. Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wenye harufu mbaya

3. kutolewa kizazi chote wakati wa matibabu kama uvimbe umeathiri sehemu kubwa ya Kizazi

4. Tatizo la kushindwa kubeba Ujauzito

5. Mvurugiko wa siku za Hedhi,ikiwemo kupata hedhi katikati ya mwezi

MATIBABU YA UVIMBE WA KIZAZI 

Kama una tatizo la Uvimbe kwenye kizazi Wasiliana na wataalam wa afya, Kuna dawa za kusaidia Uvimbe huu kuisha, Lakini pia endapo tatizo litashindikana,Njia ya mwisho kabsa ni kufanyiwa Upasuaji na Uvimbe huo kutolewa kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Kitundu wa Jua Kali,Sababu ya Kifo chake yatajwaAfyaclass Bongo Social •

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 26, 2025, Matei amesema Kitundu alianza kusumbuliwa na maradhi hayo miaka miwili iliyopita lakini familia ilimuuguza mpaka akarudi katika hali yake ya kawaida



Dar es Salaam. Matei Anamboka ambaye ni baba mdogo wa aliyekuwa mwigizaji wa filamu nchini, Radainus Vitalis 'Kitundu', amesema kilichoondoa uhai wa kijana wao ni maradhi ya kifua na tumbo.

Akizungumza na Mwananchi leo Juni 26, 2025, Matei amesema Kitundu alianza kusumbuliwa na maradhi hayo miaka miwili iliyopita lakini familia ilimuuguza mpaka akarudi katika hali yake ya kawaida.

"Marehemu alikuwa anasumbuliwa sana na kifua pamoja na tumbo, hiyo hali ilianza kutokea mwaka au miaka miwili nyuma. Tukamuuguza ambavyo tunaweza na tunamshukuru Mungu kwa muda ule baada ya kumuuguza kwa miezi sita akawa yupo vizuri, akarudi katika shughuli zake," amesema Matei.

Amesema kabla ya umauti wake, hali yake ilibadilika tena wiki mbili zilizopita mpaka kupelekea kifo.

"Tukapata taarifa anaumwa kama wiki mbili kabla ya kifo chake, sisi kama familia imetushitua hatukutegemea. Kingine marehemu hakuwa mtu wa kukaa hapa nyumbani, alikuwa anaishi huko anapifanyia shughuli zake mara nyingi tulikuwa tunawasiliana naye tu.

"Lakini baadaye tulifanya udadisi tukaambiwa alikuwa anaugua kama wiki tatu alikuwa anajiuguza mwenyewe, hali ilivyomzidia akarudi kwa familia ndiyo hivyo ndani ya wiki moja baada ya kulazwa umauti ukamkuta," amesema Matei.

Kuhusu marehemu kuacha mke au mtoto, Matei amesema Kitundu hajaacha mke wala mtoto, japo aliwahi kupata mtoto akafariki.

"Marehemu tunavyofahamu hakuwa na mtoto,lakini kama kuna taarifa nyingine tupo tayari kupokea," amesema Matei.
Kitundu alifariki dunia Jumanne jioni, Juni 24, 2025, ambapo taarifa za msiba huo zilitolewa kupitia ukurasa wa Instagram wa mzalishaji na mwongozaji wa tamthilia aliyokuwa akiigiza ya ‘Jua Kali’, Leah Mwendamseka 'Lamata.' 

Enzi za uhai wake, Kitundu aliigiza kwenye tamthilia ya Jua Kali kama kijana mwenye kipaji cha kucheza muziki anayetokea kwenye familia ya kimasikini. Kisha baadaye anapata nafasi ya kutoboa kimaisha lakini anashindwa kuitumia vizuri na kujikuta akirudi kwenye maisha ya kimasikini.

Muongozaji na mzalishaji mkuu wa tamthilia hiyo, Leah Mwendamseka 'Lamata' alibainisha kuwa kabla ya Kitundu kufariki, alikuwa anaumwa tangu mwaka jana na kupelekea kutoshiriki vizuri kwenye tamthilia ya Jua Kali.

0 Comment

NAIROBI : WATU wawili wamepoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwaAfyaclass Bongo Social •

NAIROBI : WATU wawili wamepoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa vibaya kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika hapo jana  jijini Nairobi.

Maandamano hayo yalikuwa ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu raia wa kizazi kipya, maarufu kama Gen Z, walipovamia Bunge la Kenya wakipinga sera za serikali ya Rais William Ruto. 

Polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji, hali iliyopelekea vurugu na majeruhi zaidi.Ghasia hizo zilisambaa hadi maeneo mengine ya nchi, ikiwemo Mombasa, Kisumu, Nakuru na Nyahururu. 

Wanaharakati pamoja na familia za waathirika waliongoza maandamano ya amani kuwakumbuka zaidi ya watu 64 waliouawa mwaka jana na wengine 20 ambao bado hawajulikani walipo.

"Tuko hapa kudai haki kwa mashujaa wetu. Hadi sasa hakuna afisa yeyote aliyewajibishwa. Tunataka haki, fidia, na mageuzi ya kweli katika idara ya polisi," alisema mwanaharakati Hussein Khalid.

Maandamano haya yanaendelea huku wananchi, hususan vijana, wakielezea kuchoshwa na kupanda kwa gharama ya maisha na ukatili wa polisi. Hivi karibuni, mwanablogu na mwalimu, Albert Ojwang, aliripotiwa kuuawa akiwa mikononi mwa polisi.

0 Comment

Mchambuzi maarufu wa mieleka Jim Ross ametangaza kuwa hana saratani Afyaclass Bongo Social •

Rasmi,Mchambuzi maarufu wa mieleka Jim Ross ametangaza kuwa hana saratani kufuatia upasuaji uliofanywa mwezi uliopita wa kutibu saratani ya utumbo mpana.  Mtangazaji huyo wa AEW mwenye umri wa miaka 73 alishiriki habari hiyo kwenye podikasti yake ya "Grilling JR", akielezea utulivu na matumaini anapotarajia kurejea kazini.

 "Saratani ya koloni imepita, ambapo ninafurahi sana kusema," Ross alifichua, kulingana na Wrestling News.  Aliongeza kuwa anajisikia vizuri zaidi na ameweka malengo yake ya kurejea kipaza sauti kwenye tukio linalokuja la AEW la "All In".

 "Ndio, nimechoka kukaa nyumbani, na ninafurahia fursa zinazoningojea," Ross alisema.  "Ninajisikia vizuri."

Ross pia alichukua muda kumshukuru hadharani rais wa AEW Tony Khan kwa msaada wake wakati wa vita dhidi ya saratani hyo.  "Tony Khan alikuwa mzuri sana katika mchakato huu wote," Ross alisema.  "Aliniunga mkono kwa moyo wote na ninathamini hilo. Hivyo ndivyo bosi anapaswa kutenda - tunza watu wako. Na Tony Khan hakika amenitunza vizuri."

Akiwa na uzoefu wa miongo kadhaa na kazi ya kustaajabisha katika mieleka, Ross amekumbana na changamoto kadhaa za kiafya hapo awali, lakini aliapa kushinda saratani, na sasa ametimiza ahadi hiyo.  Mashabiki wake na jamii ya wanamieleka wamefurahia sana habari njema kutoka kwa Mchambuzi huyo.

0 Comment

Madhara ya kunyonya uke,Fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Kunyonya uke (oral sex kwa mwanamke, pia hujulikana kama cunnilingus) ni tendo la ngono ambapo mtu mmoja hutumia mdomo wake (ulimi, midomo) kushughulika na sehemu za siri za mwanamke kwa lengo la kumletea raha ya kingono.

Ingawa linaweza kuwa sehemu ya mapenzi ya hiari na ya kuridhisha kati ya wenzi wawili, linaweza pia kuwa na madhara fulani kiafya. Hapa chini ni maelezo kamili kuhusu madhara ya kunyonya uke:

1. Maambukizi ya Magonjwa ya Zinaa (STIs)

Kunyonya uke kunaweza kusababisha maambukizi mbalimbali ya magonjwa ya zinaa, hasa kama hakuna matumizi ya kinga kama dental dams (kifuniko maalum cha mpira):

Magonjwa yanayoweza kuambukizwa kupitia kunyonya uke ni pamoja na:

  • Virusi vya HPV (Human Papillomavirus): husababisha saratani ya shingo ya kizazi, koo, au midomo.
  • Virusi vya HSV (Herpes Simplex Virus): husababisha vipele au vidonda kwenye uke au mdomoni.
  • Gonorrhea na Chlamydia: zinaweza kuambukiza koo na uke.
  • Syphilis: huweza kusambaa kupitia vidonda vidogo visivyoonekana.
  • Hepatitis B na C
  • Virusi vya Ukimwi (HIV): Ingawa hatari ya maambukizi kwa njia hii ni ndogo, bado ipo, hasa kama kuna majeraha mdomoni au kwenye uke.

2. Majeraha ya ndani au mdomoni

  • Kusugua sana au kutumia nguvu nyingi kunaweza kusababisha mikwaruzo au maumivu kwenye uke au mdomoni.
  • Mikwaruzo hiyo inaweza kuongeza hatari ya maambukizi.

3. Kuathirika Kisaikolojia au Kiakili

  • Tendo hili linaweza kuwa chanzo cha msongo wa mawazo, hatia au aibu, hasa kama halijafanyika kwa ridhaa au linaenda kinyume na maadili ya mtu.
  • Baadhi ya watu hukumbwa na hisia za kujidharau au kujuta baada ya tendo.

4. Uwezekano wa kuharibu usafi wa uke

  • Mdomo una bacteria tofauti na wa uke. Hii inaweza kusababisha kuchanganya flora ya uke na kupelekea maambukizi kama:
    • Bacterial vaginosis (BV) – hali ya mabadiliko ya uwiano wa bakteria wa kawaida wa uke.
    • Uke kutoa harufu mbaya, kuwasha au uchafu wa rangi isiyo ya kawaida.

Njia za Kupunguza Madhara

  • Tumia dental dam au kondomu iliyokatwa kama kinga.
  • Pima afya mara kwa mara ikiwa una mwenza zaidi ya mmoja
  • Hakikisha hakuna maambukizi yoyote ya magonjwa kati yenu wawili
  • Epuka tendo hili ikiwa kuna vidonda au majereha mdomoni au ukeni.
  • Weka usafi wa kinywa na uke.
  • Zungumza na mwenzi wako kuhusu hisia, ridhaa na mipaka.

Hitimisho

Kunyonya uke ni jambo la hiari kati ya watu wazima wanaokubaliana, lakini lina hatari kiafya hasa kwa upande wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa na usafi wa uke. Hivo ni vyema kuchukua tahadhari zote za kiafya.

0 Comment

Godfrey Steven-I wish you Good|Audio|VideoAfyaclass Bongo Social •

Godfrey Steven-I wish you Good|Audio|Video|Wimbo wa Dini


Sikiliza na Tazama Wimbo Mzuri kutoka kwa Godfrey Steven-I wish you Good|Wimbo wa Dini



0 Comment

Matokeo simba na yanga leo,Yanga inaongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Afyaclass Bongo Social •

Yanga inaongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikichukua ubingwa mara 31 huku Simba ikishika nafasi ya pili ikifanya hivyo mara 22.



Pacome Zouzoua na Clement Mzize wamekuwa mashujaa wa Yanga leo hii baada ya kuiongoza timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, yaliyoihakikisha timu hiyo ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Matokeo hayo yameifanya Yanga imalize ikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi na pointi 82 huku Simba ilimaliza katika nafasi ya pili na pointi 78.

Zouzoua alitangulia kuifungia Yanga katika dakika ya 66 kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na refa Mohamed Amin baada ya kipa Moussa Camara kumfanyia faulo kiungo huyo wa Yanga katika eneo la hatari.

Wakati Simba ikipambana kusaka bao la kusawazisha, Mzize ambaye aliingia uwanjani akitokea benchi, aliipatia Yanga bao lililozika rasmi matumaini ya Simba kupata ushindi na kutwaa ubingwa akimalizia vyema pasi ya Pacome.

Ushindi huo haukupatikana kwa kubahatisha kwa Yanga kwani ilionekana kutawala muda mwingi wa mechi ikitengeneza nafasi nyingi tofauti na Simba ambayo ilifanya hivyo mara chache huku ikitengeneza idadi ndogo ya nafasi.

Yanga ingeweza kuimaliza mechi katika kipindi cha kwanza lakini ilishindwa kutumia vyema nafasi ambazo ilitengeneza.

Mfano ni dakika ya 12 baada ya Mudathir Yahya kufanya kazi nzuri ya kumtoka Chamou Karaboue na kupiga pasi iliyoenda kwa Pacome Zouzoua ambaye akiwa analitaza lango, alipaisha mpira huo.

Dakika sita baadaye Chadrack Boka alipokea pasi nzuri ya Israel Mwenda lakini wakati wengi wakiamini angeweka mpira huo kimiani, beki huyo alipiga shuti lililotoka nje.

Simba walijibu shambulizi hilo katika dakika ya 27 baada ya Shomary Kapombe kupiga krosi nzuri kuielekeza kwa Steven Mukwala lakini kipa Djigui Diarra wa Yanga aliwahi kuokoa mpira huo.

Hadi filimbi ya refa Amin ilipopulizwa kuashiria muda wa mapumziko, timu hizo zilienda vyumbani zikiwa hazijafungana.

Hata hivyo mambo yalikuwa magumu kwa Simba katika kipindi cha pili ambacho licha ya kujaribu kufunguka kusaka mabao, ilijikuta ikiruhusu mabao hayo mawili ambayo yamefanya taji la Ligi Kuu msimu huu kwenda kwa watani wao Yanga.

Katika mchezo huo, Yanga ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Prince Dube, Pacome Zouzoua, Maxi Nzengeli na Mudathir Yahya ambao nafasi zao zilichukuliwa na Clatous Chama, Salum Abubakar, Jonathan Ikangalombo na Mzize.

Simba iliwatoa Steven Mukwala, Shomari Kapombe, Yusuph Kagoma, Joshua Mutale na Fabrice Ngoma ambao nafasi zao zilichukuliwa na Leonel Ateba, Awesu Awesu, Abdulrazack Hamza, Valentine Nouma na Kibu Denis.

Yanga imetwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 82 huku Simba ikimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 78.

Hilo ni taji la 31 la Ligi Kuu kwa Yanga huku watani zao Simba wakiwa wametwaa mara 22.

Matokeo hayo yameifanya Yanga iwe imepata ushindi katika mechi tano mfululizo za mashindano tofauti dhidi ya Simba.

Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga kilichoanza kiliundwa na Djigui Diarra, Israel Mwenda, Chadrack Boka, Dickson Job, Ibrahim Abdullah, Khalid Aucho, Duke Abuya, Mudathir Yahya, Prince Dube, Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli.

Simba ilianzisha kikosi kilichokuwa na Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Che Fondoh Malone, Chamou Karaboue, Yusuph Kagoma, Joshua Mutale, Fabrice Ngoma, Steven Mukwala, Jean Ahoua na Elie Mpanzu.

0 Comment

SERIKALI ya Zambia kusitisha mazishi ya Rais mstaafu Edgar Lungu,Afrika KusiniAfyaclass Bongo Social •

SERIKALI ya Zambia imewasilisha mahakamani maombi ya kusitisha mazishi ya faragha ya Rais mstaafu Edgar Lungu, yaliyotakiwa kufanyika Afrika Kusini, leo, Juni 25, 2025.



Kesi hiyo imesikilizwa kwa saa moja, kabla ya ibada ya mazishi yake kuanza.

Serikali ya Zambia inataka Lungu afanyiwe mazishi ya kitaifa nyumbani, kitu kinachopingwa na familia ya Lungu, kutokana na kile kilichoelezwa ni uadui wa kisiasa uliodumu kwa muda mrefu kati yake na Rais wa sasa wa Zambia, Hakainde Hichilema.

Wanafamilia ya Lungu waliokuwa wamevalia nguo nyeusi kwa ajili ya mazishi, walikwenda hadi mahakamani jijini Pretoria, Afrika Kusini, kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi hiyo ambayo ingeamua kama anaweza kuzikwa. 

Bado haiko wazi ni lini jaji atatoa uamuzi.

Lungu, ambaye aliongoza Zambia kati ya 2015 hadi 2021, alifariki dunia hospitalini nchini Afrika Kusini Juni 5, 2025 akiwa na miaka 68, kwa ugonjwa ambao haujawekwa bayana.

Maziko ya kitaifa nchini Zambia yalifutwa mara mbili, kwa sababu ya kutokubaliana juu ya mipango ya mazishi, kati ya familia na serikali.

Familia yake na wanasheria wanasema aliacha maagizo maalum kwamba hatataka Hichilema kuhudhuria mazishi yake, wakati serikali ya Zambia ikisema Hichilema alitakiwa kuongoza mazishi ya kiserikali.

Mwanasheria Mkuu wa Zambia, Mulilo Kabesha, aliwasilisha maombi hayo kwenye mahakama jijini Pretoria, Afrika Kusini jana Juni 24, 2025 iliyotaka zuio la haraka la mahakama la mazishi yaliyotarajiwa kufanyika leo, Juni 25, 2025.

Shirika la Utangazaji la Taifa la Zambia (ZNBC), limeripoti kuwa maombi hayo yanataka rais huyo wa zamani azikwe nchini Zambia kwa heshima kamili za kijeshi, kama ilivyoagizwa kwenye sheria za Zambia na kwa kuzingatia kwa maslahi ya umma.

Familia inasema kuwa ibada ya mazishi ya Lungu, ilitarajiwa kufanyika katika kanisa moja jijini Johannesburg, takribani kilomita 60 kutoka Pretoria na maziko yake yangefanyika kwa faragha.

Chanzo: DW

0 Comment

Hatma ya Msanii Diddy kujulikana hivi karibuniAfyaclass Bongo Social •

Juni  23,2025 upande wa mashtaka ulipeleka shahidi wa 34 na wa mwisho ambaye ni Afisa Maalum wa Usalama wa Ndani Joseph Cerciello, ambaye ushuhuda wake uliangazia siku 28 kutoka mwanzo wa kesi mpaka sasa.



Marekani. Mahakama ya jijini Manhattan imeendelea na kesi ya Sean “Diddy” Combs ambapo kwa sasa inaelezwa kesi hiyo ipo ukingoni huku hatma ya rapa huyo kujulikana hivi karibuni.

Juni  23,2025 upande wa mashtaka ulipeleka shahidi wa 34 na wa mwisho ambaye ni Afisa Maalum wa Usalama wa Ndani Joseph Cerciello, ambaye ushuhuda wake uliangazia siku 28 kutoka mwanzo wa kesi mpaka sasa.

Katika ushahidi wake Afisa Cerciello alieleza kuwa uchunguzi ulionesha mifumo yote ambayo Diddy alikuwa akiitumia kusafirisha wanawake kwa ajili ya biashara za kingono akitumia ushawishi wake katika muziki ili kudhibiti wanawake hao.

Aidha Cerciello alionesha rekodi za safari, mawasiliano ya kidigitali, video na mashahidi waliolazimisha kushiriki kwenye matukio ya kingono.

Katika siku hiyo hiyo tukio jingine ambalo liliwashangaza wengi ni baada ya mawakili wa Diddy akiongozwa na Marc Agnifilo kutangaza kutokuwa na mpango wa kupeleka mashahidi kwa ajili ya kumtetea rapa huyo.

Utakumbuka wiki iliyopita mawakili hao walipanga kupeleka mashahidi watatu akiwemo Diddy mwenyewe, msaidizi wa Combs Enterprises pamoja na mtaalamu wa saikolojia. Hata hivyo kwa mujibu wa mwanasheria mstaafu Mark Chutkow ameeleza kuwa uamuzi huo ni wa busara kwani utaepusha maswali yatakayo mchanganya Diddy.

Hata hivyo baada ya ushahidi kukamilika Juni 26 viongozi wa pande zote watatoa hoja zao za mwisho, kisha wajumbe wa mahakama ya kisheria wataanza mjadala wa mwisho na uamuzi wa hatima ya kesi hiyo. Kwa sasa, Diddy amekana mashtaka yote huku akikataliwa dhamana mara tatu kutokana na hofu ya kuwahonga mashahidi.

Baadhi ya mashahidi wa muhimu waliotoa ushahidi wa kuathiriwa na matukio ya kingono ni pamoja na wapenzi wa zamani wa Diddy, Jane na Cassie huku wengine ni pamoja na rapa Kid Cudi, mlinzi wa nyumbani kwa Diddy, Mia, Capricorn Clark, Kerry Morgan, Bryana Bongolan na wengineo.

Diddy anakabiliwa na mashtaka ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, njama ya kihalifu (racketeering) na usafirishaji kwa lengo la kushiriki katika ukahaba. Licha ya kukana mashtaka yote. Endapo rapa huyo atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan huko Brooklyn. Kesi yake ilianza kusikilizwa Mei 5,2025.

0 Comment

Simba imetoa ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wao Afyaclass Bongo Social •

Klabu ya Simba imetoa ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wakieleza kufurahishwa na ushirikiano walioupata kutoka kwa wapenzi wa klabu hiyo katika msimu wa 2024/25.



"Kwa Wanasimba wote, asanteni kwa ushirikiano ambao mmetupatia kwa msimu wa 2024/25. Tunajivunia kuwa na mashabiki kama nyie," ilisomeka sehemu ya ujumbe huo.

Hata hivyo, ujumbe huo umetolewa katika siku ambayo klabu hiyo ilitarajiwa kushiriki kwenye mechi kubwa ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC hali inayozua sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Tayari dalili za sintofahamu zilianza kujitokeza tangu jana, baada ya Simba kushindwa kupeleka wawakilishi kwenye mkutano rasmi na waandishi wa habari uliopangwa kuelekea mchezo huo.

Hali hiyo imezua maswali mengi kuhusu uwezekano wa Simba kujitokeza uwanjani kwa ajili ya mchezo huo.

0 Comment

Kwanini Watu hujitolea kuambukizwa magonjwaAfyaclass Bongo Social •

Kujaribu matibabu mapya au chanjo mpya kunaweza kuchukua miaka mingi, ikiwa sio miongo kukusanya taarifa za kutosha, kwa hivyo wanasayansi wanageukia njia yenye utata ambayo inahusisha kuwaambukiza makusudi virusi hatari, vimelea na bakteria watu waliojitolea.



Mwaka 2017 kulikuwa na kundi la vijana waliokuwa wakisubiri kushambuliwa na mbu waliobeba vimelea vinavyoua zaidi ya watu 600,000 kila mwaka.

Kundi hilo lilikubali kushiriki majaribio ya matibabu katika Taasisi ya Jenner ya Chuo Kikuu cha Oxford, ili kupima chanjo mpya dhidi ya malaria. Chanjo hiyo - inajulikana kama "R21."

Taasisi hiyo imekuwa ikifanya majaribio ya chanjo ya mbu tangu 2001. Kila mtu aliyejitolea aliingizwa katika maabara. Juu ya meza ndani ya maabara, kulikuwa na bakuli dogo, kama umbo la kikombe cha kahawa, na kifuniko cha kitambaa chembamba juu.

Ndani yake kuna mbu watano waliokuwa wakipiga kelele, kutoka Amerika Kaskazini, ambao walikuwa wameambukizwa vimelea vya malaria. Mtu aliyejitolea anaweka mkono wake juu ya kibakuli ili mbu waweze kumtafuna, wakiuma kupitia kitambaa chembamba na kuingia kwenye ngozi ya mtu aliyejitolea.

0 Comment

Alisema hanipendi kwa sababu tu nimetoka shule fulaniAfyaclass Bongo Social •

Baharia mbalimbali wametoa simulizi kuhusu uzoefu wao wa unyanyasaji au kutothaminiwa kwa sababu ya chimbuko, jinsia au shule walikosomea. Mark Phillip Laurilla anakumbuka alivyokaribishwa kwa kejeli na Mhandisi Mkuu wa meli:



“Alisema hanipendi kwa sababu tu nimetoka shule fulani.” - Mark Phillip Laurilla.

Jugu Weng Yohanna, Afisa Mwanafunzi, anasema alishangaa kusikia kuwa ubaharia ni taaluma ya wanaume pekee alipokuwa akisomea taaluma hiyo shuleni.

Mabadiliko yanayoletwa na sekta

Nahodha wa Meli ya Hafnia, Manindra Singh, anakiri kwamba miaka ya nyuma, unyanyasaji ulikuwa jambo la kawaida, lakini katika miaka ya karibuni hali imebadilika. Hafnia imeweka mifumo thabiti ya kupokea na kushughulikia malalamiko, kwa mujibu wa Shivas Kapoor, Mkuu wa Ajira ya Mabaharia katika kampuni hiyo.

“Tulihakikisha kuna mfumo rafiki kwa wanawake na wanaume kutoa malalamiko ya unyanyasaji.” - Kapoor

Uongozi na elimu ndio njia

Afisa Msaidizi wa Nahodha, Jing Jing Zhang, anaeleza kuwa mafunzo ya jinsi ya kuishi pamoja kama timu yenye tamaduni mbalimbali ni msingi wa kuondoa chuki na dharau. Mary Jane anasisitiza umuhimu wa kuuliza mara kwa mara jinsi wafanyakazi wanavyojisikia kazini. “Nimefanya kuwa ni desturi kuuliza kila mfanyakazi hali yake ya kihisia akiwa chomboni.”

0 Comment

Amin Mohamed Amin Omar kutoka nchini Misri mwamuzi Yanga na SimbaAfyaclass Bongo Social •



Waamuzi wa mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba wametangazwa rasmi, ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar kutoka nchini Misri.

Amin Omar ni mwamuzi mwenye uzoefu mkubwa wa kimataifa, aliyechezesha mechi kadhaa za CAF Champions League na kufahamika kwa uthabiti wake katika kusimamia michezo mikubwa.

0 Comment

Umemuandaaje mwanao kuwa mtu boraAfyaclass Bongo Social •

Tumetumia muda mwingi  kumfundisha mtoto wa kike na kusahau kuwa hiki kichwa (mume) kinatakiwa kufunzwa ili kifananie na  Kristo kwa maana nyingine tabia za Kimungu zionekane ndani ya mwanaume.



Bwana Yesu apewe sifa, karibu katika tafakari ya ujumbe wa leo. Mimi ninayekuletea ujumbe huu ni mtumishi wa Mungu Mwalimu Peace Marino  kutoka KKKT Usharika wa Ebeneza Nyashimo Jimbo la Kaskazini Busega.

Kipindi hiki watoto wamefunga shule na wapo nyumbani kwa ajili ya likizo ya masomo. Hiyo ni nafasi ya kipekee wazazi kukaa na watoto na kuwajenga katika msingi wa maadili yanayompasa ikiwamo kumfundisha kusali, kufanya maombi na kumcha Mungu kwa ujumla. Watoto wengi hupendelea kusafiri kwenda maeneo mbalimbali pamoja kutembelea ndugu jamaa na marafiki.

Licha ya hayo yote, Ujumbe tuliopewa leo ninataka kuzungumza nawe mzazi juu ya hatima bora ya vijana wetu wa kiume. Somo letu limebeba ujumbe “Umemuandaaje mwanao wa kiume kuwa mtu bora?”

Jamii nyingi zimekuwa zikimthamini mtoto wa kiume na kumpa hadhi kubwa na kusahau kuwa anahitaji mafunzo yatakayomsaidia kuwa bora katika jamii, kwenye kanisa na Taifa kwa ujumla.

Efeso 5:23b inasema "Kwa Maana mume ni kichwa cha mkewe kama Kristo naye ni kichwa cha kanisa.”

Tumetumia muda mwingi  kumfundisha mtoto wa kike na kusahau kuwa hiki kichwa (mume) kinatakiwa kufunzwa ili kifananie na  Kristo kwa maana nyingine tabia za Kimungu zionekane ndani ya mwanaume.

Tito 2:3-4. Inazungumza kwa habari ya wazee wa kike kufundisha mema na kuwapa maarifa wanawake, vijana ikiwa ni pamoja na kuwa na kiasi, kuwa safi, kufanya kazi, kuwa wema, kuwatii waume zao, kuwa wavumilivu na mambo mengine mengi. Jamii na kanisa tumejitahidi sana kutimiza jukumu hili.

Watoto wa kike wanapokosea tunawawajibisha kwelikweli na hakuna mama au baba anayetaka binti yake aharibikiwe, hivyo jicho la baba na mama liko kwa mtoto wa kike. Wakati mwingine hatujawapa nafasi ya kujieleza kwa nini amekosa au ameingia kwenye changamoto fulani badala yake huwa tunawaadhibu bila hata kujua chanzo cha tatizo. Tunafanya yote haya kwa sababu ya kuogopa kupata aibu.

Naomba nikuulize mpendwa, hivi nguvu unayotumia kumlinda binti yako ni sawa na unayotumia kumlinda mwanao wa kiume? Kwa nini? Binti akichelewa kurudi nyumbani anaadhibiwa vikali lakini kijana wa kiume hata aingie usiku jamii inaona ni sawa tu, jambo kama hili siyo sawa kwani halimuandai mwanao wa kiume kuwa bora.

Tito:2:6. Inasema “Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi.” Katika hili tunahitaji rehema ya Mungu kwani tumesahau kabisa kuwa tunalo jukumu la kuwasaidia watoto wa kiume na kama tunafanya ni kwa kiasi kidogo sana. Hatuna budi sasa kuamka na kulichukulia jambo hili kwa uzito ili kunusuru kizazi chetu.

Paulo anamwambia Timotheo 1:5 kuwa, “Naikumbuka imani uliyonayo isiyo na unafiki, ambayo ilikaa kwanza katika bibi yako Loisina katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo”

 “Kina mama hawa walimfundisha kijana wao na kumrithisha imani akakua nayo na hakuiacha. Wewe unawarithisha nini wanao, nani anajivunia wanao kutokana na jinsi ulivyowafunza vizuri?

Tupate wapi kina baba kama Ayubu tusipowafundisha? Tupate wapi kinababa ambao Mungu anajivunia tusipowafundisha? (Ayubu1:5) Ayubu aliamka asubuhi na mapema akasogeza sadaka kwa hesabu ya watoto wake wote akisema yamkini hawa wanangu wamefanya dhambi na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Tunao kina baba wangapi katika jamii zetu wanaokumbuka kutoa sadaka kwa ajili ya watoto wao au hata kufunga na kuomba kwa ajili ya watoto wao na uzao wao?

Kila binti anatamani kuolewa na kijana mwenye hofu ya Mungu ndani yake. Hiyo hofu ya Mungu atatolea wapi ikiwa hakuna wa kumfundisha? Wazazi tumekataa wachumba ambao mabinti zetu wametuletea kwa sababu tuliwaona hawana hofu ya Mungu ndani yao, kama hujaweza kumfundisha mwanao wa kiume ili afae kuwa mume wa binti fulani kina nani watamfundisha mkweo?

Binti akibeba mimba nje ya utaratibu ni kosa lisilo sameheka, mama itabidi utoe maelezo ya kutosha kwa baba yake limetokeaje jambo hilo. Mabinti wengine wamepigwa, wengine wamefukuzwa na maisha yao yakaharibika kabisa, lakini vipi kama kilichompata ni kama kile kilichompata Dina (Mwanzo 34) na Tamari (2 Samweli 13:1-14) mabinti hawa walibakwa. Wakati mwingine mabinti zetu wanapitia changamoto nyingi na ngumu na hawana namna na wapi pa kusemea. Ni lini baba au mama umekaa na binti yako na kutaka kujua anapitia changamoto gani?

Jambo kama hili linapotokea kwa watoto wa kiume hatuoni kama lina madhara linachukuliwa kama jambo la kawaida. Mwanzo 34:8 Shekemu anapomtendea hiana Dina, baba yake Shekemu (Hamori) anakwenda kwa Yakobo kuomba watoto waoane bila hata kujali ni maumivu kiasi gani Dina anapitia. Hatuoni ni wapi Hamori anamuwajibisha mwanaye wa kiume kwa kosa alilolifanya. Mpendwa dhambi yoyote anayoifanya mwanao wa kiume na ukaifumbia macho ni mbegu unapanda na matunda yake utayaona, Yesu atuhurumie.

Tunapohitimisha nikusihi, umwangalie mwanao wa kiume kwa ukaribu na kumfundisha kama unavyofanya kwa mwanao wa kike ili kila mmoja afae kwa ufalme wa Mungu. Mungu akubariki sana.

Mhubiri ni Mwalimu Peace Marino kutoka KKKT Usharika wa Ebeneza Nyashimo, Jimbo la Kaskazini Busega mkoani Simiyu.

0 Comment

Israel na Iran ni ndugu asema mke wa NetanyahuAfyaclass Bongo Social •

Mwenza wa Waziri Mkuu wa Israel Sara Netanyahu ameutumia ukurasa wake wa Instagram kuwasilisha ujumbe wa upendo na amani kwa raia wa Iran kufuatia mgogoro unao endelea baina ya nchi hizo mbili akiashiria kuwa nchi hizo mbili ni ndugu na hawapaswi kuvutana.



Ujumbe huo wa Sara Netanyahu ni wito wa nchi hizo mbili ambazo zimekuwa na mzozo kuzitaka kumaliza mzozo huo akiitaja Irani kama nchi yenye utamaduni wa kipekee na utajiri wa kihistoria ambapo Israel na Irani sio maadui huku mvutano kati ya Israel na Iran unazidi kuongezeka hasa baada ya mashambulizi ya hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka picha ya simba wawili wakiwa za nchi hizo mbili akiambatanisha ujummbe usemao “Ninyi watu wa Iran ni warithi wa utamaduni mzuri Taifa lenye vipaji na historia nzuri. Sisi si maadui zenu. Vita vyetu ni na serikali ya kidikteta inayowadhulumu, si na ninyi.

Tunaamini katika mustakabali wa amani, uhuru, na urafiki kati yetu.”

Aidha picha hiyo ya Simba waliovikwa bendera ya Israel na Iran iliyotumiwa na Sara Netanyau Chaguo la simba katika picha hiyo linaonekana kuwasilisha marejeleo ya nembo ya Iran ya zama za Shah ambaye alikuwa mfalme aliyetawala Iran hadi 1979 wakati utawala wa ayatollah wenye msimamo mkali ulipoandaa Mapinduzi ya Kiislamu.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD