NAIROBI : WATU wawili wamepoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa vibaya kufuatia maandamano makubwa yaliyofanyika hapo jana jijini Nairobi.
Maandamano hayo yalikuwa ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu raia wa kizazi kipya, maarufu kama Gen Z, walipovamia Bunge la Kenya wakipinga sera za serikali ya Rais William Ruto.
Polisi walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji, hali iliyopelekea vurugu na majeruhi zaidi.Ghasia hizo zilisambaa hadi maeneo mengine ya nchi, ikiwemo Mombasa, Kisumu, Nakuru na Nyahururu.
Wanaharakati pamoja na familia za waathirika waliongoza maandamano ya amani kuwakumbuka zaidi ya watu 64 waliouawa mwaka jana na wengine 20 ambao bado hawajulikani walipo.
"Tuko hapa kudai haki kwa mashujaa wetu. Hadi sasa hakuna afisa yeyote aliyewajibishwa. Tunataka haki, fidia, na mageuzi ya kweli katika idara ya polisi," alisema mwanaharakati Hussein Khalid.
Maandamano haya yanaendelea huku wananchi, hususan vijana, wakielezea kuchoshwa na kupanda kwa gharama ya maisha na ukatili wa polisi. Hivi karibuni, mwanablogu na mwalimu, Albert Ojwang, aliripotiwa kuuawa akiwa mikononi mwa polisi.
REPLY HAPA
image quote pre code