Ajali ya Boti yaua Watu 27 Ghuba ya Ha Long, Vietnam, Leo

Ajali ya Boti yaua Watu 27 Ghuba ya Ha Long, Vietnam, Leo

#1

Takriban watu 27 wamefariki baada ya boti ya watalii kupinduka katika Ghuba ya Ha Long, Vietnam, Leo Julai 19, 2025 kutokana na hali mbaya ya hewa, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.



Boti hiyo, iliyokuwa imebeba watu 53, ilipinduka majira ya saa nane mchana wakati Dhoruba ya Wipha ilipokuwa ikikaribia kutoka Bahari ya Vietnam Mashariki, ikileta upepo mkali, mvua kubwa na radi.

Ripoti zinaeleza kuwa wengi wa waliokuwemo ni watalii kutoka jiji la Hanoi. Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kuhusu uraia wa wahanga huku uokoaji ukiendelea.

Ghuba ya Ha Long, takriban kilomita 200 kutoka Hanoi, ni kivutio maarufu cha utalii kinachopokea maelfu ya wageni kila mwaka. Ziara za boti ni moja ya shughuli kuu za vivutio hivyo.

Dhoruba ya Wipha ni kimbunga cha tatu kufika kwenye Bahari ya Vietnam Mashariki mwaka huu, na inatarajiwa kutua katika pwani ya kaskazini ya nchi hiyo mapema wiki ijayo.

Hali ya hewa hiyo pia ilisababisha usumbufu katika safari za ndege, ambapo ndege tisa zilielekezwa viwanja vingine na ndege tatu za kuondoka kusimamishwa kwa muda.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code