Msongo wa mawazo hauathiri mtu mmoja pekee unaweza kuacha athari kwa kizazi kinachofuata kupitia njia za kibaiolojia, si kwa tabia tu.
Utafiti wa mwaka 2016 uliochapishwa katika jarida la Nature Neuroscience uligundua kuwa panya dume waliowekwa kwenye mazingira ya msongo wa kudumu walipitisha athari za msongo huo kwa kizazi chao kupitia molekuli maalum zilizopo ndani ya mbegu zao za kiume, ingawa mlolongo wao wa DNA haukubadilika.
Tofauti na kubadilisha vinasaba (genes), msongo huo uliathiri viwango vya RNA ndogo zisizo na msimbo (non-coding RNAs) ndani ya mbegu. Molekuli hizi zilionekana kuwa na ushawishi mkubwa katika hatua za awali za ukuaji wa kiinitete na katika utendaji wa ubongo wa watoto, hivyo kubadili namna wanavyokabiliana na msongo wa mawazo katika maisha yao.
Namna Msongo wa Mawazo Unavyorithishwa:
1. Vibeba ujumbe wa Kiumolekiuli (Molecular Messengers):
Panya dume waliokuwa kwenye msongo wa mawazo walionyesha viwango vya juu vya aina tisa za microRNA maalum katika mbegu zao. MicroRNA hizi hufanya kazi kama ishara au ujumbe wa kibaolojia unaoathiri namna vinasaba hujieleza baada ya utungwaji mimba.
2. Mabadiliko ya Tabia (Behavioral Changes):
Watafiti walipochukua RNA hizi na kuzidunga katika viinitete vya panya waliokuwa na afya, watoto waliotokana nao walionyesha mabadiliko ya mwitikio dhidi ya msongo wa mawazo. Walionekana kuwa na kiwango cha chini cha wasiwasi na walionesha tabia tofauti ikilinganishwa na wengine.
3. Ukuaji wa Ubongo (Brain Development):
Watoto wa panya waliopokea RNA hizo walikuwa na mabadiliko ya uelekezaji wa vinasaba katika sehemu ya hypothalamus ya ubongo—eneo linalohusika moja kwa moja na udhibiti wa msongo wa mawazo. Mabadiliko hayo yalihusiana na miundo ya ubongo na ulinzi wa ubongo dhidi ya sumu kupitia kizuizi cha damu na ubongo (blood-brain barrier).
4. Athari za Mapema (Early Effects):
RNA zilizobadilika kutoka kwa baba zilianza kufanya kazi mara tu baada ya utungwaji mimba. Ziliharibu baadhi ya RNA kutoka kwa mama na kuchochea mabadiliko ya muda mrefu katika maendeleo ya ubongo wa mtoto.
image quote pre code