AJIRA MPYA:Serikali yamwaga ajira mpya bandari

AJIRA MPYA:Serikali yamwaga ajira mpya bandari

#1

Dar es Salaam. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) imetangaza nafasi 184 za kazi.



Tangazo hilo la ajira limetolewa Juni 27, 2025 ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kuongeza ufanisi ndani ya taasisi zake.

Kwa upande wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imetangaza nafasi 176 kwa Watanzania wenye sifa stahiki na wanaojituma, kama iliyoorodheshwa hapa chini.

Miongoni mwa nafasi hizo ni pamoja na zimamoto, wataalamu wa mashine za ukaguzi, nahodha, nahonda wasaidizi, wakufunzi wa unahodha na nafasi nyinginezo.

Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimetangaza nafasi nane zikiwemo za wakufunzi.

Katika masharti ya jumla ya kwa waombaji wanatakiwa wawe Raia wa Tanzania wenye umri usiozidi miaka 45.

Watu wenye ulemavu wanahimizwa kuomba, maombi yaambatane na wasifu (CV) wa kisasa, wenye mawasiliano ya uhakika.

Wajaze taarifa kwa kuzingatia tangazo husika, wawasilishe vyeti vilivyothibitishwa, stashahada au shahada na transkripti za kidato cha nne na sita, vyeti vya usajili kitaaluma pamoja na cheti cha kuzaliwa.

Pia wanatakiwa waambatanishe picha ndogo (passport size) ya hivi karibuni.

Watumishi wa umma hawaruhusiwi kuomba, wastaafu wa umma hawaruhusiwi kuomba, wataje watu watatu wanaowajua (referee), wenye mawasiliano ya uhakika, vyeti vya nje vya O/A-Level vithibitishwe na NECTA.

Vyeti vya taaluma vya nje vibatilishwe na TCU/NACTE, barua ya maombi isainiwe, iwe kwa Kiswahili au Kiingereza na ipelekwe kwa Katibu, Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira, S.L.P 2320, Dodoma.

Mwisho wa kutuma maombi hayo ni Julai, 9, 2025 na waliochaguliwa kwa usaili watapewa taarifa na vyeti vya kughushi vitasababisha hatua za kisheria.

REPLY HAPA


image quote pre code