Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema licha ya kwamba gharama za upimaji DNA nchini zinafikia hadi Tsh milioni moja lakini Serikali imeamua kugharamia gharama za ziada ili kuwapunguzia Wananchi mzigo ambapo kwa sasa kila Mtu analipia Tsh. laki 1 tu kupima DNA na wanapokuwa Baba, Mama na Mtoto wanalipia Tsh. laki 3 wote kwa pamoja.
Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai , Biolojia na Vinasaba wa Mamlaka hiyo Dkt. Fidelis Buyoge amesema hayo kwenye mahojiano maalum na Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba ofisini kwake Jijini Dar es salaam ambapo
amesema gharama halisi kwa Mtu mmoja inazidi Tsh. laki mbili lakini Serikali inabeba gharama nyingine na Mtu sasa anatozwa laki 1 na kwa Afrika Mashariki Tanzania ndio yenye gharama ndogo za upimaji DNA ukilinganisha na nchi nyingine “Ukienda nchi jirani sitaki kuitaja jina gharama ya kupima kwa Mtu mmoja ni laki 1 na elfu 70”
Dkt. Buyoge amesema takwimu za January hadi December 2024 waliopima DNA kwenye upande wa masuala ya uzazi ni Watu 524 lakini takwimu za mwaka huu bado hazijatolewa ambapo amesema majibu hutolewa ndani ya siku 21 tangu Mtu kupimwa lakini zinaweza hata zisifikie siku hizo hata ndani ya siku 5 majibu yakiwa tayari yanatolewa kupitia kwa Mamlaka ombezi mfano Mahakama, Wakili au Afisa Ustawi wa Jamii na kwamba Mtu aliyepima DNA au Wazazi watachukua majibu kutoka kwenye Mamlaka hizo.
Amesema hata Mtu binafsi anaweza kuamua kwenda kupima DNA na rekodi zake zikabaki tu na sio lazima kuwe na migogoro ya masuala ya uzazi huku akisisitiza kuwa DNA inasaidia hata kwenye mirathi ili Ndugu wajue uhalali wa Wanafamilia kwakuwa Watoto wa Baba na Mama mmoja DNA zao hufanana “Kuhusu Watu wanaopima kujua uhalali wa Mtoto hatujawahi kuwa na kesi za ambazo zimetufikia za Watu kugombana baada ya majibu”
image quote pre code