Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050
KATIBU Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango, Dk Fred Msemwa ametaja sifa za Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Dk Msemwa alizitaja sifa hizo wakati wa uzinduzi wa dira hiyo uliofanyika jijini Dodoma katika Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete (JKCC) jana.
Dk Msemwa alisema dira hiyo imeshirikisha makundi yote muhimu sambamba na mtu mmoja mmoja.
Alisema katika maandalizi ya dira hiyo walikusanya maoni kwa wananchi yaliyojumuishwa katika rasimu ya dira hiyo na baadaye kukamilisha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Dk Msemwa alisema watu binafsi walihusishwa katika hatua za maandalizi, jambo linaloifanya kuwa ya kipekee na inayowakilisha masilahi ya wote.
Alisema maandalizi ya dira hiyo yalihusisha wataalamu wa ndani waliohusika katika hatua zote kuanzia maandalizi, uchambuzi, hadi uhakiki wa dira hiyo, hali inayoonesha uwezo mkubwa wa rasilimaliwatu wa ndani ya nchi.
Pia, Dk Msemwa alisema maandalizi ya dira hiyo yamegharamiwa na serikali kupitia mapato yake.
Alisema serikali iligharamia mchakato wa uandaaji wa dira hiyo, kazi iliyochukua muda mrefu na yenye gharama kubwa.
“Kazi ya kuandaa dira ni kazi yenye gharama kubwa, gharama zote za uandishi wa Dira ya 2050 zimelipwa na serikali yako unayoingoza kupitia Wizara ya Fedha,” alisema Dk Msemwa.
Alisema katika kuiandaa tume hiyo iliandaa miongozo iliyotumika kukusanya, kuchambua maoni na katika uandishi.
Dk Msemwa alisema tume hiyo iliunda mfumo wa uongozi na usimamizi na ikaunda timu kuu ya uandishi wa dira iliyoongozwa na Dk Asha Rose Migiro.
“Iliundwa sekretarieti ya uongozi kwa upande wa Tanzania Bara iliyoongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kwa upande wa Zanzibar ilikuwa inawakilishwa na Makamu wa Pili wa Rais (Hemed Suleiman Abdullah),” alisema.
Dk Msemwa alisema pia, tume hiyo ilifanya mapitio na tathmini ya dira inayomalizika ili kuwezesha timu kuu ya uandishi wa dira kutambua mafanikio na maeneo yaliyohitajika kujumuishwa katika dira mpya.
Alisema baadaye tume hiyo ilihamia katika mchakato wa kukusanya maoni kwa wananchi uliofanyika kwa ufanisi na walikusanya maoni ya ana kwa ana kwenye kaya zao kwa Watanzania 1,174,000.
Pia, mchakato huo ulihusisha kutuma maoni kwa njia ya ujumbe usio na malipo na zaidi ya watu 8,000 walishiriki huku mitandao ya kijamii ikishirikisha zaidi ya Watanzania 100,000 na kupitia mikutano na makongamano walipata maoni kwa watu zaidi ya 22,000.
Alisema mchakato huo pia ulihusisha maoni kutoka nchi nyingine zenye uchumi wa kati na juu, ikiwemo Afrika Kusini ili kupata uzoefu kati
image quote pre code