Ruzuku yatolewa kwa wazazi wenye watoto wadogo China

Ruzuku yatolewa kwa wazazi wenye watoto wadogo China

#1

Wazazi nchini China wanapewa ruzuku ya Yuan 3,600 (sawa na Sh 375,000) kwa mwaka kwa kila mtoto aliye na umri chini ya miaka mitatu, ikiwa ni mara ya kwanza kwa serikali kutoa mpango wa kitaifa unaolenga kuongeza viwango vya uzazi.



Taarifa zinaeleza kuwa kiwango cha uzazi nchini humo kimekuwa kikishuka licha ya Serikali ya Kikomunisti kuondoa takriban miaka kumi iliyopita sera yake tata ya mtoto mmoja.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, ruzuku hiyo itasaidia familia karibu milioni 20 kukabiliana na gharama za malezi ya watoto.

Mikoa kadhaa nchini humo imewahi kufanya majaribio ya aina mbalimbali za malipo ili kuhimiza watu kuzaa zaidi, huku taifa hilo la pili kwa uchumi mkubwa duniani likikabiliwa na changamoto ya idadi ndogo ya watu.

Mpango huo uliotangazwa Jumatatu unawapa wazazi hadi yuan 10,800 kwa kila mtoto. Shirika la Utangazaji la Serikali, CCTV, limeeleza kuwa utekelezaji wa mpango huo utaanza rasmi mwanzoni mwa mwaka huu.

Aidha, familia zilizo na watoto waliozaliwa kati ya mwaka 2022 na 2024 zitakuwa na nafasi ya kuomba ruzuku hiyo. Hatua hii ni sehemu ya juhudi endelevu za serikali za mitaa kuongeza viwango vya uzazi nchini China.

Chanzo: BBC

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code