Sudan kuzuia Whatsapp Call Audio na Video

Sudan kuzuia Whatsapp Call Audio na Video

#1

Mamlaka ya mawasiliano nchini Sudan, imesema mwishoni mwa juma hili kuwa itazuia upigaji wa simu na video kupitia mtandao wa WhatsApp, zikisema ni kwa sababu za tishio la usalama wa taifa hilo.



Kwa mujibu wa gazeti la mtandao la Sudan Tribune, hatua hii itaenda kuwaathiri maelfu ya raia wa Sudan ambao wanategemea programu ya WhatsApp kwa mawasiliano, wakati huu pia huduma ya intaneti ikiwa imetatizika pakubwa nchini humo.

Katika taarifa yake, mamlaka ya mawasiliano inasema udhibiti wa huduma za mawasiliano ya simu kwa njia ya WhatsApp utaanza kufanyika kuanzia Ijumaa ya wiki hii hadi pale kutakapotolewa maelekezo mengine.

Aidha mamlaka zinasema huduma nyingine za progarmu hiyo kama vile kutuma ujumbe mfupi wa maandishi na mawasiliano ya makundi zitasalia kama kawaida.

Uamuzi huu pia utawaathiria raia wanaoishi nje ya Sudan, ambapo wanategemea kupiga simu za kawaida na video kwa kutumia WhatsApp kuwasiliana na ndugu zao walioko nyumbani na ambao wanapitia madhila ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code