Bila kujali hali yako ya kifedha, kuwafuatilia watu matajiri zaidi—iwe kwa kuvutiwa, husuda, au chuki—huenda kunafurahisha zaidi na hakuhitaji utafiti kama vile kutafuta rehani, mnunuzi wa mtandaoni, au kusoma masuala ya fedha na uchumi.
Mvuto wa familia tajiri huonyesha utamaduni unaoabudu mali na kuwaabudu matajiri.
Wale walio katika ngazi ya juu ya biashara ni watu mashuhuri machoni mwa watu wengi, na wanafuatiliwa kwa uwezo wao wa kudumisha hali hii ya kumiliki mali.
Ifuatayo ni Orodha ya familia 10 zilizojipatia utajiri wao kupitia biashara mbalimbali duniani.
10. Familia ya Thompson
Familia ya Thomson kutoka nchini Canada ina wastani wa dola bilioni 87.1, hasa kutokana na umiliki wao wa Thomson Reuters, kampuni ya huduma za vyombo vya habari na habari.
Familia hii ilianza kujpatia utajiri mwaka wa 1934 wakati Roy Thomson alipozindua kituo kimoja cha redio huko Ontario, Canada.
Haraka alijitanua katika uwanja wa magazeti na baadaye akaanzisha Shirika la Thomson. Wazao wake waliunganisha kampuni ya Thompson na Reuters katika 2008. Hii ilisaidia katika kuunda nguvu ya kimataifa katika huduma za habari.
9. Familia ya Wertheimer
Familia ya Wertheimer ya Ufaransa ina wastani wa dola bilioni 88 kutoka kwa umiliki wao wa chapa ya kifahari ya Chanel.
Pierre Wertheimer alishirikiana na Coco Chanel katika miaka ya 1920 ili kujenga chapa maarufu ya Chanel.
Hawakugundua kuwa chapa hii ingekuwa mwongozo wa mtindo wa kifahari na wa hali ya juu.
Watoto wake, Alain na Gérard Wertheimer, bado wanamiliki na kuendesha chapa hii wakidumisha hadhi ya chapa hiyo katika ulimwengu wa mitindo karibu karne moja baadaye.
8. Familia ya Ambani
Familia ya Ambani ya India inamiliki wastani wa $99.6 bilioni, hasa kutokana na ushiriki wao katika biashara za nishati, mawasiliano ya simu na zile za rejareja.
Dhirubhai Ambani alianzisha kiwanda cha Reliance Industries mwaka wa 1958, akijihusisha na biashara ndogo ya nguo.
Lakini kupitia hamu na upanuzi wa biashara kemikali za petroli, mawasiliano ya simu na rejareja, Reliance iliibuka na kuwakampuni kubwa ya kibinafsi nchini India.
Hii leo, wanawe Mukesh na Anil wameendeleza urithi huo, huku Mukesh akitawala utajiri wa familia.
Ushawishi wa Mukesh Ambani umeenea na ni zaidi ya uongozi wa kampuni, kwani anaishi katika jumba la kifahari la orofa 27, linalosifiwa kuwa makazi ghali zaidi ya kibinafsi ulimwenguni.
Ushuhuda huu wa utajiri unaonesha umashuhuri wa familia ya Ambani na urithi wa kudumu wa maono ya ujasiriamali ya Dhirubhai ndani ya nyanja za biashara na maisha ya anasa.
7. Familia ya Mars
Familia ya Mars, pia kutoka Marekani, inamiliki $133.8 bilioni, hasa kutokana na umiliki wao wa Mars Inc., inayojulikana kwa kutengeneza peremende na chokoleti mbali na bidhaa za utunzaji wa wanyama.
Frank Mars alianza kutengeneza na kuuza peremende kutoka jikoni mwake mwaka wa 1911.
Mwanawe, Forrest Mars Sr., baadaye alivumbua chapa ya M&M's, ambayo inauza bidhaa maarufu duniani katika nyakati za kisasa. Alipanua zaidi kampuni kimataifa.
Zaidi ya karne moja baadaye, Mars Inc. inasalia kuwa kampuni inayomilikiwa kwa faragha, na familia inaendelea kufurahia mojawapo ya bahati kubwa zaidi duniani katika kutoa huduma za chakula na utunzaji wa wanyama.
6. Familia ya Al Saud
Familia ya Al Saud nchini Saudi Arabia ina wastani wa dola bilioni 140, kufuatia udhibiti wao wa mali ya mafuta ya Familia ya Kifalme ya Saudia, pamoja na Saudi Aramco, na vitega uchumi vingine.
Nasaba ya Al Saud ilijiimarisha katika karne ya 18 na Muhammad bin Saud. Hata hivyo, utajiri mkubwa wa familia hiyo uliunganishwa chini ya Mfalme Abdulaziz Ibn Saud mwaka wa 1932.
Ugunduzi wa hifadhi kubwa ya mafuta katika miaka ya 1930 ulisababisha familia kujiweka katika ustawi usio na kifani, ambao mwingi unahusishwa na Saudi Aramco.
Katika ngazi ya mtu binafsi, Mwanamfalme Mohammed bin Salman anamiliki mali yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 1.
Mandhari hii ya utajiri wa pande nyingi inasisitiza njia mbalimbali ambazo familia ya kifalme ya Saudi imekusanya na inaendelea kudhibiti ushawishi wake mkubwa wa kifedha.
5. Familia ya Koch
Familia ya Koch, yenye makao yake nchini Marekani, ina wastani wa dola bilioni 148.5 kutokana kiwanda chao cha Koch Industries.
Fred C. Koch alianzisha mizizi ya Koch Industries mwaka wa 1940. Hapo awali walizingatia sana biashara ya kusafisha mafuta.
Wanawe, Charles na David Koch, wanastahili sifa zao kwani wamepanua kampuni hiyo kuwa mojawapo ya makampuni makubwa zaidi ya kibinafsi duniani.
Utajiri wa familia ya Koch leo ni onyesho la miongo kadhaa ya upanuzi wa tasnia kutoka kwa nishati hadi utengenezaji.
Utajiri wa Charles Koch unatokana na biashara ya mafuta iliyoanzishwa na babake, lakini hii leo, anajulikana zaidi na umma kwa siasa zake, akitumia fedha zake nyingi kufadhili wagombea na wasomi hususan maprofesa wa vyuo vikuu, na kushawishi nafasi za sera, yote yakilenga kuendeleza ajenda ya kihafidhina.
4. Familia ya Hermes
Utajiri wa familia ya Hermès (Dumas), inayomiliki wastani wa dola bilioni 170.6, unatokana na duka kubwa la kifahari la Hermès, lililoko Ufaransa.
Mwanzo wa ufalme wa familia ya Hermès ulikuwa mnamo 1837.
Thierry Hermès alianza safari yake ya kibiashara kwa kufungua duka kubwa mjini Paris. Zaidi ya karne mbili, Hermès imebadilika na kuwa ishara ya kimataifa ya mtindo wa kifahari na ubora wa hali ya juu wa ufundi.
Tawi la Dumas la familia limeendelea kudumisha udhibiti thabiti wa uzalishaji, kuhakikisha upekee wa chapa na mafanikio makubwa.
Familia ya Hermès inashikilia hisa kubwa katika kampuni hiyo, na karibu 80% ya hisa bado zinamilikiwa na wanafamilia.
Familia kwa jadi imekuwa na jukumu muhimu katika usimamizi wa Hermès, huku wanafamilia mbalimbali wakishikilia nyadhifa za uongozi .
3. Familia ya Al Thani
Familia ya Al Thani ya Qatar inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na dola bilioni 172.9, zilizotokana na usimamizi wao wa rasilimali na uwekezaji wa gesi asilia ya Familia ya Kifalme ya Qatar.
Familia hiyo inatoka kwa kabila la Tamīm, ambalo lilihamia mashariki kutoka Arabia ya kati hadi rasi ya Qatar
Familia hii ya kifalme imetawala Qatar tangu katikati ya karne ya 19. Sheikh Mohammed bin Thani alikuwa mtawala wa kwanza mwaka wa 1868.
Utajiri wao uliongezeka zaidi karne ya 20 kufuatia uchimbaji mkubwa wa hifadhi ya gesi asilia na mafuta ya Qatar, na kuwaweka kama moja ya familia tajiri zaidi za kifalme leo, ambayo inaonekana kuwa njia sawa kwa wengi wa familia za kifalme za Saudi Arabia.
2. Familia ya AL Nahyan
Familia ya Al Nahyan ni familia inayotawala ya Imarati ya Abu Dhabi na mojawapo ya familia sita zinazotawala za Umoja wa Falme za Kiarabu.
Wao ni tawi la Al Falahi, tawi la kabila la Bani Yas, na wana uhusiano wa karibu na familia ya Al Maktoum, inayotawala Dubai.
Familia ya Al Nahyan kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu ina wastani wa dola bilioni 323.9, zinazotokana na udhibiti wao wa mali ya mafuta na uwekezaji ya Familia ya Kifalme ya Abu Dhabi.
Abu Dhabi, mojawapo ya mataifa saba ya emarati inayojumuisha Falme za Kiarabu, inasimama kama mji mkuu wa taifa hilo na ina sehemu kubwa ya hifadhi yake ya mafuta.
Kwa miongo kadhaa, familia ya Al Nahyan imetawala eneo ambalo sasa linaunda UAE, kabla ya zama za mabadiliko zilizoletwa na ukuaji wa mafuta, ambao ulibadilisha uchumi na bahati ya familia ya kifalme.
Familia ya Al Nahyan ni sehemu ya nasaba inayotawala ya Abu Dhabi, yenye mizizi iliyoanzia karne nyingi zilizopita.
Mpito wao kuelekea utajiri wa kisasa ulianza kushamiri katika karne ya 20 na ugunduzi wa mafuta katika UAE katika miaka ya 1950.
Walilenga katika ujenzi wa jalada la uwekezaji wa kimataifa huku wakidumisha ukoo wao wa kifalme na utawala huko Abu Dhabi kwa wakati mmoja.
1. Familia ya Walton
Familia ya Walton inajulikana zaidi kwa umiliki wake wa duka la jumla la Walmart - ambaye ni muuzaji mkubwa zaidi duniani.
Inachukuliwa kuwa familia tajiri zaidi ulimwenguni kutokana na hisa zao kubwa katika duka la Walmart, na jumla ya utajiri unaokadiriwa kuwa $432.4 bilioni.
Utajiri wa familia kimsingi unatokana na mafanikio ya duka hilo na umeenea katika nyanja mbalimbali za biashara na juhudi za uhisani.
Wao ni wazao la wanafamilia Sam Walton, ambaye alikuwa mwanzilishi, na kaka yake Bud Walton, mwanzilishi mwenza wa Walmart katika mwaka wa 1962.
Biashara hii ilianza na duka moja l huko Arkansas.
Kwa miongo kadhaa, duka la Walmart lilipanua himaya yake hadi na kuwa mnyororo mkubwa wa maduka ya rejareja ulimwenguni, unaopatikana kote ulimwenguni katika karibu kila jiji.
Katika nchi za ulimwengu wa kwanza, duka la Walmart linatawala kama duka kuu. Utajiri wa familia umehifadhiwa na kukua kwa uangalifu, huku warithi wengi wakisimamia amana na misingi inayohusishwa na kampuni hiyo.
image quote pre code