Klabu ya Simba imetoa ujumbe wa shukrani kwa mashabiki wao kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wakieleza kufurahishwa na ushirikiano walioupata kutoka kwa wapenzi wa klabu hiyo katika msimu wa 2024/25.
"Kwa Wanasimba wote, asanteni kwa ushirikiano ambao mmetupatia kwa msimu wa 2024/25. Tunajivunia kuwa na mashabiki kama nyie," ilisomeka sehemu ya ujumbe huo.
Hata hivyo, ujumbe huo umetolewa katika siku ambayo klabu hiyo ilitarajiwa kushiriki kwenye mechi kubwa ya Dabi ya Kariakoo dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC hali inayozua sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka nchini.
Tayari dalili za sintofahamu zilianza kujitokeza tangu jana, baada ya Simba kushindwa kupeleka wawakilishi kwenye mkutano rasmi na waandishi wa habari uliopangwa kuelekea mchezo huo.
Hali hiyo imezua maswali mengi kuhusu uwezekano wa Simba kujitokeza uwanjani kwa ajili ya mchezo huo.
REPLY HAPA
image quote pre code