Viwango vya kubadili fedha nchini Tanzania Julai 30, 2025Afyaclass Bongo Social •

Viwango vya kubadili fedha nchini Tanzania Julai 30, 2025

Viwango vya kubadilisha fedha za kigeni dhidi ya Shilingi ya Tanzania kutoka Benki za CRDB na NMB unavyoweza kutumia katika shughuli zako za biashara leo Julai 30, 2025.

Viwango hivi, vinavyotarajiwa kubadilika kutokana na mwenendo wa soko wa kila siku, husaidia watumiaji wa sarafu za kigeni kufanya manunuzi ikiwemo kuingiza bidhaa kutoka nje ya nchi.Credits:Nukta



0 Comment

Ugonjwa wa Kipindupindu watesa Afrika Magharibi na Kati – DRC ikiwa Kitovu cha MlipukoAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Kipindupindu watesa Afrika Magharibi na Kati – DRC ikiwa Kitovu cha Mlipuko



Wakati mvua zikiripotiwa kuanza kunyesha katika maeneo mbalimba ya Afrika Magharibi na Kati, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Watoto UNICEF limeripoti kuwa takribani watoto 80,000 wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa ugonjwa wa kipindupindu.

Taarifa iliyotolewa leo na shirika hilo kutoka Dakar Senegal imeripoti kuwa nchi 12 zimeathirika na mlipuko huu unaoenea kwa kasi, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo -DRC ikitajwa kuwa ndiyo iliyoathirika zaidi.

DRC hali ni mbaya

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya ya DRC, zaidi ya wagonjwa 38,000 wa kipindupindu na vifo 951 vimeripotiwa nchini humo mwezi huu wa Julai pekee. Takribani asilimia 25.6 ya wagonjwa wa kipindupindu ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

Mkurugenzi wa UNICEF wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Gilles Fagninou amesema “Hii ni hali ya dharura inayohitaji hatua za haraka, ni suala la maisha na kifo.”

Maeneo yaliyoathirika zaidi ni pamoja na majimbo ya South Kivu, North Kivu, Haut Katanga, Tshopo, Haut Lomami, Tanganyika, na Maniema.

Jiji la Kinshasa limeingia kwenye hali ya dharura baada ya ongezeko kubwa la maambukizi ndani ya wiki nne zilizopita kufuatia mafuriko makubwa na mvua zinazoendelea, huku kiwango cha vifo kwa wagonjwa kikifikia asilimia 8, hiki ni kiwango cha kutisha kwa muktadha wa ugonjwa huu unaotibika haraka iwapo utagundulika mapema.

“Hali mbaya ya mvua, mafuriko na watu wengi waliolazimika kuhama makazi yao vinaongeza kasi ya kusambaa kwa kipindupindu na kuweka maisha ya watoto hatarini,” amesemaFagninou

UNICEF inaonya kuwa bila hatua madhubuti za kudhibiti mlipuko huu, DRC inaweza kukumbwa na janga la kipindupindu kubwa zaidi tangu mwaka 2017.

Hali ilivyo katika mataifa mengine

Nchi nyingine zilizoathirika ni Nigeria (wagonjwa 3,109 na vifo 86), Chad (wagonjwa 55 na vifo 4), Ghana (wagonjwa 612), Côte d’Ivoire (wagonjwa 322 na vifo 15), na Togo (wagonjwa 209 na vifo 5).

Nchi kama Niger, Benin, Liberia, Jamhuri ya Afrika ya Kati, na Cameroon zinaendelea kufuatiliwa kwa karibu.

Mkuu huyo wa kanda wa UNICEF amesema “Tupo kwenye mbio dhidi ya wakati, tukishirikiana na serikali kutoa huduma muhimu kama maji safi na salama, lishe na huduma za afya kwa watoto walio katika hatari kubwa. Tunafanya kila jitihada kuhakikisha hakuna mtoto anayesahaulika.”

UNICEF imekuwa mstari wa mbele kusambaza huduma za afya, maji safi, vifaa vya usafi na katika utoaji wa chanjo, pamoja na kuelimisha jamii kuhusu kinga na tiba ya kipindupindu.

Hata hivyo, shirika hilo linahitaji dola milioni 20 ndani ya miezi mitatu ijayo ili kuongeza kasi ya msaada katika nchi zilizoathirika.

0 Comment

Obby Alpha-Makosa|Audio|Sikiliza|downloadAfyaclass Bongo Social •

 Obby Alpha-Makosa|Audio|Sikiliza|download

Listen to “Obby Alpha – Makosa” below;

0 Comment

Tsunami yaipiga Urusi pamoja na JapanAfyaclass Bongo Social •

Madhara na uhamishwaji wa watu umeripotiwa kwenye mikoa ya Urusi iliyo karibu na kitovu cha tetemeko hilo katika Rasi ya Kamchatka.



Tetemeko hilo ni kubwa kabisa kuwahi kulipiga eneo hilo tangu mwaka 1952, kwa mujibu wa Mamlaka ya Jiolojia ya Urusi.

Tsunami iliyopelekea mawimbi ya bahari yenye ukubwa wa hadi mita 30 imeripotiwa katika visiwa vya Hokkaido vya Japan na visiwa vya Kuril vinavyomilikiwa na Urusi, na yanakhofiwa kuelekea pia Ufilipino, Chile na Visiwa vya Solomon.

Tayari Ufilipino nayo imetangaza tahadhari ya kiwango cha juu ya tsunami.

Athari za tetemeko hilo zinatazamiwa kuonekana hadi nchini Marekani kwenye miji ya Carlifornia na Washington. 

0 Comment

Dawa za ARV,Matumizi Sahihi ya dawa za ARVAfyaclass Bongo Social •

Dawa za ARV,Matumizi Sahihi ya dawa za ARV



Moja kati ya vitu vya msingi vya kuzingatia ukiwa muathirika wa ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni matumizi sahihi ya dawa.Watu wengi wamepotoshwa na taarifa za uongo kuwa  dawa hizi hupunguza nguvu za kiume hivyo wagonjwa wengi wa UKIMWI hawatumii dawa  hizi na badala yake hutumia mitishamba au kutokutumia dawa kabisa.

Tafiti nyingi zimefanyika na kuonyesha kwamba dawa hizi zina uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa yatokanayo na UKIMWI na kuzuia vifo. Aidha dawa  hizi zimeonyosha uwezo mkubwa wa kupunguza maambukizi ya mama kwa mtoto.Matumizi ya dawa  za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI kwa waathirika wa ugonjwa huu yanahusishwa na  kupungua kwa hatari ya kueneza maambukizi ya virusi vya VVU/UKIMWI wakati wa kushiriki tendo la ndo  kwa sababu ya uwezo wake wa kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.

KUKMBUKA dawa hizi sio tiba ya virusi vya VVU/UKIMWI.

Utaratibu wa Kuanza Dawa

Kulingana na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI anashauriwa kuanza dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI mara tu anapogundulika kuwa ni muathirika wa virusi vya VVU/UKIMWI na kupewa ushauri nasaha. Hii husaidia sana kupunguza makali ya virusi hivi.

Utaratibu wa kuanza dawa huambatana na kujisajili kwenye za kliniki za CTC ambazo zipo kwenye takribani vituo vyote vya afya nchini. Ukishajisajili utapewa namba pamoja na kadi ambayo itakuwa na taarifa zako zote muhimu kama muda au tarehe ya kumuona dakatri, aina na kiwango cha dawa  unachotumia , wingi wa virusi vya VVU kwenye damu (viral load) na kiwango cha CD4.

Endapo uligundulika na virusi vya VVU/UKIMWI na umeshaanza kupata magonjwa nyemelezi, basi utaanza matibabu ya magonjwa hayo na kuanzishiwa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ndani ya wiki mbili.

Kuna baadhi ya magonjwa ikiwemo kifua kikuu (PTB)   pamoja na ugonjwa wa kukakamaa shingo (Cryptococcoal Meningitis) huwa kuanza kutumia dawa haraka sio vizuri kwani inaongeza hatari ya kupata mchafuko wa kinga ya mwili (Immune Reconstitution Inflammatory Syndrome- IRIS) ambayo huzidisha dalili za magonjwa nyemelezi.

Hali hii hutokea kwa sababu madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI husaidia kuongeza kinga ya mwili na hivyo mwili huanza vita na magonjwa nyemelezi ambayo mwanzo mwili ulikuwa hauna uwezo wa kuyadhiti hii huleta mchafuko wa kinga ya mwili na kuzidisha  dalili zilizopo au kusababisha dalili mpya za magonjwa nyemelezi.

Matumizi Sahihi ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya VVU/UKIMWI (ARV)

Matumizi sahihi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI ni muhimu sana kwani usipofanya hivyo unaweza kupata madhara makubwa zaidi ikiwemo ugonjwa wa UKIMWI kuja kwa kasi zaidi, hali hii huchangia sana mgonjwa kupoteza maisha. Hivyo hakikisha unapata maelekezo yote kuhusu utumiaji wa dawa kutoka kwa daktari wako.

Dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI zipo kwenye makundi mbalimbali. Tafiti tofauti pamoja na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI zimependekeza matumizi ya dawa zifuatazo; Tenofovir disoproxil fumarate(TDF), Lamuvidine(3TC), Dultegravir(DTG) kama dawa za kwanza dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (first line treatment).

Yapo makundi mbalimbali ya mchanganyiko wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI ambayo  yanaweza kutumika kulingana na kundi analotoka mgonjwa  mfano watoto wadogo, mama mjamzito au kulingana na jinsi ambavyo dawa hizi  hufanya kazi kwa mtu binafsi n.k

Dawa hizi za mchanganyiko hupatikana kama dawa moja  ambayo humezwa kila siku. Dawa hii ya mchanganyiko wa madawa mbalimbali ina nguvu sana hivyo unashauriwa kula lishe bora wakati wote ili kupunguza maudhi madogo madogo yanayotokana na dawa hizi.

Hata hivyo,imeripotiwa kuwa baadhi ya waathirika hupata madhara kutokana na matumizi ya dawa hizi zilizochanganywa  kwa pamoja, endapo mgonjwa atapata madhara ya dawa hizi, basi anashauriwa kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kugundua  ni aina gani  ya dawa inayomsababishia mgonjwa madhara.

Pindi unapougua epuka kununua madawa na kutumia bila kumuona daktari wako. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya dawa huingiliana na dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI katika utendaji kazi hivyo hupelekea kupungua kwa nguvu ya dawa au dawa kubaki mwilini kwa muda mrefu sana (toxicity). Mambo yote hayo tajwa yana madhara kwa mtumiaji.

Pia unashauriwa kupunguza na kuacha unywaji wa pombe.

Muhimu: Hakikisha unameza dawa kwa kufuata maelekezo ya daktari na epuka kuruka ruka kumeza dawa au utoro wa kuhurudhia kliniki ili kuepuka  madhara  zaidi. Credits:TanzMed.

0 Comment

Ugonjwa wa Appendix Au Kidole Tumbo,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Appendix Au Kidole Tumbo,chanzo,dalili na Tiba

Appendix au kidole tumbo ni sehemu ya muendelezo wa utumbo mkubwa au mpana mwishoni, ambapo huwa na kitu mithili ya kidole chako cha mwisho cha mkononi,

Mtu huweza kuwa na tatizo kwenye appendix, hali ambayo ikampelekea kuhitaji matibabu, mfano ni tatizo kama vile appendicitis.

Appendicitis- ni hali ambayo huhusisha appendix kuvimba na kujazwa na usaha, kisha kusababisha maumivu.

Dalili za Ugonjwa Wa Appendix Au Kidole Tumbo

Je, Ugonjwa Wa Appendix una dalili Zipi? Dalili za tatizo kwenye Appendix ni Pamoja na;

1. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza upande wa kulia mwa tumbo la chini

2. Kupata Maumivu ya ghafla ambayo huanza karibu na kitovu chako na mara nyingi huhamia kwenye tumbo lako la chini upande wa kulia

3. Kupata Maumivu ambayo huongezeka ikiwa unakohoa, kutembea au kufanya shughuli zingine

4. Kupata shida ya Kichefuchefu na kutapika

5. Kukosa hamu ya kula chakula

6. Kupata Homa ya kiwango cha chini(Low-grade fever) ambayo inaweza kuwa mbaya zaidi ugonjwa unavyoendelea

7. Kupata tatizo la kujisaidia choo kigumu au kuharisha(Constipation or diarrhea)

8. Kuvimbiwa,tumbo kujaa gesi, Kuvimba kwa tumbo(Abdominal bloating) N.k

9. Kuwa na tatizo la gesi tumboni(Flatulence) n.k

Chanzo cha Ugonjwa Wa Appendix

Kwa kawaida baada ya chakula kuyeyushwa na umeng'enyaji kuendelea, kuna baadhi ya myeyusho wa chakula hupitia sehemu hii ya kidole tumbo au appendix.

Sasa endapo chakula kitapita hapa pamoja na vitu vidogo vidogo vigumu kama vile; mchanga N.K, vitu hivi haviwezi kupita hapa, hivo hujilundika hapa kila siku unapokula chakula kilichochanganyika na vitu hivi vigumu.

Hali hii huendelea hadi kufikia hatua ya kidole tumbo au appendix kuziba kwa juu pamoja na kuvimba na mtu kuanza kupata maumivu makali. Hapo ndipo chanzo cha tatizo la appendix huanza.

VIPIMO vya Ugonjwa wa Appendix

Vipo baadhi ya vipimo ambavyo huweza kufanyika kwa mtu mwenye dalili za ugonjwa wa appendix, na vipimo hivo ni kama vile;

  • vipimo vya damu,
  • ultrasound,
  • Ct Scan N.K

Pia Mgonjwa anaweza kuchunguzwa dalili,historia ya ugonjwa pamoja na uchunguzi kwa njia ya kupapasa mikono ambayo hufanywa na mtaalam wa afya au dactari.

MATIBABU YA UGONJWA WA APPENDIX

- Matibabu ya ugonjwa wa appendix au kidole tumbo huhusisha matumizi ya dawa mbali mbali katika hatua za mwanzoni za ugonjwa, lakini kama tatizo litaendelea mgonjwa atafanyiwa upasuaji na kuondoa kabsa hicho kidole tumbo.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

Dalili za Tatizo la Acid reflux,chanzo na TibaAfyaclass Bongo Social •

Dalili za Tatizo la Acid reflux,chanzo na Tiba

Tatizo hili hutokea pale ambapo Acid kutoka Tumboni hupanda juu kwenye mrija unaounganisha tumbo na Mdomo yaani esophagus,

Hali hii ya acid kupanda juu kutoka tumboni ndyo huanza kuleta shida mbali mbali.

Dalili za acid reflux

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

– Mtu kuhisi Kiungulia(heartburn) mara kwa mara, hasa baada ya Kula, ambapo huzidi sana wakati wa Usiku au wakati wowote ukiwa umelala

– Mtu kupata shida ya chakula alichomeza au kinywaji alichokunywa kupanda juu au kurudi mdomoni yaani regurgitation

– Mtu Kupata maumivu ya tumbo juu ya kitovu karibu na mbavu au kupata maumivu ya Kifua(kichomi)

– Mtu kupata shida ya Kumeza Kitu yaani dysphagia

– Mtu kuhisi kama kuna kitu kimebakia Kooni

– Wakati mwingine unaweza kupata kikohozi ambacho hakiishi,hasa kama shida hii ya Acid Reflux hutokea wakati wa Usku

- Kama una tatizo la Pumu,Hali inaweza kuwa mbaya Zaidi.

JE,UNA TATIZO HILI NA HUJAPATA TIBA?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE +255758286584.

Karibu kwenye Afyaclass WhatsApp Channel

Jiunge nasi leo na upate elimu ya afya kwa lugha nyepesi, kila siku moja kwa moja kwenye WhatsApp yako.

  • 🩺 Ushauri wa kitaalamu wa afya
  • 🍲 Lishe bora kwa familia
  • 🤰 Elimu ya afya ya mama na mtoto
  • 🌿 Tiba rahisi na ushauri wa kiafya

Elimu hii ni Muhimu sana. Boresha afya.

Tafuta msaada wa matibabu mara moja ikiwa una maumivu ya kifua, hasa ikiwa pia unabanwa na pumzi, au unapata maumivu ya taya au mkono.  Hizi zinaweza kuwa dalili za matatizo mengine kama vile mshtuko wa moyo.

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA MTU KUPATA TATIZO LA ACID REFLUX

1. Mtu kuwa na Uzito mkubwa kupita kiasi(Overweight/Obesity)

2. Mwanamke Kuwa Mjamzito

3. Mtu kuwa na tatizo la tumbo kuchelewa kutoa vitu ikiwemo chakula kwenda sehemu zingine yaani Delayed stomach emptying

4. Uvutaji wa Sigara

5. Mtu kula chakula kingi sana kwa wakati mmoja

6. Mtu kuchelewa sana kula chakula wakati wa Usku

7. Kula aina ya vyakula kwa kiwango kikubwa sana,mfano vyakula vya mafuta mengi n.k

8. Mtu kunywa Pombe au Kahawa mara kwa mara

9. Kuwa na matatizo ya Connective tissues kama vile scleroderma

10. Matumizi ya baadhi ya Dawa mara kwa mara,mfano Asprin n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ruzuku yatolewa kwa wazazi wenye watoto wadogo ChinaAfyaclass Bongo Social •

Wazazi nchini China wanapewa ruzuku ya Yuan 3,600 (sawa na Sh 375,000) kwa mwaka kwa kila mtoto aliye na umri chini ya miaka mitatu, ikiwa ni mara ya kwanza kwa serikali kutoa mpango wa kitaifa unaolenga kuongeza viwango vya uzazi.



Taarifa zinaeleza kuwa kiwango cha uzazi nchini humo kimekuwa kikishuka licha ya Serikali ya Kikomunisti kuondoa takriban miaka kumi iliyopita sera yake tata ya mtoto mmoja.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, ruzuku hiyo itasaidia familia karibu milioni 20 kukabiliana na gharama za malezi ya watoto.

Mikoa kadhaa nchini humo imewahi kufanya majaribio ya aina mbalimbali za malipo ili kuhimiza watu kuzaa zaidi, huku taifa hilo la pili kwa uchumi mkubwa duniani likikabiliwa na changamoto ya idadi ndogo ya watu.

Mpango huo uliotangazwa Jumatatu unawapa wazazi hadi yuan 10,800 kwa kila mtoto. Shirika la Utangazaji la Serikali, CCTV, limeeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza rasmi mwanzoni mwa mwaka huu.

Aidha, familia zilizo na watoto waliozaliwa kati ya mwaka 2022 na 2024 zitakuwa na nafasi ya kuomba ruzuku hiyo. Hatua hii ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali za mitaa kuongeza viwango vya uzazi nchini China.

Chanzo: BBC

0 Comment

Utafiti,Mbegu za Kiume huweza kubeba alama za Msongo wa mawazo kutoka kwa BabaAfyaclass Bongo Social •

Msongo wa mawazo hauathiri mtu mmoja pekee unaweza kuacha athari kwa kizazi kinachofuata kupitia njia za kibaiolojia, si kwa tabia tu.



Utafiti wa mwaka 2016 uliochapishwa katika jarida la Nature Neuroscience uligundua kuwa panya dume waliowekwa kwenye mazingira ya msongo wa kudumu walipitisha athari za msongo huo kwa kizazi chao kupitia molekuli maalum zilizopo ndani ya mbegu zao za kiume, ingawa mlolongo wao wa DNA haukubadilika.

Tofauti na kubadilisha vinasaba (genes), msongo huo uliathiri viwango vya RNA ndogo zisizo na msimbo (non-coding RNAs) ndani ya mbegu. Molekuli hizi zilionekana kuwa na ushawishi mkubwa katika hatua za awali za ukuaji wa kiinitete na katika utendaji wa ubongo wa watoto, hivyo kubadili namna wanavyokabiliana na msongo wa mawazo katika maisha yao. 



Namna Msongo wa Mawazo Unavyorithishwa:

1. Vibeba ujumbe wa Kiumolekiuli (Molecular Messengers):

Panya dume waliokuwa kwenye msongo wa mawazo walionyesha viwango vya juu vya aina tisa za microRNA maalum katika mbegu zao. MicroRNA hizi hufanya kazi kama ishara au ujumbe wa kibaolojia unaoathiri namna vinasaba hujieleza baada ya utungwaji mimba.

2. Mabadiliko ya Tabia (Behavioral Changes):

Watafiti walipochukua RNA hizi na kuzidunga katika viinitete vya panya waliokuwa na afya, watoto waliotokana nao walionyesha mabadiliko ya mwitikio dhidi ya msongo wa mawazo. Walionekana kuwa na kiwango cha chini cha wasiwasi na walionesha tabia tofauti ikilinganishwa na wengine.

3. Ukuaji wa Ubongo (Brain Development):

Watoto wa panya waliopokea RNA hizo walikuwa na mabadiliko ya uelekezaji wa vinasaba katika sehemu ya hypothalamus ya ubongo—eneo linalohusika moja kwa moja na udhibiti wa msongo wa mawazo. Mabadiliko hayo yalihusiana na miundo ya ubongo na ulinzi wa ubongo dhidi ya sumu kupitia kizuizi cha damu na ubongo (blood-brain barrier).

4. Athari za Mapema (Early Effects):

RNA zilizobadilika kutoka kwa baba zilianza kufanya kazi mara tu baada ya utungwaji mimba. Ziliharibu baadhi ya RNA kutoka kwa mama na kuchochea mabadiliko ya muda mrefu katika maendeleo ya ubongo wa mtoto.

0 Comment

Ugonjwa wa Ngozi,Scabies,Soma hapa kufahamuAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Ngozi,Scabies,Soma hapa kufahamu



Scabies huhusisha mtu kuwa na vipele na muwasho kwenye ngozi yake ambapo chanzo chake ni utitiri mdogo sana yaani tiny burrowing mite ambao hujulikana kama Sarcoptes scabiei.  Mtu hupata muwasho sana kwenye eneo ambalo utitiri huo umechimba.

Na wakati mwingine hali huwa mbaya Zaidi nyakati za Usiku ambapo Utitiri huu huhitaji kuchimba Zaidi.

Scabies inaambukiza na inaweza kuenea haraka kupitia mawasiliano ya karibu ya mtu na mtu katika familia, kikundi cha watoto, darasa la shule, nyumba ya uuguzi au gereza n.k. Kwa sababu upele huenea kwa urahisi, wahudumu wa afya mara nyingi hupendekeza kutibu familia nzima au watu wowote wa karibu.”

SCABIES: Makala 

Scabies, ni ugonjwa wa ngozi unaohusishwa na kuwasha na madoa madogo mekundu kwenye ngozi, yanayosababishwa na utitiri wa kuwasha(itchy mite).

Aina ya Utitiri huu yaani tiny burrowing mite hujulikana kwa kitaalam kama Sarcoptes scabiei.

Dalili za Scabies

DALILI ZA UGONJWA WA SCABIES NI PAMOJA NA;

– Mtu kupata muwasho sana kwenye ngozi yake, na sana sana muwasho huu huzidi sana wakati wa usiku

– Kuanza kupata upele kwenye ngozi

– Ngozi kuanza kuwa na madoa doa mekundu

– Na maeneo ya ngozi ambayo huweza kuathiriwa zaidi ni pamoja na;

• Kati kati ya vidole

• Eneo la kwapani

• Kuzunguka kiuno

• Kwenye mikono

• Chini ya miguu kwenye sole

• Kuzunguka maziwa au matiti

• Kwenye sehemu za siri za Mwanaume(Around the male genital area)

• Eneo la matakoni

• Kwenye magoti

• Na kwa upande wa watoto wadogo, sana sana hutokea kwenye kichwa(Scalp), viganja vya mikono pamoja na miguuni.

MATIBABU YA SCABIES

– Zipo njia mbali mbali za kutibu Ugonjwa huu wa Scabies pamoja na vitu vya kuzingatia na kufanya ukiwa nyumbani, ikiwemo swala la usafi wa mwili pamoja nguo zako,

Na kwa upande wa tiba huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali ikiwemo za kunywa au Cream za kupaka n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Tatizo la Acid reflux husababishwa na nini,Acid reflux ni nini,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la Acid reflux husababishwa na nini,Acid reflux ni nini,dalili na Tiba

Tatizo la Gastroesophageal reflux disease (GERD), ni tatizo ambalo huwapata Watu wengi,Tatizo hili hujulikana kwa jina Lingine kama Acid Reflux,

Tatizo hili hutokea pale ambapo Acid kutoka Tumboni hupanda juu kwenye mrija unaounganisha tumbo na Mdomo yaani esophagus,

Hali hii ya acid kupanda juu kutoka tumboni ndyo huanza kuleta shida mbali mbali.

Dalili za acid reflux

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

– Mtu kuhisi Kiungulia(heartburn) mara kwa mara, hasa baada ya Kula, ambapo huzidi sana wakati wa Usiku au wakati wowote ukiwa umelala

– Mtu kupata shida ya chakula alichomeza au kinywaji alichokunywa kupanda juu au kurudi mdomoni yaani regurgitation

– Mtu Kupata maumivu ya tumbo juu ya kitovu karibu na mbavu au kupata maumivu ya Kifua(kichomi)

– Mtu kupata shida ya Kumeza Kitu yaani dysphagia

– Mtu kuhisi kama kuna kitu kimebakia Kooni

– Wakati mwingine unaweza kupata kikohozi ambacho hakiishi,hasa kama shida hii ya Acid Reflux hutokea wakati wa Usku

- Kama una tatizo la Pumu,Hali inaweza kuwa mbaya Zaidi

Tafuta msaada wa matibabu mara moja ikiwa una maumivu ya kifua, hasa ikiwa pia unabanwa na pumzi, au unapata maumivu ya taya au mkono.  Hizi zinaweza kuwa dalili za matatizo mengine kama vile mshtuko wa moyo.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA Acid reflux

Tatizo hili hutokea pale ambapo Acid hutoka tumboni na kupanda juu kwenye njia ya chakula Mara kwa mara,

Na wakati mwingine content ambazo sio acid pia huweza kupanda juu kutoka tumboni.

Na hii hutokea Pale ambapo band ya Misuli ya Mrivingo inayojulikana kama (lower esophageal sphincter)
ambayo hufanya kazi ya kufunga na kufungua wakati kitu kikiingia au kutoka tumboni kushindwa kufanya kazi vizuri,

endapo Sphincter hii haifungi na kufunguka kama inavyotakiwa au band ya misuli hii ya Mviringo ambayo inabana sehemu ya juu ya tumbo imekuwa dhaifu,basi huweza kupelekea acid ya tumboni pamoja na vitu vingine kuweza kutoka Tumboni na kupanda Juu.

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA MTU KUPATA TATIZO LA ACID REFLUX

1. Mtu kuwa na Uzito mkubwa kupita kiasi(Overweight/Obesity)

2. Mwanamke Kuwa Mjamzito

3. Mtu kuwa na tatizo la tumbo kuchelewa kutoa vitu ikiwemo chakula kwenda sehemu zingine yaani Delayed stomach emptying

4. Uvutaji wa Sigara

5. Mtu kula chakula kingi sana kwa wakati mmoja

6. Mtu kuchelewa sana kula chakula wakati wa Usku

7. Kula aina ya vyakula kwa kiwango kikubwa sana,mfano vyakula vya mafuta mengi n.k

8. Mtu kunywa Pombe au Kahawa mara kwa mara

9. Kuwa na matatizo ya Connective tissues kama vile scleroderma

10. Matumizi ya baadhi ya Dawa mara kwa mara,mfano Asprin n.k


Madhara ya Tatizo la Acid Reflux(Complications)

 Baada ya muda, Tatizo la Acid reflux huweza kusababisha Madhara mbali mbali ikiwemo;

- kuvimba kwa muda mrefu kwenye Umio au esophagus:

 Kuvimba kwa tishu kwenye umio, hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama esophagitis huweza kutokea kama madhara ya tatizo la acid reflux.

 Asidi ya tumbo inaweza kuvunja tishu kwenye umio. Hali Hii inaweza kusababisha kuvimba, kutokwa na damu na wakati mwingine vidonda.  Esophagitis inaweza kusababisha maumivu na kufanya kumeza vitu kuwa ngumu.

 - Kupungua kwa Umio,narrowing, hali inayoitwa esophageal stricture

 Uharibifu wa Umio kutokana na asidi ya tumbo husababisha kuundwa kwa tishu zenye kovu.  Tissue hizi zenye kovu hupunguza njia ya chakula, na kusababisha matatizo ya kumeza.

- Hatari ya kupata Saratani kutokana na Mabadiliko ya Seli Za umio, hali inayojulikana kama Barrett esophagus. 

 Uharibifu kutokana na asidi unaweza kusababisha mabadiliko katika tishu zinazozunguka umio.  Mabadiliko haya yanahusishwa na hatari ya kuongezeka kwa saratani ya Umio.

Utambuzi wa Tatizo la Acid Reflux,Diagnosis

Mtaalamu wa afya anaweza kutambua tatizo la Acid reflux kulingana na historia, dalili na Uchunguzi wa kimwili.

 Ili kuthibitisha utambuzi wa tatizo la Acid reflux, au kuangalia matatizo mengine, mtaalamu wa huduma anaweza kupendekeza vipimo mbali mbali ikiwemo:

  • Kipimo cha Upper endoscopy; Kipimo hiki cha Endoscopy hutumia kamera ndogo kwenye mwisho wa bomba linalonyumbulika ili kuchunguza mfumo wa juu wa usagaji chakula.  Kamera hii husaidia kutoa mtazamo wa ndani ya umio na tumbo.  Matokeo ya kipimo hiki yanaweza yasionyeshe moja kwa moja wakati acid reflux ipo, lakini endoscopy inaweza kupata kuvimba kwa umio au matatizo mengine.

Endoscopy pia inaweza kutumika kukusanya sampuli ya tishu, inayoitwa biopsy, ili kupima matatizo mengine kama vile Barrett esophagus.  Katika baadhi ya matukio, ikiwa kupungua(narrow) kunaonekana kwenye Umio, endoscopy inaweza kunyoosha au kupanua Umio wakati wa utaratibu huu.  Hii hufanyika ili kuboresha na kuondoa hali ya kupata shida ya kumeza.

  • Kipimo cha Ambulatory acid (pH) probe test; Kichunguzi hiki huwekwa kwenye umio ili kutambua ni lini, na kwa muda gani, asidi ya tumbo inarudi pale.  Mfuatiliaji huunganisha kwenye kompyuta ndogo ambayo huvaliwa kiunoni au kwa kamba juu ya bega

Kichunguzi hiki kinaweza kuwa na mirija Myembamba, inayonyumbulika, inayoitwa katheta, ambayo imeunganishwa kupitia pua hadi kwenye umio.  Au inaweza kuwa na capsule ambayo imewekwa kwenye umio wakati wa endoscope.  Capsule hupita kwenye kinyesi baada ya siku mbili

  • Kipimo cha X-ray;X-rays huchukuliwa baada ya kunywa Maji ambayo hupita na kujaza utando wa ndani wa njia ya utumbo.  Zoezi hilo linaruhusu mtaalamu wa afya kuona silhouette ya Umio na tumbo.  Hii ni muhimu sana kwa watu ambao wana shida ya kumeza kitu.

Wakati mwingine, X-ray hufanyika baada ya kumeza kidonge cha bariamu.  Hii inaweza kusaidia kutambua Upungufu wa umio unaoingilia kumeza.

  • Kipimo cha Esophageal manometry; Kipimo hiki hupima mikazo ya misuli kwenye umio wakati wa kumeza kitu.  Manometry ya umio pia hupima uratibu na nguvu inayotolewa na misuli ya umio.  Hii kawaida hufanywa kwa watu ambao wana shida ya kumeza vitu.
  • Kipimo cha Transnasal esophagoscopy; Uchunguzi huu unafanywa ili kuangalia uharibifu wowote kwenye umio.  Mrija mwembamba unaonyumbulika wenye kamera ya video huwekwa kupitia puani na kusogezwa chini ya koo hadi kwenye umio.  Kamera hutuma picha kwenye skrini ya video.

MATIBABU YA TATIZO HILI La Acid Reflux

Tiba ya tatizo hili huweza kuhusisha matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Antiacids za kuneutralize acid tumboni, kupunguza uzalishwaji wa Acid tumboni au Kuzuia kabsa uzalishwaji wa Acid Tumboni.

Kwahyo kwa ujumla,Matibabu ya Tatizo la Acid reflux huweza kuhusisha;

✓ Antacids ambazo hupunguza asidi ya tumbo; 

Dawa hizi hupunguza kiwango cha acid(neutralize) kilichopo tumboni

✓ Dawa za kupunguza Uzalishwaji wa asidi;

 Dawa hizi hujulikana kama histamine (H-2) blockers —

H-2 blockers hazifanyi kazi haraka kama vile antacids, lakini hutoa utulivu wa muda mrefu na Zinaweza kupunguza uzalishaji wa asidi kutoka tumbo kwa hadi saa 12.  Matoleo yenye nguvu zaidi yanapatikana kwa agizo la maelekezo ya Wataalam wa afya.

✓ Dawa zinazozuia kabsa uzalishwaji wa asidi na kuponya Umio;

Dawa hizi hujulikana kama proton pump inhibitors — Dawa hizi ni vizuizi vya asidi kali kuliko vizuizi vya H-2 na huruhusu muda wa tishu zilizoharibika za umio kupona.

 Ukianza kutumia dawa isiyoandikiwa na daktari kwa GERD, hakikisha kuwa umemwarifu mtoa huduma wako.

✓ Dawa Zingine ni pamoja na dawa jamii ya 

  • Prescription-strength proton pump inhibitors.
  •  Prescription-strength H-2 blockers.N.k

✓ Upasuaji

Tatizo la Acid reflux au GERD kwa kawaida linaweza kudhibitiwa kwa dawa.  Lakini ikiwa dawa hazisaidii au ungependa kuepuka matumizi ya muda mrefu ya dawa, mtaalamu wa afya anaweza kupendekeza Upasuaji, Kuna aina mbali mbali za Upasuaji kulingana na chanzo husika ikiwemo:

  • Fundoplication.
  • LINX device.
  •  Transoral incisionless fundoplication (TIF). Utaratibu huu mpya unahusisha kukaza sphincter ya chini ya esophageal kwa kuunda sehemu ya kuzunguka umio ya chini kwa kutumia vifungo vya polypropen.  TIF inafanywa kupitia mdomo kwa kutumia endoscope na haihitaji kuchanwa kwa upasuaji.  Faida zake ni pamoja na wakati wa kupona ni haraka Zaidi.

Kwa sababu unene unaweza kuwa sababu ya hatari kwa tatizo la Acid reflux au GERD, mtaalamu wa afya anaweza kupendekeza upasuaji wa kupunguza uzito kama chaguo la matibabu.  Zungumza na timu yako ya afya ili kujua kama wewe ni mtu anayehitaji aina hii ya upasuaji.

Zingatia Vitu hivi Ni Muhimu kwako Zaidi;

Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kusaidia kupunguza Tatizo la Acid Reflux, Jaribu njia hizi;

• Hakikisha Unadhibiti Uzito wa mwili;

Uzito mkubwa huweka shinikizo kwenye tumbo, kusukuma juu ya tumbo na kusababisha asidi reflux kwenye umio, Hivo hakikisha unadhibiti shida ya Uzito mkubwa wa mwili.

 • Acha kuvuta sigara;

 Uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa sphincter ya chini ya umio kufanya kazi vizuri, Hali hii hukuweka kwenye hatari Zaidi ya kupata tatizo la Acid reflux.

 • Weka kichwa juu ukiwa kwenye kitanda chako;

Ikiwa unapata kiungulia mara kwa mara unapojaribu kulala, weka Mto au kitu kingine ambacho kitainua kichwa juu, au kwa wengine hutumia vitanda ambavyo unaweza kuvipandisha Usawa unaotaka wewe, hakikisha hulali flat kabsa. 

 Inua ncha ya kichwa kwa inchi 6 hadi 9.  Ikiwa huwezi kuinua kitanda chako, unaweza kuingiza kitu ili kuinua mwili wako kutoka kiuno kwenda juu.  Kuinua kichwa chako kwa mito ya ziada n.k

 • Anza kwa upande wako wa kushoto;

 Unapoenda kulala, anza kwa kulala upande wako wa kushoto ili kusaidia kupunguza uwezekano wa kuwa na acid reflux.

 • Usilale chini muda huo huo baada ya kula chakula;

 Subiri angalau masaa matatu baada ya kula kabla ya kulala.

• Kula chakula polepole na kutafuna vizuri;

 Weka uma wako chini kila baada ya kuuma na uichukue tena mara baada ya kutafuna na kumeza.

 • Usitumie vyakula na vinywaji vinavyosababisha Zaidi acid reflux;

Vichochezi vya kawaida ni pamoja na pombe, chokoleti, kafeini, vyakula vya mafuta au peremende. Epuka vitu kama hivi.

 • Usivae nguo za kubana;

  Nguo ambazo zinabana sana karibu na kiuno huweka shinikizo kwenye tumbo na sphincter ya chini ya esophageal. Hali hii huongeza hatari ya wewe kupata tatizo la Acid reflux.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Vifo vya Wajawazito vyapungua kwa Asilimia 78 Mkoani ArushaAfyaclass Bongo Social •


KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, mkoa wa Arusha umefanikiwa kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 78, kutoka vifo 50 mwaka 2021 hadi vifo 11 mwaka 2025.



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, amesema hayo Julai 20 jijini Dodoma, wakati akieleza mafaniko ya mkoa huo katika kipindi cha uongozi wa serikali ya awamu ya sita kwa waandishi wa habari.

“Uboreshaji wa huduma za afya umerahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo mbalimbali ndani ya mkoa wa Arusha na kuwezesha kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 78, kutoka vifo 50 (2021) hadi vifo 11 mwaka (2025).

Miongoni mwa wanahabari kwenye mkutano huo“Lakini vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 859 mwaka 2021 hadi vifo 117 mwaka 2025 sawa na asilimia 86.4,”amesema Kihongosi

Amesema, pia kuanzishwa kwa Mfumo wa Rufaa wa M-Mama, kumesaidia jumla ya akina mama wajawazito 1,332 kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha, amesema mkoa umetekeleza programu ya elimu bila malipo kwa gharama ya Sh. bilioni 168.2 wanafunzi walionufaika imeongezeka kutoka wanafunzi 390,910 (2021) hadi 430,511 (2025).

0 Comment

Orodha ya familia 10 tajiri zaidi duniani 2025Afyaclass Bongo Social •

Bila kujali hali yako ya kifedha, kuwafuatilia watu matajiri zaidi—iwe kwa kuvutiwa, husuda, au chuki—huenda kunafurahisha zaidi na hakuhitaji utafiti kama vile kutafuta rehani, mnunuzi wa mtandaoni, au kusoma masuala ya fedha na uchumi.



Mvuto wa familia tajiri huonyesha utamaduni unaoabudu mali na kuwaabudu matajiri.

Wale walio katika ngazi ya juu ya biashara ni watu mashuhuri machoni mwa watu wengi, na wanafuatiliwa kwa uwezo wao wa kudumisha hali hii ya kumiliki mali.

Ifuatayo ni Orodha ya familia 10 zilizojipatia utajiri wao kupitia biashara mbalimbali duniani.

10. Familia ya Thompson

Familia ya Thomson kutoka nchini Canada ina wastani wa dola bilioni 87.1, hasa kutokana na umiliki wao wa Thomson Reuters, kampuni ya huduma za vyombo vya habari na habari.

Familia hii ilianza kujpatia utajiri mwaka wa 1934 wakati Roy Thomson alipozindua kituo kimoja cha redio huko Ontario, Canada.

Haraka alijitanua katika uwanja wa magazeti na baadaye akaanzisha Shirika la Thomson. Wazao wake waliunganisha kampuni ya Thompson na Reuters katika 2008. Hii ilisaidia katika kuunda nguvu ya kimataifa katika huduma za habari.

9. Familia ya Wertheimer

Familia ya Wertheimer ya Ufaransa ina wastani wa dola bilioni 88 kutoka kwa umiliki wao wa chapa ya kifahari ya Chanel.

Pierre Wertheimer alishirikiana na Coco Chanel katika miaka ya 1920 ili kujenga chapa maarufu ya Chanel.

Hawakugundua kuwa chapa hii ingekuwa mwongozo wa mtindo wa kifahari na wa hali ya juu.

Watoto wake, Alain na Gérard Wertheimer, bado wanamiliki na kuendesha chapa hii wakidumisha hadhi ya chapa hiyo katika ulimwengu wa mitindo karibu karne moja baadaye.

8. Familia ya Ambani

Familia ya Ambani ya India inamiliki wastani wa $99.6 bilioni, hasa kutokana na ushiriki wao katika biashara za nishati, mawasiliano ya simu na zile za rejareja.

Dhirubhai Ambani alianzisha kiwanda cha Reliance Industries mwaka wa 1958, akijihusisha na biashara ndogo ya nguo.

Lakini kupitia hamu na upanuzi wa biashara kemikali za petroli, mawasiliano ya simu na rejareja, Reliance iliibuka na kuwakampuni kubwa ya kibinafsi nchini India.

Hii leo, wanawe Mukesh na Anil wameendeleza urithi huo, huku Mukesh akitawala utajiri wa familia.

Ushawishi wa Mukesh Ambani umeenea na ni zaidi ya uongozi wa kampuni, kwani anaishi katika jumba la kifahari la orofa 27, linalosifiwa kuwa makazi ghali zaidi ya kibinafsi ulimwenguni.

Ushuhuda huu wa utajiri unaonesha umashuhuri wa familia ya Ambani na urithi wa kudumu wa maono ya ujasiriamali ya Dhirubhai ndani ya nyanja za biashara na maisha ya anasa.

7. Familia ya Mars

Familia ya Mars, pia kutoka Marekani, inamiliki $133.8 bilioni, hasa kutokana na umiliki wao wa Mars Inc., inayojulikana kwa kutengeneza peremende na chokoleti mbali na bidhaa za utunzaji wa wanyama.

Frank Mars alianza kutengeneza na kuuza peremende kutoka jikoni mwake mwaka wa 1911.

Mwanawe, Forrest Mars Sr., baadaye alivumbua chapa ya M&M's, ambayo inauza bidhaa maarufu duniani katika nyakati za kisasa. Alipanua zaidi kampuni kimataifa.

Zaidi ya karne moja baadaye, Mars Inc. inasalia kuwa kampuni inayomilikiwa kwa faragha, na familia inaendelea kufurahia mojawapo ya bahati kubwa zaidi duniani katika kutoa huduma za chakula na utunzaji wa wanyama.

6. Familia ya Al Saud

Familia ya Al Saud nchini Saudi Arabia ina wastani wa dola bilioni 140, kufuatia udhibiti wao wa mali ya mafuta ya Familia ya Kifalme ya Saudia, pamoja na Saudi Aramco, na vitega uchumi vingine.

Nasaba ya Al Saud ilijiimarisha katika karne ya 18 na Muhammad bin Saud. Hata hivyo, utajiri mkubwa wa familia hiyo uliunganishwa chini ya Mfalme Abdulaziz Ibn Saud mwaka wa 1932.

Ugunduzi wa hifadhi kubwa ya mafuta katika miaka ya 1930 ulisababisha familia kujiweka katika ustawi usio na kifani, ambao mwingi unahusishwa na Saudi Aramco.

Katika ngazi ya mtu binafsi, Mwanamfalme Mohammed bin Salman anamiliki mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1.

Mandhari hii ya utajiri wa pande nyingi inasisitiza njia mbalimbali ambazo familia ya kifalme ya Saudi imekusanya na inaendelea kudhibiti ushawishi wake mkubwa wa kifedha.

5. Familia ya Koch

Familia ya Koch, yenye makao yake nchini Marekani, ina wastani wa dola bilioni 148.5 kutokana kiwanda chao cha Koch Industries.

Fred C. Koch alianzisha mizizi ya Koch Industries mwaka wa 1940. Hapo awali walizingatia sana biashara ya kusafisha mafuta.

Wanawe, Charles na David Koch, wanastahili sifa zao kwani wamepanua kampuni hiyo kuwa mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya kibinafsi duniani.

Utajiri wa familia ya Koch leo ni onyesho la miongo kadhaa ya upanuzi wa tasnia kutoka kwa nishati hadi utengenezaji.

Utajiri wa Charles Koch unatokana na biashara ya mafuta iliyoanzishwa na babake, lakini hii leo, anajulikana zaidi na umma kwa siasa zake, akitumia fedha zake nyingi kufadhili wagombea na wasomi hususan maprofesa wa vyuo vikuu, na kushawishi nafasi za sera, yote yakilenga kuendeleza ajenda ya kihafidhina.

4. Familia ya Hermes

Utajiri wa familia ya Hermès (Dumas), inayomiliki wastani wa dola bilioni 170.6, unatokana na duka kubwa la kifahari la Hermès, lililoko Ufaransa.

Mwanzo wa ufalme wa familia ya Hermès ulikuwa mnamo 1837.

Thierry Hermès alianza safari yake ya kibiashara kwa kufungua duka kubwa mjini Paris. Zaidi ya karne mbili, Hermès imebadilika na kuwa ishara ya kimataifa ya mtindo wa kifahari na ubora wa hali ya juu wa ufundi.

Tawi la Dumas la familia limeendelea kudumisha udhibiti thabiti wa uzalishaji, kuhakikisha upekee wa chapa na mafanikio makubwa.

Familia ya Hermès inashikilia hisa kubwa katika kampuni hiyo, na karibu 80% ya hisa bado zinamilikiwa na wanafamilia.

Familia kwa jadi imekuwa na jukumu muhimu katika usimamizi wa Hermès, huku wanafamilia mbalimbali wakishikilia nyadhifa za uongozi .

3. Familia ya Al Thani

Familia ya Al Thani ya Qatar inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na dola bilioni 172.9, zilizotokana na usimamizi wao wa rasilimali na uwekezaji wa gesi asilia ya Familia ya Kifalme ya Qatar.

Familia hiyo inatoka kwa kabila la Tamīm, ambalo lilihamia mashariki kutoka Arabia ya kati hadi rasi ya Qatar

Familia hii ya kifalme imetawala Qatar tangu katikati ya karne ya 19. Sheikh Mohammed bin Thani alikuwa mtawala wa kwanza mwaka wa 1868.

Utajiri wao uliongezeka zaidi karne ya 20 kufuatia uchimbaji mkubwa wa hifadhi ya gesi asilia na mafuta ya Qatar, na kuwaweka kama moja ya familia tajiri zaidi za kifalme leo, ambayo inaonekana kuwa njia sawa kwa wengi wa familia za kifalme za Saudi Arabia.

2. Familia ya AL Nahyan

Familia ya Al Nahyan ni familia inayotawala ya Imarati ya Abu Dhabi na mojawapo ya familia sita zinazotawala za Umoja wa Falme za Kiarabu.

Wao ni tawi la Al Falahi, tawi la kabila la Bani Yas, na wana uhusiano wa karibu na familia ya Al Maktoum, inayotawala Dubai.

Familia ya Al Nahyan kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ina wastani wa dola bilioni 323.9, zinazotokana na udhibiti wao wa mali ya mafuta na uwekezaji ya Familia ya Kifalme ya Abu Dhabi.

Abu Dhabi, mojawapo ya mataifa saba ya emarati inayojumuisha Falme za Kiarabu, inasimama kama mji mkuu wa taifa hilo na ina sehemu kubwa ya hifadhi yake ya mafuta.

Kwa miongo kadhaa, familia ya Al Nahyan imetawala eneo ambalo sasa linaunda UAE, kabla ya zama za mabadiliko zilizoletwa na ukuaji wa mafuta, ambao ulibadilisha uchumi na bahati ya familia ya kifalme.

Familia ya Al Nahyan ni sehemu ya nasaba inayotawala ya Abu Dhabi, yenye mizizi iliyoanzia karne nyingi zilizopita.

Mpito wao kuelekea utajiri wa kisasa ulianza kushamiri katika karne ya 20 na ugunduzi wa mafuta katika UAE katika miaka ya 1950.

Walilenga katika ujenzi wa jalada la uwekezaji wa kimataifa huku wakidumisha ukoo wao wa kifalme na utawala huko Abu Dhabi kwa wakati mmoja.

1. Familia ya Walton

Familia ya Walton inajulikana zaidi kwa umiliki wake wa duka la jumla la Walmart - ambaye ni muuzaji mkubwa zaidi duniani.

Inachukuliwa kuwa familia tajiri zaidi ulimwenguni kutokana na hisa zao kubwa katika duka la Walmart, na jumla ya utajiri unaokadiriwa kuwa $432.4 bilioni.

Utajiri wa familia kimsingi unatokana na mafanikio ya duka hilo na umeenea katika nyanja mbalimbali za biashara na juhudi za uhisani.

Wao ni wazao la wanafamilia Sam Walton, ambaye alikuwa mwanzilishi, na kaka yake Bud Walton, mwanzilishi mwenza wa Walmart katika mwaka wa 1962.

Biashara hii ilianza na duka moja l huko Arkansas.

Kwa miongo kadhaa, duka la Walmart lilipanua himaya yake hadi na kuwa mnyororo mkubwa wa maduka ya rejareja ulimwenguni, unaopatikana kote ulimwenguni katika karibu kila jiji.

Katika nchi za ulimwengu wa kwanza, duka la Walmart linatawala kama duka kuu. Utajiri wa familia umehifadhiwa na kukua kwa uangalifu, huku warithi wengi wakisimamia amana na misingi inayohusishwa na kampuni hiyo.

0 Comment

Mtoto Aliyepotea Tabora Akutwa Amefariki Ndani ya KisimaAfyaclass Bongo Social •

Mtoto Ramin, mwenye umri wa miaka mitatu, ambaye aliripotiwa kupotea siku kadhaa zilizopita huku taarifa zake zikisambazwa kwa kasi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, amekutwa akiwa tayari amefariki dunia.



Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa familia na majirani, mwili wa mtoto huyo umekutwa leo ndani ya kisima kilichopo nyumbani kwao, mkoani Tabora.

Tukio hili limetokea baada ya juhudi kubwa za kumtafuta mtoto huyo, juhudi ambazo zilijumuisha familia, majirani, na wananchi walioguswa kupitia mitandao ya kijamii kwa kusambaza taarifa za kutoweka kwake.

Hadi sasa, mamlaka za usalama zinaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mazingira kamili ya tukio hilo. Ripoti rasmi kutoka Jeshi la Polisi inasubiriwa ili kutoa mwangaza zaidi kuhusu chanzo halisi cha kifo hicho.

Tukio hili limeibua majonzi makubwa kwa jamii ya eneo hilo na watumiaji wa mitandao waliokuwa wakifuatilia kwa karibu hatma ya mtoto huyo.

0 Comment

Sudan kuzuia Whatsapp Call Audio na VideoAfyaclass Bongo Social •

Mamlaka ya mawasiliano nchini Sudan, imesema mwishoni mwa juma hili kuwa itazuia upigaji wa simu na video kupitia mtandao wa WhatsApp, zikisema ni kwa sababu za tishio la usalama wa taifa hilo.



Kwa mujibu wa gazeti la mtandao la Sudan Tribune, hatua hii itaenda kuwaathiri maelfu ya raia wa Sudan ambao wanategemea programu ya WhatsApp kwa mawasiliano, wakati huu pia huduma ya intaneti ikiwa imetatizika pakubwa nchini humo.

Katika taarifa yake, mamlaka ya mawasiliano inasema udhibiti wa huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya WhatsApp utaanza kufanyika kuanzia Ijumaa ya wiki hii hadi pale kutakapotolewa maelekezo mengine.

Aidha mamlaka zinasema huduma nyingine za progarmu hiyo kama vile kutuma ujumbe mfupi wa maandishi na mawasiliano ya makundi zitasalia kama kawaida.

Uamuzi huu pia utawaathiria raia wanaoishi nje ya Sudan, ambapo wanategemea kupiga simu za kawaida na video kwa kutumia WhatsApp kuwasiliana na ndugu zao walioko nyumbani na ambao wanapitia madhila ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

0 Comment

Ajali ya Boti yaua Watu 27 Ghuba ya Ha Long, Vietnam, LeoAfyaclass Bongo Social •

Takriban watu 27 wamefariki baada ya boti ya watalii kupinduka katika Ghuba ya Ha Long, Vietnam, Leo Julai 19, 2025 kutokana na hali mbaya ya hewa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.



Boti hiyo, iliyokuwa imebeba watu 53, ilipinduka majira ya saa nane mchana wakati Dhoruba ya Wipha ilipokuwa ikikaribia kutoka Bahari ya Vietnam Mashariki, ikileta upepo mkali, mvua kubwa na radi.

Ripoti zinaeleza kuwa wengi wa waliokuwemo ni watalii kutoka jiji la Hanoi. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu uraia wa wahanga huku uokoaji ukiendelea.

Ghuba ya Ha Long, takriban kilomita 200 kutoka Hanoi, ni kivutio maarufu cha utalii kinachopokea maelfu ya wageni kila mwaka. Ziara za boti ni moja ya shughuli kuu za vivutio hivyo.

Dhoruba ya Wipha ni kimbunga cha tatu kufika kwenye Bahari ya Vietnam Mashariki mwaka huu, na inatarajiwa kutua katika pwani ya kaskazini ya nchi hiyo mapema wiki ijayo.

Hali ya hewa hiyo pia ilisababisha usumbufu katika safari za ndege, ambapo ndege tisa zilielekezwa viwanja vingine na ndege tatu za kuondoka kusimamishwa kwa muda.

0 Comment

Kumwaga Mbegu au Manii Ukiwa umelala huzuia Saratani ya Kibofu?Afyaclass Bongo Social •

Linapokuja suala la afya ya wanaume, saratani ya kibofu cha mkojo inachukua nafasi kubwa. Ni aina ya pili ya saratani inayogunduliwa kwa wingi kwa wanaume duniani kote, ikifuatiwa na saratani ya mapafu.



Kwa sababu tezi dume ni kiungo cha uzazi ambacho kazi yake kuu ni kusaidia kuzalisha mbegu za kiume – yaani majimaji ambayo hubeba manii wakati wa mshindo.

Watafiti kwa muda mrefu wamekuwa wakijiuliza kuhusu athari za mambo ya ngono kwenye saratani ya tezi dume. Je, kumwaga mbegu za kiume hukulinda dhidi ya hatari ya saratani ya kibofu?

Kuna ushahidi wa kuunga mkono swali hili. Utafiti uliofanywa katika kipindi cha miaka 33 iliyopita ulionesha kuwa tafiti saba kati ya 11 – ziliona kuna manufaa ya kumwaga mbegu dhidi ya saratani ya tezi dume.

Vile vile, kumwaga manii kunaweza kuogeza kinga ya mwili ya kibofu na kupunguza hatari ya maambukizi – ambayo ndiyo chanzo cha kukuwa kwa saratani.

Kumwaga mbegu za kiume pia kunaweza kupunguza shughuli za mfumo wa neva, na huzuia seli fulani za kibofu kugawanyika, na kupunguza hatari ya kuwa na saratani.

Umri ni muhimu pia. Kumwaga mbegu mara nyingi hutoa kinga zaidi kwa watu kati ya umri wa miaka 20 na 50 na kuendelea. Lakini kuna hatari kwa vijana wa umri wa miaka 20 na chini ya hapo.

Kumwaga manii mengi wakati wa ujana - kibofu bado kikiwa hakijakoma na kuna hatari ya kupata saratani ya kibofu miongo kadhaa baadaye.

Utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani ulionesha kuwa wanaume wanaomwaga manii mara 21 au zaidi kwa mwezi wana hatari ndogo ya kupata saratani ya tezi dume kwa 31% kuliko wanaume wanaomwaga mara nne hadi saba kwa mwezi.

Matokeo kama hayo yalipatikana nchini Australia, ambapo saratani ya tezi dume ilikuwa chini ya 36% kwa wanaume walio chini ya umri wa miaka 70, kwa wanaume waliomwaga mara tano hadi saba kwa wiki, ikilinganishwa na wanaume waliomwaga chini ya mara tatu kwa wiki.

Lakini utafiti mwingine unaeleza kuwa kumwaga mbegu zaidi ya mara nne kwa mwezi kunahesabiwa ni kumwaga mara kwa mara na hilo hutoa kinga kwa rika fulani la watu.

Kumwaga mbegu kunaweza kukulinda dhidi ya saratani ya kibofu, lakini pia yawezekana wanaume wanaomwaga manii mara kwa mara wana maisha bora, ambayo hupunguza uwezekano wa kupata saratani.

Kuwa na mzungumko mdogo wa kumwaga mbegu, kunaweza kuhusishwa na kupungua kwa shughuli za kimwili na talaka – hayo ni mambo ambayo yanaweza kuchangia kukua kwa saratani.

Homoni za testosterone ni muhimu

Homoni ya testosterone, inafahamika kwa kuongeza hamu ya tendo la ndoa, hivyo mwanaume mwenye viwango vya chini vya testosterone anaweza asiwe na hamu ya tendo.

Maoni ya zamani yalikuwa; viwango vya juu vya testosterone kwa wanaume huongeza hatari ya saratani ya kibofu, maoni ya sasa yanaonesha haiongezi hatari hii, na badala yake kiwango cha chini cha testosterone ndicho huongeza hatari.

Wanaume walio na saratani ya kibofu, huonesha kuwa viwango vya testosterone ni vya chini. Hivyo kuwa na homoni nyingi za testosterone hupunguza hatari ya saratani ya kibofu kwa wanaume na kuongeza motisha yao ya kushiriki katika shughuli za ngono.

Utafiti mwingine ulionesha kuwa wanaume ambao humwaga mara kwa mara - wana viwango vya juu vya homoni ya testosterone. Na hawa ndiyo wanaume ambao pia wana hatari ndogo ya saratani ya kibofu.

Shughuli ya ngono na kumwaga mbegu za kiume zina faida kwa kibofu, ikiwa ni pamoja na athari chanya kwenye moyo, ubongo, mfumo wa kinga, usingizi na hisia.

Licha ya kuwa uhusiano kati ya kumwaga manii na saratani ya kibofu haueleweki kikamilifu - na kuna hitaji la kweli la kusoma zaidi – lakini ukweli unabaki kuwa kumwaga ni sehemu ya maisha ya afya kwa mwanaume.

0 Comment

Watumishi 700 kutoka kwenye taasisi mbalimbali za serikali kukutana ArushaAfyaclass Bongo Social •

Watumishi 700 kutoka kwenye taasisi mbalimbali za serikali wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya Waalamu wa Usimamizi wa RasilimaliWatu na Utawala katika Utumishi wa Umma (TAPA-HR),utakaofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), 22 hadi 25 Julai,2025.



Hayo yalisemwa jana jijini Arusha na Mwenyekiti wa TAPA-HR, Grace Meshy,wakati akizungumza na waandishi wa habari na alisema mkutano utafunguliwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora,George Simbachawene.

Alisema Jumuiya za Wataalamu hao,imeundwa kutekeleza malengo ikiwamo kuhakikisha kunakuwa na fursa ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala, kukuza ujuzi na weledi katika masuala ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala.

Pia alisema wanajukumu la kuhifadhi na kusambaza taarifa za kitaaluma katika kada ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala kwa njia ya machapisho, mikutano, ziara za mafunzo,makongamano ya kitaaluma, midahalo na kuweza kujiunga na mitandao ya kitaaluma ya kitaifa na kimataifa.

Mwenyekiti huyo,alisema malengo mengine ya kuundwa TAPA-HR  ni pamoja na kuimarisha maadili ya kitaaluma katika masuala ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala,kukuza ushirikiano wa kitaifa na kimataifa kupitia mashirika na taasisi zinazojishughulisha na ukuaji na usimamiaji wa rasilimaliwatu na Kuimarisha utekelezaji wa mifumo inayotumika katika utumishi wa umma inayotumika katika usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala ili kufikisha huduma kwa umma na kuleta ustawi kwa umma.

Hata hivyo,alisema mkutano huo, umelenga kuwakutanisha wataalamu wa kada ya usimamizi wa rasilimaliwatu na utawala katika Utumishi wa Umma kutoka Tanzania bara na visiwani ili kuwajengea uwezo zaidi na kuongeza tija katika ufikiaji wa malengo makuu ya taasisi zao na ustawi wa wananchi kwa jumla.

Alisema kamati ya maandalizi ya mkutano imeandaa mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha utendaji kazi wa watumishi hao, na zitawasilishwa na wawezeshaji nguli katika utumishi wa umma ambao watapata nafasi ya kueleza uzoefu wao.

Aidha amewaomba waajiri wote katika Wizara,Tawala za Mikoa Mamlaka ya Serikali za Mitaa,Wakala wa Serikali,Mashirika ya Umma,Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki,pamoja na Idara zinazojitegemea kuwawezesha Wataalamu wao wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala kushiriki katika mkutano huo mkuu wa kitaalamu ili waweze kuwajengea uwezo katika kutekeleza majukumu yao mahala pa kazi.


0 Comment

Majibu ya Kupima DNA Tanzania ni Siku 21, Wazazi na Mtoto Gharama ni Laki 3Afyaclass Bongo Social •

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema licha ya kwamba gharama za upimaji DNA nchini zinafikia hadi Tsh milioni moja lakini Serikali imeamua kugharamia gharama za ziada ili kuwapunguzia Wananchi mzigo ambapo kwa sasa kila Mtu analipia Tsh. laki 1 tu kupima DNA na wanapokuwa Baba, Mama na Mtoto wanalipia Tsh. laki 3 wote kwa pamoja.



Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai , Biolojia na Vinasaba wa Mamlaka hiyo Dkt. Fidelis Buyoge amesema hayo kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba ofisini kwake Jijini Dar es salaam ambapo

amesema gharama halisi kwa Mtu mmoja inazidi Tsh. laki mbili lakini Serikali inabeba gharama nyingine na Mtu sasa anatozwa laki 1 na kwa Afrika Mashariki Tanzania ndio yenye gharama ndogo za upimaji DNA ukilinganisha na nchi nyingine “Ukienda nchi jirani sitaki kuitaja jina gharama ya kupima kwa Mtu mmoja ni laki 1 na elfu 70”

Dkt. Buyoge amesema takwimu za January hadi December 2024 waliopima DNA kwenye upande wa masuala ya uzazi ni Watu 524 lakini takwimu za mwaka huu bado hazijatolewa ambapo amesema majibu hutolewa ndani ya siku 21 tangu Mtu kupimwa lakini zinaweza hata zisifikie siku hizo hata ndani ya siku 5 majibu yakiwa tayari yanatolewa kupitia kwa Mamlaka ombezi mfano Mahakama, Wakili au Afisa Ustawi wa Jamii na kwamba Mtu aliyepima DNA au Wazazi watachukua majibu kutoka kwenye Mamlaka hizo.

Amesema hata Mtu binafsi anaweza kuamua kwenda kupima DNA na rekodi zake zikabaki tu na sio lazima kuwe na migogoro ya masuala ya uzazi huku akisisitiza kuwa DNA inasaidia hata kwenye mirathi ili Ndugu wajue uhalali wa Wanafamilia kwakuwa Watoto wa Baba na Mama mmoja DNA zao hufanana “Kuhusu Watu wanaopima kujua uhalali wa Mtoto hatujawahi kuwa na kesi za ambazo zimetufikia za Watu kugombana baada ya majibu”

0 Comment

Mapacha tisa wa Mali watimiza miaka 4 kwa SasaAfyaclass Bongo Social •

Mnamo mwaka 2021, dunia ilishuhudia muujiza wa kipekee: mama Halima Cissé kutoka Mali alijifungua watoto tisa kwa mpigo — wavulana wanne na wasichana watano — tukio ambalo halijawahi kutokea tena kwa mafanikio duniani!



Serikali ya Mali iliwasafirisha yeye na mume wake, Abdelkader Arby, hadi Morocco kwa matibabu ya hali ya juu baada ya kugundua alikuwa na ujauzito wa mapacha 7. Lakini walipofika Morocco, walipokea mshangao mkubwa — walikuwa ni mapacha tisa!

Kutokana na tukio hilo la kipekee, Halima Cissé aliandikishwa rasmi katika Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness (Guinness World Records) kama mwanamke wa kwanza kuwahi kujifungua watoto tisa kwa mpigo na wote wakaishi, jambo lililovutia dunia nzima.

Sasa mapacha hao wametimiza miaka minne, wakiwa na afya njema na furaha kubwa. Wazazi wao hivi karibuni walisherehekea siku hiyo ya kipekee kwa kushiriki picha na kumbukumbu kupitia Instagram, wakikumbuka safari yao ya ajabu ya uzazi.

0 Comment

Faida za Mchaichai kwa mtu aliyekula vyakula vya mafutaAfyaclass Bongo Social •

Mchaichai (lemongrass) ni mmea wa asili unaotumika sana kama tiba mbadala. Kwa mtu aliyekula vyakula vingi vya mafuta, mchaichai husaidia kwa njia zifuatazo:



Faida za Mchaichai kwa mtu aliyekula vyakula vya mafuta:

  1. Husaidia kusafisha ini na mfumo wa mmeng’enyo:
    Mchaichai una uwezo wa kusaidia ini kuchuja sumu na taka zinazotokana na mafuta mengi mwilini.

  2. Huchochea mmeng’enyo wa chakula:
    Husaidia kuyeyusha mafuta kwa haraka na kupunguza hali ya kusikia tumbo zito au kujaa gesi.

  3. Hupunguza lehemu (cholesterol) mbaya mwilini:
    Mchaichai una kiambata kinachosaidia kushusha kiwango cha LDL cholesterol (lehemu mbaya), kinachoongezeka kutokana na ulaji wa mafuta mengi.

  4. Huondoa gesi tumboni na kuzuia kuvimbiwa:
    Baada ya kula mafuta mengi, tumbo huweza kujaa gesi—mchaichai husaidia kutoa gesi hiyo kwa urahisi.

  5. Husaidia kupunguza uzito:
    Ina uwezo wa kuamsha mwako wa mafuta mwilini (fat metabolism), hivyo kusaidia katika kupunguza uzito unaotokana na mafuta kupita kiasi.

  6. Hupunguza msongamano wa damu na hatari ya shinikizo la damu:
    Kwa kuwa vyakula vya mafuta huongeza hatari ya shinikizo la damu, mchaichai husaidia kupunguza msongamano wa mishipa ya damu na kupunguza presha.

  7. Ni diuretic ya asili:
    Huchochea mkojo, hivyo kusaidia kutoa chumvi na maji yaliyokithiri mwilini baada ya kula chakula chenye mafuta mengi.

Jinsi ya kutumia mchaichai baada ya kula vyakula vya mafuta:

  • Chemsha maji na weka majani ya mchaichai (au tangawizi na limao kwa ladha zaidi), kunywa kikombe kimoja baada ya mlo mzito.
  • Unaweza pia kukaanga kidogo mchaichai na kutumia kama kiungo kwenye chakula chako cha jioni au supu.
0 Comment

Sasa ChatGPT kufikiri kwa niaba ya MtumiajiAfyaclass Bongo Social •

Kampuni ya OpenAI imetangaza kuzindua kipengele kipya katika akili mnemba yake ya ChatGPT kitakachomruhusu Roboti huyo kufanya baadhi ya majukumu ikiwemo kufikiri kwa niaba ya Mtumiaji ikiwa ni sehemu ya mapinduzi ya mtandao ambapo Watumiaji badala ya kuhama program kupata na kutafuta taarifa kwa mikono, atategemea Mawakala wa AI kufanya kila kitu.



Kipengele hicho kipya cha ChatGPT ambacho kimepewa jina la Wakala “Agent Mode” kitaanza kufanya kazi hivi karibuni na kitakwenda kuongeza ushindani katika Makampuni ya kiteknolojia hususani Google na OpenAI ambazo zote zinatengeneza akili mnemba ambayo ina lengo la kutoa usaidizi.

Aidha kwa mujibu wa OpenAI, kipengele hicho cha Wakala kwa sasa kitaiwezesha akili mnemba ya ChatGPT kufikiri na kutekeleza majukumu kwa kutumia mfumo wake wa kidigitali wa kompyuta (virtual computer) ambayo itaiwezesha kufanya mambo magumu kwa mafano Mtumiaji akiitaka imwangalizie kalenda na kumwambia matukio yajayo pamoja na kuiambia ikusaidie kutaja viungo vitakavyotumika kwa aina ya chakula itaweza kufanya hivyo.

Aidha katika video ya maelezo OpenAI Mtumiaji mmoja aliiambia ChatGPT iweze kumwandalia na kumshauri aina ya mavazi ya kuvaa kwa ajili ya harusi na kutaka impe mapendekezo ya nguo tano tofauti kama vile kanisani, hotelini na ukumbini na ilifanya hivyo ambapo kwa mujibu wa OpenAI kipengele hicho kipya kitapatkana kwa wale ambao watalipia kuanzia ChatGPT Pro, Plus au Team Plan.

Aidha ChatGPT imesema kipengele hicho kipya kimekuja na hatari katika kupambana na taarifa za faragha za Watumiaji wake ambapo kampuni hiyo imeendelea kuonya kuwa watumiaji wake wasitoe taarifa zao za muhimu na za faragha kwa akili mnemba hiyo ambapo pia wamesema kuwa haitaweza kufanya kazi na kufikia sehemu kama Baruapepe ambazo zitahitaji uangalizi wa mtuniaji mwenyewe pamoja na kazi hatarishi kama vile kazi za kibenki.

0 Comment

Dira ya taifa 2050,Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050Afyaclass Bongo Social •

Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050



KATIBU Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Fred Msemwa ametaja sifa za Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Dk Msemwa alizitaja sifa hizo wakati wa uzinduzi wa dira hiyo uliofanyika jijini Dodoma katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jana.

Dk Msemwa alisema dira hiyo imeshirikisha makundi yote muhimu sambamba na mtu mmoja mmoja.

Alisema katika maandalizi ya dira hiyo walikusanya maoni kwa wananchi yaliyojumuishwa katika rasimu ya dira hiyo na baadaye kukamilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Dk Msemwa alisema watu binafsi walihusishwa katika hatua za maandalizi, jambo linaloifanya kuwa ya kipekee na inayowakilisha masilahi ya wote.

Alisema maandalizi ya dira hiyo yalihusisha wataalamu wa ndani waliohusika katika hatua zote kuanzia maandalizi, uchambuzi, hadi uhakiki wa dira hiyo, hali inayoonesha uwezo mkubwa wa rasilimaliwatu wa ndani ya nchi.

Pia, Dk Msemwa alisema maandalizi ya dira hiyo yamegharamiwa na serikali kupitia mapato yake.

Alisema serikali iligharamia mchakato wa uandaaji wa dira hiyo, kazi iliyochukua muda mrefu na yenye gharama kubwa.

“Kazi ya kuandaa dira ni kazi yenye gharama kubwa, gharama zote za uandishi wa Dira ya 2050 zimelipwa na serikali yako unayoingoza kupitia Wizara ya Fedha,” alisema Dk Msemwa.

Alisema katika kuiandaa tume hiyo iliandaa miongozo iliyotumika kukusanya, kuchambua maoni na katika uandishi.

Dk Msemwa alisema tume hiyo iliunda mfumo wa uongozi na usimamizi na ikaunda timu kuu ya uandishi wa dira iliyoongozwa na Dk Asha Rose Migiro.

“Iliundwa sekretarieti ya uongozi kwa upande wa Tanzania Bara iliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kwa upande wa Zanzibar ilikuwa inawakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais (Hemed Suleiman Abdullah),” alisema.

Dk Msemwa alisema pia, tume hiyo ilifanya mapitio na tathmini ya dira inayomalizika ili kuwezesha timu kuu ya uandishi wa dira kutambua mafanikio na maeneo yaliyohitajika kujumuishwa katika dira mpya.

Alisema baadaye tume hiyo ilihamia katika mchakato wa kukusanya maoni kwa wananchi uliofanyika kwa ufanisi na walikusanya maoni ya ana kwa ana kwenye kaya zao kwa Watanzania 1,174,000.

Pia, mchakato huo ulihusisha kutuma maoni kwa njia ya ujumbe usio na malipo na zaidi ya watu 8,000 walishiriki huku mitandao ya kijamii ikishirikisha zaidi ya Watanzania 100,000 na kupitia mikutano na makongamano walipata maoni kwa watu zaidi ya 22,000.

Alisema mchakato huo pia ulihusisha maoni kutoka nchi nyingine zenye uchumi wa kati na juu, ikiwemo Afrika Kusini ili kupata uzoefu kati

0 Comment

Maumivu ya magoti,chanzo,dalili na tibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo hili huweza kutokea kwa kila mtu bila kujali umri wala jinsia yake. na zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuhusishwa moja kwa moja na maumivu makali ya magoti.



SABABU ZA MAUMIVU YA MAGOTI NI PAMOJA NA;

- Mtu kupata ajali,kuanguka na kuumia kwenye goti au magoti n.k

- Mtu kuwa na matatizo ya mifupa

- Maambukizi ya magonjwa mbali mbali

- Mtu kukaa kwa muda mrefu

- Kutokufanya mazoezi ya mwili pamoja na viungo

- Mtu kuwa na historia ya kuumia goti au magoti hapo nyuma

- Mtu kuwa na matatizo ya Gauti

- Kuwa na shida ya unene au uzito kupita kiasi

DALILI ZA TATIZO HILI LA MAUMIVU MAKALI KWENYE MAGOTI

✓ Sehemu ya goti kubadilika rangi na kuwa nyekundu kuliko kawaida

✓ Kupata maumivu makali ya goti

✓ Goti kukaza sana 

✓ Kushindwa kunyoosha mguu

✓ Kushindwa kutembea 

MATIBABU YA TATIZO HILI

Matibabu ya tatizo hili hutegemea chanzo chake,hivo mgonjwa atapewa dawa za kutuliza maumivu pamoja na matibabu mengine kulingana na chanzo cha tatizo kama vile; Kutibu matatizo ya mifupa,gauti, majeraha,kuvunjika N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko-WHOAfyaclass Bongo Social •

Shirika la Afya Duniani (WHO) kupitia Wizara ya Afya limekabidhi vifaa vya afya vya kuimarisha tiba ya magonjwa ya mlipuko katika wilaya za Biharamulo na Muleba mkoani Kagera vyenye thamani ya Shilingi Milioni 112 ikiwa ni s muendelezo wa kupambana na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa yakijitokeza katika mkoa huo.



Akipokea vifaa hivyo Julai 15, 2025 kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe Kaimu Mkurugenzi wa Dharura na Maafa kutoka Wizara ya Afya Dkt. Erasto Sylvanus amesema kuwa vifa vilivyopokelewa ni vitanda vya kisasa vya kulaza wagonjwa, mshine za kufulia mashuka,stendi za kuwekea dawa ndoo za kuhifadhi maji na kufanyia usafi katika vituo vya afya pamoja na vifaa vya kufanya uchunguzi wa kina.

“vifaa hivi vilivyopokelewa ni jitihada zinazoendelea kufanyika katika kurejesha hali nzuri ya kupambana na magonjwa ya mlipuko na kupitia vifaa hivi vitaongeza ujuzi na utendaji kazi kwa wataalam wa afya mkoani Kagera tunaishukuru WHO kwa utayari na usaidizi mzuri katika kipindi chote ambacho nchi ya Tanzania na mkoa wa Kagera ulikumbwa na mlipuko wa ugonjwa,” amesema Dkt. Silvanus.

Aidha Dkt Slvanus ametoa wito kwa halmashauri zote za mkoa wa Kagera kutenga bajeti ya ndani kwa ajili ya kukabiliana magonjwa ya mlipuko yanayojitokeza kwa dharura kwakuwa mpaka sasa tayari wamekuwa na uzoefu juu ya magonjwa mbalimbali ya mlipuko.

Naye Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa WHO Dkt. Galberth Fadjo amesema kuwa shirika hilo kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameweka jitihada kubwa na kuchukua hatua za haraka ya kudhibiti magonjwa yenye nguvu kama Murbug yasisambae zaidi.

Mwakilishi wa huduma za Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Kutoka Ofisi ya Rais na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Dkt. Ernest Kyungu amesema wizara hiyo itaendelea kuratibu ili vifa hivyo vitumike kwa usahihi kutokana na miongozo na kanuni ikiwemo kuwapatia ujuzi watumiaji kupitia mafunzo kazini.

Katibu tawala wa mkoa wa Kagera Stephen Ndaki amesema Mkoa wa Kagera utaendelea kujiweka tayari kwa ajili ya kukabiliana na dharura zote za mlipuko kutokana mkoa huo kupakana na nchi jirani za ukanda wa Afrika Mashariki na ambazo hukumbwa na magonjwa ya milipuko na kutoa wito kwa wataalamu kuvitunza vizuri vifaa hivyo vilivyotolewa na kuongeza ujuzi wa kuvitumia pamoja na kuendelea kutoa taarifa kwa wananchi juu ya kujikinga na ugonjwa huo bila kujali kama Kuna ugonjwa au hakuna ugonjwa.

Ugongwa wa mlipuko wa Marburg ulitokea nchini Tanzania mwezi Machi mwaka 2023 katika Wilaya ya Bukoba ambapo watu sita walifariki dunia kati ya visa tisa vilivyoripotiwa.

Mnamo Januari 20 mwaka 2025 tovuti ya wizara ya Afya ilitangaza mlipuko wa pili katika wilaya ya Biharamulo na jumla ya watu 10 walifariki dunia ambapo wawili kati yao walithishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Marburg na wanne walihesabika.

0 Comment

Mapigano Syria Waliokufa wafikia watu 500Afyaclass Bongo Social •

Idadi ya vifo vilivyotokana na ghasia kusini mwa mji wa Sweida nchini Syria inaendelea kuongezeka na sasa imepindukia 500 kufuatia mapigano makali yaliyozuka Julai 13.



Idadi ya vifo vilivyotokana na ghasia kusini mwa mji wa Sweida nchini Syria inaendelea kuongezeka na sasa imepindukia 500 kufuatia mapigano makali yaliyozuka Julai 13.

Shirika linalofuatilia haki za binadamu la Syria lenye makao yake makuu Uingereza limerekodi vifo vya raia 83 wa jamii ya Druze katika mitaa ya mji wa Sweida na viunga vyake vya karibu huku likisema vikosi vya serikali ndio vimehusika na mauaji hayo.

Katika ripoti nyingine, shirika hilo limesema watu watatu wa jamii ya Bedui akiwemo mwanamke, mtoto na mwanaume wameuawa na wapiganaji wa Druze mjini humo.Vikosi vya Syria vyaanza kujiondoa kutoka mjini Sweida

Hadi kufikia jana vikosi vya serikali ya Syria kwa kiasi kikubwa vilijiondoa katika jimbo la Sweida baada ya siku kadhaa za mapigano na wanamgambo wanaohusishwa na jamii ya watu walio wachache wa Druze.

Via:Dw.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD