Dalili za uvimbe kwenye kizazi pamoja na Chanzo chake

Dalili za uvimbe kwenye kizazi pamoja na Chanzo chake

#1

UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Uvimbe kwenye Kizazi ambapo kwa Kitaalam Hujulikana kama "FIBROIDS"- ni aina ya Uvimbe ambao hutokea katika kuta za ndani za Mji wa mimba(Kizazi)au huweza kutokea katikati ya kuta za Mji wa mimba,hivo kuleta madhara mengi. 



Kuta hizo za Mji wa mimba au Uterus zimegawanyika katika Maeneo au sehemu kuu Tatu.

  1. Ukuta wa Ndani kabsa-ambao hujulikana kitaalam kama Endometrium
  2. Ukuta wa katikati-ambao kitaalam hujilikana kama Myometrium
  3. Na ukuta wa Nje ya Uzazi-ambao kitaalam hujulikana kama Perimetrium

Kumbuka; Uvimbe kwenye kizazi Huweza kutokea katika maeneo mbali mbali ya Kizazi Mfano;  

- Kuna Uvimbe unaoweza kutokea kwenye vifuko vya mayai

- Kuna uvimbe kwenye kuta za Mji wa Uzazi kama nilivyoelezea hapo mwanzoni

- Kuna uvimbe unaoweza kutokea kwenye Mirija ya Uzazi n.k.

CHANZO CHA UVIMBE KWENYE KIZAZI NI NINI?

Hakuna sababu ya Moja kwa moja ya mtu kupata Tatizo hili la Uvimbe wa kizazi,Japo kuna vitu ambavyo huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Uvimbe huu wa kwenye Kizazi, Kama vile;

1. Mabadiliko ya Vichocheo muhimu mwilini,hasa vile vinavyohusika na Ukuaji wa seli hai za mwili kama vile progesterone,estrogen,n.k

2. Tatizo la Unene pamoja na Uzito kupita kiasi

3. Kuwa na historia ya Tatizo la Uvimbe wa Kizazi katika Familia yenu

4. Mabadiliko flani ya Kigenetic,Kitaalam hujulikana kama genetic mutations

5. Umri mkubwa, Mwanamke ambaye hajawahi kupata mtoto hadi kufikia umri mkubwa anaweza kuwa kwenye hatari hii pia

6. Mwanamke kuwahi Sana kupata Hedhi au tunasema Hedhi ya Mapema: Kuanza kupata hedhi katika umri mdogo kunaweza kuwa sababu ya hatari

7. Baadhi ya vyakula,Zipo tafiti mbali mbali ambazo huonyesha kwamba ulaji mwingi wa nyama nyekundu na pombe unaweza kuongeza hatari hii, ilhali ulaji mwingi wa matunda, mboga mboga, na nyuzinyuzi unaweza kuwa kinga kwa tatizo hili.

DALILI ZA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili ambazo huweza Kujitokeza kwa mtu mwenye tatizo la Uvimbe kwenye kizazi;

  • Kutokwa na Damu nyingi ya Hedhi (Heavy menstrual bleeding)
  • Kupata period kwa muda mrefu bila kukata au kupata period katikati ya mwezi au mara kwa mara
  • Kupata Maumivu makali ya Tumbo wakati wa Hedhi
  • Kupata maumivu makali ya Tumbo na Kiuno hasa wakati wa Tendo la Ndoa
  • Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wakati mwingine huambatana na harufu kali sehemu za Siri,hasa hasa kama uvimbe umeziba mirija ya Uzazi(fallopian Tubes)
  • Kutokwa na Damu wakati wa tendo la Ndoa
  • mvurugiko wa Mpangilio wa siku za Hedhi.
  • Lakini pia Uvimbe ukiwa Mkubwa sana huweza kuleta dalili kama;Kukojoa mara kwa mara,kwani nafasi kubwa ya uvimbe husababisha mgandamizo wa kibofu cha Mkojo, Kupata Choo kigumu sana,hata kukuletea maumivu makali sehemu ya Haja kubwa pamoja na Michubuko

MADHARA YA KUWA NA TATIZO LA UVIMBE WA KIZAZI 

1. Maumivu makali wakati wa Hedhi na wakati wa Tendo la Ndoa

2. Kutokwa na Uchafu mwingi ukeni na wenye harufu mbaya

3. kutolewa kizazi chote wakati wa matibabu kama uvimbe umeathiri sehemu kubwa ya Kizazi

4. Tatizo la kushindwa kubeba Ujauzito

5. Mvurugiko wa siku za Hedhi,ikiwemo kupata hedhi katikati ya mwezi

MATIBABU YA UVIMBE WA KIZAZI 

Kama una tatizo la Uvimbe kwenye kizazi Wasiliana na wataalam wa afya, Kuna dawa za kusaidia Uvimbe huu kuisha, Lakini pia endapo tatizo litashindikana,Njia ya mwisho kabsa ni kufanyiwa Upasuaji na Uvimbe huo kutolewa kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code