Kichaa cha mbwa,chanzo,dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Rabies (kichaa cha mbwa) ni ugonjwa hatari wa maambukizi unaosababishwa na virusi vya rabies. Virusi hivi hushambulia mfumo wa neva (ubongo na uti wa mgongo).

 Jinsi unavyopata:

Kupitia kung’atwa au kukwaruzwa na mnyama mwenye maambukizi (hasa mbwa, lakini pia paka, popo n.k.).

Kupitia mate ya mnyama aliyeambukizwa yakiingia kwenye jeraha lililo wazi au utando (mf. machoni, mdomoni).

Dalili kuu kwa binadamu:

-Maumivu au ganzi sehemu ya jeraha

-Homa, uchovu, maumivu ya kichwa

-Wasiwasi, usingizi au dalili za kuchanganyikiwa

-Maumivu ya misuli na kichefuchefu

-Kuwa na hali ya Kuogopa maji (hydrophobia) au mwanga

-Degedege na hatimaye kupoteza fahamu

-Kubweka kama Mbwa

⚠️ Muhimu: Rabies(Kichaa cha Mbwa) mara nyingi husababisha kifo mara dalili zinapoanza kuonekana.

Kuzuia:

Chanjo ya mbwa na paka (wanaonyonya damu pia wanaweza kuwa chanzo)

Chanjo kwa binadamu walioumia au kung’atwa kabla dalili hazijaanza (Post Exposure Prophylaxis – PEP)

Usipuuze kung’atwa na mbwa, paka, au popo – nenda hospitali mara moja kwa chanjo.

0 Comment

WEWE NI SHUJAA,TUMIA UWEZO HUO HUO ULIOKUWA NAOAfyaclass Bongo Social •

WEWE NI SHUJAA,TUMIA UWEZO HUO HUO ULIOKUWA NAO



Mstari wa Kusimamia ni Waamuzi 6:11-16

Waamuzi 6:11 Malaika wa Bwana akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.

Mstari 12 Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, Bwana yu pamoja nawe, Ee shujaa.

Mstari 13 Gideoni akamwambia, Ee Bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametupata? Yako wapi matendo yake ya ajabu, waliyotuhadithia baba zetu, wakisema, Je! Siye Bwana, aliyetuleta huku kutoka Misri? Ila sasa ametutupa, naye ametutia katika mikono ya Midiani.

Mstari 14 Bwana akamtazama, akasema, Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani. Je! Si mimi ninayekutuma?

Mstari 15 Akamwambia, Ee Bwana, nitawaokoa Israeli kwa jinsi gani? Tazama, jamaa zangu ndio walio maskini sana katika Manase, na mimi ndimi niliye mdogo katika nyumba ya baba yangu.

Mstari 16 Bwana akamwambia, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja.

Usijidharau wewe ni Shujaa, Kipo kitu ambacho Mungu kaweka ndani yako, kwa uwezo huo huo inuka wewe ni Shujaa ukatende mambo makubwa,

Haijalishi kwenu ni Maskini Sana,Haijalishi wewe ni mdogo kuliko wote, wala haijalishi upo ndani ya mapango umejificha saa hii Kama Gideoni,uwezo wako hauonekani na Mtu yeyote. Bwana yu Pamoja nawe,Ee shujaa,Enenda kwa uwezo wako huu,utafanya mambo makubwa.

0 Comment

Sababu za hedhi kuchelewa na kubadilika badilikaAfyaclass Bongo Social •

Sababu za hedhi kuchelewa na kubadilika badilika

Nini kinasababisha hedhi kuchelewa

Endapo una aina ya mzunguko wa hedhi ambao haubadiliki badiliki yaani regular menstrual cycles, kuna wakati unaweza kukutana na vipindi vya hedhi kuchelewa kuliko kawaida,

Hii huweza kukupa wasi wasi nini kinaendelea mwilini, Moja ya Sababu ya haraka haraka ambayo unaweza kufikiria ni kuhusu kubeba Mimba.

Katika Makala ya Leo,tumechambua Sababu kuu zinazoweza kukusababishia Hedhi yako ichelewe.

Nini kinasababisha hedhi kuchelewa

Zipo Sababu nyingi ambazo huweza kuchangia tatizo hili, na Baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na;

1.Ujauzito,

2.Mabadiliko ya homoni – msongo wa mawazo, uchovu mwingi, au mabadiliko ya chakula/mazingira yanaweza kuchelewesha siku.

3.Magonjwa ya mfumo wa uzazi – mfano PCOS (polycystic ovarian syndrome), matatizo ya tezi (thyroid), au maambukizi.

4.Dawa fulani – mfano dawa za homoni, kupanga uzazi, au zingine.

5.Uzito kubadilika ghafla – kupungua sana au kuongezeka haraka.

Tuchambue Vizuri Sababu hizo.....

1. Kufanya Mazoezi kupita kiasi, Exercising Rigorously

Kila kitu kinataka kiasi, hata Mazoezi tunasema yana Faida nyingi mwilini lakini pia yanataka Kiasi,

Unaweza kuona shida ya kuchelewa kwa hedhi kutokana na kufanya mazoezi mazito. Mazoezi ya nguvu ya mara kwa mara yanaweza kusababisha vipindi visivyo kawaida vya hedhi ikiwemo kukosa hedhi. Unaweza pia kupata hedhi isiyo ya kawaida ikiwa utaanza kufanya mazoezi tena baada ya kutofanya kwa muda.

Mazoezi kupita kiasi husababisha physical stress mwilini mwako, Hali ambayo huuambia Ubongo Kuacha kuzalisha vichocheo yaani reproductive hormones.

Moja ya vichocheo hivo ni Pamoja na gonadotropin-releasing hormone (GnRH).  Hormone hii ndyo inayohusika na Muda wa Hedhi yako kutoka,Ikiwa Ubongo haujaitoa au unaitoa Taratibu sana hedhi inaweza kuacha Kutoka.

2.  Mabadiliko kwenye Uzito wa Mwili

Kichocheo cha Estrogen kwa asilimia kubwa huzalishwa kutoka kwenye tishu zinazotengeneza mafuta baada ya kipindi cha Ukomo wa Hedhi(menopause),tishu hizi hufahamika kama adipose tissue,

Ingawa,Mwanamke mwenye mafuta yaliyozidi,mwili wake huweza kuzalisha estrogen nyingi kipindi chochote cha Maisha yake sio tena baada ya kufikia ukomo wa hedhi. Hii ina maana kadri kiwango cha Mafuta kinapozidi mwilini ndivo kiwango cha estrogen huongezeka pia.

Matokeo yake,Estrogen ikizidi huathiri mzunguko wa hedhi na kuleta madhara kama vile;

  • Kuvuja damu nyingi ya Hedhi
  • Kukosa Hedhi
  • Hedhi kuchelewa kutoka
  • Au Hedhi kutokutoka kwa mpangilio

Hivo ukiwa na Uzito Mkubwa upo kwenye hatari hii,

FAHAMU,Kama Uzito wako wa mwili unapungua kupita kiasi kwa kasi sana upo kwenye hatari ya Kupata mabadiliko ya Hedhi Pia.

Estrojeni ni muhimu kwa ajili ya kujenga ukuta wa uterasi kwa mimba inayoweza kutokea wakati wa mzunguko wa hedhi. Unapopoteza uzito mwingi, mwili wako hautoi estrojeni ya kutosha.

3. Kuwa na Msongo wa Mawazo au Stress

Hali ya Stress inaweza kusababisha mabadiliko ya Hedhi ikiwemo hedhi kuchelewa kutoka,

Utafiti umeonyesha kuwa watu walio na viwango vya juu vya mfadhaiko,Msongo wa mawazo au Stress pia walikuwa wakipata vipindi visivyo kawaida vya HEDHI.

Wakati STRESS inaathiri muda wa hedhi, inaweza kuathiri uzazi Pia. Wale ambao wana Stress kwa kiwango kikubwa wanaweza kuwa na wakati mgumu zaidi wa kupata mimba au kuwa na ujauzito usio na matatizo.

4. Mabadiliko ya vichocheo au Hormones mwilini

Mfano kwenye tezi la thyroid—Homoni za tezi la Thyroid huwajibika kwa udhibiti wa nishati ya mwili wako na huathiri viungo vingi. Viwango vya homoni za tezi hili vinapokuwa juu au chini, utendaji wa mwili wako unaweza kubadilika—pamoja na utendajikazi wako wa mzunguko wa hedhi.

Kwa wale wanaozalisha kiwango kikubwa cha thyroid hormone— huweza kupata Hedhi karibu karibu , Na wale ambao hawazalishi thyroid hormone ya kutosha huweza kupata hedhi kwa kuchelewa au mara chache Zaidi

5. Kuwa kwenye Mazingira yenye Dawa za kuua wadudu,Exposure to Pesticides

Pesticides zinaweza kuwa na uhusiano wa karibu na mabadiliko ya Hedhi yaani irregular periods.

Washiriki wa utafiti mmoja walikuwa wamekabiliwa na dawa za kuulia wadudu kutokana na kufanya kazi kwenye mashamba, kuishi ndani yake, au vyote viwili.

Wengi walikabiliwa na viuatilifu vya kemikali vinavyovuruga mfumo wa endocrine, dawa ya kuua wadudu inayojulikana kusababisha mabadiliko ya hedhi. Washiriki waliripoti hitilafu katika urefu wa mzunguko wao na kutokuwepo kwa kipindi chao cha Hedhi kwa zaidi ya siku 90.

6. Unyonyeshaji

Ukichagua kunyonyesha mara kwa mara, kipindi chako cha Hedhi hakirudi mara moja. Hii inajulikana kama Lactational amenorrhea, Na hutokea baada ya mtu kujifungua na huongeza muda wa mtu kupata mimba tena. Kwa sababu hiyo, baadhi ya watu huitumia kama njia ya uzazi wa Mpango.

7. Umri

Kipindi chako cha Hedhi kinaweza kisiwe cha kueleweka hadi miaka yako inapofikia 20. Hata hivyo, unapokaribia kukoma hedhi, hedhi inaweza kuwa isiyo ya kawaida tena.

Ingawa labda unatarajia kupata Hedhi kidogo unapokaribia kukoma kwa hedhi, inaweza kutofautiana kulingana na wakati wake. Kwa mfano, hedhi yako inaweza kusimama kwa miezi michache kisha kurudi bila kutarajia.

Hizo ndyo baadhi ya Sababu za Kuchelewa kwa Hedhi…!!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILINE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Shinikizo la damu kuwaweka hatarini watu zaidi ya bilioni moja duniani – Ripoti ya WHOAfyaclass Bongo Social •

Shinikizo la damu lisilodhibitiwa lawaweka hatarini watu zaidi ya bilioni moja duniani – Ripoti ya WHO



Dk. Shuaib anaangalia shinikizo la damu na kutoa nyenzo za elimu kwa wanawake wakati wa kampeni ya uhamasishaji dhidi ya ukeketaji wa wanawake (FGM) katika kambi ya Rabbi Yasir kwa wakimbizi wa ndani nje kidogo ya Mogadishu.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limezindua ripoti yake ya pili ya kimataifa kuhusu shinikizo la damu, ikionesha kuwa watu bilioni 1.4 waliishi na tatizo hilo mnamo mwaka 2024. Hata hivyo, ni zaidi kidogo ya mtu mmoja kati ya watano walioweza kulidhibiti kupitia dawa au kubadili mitindo ya maisha yenye hatari kiafya.

Ripoti hiyo mpya imezinduliwa leo  Jumanne,tarehe 23 mwezi Septemba 2025 wakati wa hafla iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya WHO na taasisi kama Bloomberg Philanthropies na Resolve to Save Lives wakati wa Mkutano wa 80 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Pia ripoti imebaini kuwa ni asilimia 28 pekee ya nchi zenye kipato cha chini zinazoripoti upatikanaji wa dawa zote zinazopendekezwa na WHO katika maduka ya dawa au vituo vya afya vya msingi.

Shinikizo la damu ni nini?

Shinikizo la damu ni moja ya visababishi vikuu vya mshtuko wa moyo, kiharusi, ugonjwa sugu wa figo na hata shida ya kupoteza kumbukumbu. Ni tatizo linaloweza kuzuilika na kutibika, lakini bila hatua za haraka, mamilioni wataendelea kufariki mapema huku nchi zikikabiliwa na hasara kubwa za kiuchumi. Kuanzia mwaka 2011 hadi 2025, magonjwa ya moyo na mishipa—yakiwemo shinikizo la damu—yanakadiriwa kugharimu nchi zenye kipato cha chini na cha kati kiasi cha dola trilioni 3.7 za Kimarekani, sawa na takribani  asilimia 2 ya jumla ya pato lao la taifa.

Kwa kila saa moja, maisha zaidi ya 1,000 yanapotea kutokana na kiharusi na mshtuko wa moyo unaosababishwa na shinikizo la damu, na vifo vingi kati ya hivyo vinaweza kuzuilika,” amesema Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Ameongeza Dr. Tedros “Nchi zina nyenzo za kubadili hali hii. Kwa dhamira ya kisiasa, uwekezaji endelevu na mabadiliko ya mifumo ya huduma za afya ili kujumuisha udhibiti wa shinikizo la damu, tunaweza kuokoa mamilioni ya maisha na kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wote.”

Kwa mujibu wa Dkt. Kelly Henning, kiongozi wa mpango wa afya ya umma wa Bloomberg Philanthropies: “Shinikizo la damu lisilodhibitiwa husababisha idadi ya vifo zaidi ya milioni 10 kila mwaka, licha ya kuwa ni tatizo linaloweza kuzuilika na kutibika. Nchi zinazojumuisha huduma za shinikizo la damu katika bima ya afya kwa wote na huduma za msingi zinafanya maendeleo makubwa, lakini nchi nyingi zenye kipato cha chini na cha kati bado zimesalia nyuma. Sera madhubuti za kuongeza uelewa na upatikanaji wa matibabu ni muhimu ili kupunguza maradhi ya moyo na vifo vinavyoweza kuzuilika.”

Vikwazo vinavyoendelea

Takwimu kutoka nchi na maeneo 195 zinaonesha kuwa nchi 99 zina viwango vya udhibiti wa shinikizo la damu chini ya asilimia 20. Wengi wa waathirika wanaishi katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati ambako mifumo ya afya ina changamoto za rasilimali.

Ripoti imeweka wazi mapengo makubwa katika kinga, uchunguzi, matibabu na ufuatiliaji wa muda mrefu. Vikwazo vikuu ni pamoja na sera dhaifu za afya ya umma dhidi ya hatari kama vile matumizi ya pombe na tumbaku, kutofanya mazoezi, ulaji mwingi wa chumvi na mafuta yenye madhara; ukosefu wa vifaa vya kisasa vya kupima shinikizo la damu; uhaba wa miongozo ya matibabu na timu za afya ya msingi zilizo na ujuzi; upungufu wa mnyororo wa ugavi na gharama kubwa za dawa; ukosefu wa kinga ya kifedha kwa wagonjwa; pamoja na mifumo dhaifu ya taarifa za ufuatiliaji.

Upatikanaji wa dawa – nguzo ya mafanikio

Dawa za shinikizo la damu ni miongoni mwa nyenzo bora zaidi na nafuu za afya ya umma. Hata hivyo, nchi 7 kati ya 25 zenye kipato cha chini (sawa na asilimia 28) ndizo pekee zinaripoti kuwa dawa zote zinazopendekezwa na WHO zinapatikana kwa ujumla, ikilinganishwa na asilimia 93 ya nchi zenye kipato cha juu.

Dawa salama, bora na za gharama nafuu za kudhibiti shinikizo la damu zipo, lakini bado watu wengi sana hawazipati,” amesema Dkt. Tom Frieden, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Resolve to Save Lives. “Kuziba pengo hili kutaokoa maisha na pia kuokoa mabilioni ya dola kila mwaka.”

Mafanikio katika nchi mbalimbali licha ya changamoto

Licha ya changamoto, baadhi ya nchi zimeonesha mafanikio makubwa kwa kuingiza huduma za shinikizo la damu katika bima ya afya kwa wote, kuimarisha huduma za msingi na kushirikisha jamii:

Bangladesh: imeongeza udhibiti wa shinikizo la damu kutoka asilimia 15 hadi asilimia 56 katika baadhi ya maeneo kati ya mwaka 2019 na 2025 kwa kujumuisha huduma hizo katika kifurushi cha huduma muhimu za afya na kuimarisha uchunguzi na ufuatiliaji.

Ufilipino: umejumuisha ipasavyo kifurushi cha kiufundi cha WHO kinachoitwa HEARTS katika huduma za kijamii kote nchini.

Korea Kusini: imefanya mageuzi ya kiafya kwa kupunguza gharama za dawa za shinikizo la damu na ada za wagonjwa, na kufanikisha viwango vya juu vya udhibiti wa shinikizo la damu kitaifa – asilimia 59 mwaka 2022.

WHO imetoa wito kwa nchi zote kujumuisha udhibiti wa shinikizo la damu katika mageuzi ya huduma za afya kwa wote. Utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti unaweza kuzuia mamilioni ya vifo vya mapema na kupunguza gharama kubwa za kijamii na kiuchumi zinazotokana na tatizo hili.

0 Comment

Wanamke hupata U.T.I kwa urahisi zaidi kuliko wanaumeAfyaclass Bongo Social •

wanamke hupata U.T.I kwa urahisi zaidi kuliko wanaume.

Sababu kuu ni tofauti za kimaumbile kati ya jinsia hizo:

1. Urefu wa urethra (mrija wa mkojo):

  • Kwa mwanamke, urethra ni fupi zaidi (takriban sentimita 4) kuliko ya mwanaume (takriban sentimita 15–20).
  • Hii inamaanisha bakteria husafiri umbali mfupi kufika kwenye kibofu cha mkojo kwa mwanamke.

2. Karibu na njia ya haja kubwa:

  • Urethra ya mwanamke ipo karibu zaidi na anus (tundu la haja kubwa).
  • Bakteria kama E. coli kutoka kwenye haja kubwa hupata urahisi wa kuingia kwenye mrija wa mkojo.

3. Athari za homoni na mabadiliko ya mwili:

  • Wakati wa ujauzito au mabadiliko ya homoni, misuli na mirija ya mkojo inaweza kulegea, hivyo kuruhusu bakteria kuongezeka.
  • Pia ukavu ukeni baada ya kukoma hedhi unaweza kuongeza hatari ya maambukizi.

4. Tabia na sababu za mazingira:

  • Kufutwa vibaya baada ya haja kubwa (kutoka nyuma kwenda mbele) hupeleka bakteria karibu na urethra.
  • Kufanya tendo la ndoa mara nyingi pia huongeza uwezekano wa bakteria kusukumwa kuelekea urethra.
  • Kutokukojoa mara baada ya tendo la ndoa pia ni sababu.

Kwa wanaume, mrija mrefu na majimaji ya tezi dume (prostate secretions) husaidia kuzuia maambukizi — ndiyo maana kwao ni nadra ikilinganishwa na Wanawake.

0 Comment

Vyakula Vya Kuondoa Gesi Tumboni Au Tumbo KujaaAfyaclass Bongo Social •

Vyakula Vya Kuondoa Gesi Tumboni Au Tumbo Kujaa

Watu wengi wamekuwa wakiniomba mada hii japo nilishawahi kuitoa huko nyuma baada ya kuhangaika sana na matumbo yao kujaa gesi na pengine kuvimba. Leo hii nitairudia kwa kuletea baadhi ya vyakula vya kuondoa hili tatizo kama linakusumbua kwa muda mrefu. Pia kuna dawa maalum.

Kwa njia moja au nyingine, unajikuta tumbo limechafuka kwa kujaa gesi, kuuma na hata kuunguruma, unahisi unahitaji kunywa dawa ili litulie.

Katika makala ya leo utajifunza njia bora ya kutuliza mchafuko wa tumbo kwa kutumia vyakula badala ya dawa za kisasa ambazo hutuliza dalili na haziondoi tatizo.

Kabla ya kukimbilia kwenye tiba ni vizuri kwanza kujua chanzo cha tatizo na katika hili unahitaji kujua ni vyakula gani ukila vinasababisha matatizo ya tumbo. Aina ya vyakula inaweza kutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kuna aina ya vyakula vinajulikana zaidi kusababisha matatizo ya tumbo.

Vyakula na vinywaji vinavyochangia tumbo kujaa na ukosefu wa choo kwa muda mrefu huwa ni soda, ulevi (hasa bia), vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye chumvi nyingi.

Vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakula na uondoaji wa uchafu kwenye utumbo, hivyo huwa kikwazo katika mfumo mzima wa usagaji chakula kwa urahisi.

Ili kujiepusha na matizo ya tumbo ya muda mrefu na hata kuzuia uwezekano wa kuumwa na tumbo mara kwa mara, unashauriwa kula vifuatavyo, karibu kila siku ili kulifanya tumbo lako kuwa safi wakati wote:

PAPAI (PAPAYA)
Baadhi ya utafiti uliyopo, unaonesha kwamba ‘enzyme’ waliyomo kwenye papai husaidia usagaji wa chakula tumboni hivyo kulifanya tunda hili kuitwa na mtafiti wa zama za kale Christopher Columbus kama ‘tunda la malaika’.
Watafiti wamebaini kuwa tunda hili, lenye ladha tamu na harufu nzuri, huboresha mfumo wa usagaji chakula, husafisha utumbo, huzuia magonjwa ya uvimbe tumboni na huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

“Vitamini na virutubisho vya papai vina faida nyingi, lakini faida kubwa ya papai ipo kwenye kirutubisho (Enzyme) aina ya ‘Papain’ ambacho hujulikana kwa uwezo mkubwa ilionao wa usagaji mzuri wa chakula tumboni,” anasema Dk. Cari Case mwandishi wa blogu ya masuala ya afya.

Mwandishi huyo anaongeza kwa kusema kuwa papai limekuwa likitumika kama tiba tangu karne ya 18, lakini utafiti wa kisayansi haukugundua faida za papai hadi mwaka 1870 wanasayansi walipogundua kirutubisho cha papain kilichomo kwenye papai na tangu wakati huo tafiti nyingi zimekuwa zikifanywa kuhusu faida za tunda hili na uwezo wa tiba iliyonalo.

MTINDI (YOGURT)
Hata kama wewe si mpenzi wa mtindi, jaribu kunywa na utaupenda, hasa uwezo wake wa kuondoa matatizo ya kujaa gesi tumboni pamoja na matatizo mengine. Mtindi mzuri ni ule ‘plain’ ambao haujachanganywa na ladha au vitu vingine kwa lengo la kuongeza ladha. Bakteria asilia waliyomo kwenye maziwa mtindi ndiyo hufanya usagaji wa chakula kuwa mwepesi.

Mwisho, ili kupata faida ya papai na mtindi kama ilivyoelezwa hapo juu, ni vizuri ukala mara kwa mara kama siyo kila siku, kabla au mara baada ya kula vyakula ambavyo vinaweza kukuletea shida tumboni, au ukaweka mazoea ya kula kila siku ili kuliweka tumbo lako katika hali salama.

0 Comment

Mama aweka rekodi ya dunia kujifungua Mtoto mwenye kilo 6Afyaclass Bongo Social •

Mama mmoja wa miaka 40 kutoka Florida ameandika historia baada ya kuzaa mtoto mkubwa zaidi kwenye hospitali ya Mt.. Joseph’s-South.



Daniella Hines alijifungua mwanae, Annan, tarehe 3 Septemba, akiwa na uzito wa paundi 13 na ounces 15 (takriban kilo 6), karibu mara mbili ya uzito wa wastani wa mtoto wa kuzaliwa.

Wauguzi na madaktari walieleza kuwa mtoto huyo mara moja aligeuka kuwa gumzo kwenye wodi ya wazazi. Hii sio mara ya kwanza kwa Hines kupata mtoto mkubwa; mwanae mkubwa, Andre Jr., alizaliwa akiwa na paundi 12 na ounces 11.



“Hakuwa mdogo kabisa. Nilijiuliza, ‘Mtoto huyu ni wa nani? Amekuja kutoka tumboni kwangu kweli?’” Hines alisema, akiongeza kuwa wafanyakazi wa hospitali walikuwa wakiingia mara kwa mara kumwona mtoto ambaye alihisi kama “supastaa mchanga''

Hines na mumewe, wote wakiwa na urefu zaidi ya futi 6, wanaamini kuwa vinasaba vilichangia uzito wa mtoto. Ingawa bado ana wiki moja tu, Annan tayari ni mtoto mtulivu—isipokuwa anapokuwa na njaa.

0 Comment

Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na TibaAfyaclass Bongo Social •

Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na Tiba

Hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini kwa kitaalam hujulikana kama Formication

Baadhi ya watu hupatwa na shida hii ya kuhisi kama kuna Vitu vinatembea Mwilini Kila wakati,

Je chanzo chake ni nini?

Chanzo cha Kuhisi vitu vinatembea mwilini

Zipo Sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii,na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na hizi:

1. Ugonjwa wa brucella:

Kwa Asilimia Kubwa hizi ni dalili za Ugonjwa wa Brucella

Ugonjwa wa Brucella ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Brucellosis na chanzo chake kikubwa ni maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama BRUCELLA,

Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng'ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k, 

Baadhi ya dalili zake ni:

  • Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara
  • Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa
  • Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali au kuwa na Homa
  • Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote
  • Mwili kuchoka Sana
  • Kupata maumivu ya Viungo,joint n.k.

2. Matatizo kwenye mfumo wa Neva(Neurological conditions): 

Kwa Mtu mwenye ugonjwa wowote unaoathiri utendaji kazi wa Neva anaweza kupata dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini, Mfano ni magonjwa kama vile;

  •  Ugonjwa wa kisukari ambao husababisha hali inayoitwa diabetic neuropathy n.k.

3. Kuwa na matatizo katika afya ya Akili: 

Wakati mwingine ukiwa na Msongo wa mawazo mkubwa,Hofu sana,au hali zingine zinazohusu afya ya akili unaweza kupata dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini

4. Matumizi ya baadhi ya Dawa: 

Zipo baadhi ya dawa ukitumia unaweza kupata hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini

5. Matatizo ya Ngozi(Skin conditions): 

Yapo baadhi ya matatizo ya ngozi kama vile;

  • Tatizo la ngozi kuwa kavu(Dry skin), 
  • Mzio kwenye ngozi(Skin allergic reactions), 
  • Au matatizo kama scabies wakati mwingine huweza kusababisha hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini

6. Upungufu wa Virutubisho mwilini(Nutritional deficiencies): 

Baadhi ya tafiti zinaonyesha,Kuwa na kiwango kidogo cha madini kama vile magnesium au upungufu wa Vitamini B mwilini huweza kuchangia pia dalili hii ya  Kuhisi vitu vinatembea mwilini

7. Mabadiliko ya Vichocheo mwilini(Hormonal changes): 

Mfano kwa Baadhi ya Wanawake wakifika kipindi cha ukomo wa hedhi(menopause) hupata mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini, hali ambayo huweza kuchangia dalili hii pia ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Hedhi ya muda mrefu au hedhi mfululizo chanzo chakeAfyaclass Bongo Social •

Hedhi ya muda mrefu au hedhi mfululizo (inayodumu zaidi ya siku 7 au kurudi mara kwa mara bila kupumzika) mara nyingi ni ishara ya tatizo la kiafya. Sababu zake kuu ni:



Vyanzo vya hedhi ya muda mrefu/mfululizo

1. Mabadiliko ya homoni, au Tatizo la hormone imbalance

  • Upungufu wa homoni ya progesterone au ongezeko la estrogen huchangia ukuta wa mfuko wa uzazi kukua kupita kiasi na kutoka damu nyingi.
  • Mara nyingi hutokea kwa wasichana walio katika balehe au wanawake wanaokaribia kukoma hedhi.

2. Uvimbe na ukuaji usio wa kawaida

Hapa tunazungumzia matatizo mbali mbali kwenye kizazi kama vile;

  • Tatizo la Fibroids (uvimbe kwenye mfuko wa uzazi).
  • Polyps za kwenye kizazi.
  • Saratani ya mfuko wa uzazi au shingo ya kizazi.n.k

3. Magonjwa ya damu na matatizo ya kuganda kwa damu

Upungufu wa chembe sahani (platelets).

Magonjwa ya kurithi ya damu kama hemophilia.n.k. huweza pia kuchangia hali hii

4. Matumizi ya baadhi ya dawa,Mfano;

Vidonge vya uzazi wa mpango visivyotumika ipasavyo.

Dawa za kupunguza damu (anticoagulants).n.k.

5. Madhara ya baadhi ya Njia za uzazi wa mpango,kama vile;

  • Vidonge
  • Sindano n.k.

6. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali

Mfano; Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke au (PID).n.k.

7. Sababu nyingine

Msongo wa mawazo, uzito mkubwa kupita kiasi au kupungua ghafla, matatizo ya tezi (thyroid disorders). n.k.

🔔 Tahadhari:
Hedhi ya muda mrefu au mfululizo huweza kusababisha upungufu wa damu (anemia) kwa haraka.

Ikiwa damu inatoka kwa wingi sana (unabadili pedi kila chini ya saa 1–2), unaona damu yenye mabonge makubwa, au unahisi kizunguzungu na kuchoka sana, unapaswa kumuona daktari haraka.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Imani ina nguvu ya Kufungua Lango la Uponyaji kwakoAfyaclass Bongo Social •

Imani ina nguvu ya Kufungua Lango la Uponyaji kwako,bila kujali aina ya Ugonjwa ulionao,wala Muda wa Ugonjwa unaokusumbua. Soma kisa hiki...

Tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, amehangaika kila mahali,kaenda kwa matabibu wengi,katumia vyote alivyokuwa navyo asipate kupona ugonjwa wake.

Akaenda kwa YESU kwa Imani akisema Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona.

Mathayo 9:22 "Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu; IMANI YAKO IMEKUPONYA. Yule mwanamke akapona tangu saa ile".

Marko 5:29 "Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule".

Soma "Mathayo 9:20–22,Marko 5:25–34"

Na wewe Nenda kwa Yesu kwa Imani,Peleka Ugonjwa wako kwake,Utapokea Uponyaji.....

0 Comment

Tatizo La Homoni Imbalance Kwa WanaumeAfyaclass Bongo Social •

Tatizo La Homoni Imbalance Kwa Wanaume



Tatizo la homoni imbalance kwa wanaume hutokea pale ambapo viwango vya homoni za kiume (hasa testosterone) au homoni nyingine mwilini vinakuwa juu mno au chini mno kuliko kawaida.

Sababu zinazoweza kusababisha homoni imbalance kwa wanaume

Kupungua kwa testosterone (Low T) – hutokea kadri umri unavyoongezeka au kwa matatizo ya kiafya.

Matatizo ya tezi aina ya (pituitary gland)

Unene kupita kiasi (obesity).

Kisukari aina ya 2.

Matumizi ya dawa fulani (mf. steroids, chemotherapy).

Magonjwa ya ini, figo au tezi la thyroid.

Poor Diet: kula vyakula vyenye Sukari nyingi kwa kiwango kikubwa pamoja na vyakula vya kusindika au processed foods inaweza kusababisha ukinzani wa insulini na matatizo ya homoni.

Ukosefu wa Mazoezi: Mazoezi ya mara kwa mara ni muhimu ili kudumisha viwango vya homoni mwilini. 

Msongo wa mawazo wa Muda mrefu(Chronic Stress): Msongo wa mawazo wa muda mrefu husababisha viwango vya cortisol kuwa juu ambapo hali hii inaweza kushusha homoni nyingine. 

Dalili za homoni imbalance kwa wanaume

Kupungua kwa nguvu za kiume (low libido),

hamu ya tendo kupungua au kuisha kabsa

Uume kulegea na kuwa dhaifu au kushindwa kabisa kusimama.

Uchovu wa mara kwa mara na kukosa nguvu.

Kupungua kwa nguvu kwenye misuli na kuongezeka kwa mafuta tumboni.

Mabadiliko ya hisia: kuwa na huzuni, msongo, au hasira za haraka.

Kuongezeka au kupungua kwa nywele mwilini.

Kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu na uwezo wa kuzingatia.

Matiti kuongezeka ukubwa (gynecomastia) kutokana na estrogen kuongezeka. n.k.

Je,Una tatizo hili na hujapata Tiba bado?

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mruhusu Mungu akuonyeshe Njia utakayoiendeaAfyaclass Bongo Social •

Ujumbe wa Leo kwako,Unakukumbusha kwamba Mungu ni njia na jibu la kila Swali ulilonalo.

Mruhusu YEYE akuonyeshe njia utakayoiendea. "Zaburi 32:8- Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama".

Weka tumaini lako lote kwake, weka Imani yako yote kwake nawe utapata jambo jema, faraja, au suluhisho la kila tatizo ulilonalo.

Tumia akili zako kwa kadri Mungu alivyokujalia, lakini kamwe tumaini lako lisiwe kwenye akili zako, Mtumaini Mungu Peke yake kwa moyo wako wote,Mtegemee yeye Peke yake, Nawe Utafanikiwa......

"Mithali 3:5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe".

Ukitegemea akili zako mwenyewe utakwama, Mtegemee Mungu.

Nimatumaini yangu kwamba, Tumaini lako sasa lipo kwa Mungu wako,wala hutegemei akili zako mwenyewe.

Mungu akubariki Sana, na Siku njema kwako......🙏🙏🙏🙏

0 Comment

Mbunifu na Mwanamitindo mashuhuri duniani kutoka nchini Italia Giorgio Armani, amefariki dunia Afyaclass Bongo Social •

Mbunifu na Mwanamitindo mashuhuri duniani kutoka nchini Italia Giorgio Armani, amefariki dunia hii leo Septemba 4, 2025 akiwa na umri wa miaka 91, Kampuni yake imethibitisha.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Kampuni ya Giorgio Armani imeeleza “kwa huzuni isiyo na kifani Kampuni ya Armani Group inatangaza kifo cha muasisi wake, mbunifu na nguvu isiyochoka ya kuendesha chapa hii Giorgio Armani”

Armani alikuwa mbunifu na nembo ya mitindo na ustadi wa Kitaliano wa kisasa na  alijulikana kwa kuchanganya ubunifu wa hali ya juu na ujasiriamali, akiendesha kampuni iliyokuwa ikipata mauzo ya takribani Euro bilioni 2.3 kwa mwaka.

Kwa muda fulani alikuwa akisumbuliwa na maradhi na Juni mwaka huu alilazimika kukosa maonesho ya kampuni yake katika Milan Men’s Fashion Week ikiwa ni mara ya kwanza katika taaluma yake yote kukosa kushiriki kwenye maonesho ya mitindo aliyoyasimamia.

Kampuni ya Armani Group ndio wamiliki wa bidhaa mbalimbali za mavazi ya kike na kiume ya Emperial Armani pamoja na Perfume za Emperial Armani pamoja na saa zake ambapo kwa mujibu wa jarida la Forbes mpaka anafariki alikuwa na utajiri wa bilioni 12.1.

0 Comment

Israel yazindua Satelaiti mpya ya kijasusiAfyaclass Bongo Social •

Israel yazindua Satelaiti mpya ya kijasusi

Israel imesema imefanikiwa kurusha satelaiti mpya ya kijasusi angani, hatua ambayo itaimarisha kwa kiwango kikubwa uwezo wake wa upelelezi katika eneno la Mashariki ya Kati. Kwa mujibu wa maafisa wa Israel, satelaiti hii inaweza kupiga picha za vitu vidogo hadi ukubwa wa sentimita 50, mchana na usiku.

Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, alisema uzinduzi wa satelaiti hiyo, iliyopewa jina la "Horizon 19," ni ujumbe wa moja kwa moja kwa maadui kwamba "tunawaangalia kila wakati na katika hali zote."

Bw. Katz alielezea urushaji huo kuwa ni "mafanikio ya hali ya juu kabisa" ambayo ni mataifa machache pekee duniani yanaweza kuyafikia.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Israel, satelaiti hiyo ilirushwa angani usiku wa Jumanne, Septemba 2, kwa msaada wa roketi cha Shavit, na kufika kwenye obiti ya dunia kwa mafanikio.

Urushwaji wa satelaiti hii mpya unafuatia miezi miwili baada ya vita vya siku 12 kati ya Israel na Iran, ambapo Israel ilishambulia vituo vya kijeshi na vile vya nyuklia vya Iran pamoja na baadhi ya maeneo ya makazi vilivyoko zaidi ya umbali wa kilomita 1,000.

0 Comment

Boti ya Kifahari Yazama Dakika 15 Baada ya UzinduziAfyaclass Bongo Social •

Boti ya Kifahari Yazama Dakika 15 Baada ya Uzinduzi



BOTI mpya ya kifahari (yacht) yenye thamani ya Dola za Kimarekani 940,000 (sawa na takribani Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania) imezama dakika 15 pekee baada ya kuzinduliwa rasmi majini, tukio lililoacha wengi midomo wazi.

Ajali hiyo imetokea takribani mita 200 kutoka ufukweni katika wilaya ya Eregli, mkoa wa Zonguldak, kaskazini mwa Uturuki, siku ya Jumanne.

Mashuhuda walisema yacht hiyo ilianza kupoteza mlingano mara tu baada ya kushushwa majini, na hatimaye kuzama kwa haraka. Mmiliki wa meli hiyo, ambaye alikuwemo ndani, alilazimika kuogelea mwenyewe kuelekea ufukweni. Hakuna taarifa za majeruhi wengine zilizoripotiwa.

Tukio hili limezua mjadala mkali mitandaoni, wengi wakishangazwa na jinsi chombo cha kifahari chenye thamani kubwa kiasi hicho kilivyoshindwa kudumu hata robo saa baharini. Wengine wameeleza masikitiko yao kwa hasara kubwa iliyompata mmiliki, huku baadhi wakigeuza tukio hilo kuwa utani mitandaoni.

0 Comment

Kwanini Usitumie chumvi nyingi sana,hizi hapa ni Sababu kuuAfyaclass Bongo Social •

Kwanini Usitumie chumvi nyingi sana,hizi hapa ni Sababu kuu

Sababu kuu za kuto kutumia chumvi nyingi sana ni kwamba chumvi (hasa chumvi ya kawaida – sodium chloride) ikizidi mwilini inaleta madhara kwa afya. Hapa kuna sababu muhimu:

1. Shinikizo la damu kupanda (High blood pressure)
Kiasi kikubwa cha sodium hufanya mwili ushikilie maji mengi, na hivyo kuongeza mzigo kwenye moyo na mishipa ya damu. Hii husababisha presha ya damu kupanda.

2. Hatari ya magonjwa ya moyo na kiharusi
Shinikizo la damu la muda mrefu huongeza uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo na kiharusi.

3. Madhara kwa figo
Figo ndizo husafisha chumvi iliyozidi mwilini. Kiwango kikubwa cha chumvi huzichosha figo na kuongeza uwezekano wa kupata;

4. Uvimbe mwilini (Edema)
Kwa sababu chumvi huvuta maji, matumizi makubwa husababisha miguu, uso au mikono kuvimba kutokana na maji kuzidi mwilini.

5. Osteoporosis (mifupa kuwa dhaifu)
Chumvi nyingi husababisha mwili kupoteza calcium kupitia mkojo, jambo linaloweza kudhoofisha mifupa na kuongeza hatari ya kuvunjika kwa urahisi.

6. Madhara kwa tumbo
Utafiti unaonyesha chumvi nyingi huongeza hatari ya vidonda vya tumbo na hata saratani ya tumbo (stomach cancer).

🔹 WHO inapendekeza mtu mzima asitumie zaidi ya gramu 5 za chumvi kwa siku (takribani kijiko cha chai kimoja cha chumvi).

0 Comment

Kuku Zaidi ya millioni 40 kupatiwa chanjo bureAfyaclass Bongo Social •

Kuku Zaidi ya millioni 40 kupatiwa chanjo bure

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia imepanga kutoa chanjo za kuku milioni arobaini (40) ambapo jumla ya dozi 19,099,100 za chanjo ya Homa ya Mapafu ya Ng'ombe (CBPP) zimenunuliwa kwa ajili ya kuchanja ng'ombe 19,099,100.

Pia zimepatikana dozi 17,224,200 za chanjo ya Sotoka ya Mbuzi na Kondoo kwa ajili ya kuchanja mbuzi na kondoo 17,224,200, na dozi 40,000,000 za chanjo ya ugonjwa wa kideri/mdondo (ND), ndui na mafua ya kuku kwa ajili ya kuchanja kuku wa asili 40,000,000.

Hata hivyo chini ya Rais Samia, ruzuku ya chanjo na mifumo ya utambuzi wa mifugo imeimarishwa ambapo hadi mwaka 2025 zaidi ya dozi milioni 100 za chanjo zimesambazwa kwa mifugo, huku mfumo wa hereni za kielektroniki ukiwezesha kutambua zaidi ya ng'ombe milioni 3.5.

Hatua hii inalenga kupata ithibati ya WOAH ili Tanzania iweze kuuza mifugo na nyama yake katika masoko ya kimataifa yenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 2 kwa mwaka. Aidha, Mradi wa Chanjo Kitaifa umeanzishwa ukiwa na uwezo wa kuzalisha dozi milioni 50 za chanjo za mifugo kwa mwaka, mradi huu umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 216 na unatarajiwa kupunguza gharama za uagizaji chanjo kutoka nje kwa zaidi ya asilimia 70, kuongeza imani ya walaji wa mazao ya mifugo kutoka ndani na nje ya nchi, na kufungua masoko mapya ya kuuza nyama, maziwa na ngozi katika nchi za Mashariki ya Kati na Asia.

0 Comment

Uume kulegea na kusinyaa Chanzo chake hiki hapaAfyaclass Bongo Social •

Uume kulegea na kusinyaa (kupungua ukubwa au kulegea misuli ya uume) inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali ya kiafya au kisaikolojia. Sababu kuu ni:



1. Sababu za kiafya

  • Mzunguko wa damu hafifu – Shida za mishipa (atherosclerosis, shinikizo la damu, kisukari) hupunguza mtiririko wa damu kwenda uume.
  • Upungufu wa homoni – Kiwango cha chini cha testosterone kinaweza kusababisha uume kulegea na kusinyaa.
  • Matumizi ya dawa – Baadhi ya dawa za presha, depression, au usingizi huathiri nguvu za kiume.
  • Magonjwa sugu – Kisukari, magonjwa ya figo, ini au neva.
  • Ugonjwa wa Peyronie – Kuzalisha kovu kwenye uume husababisha kubadilika umbo, kusinyaa au maumivu.

2. Sababu za kisaikolojia

  • Msongo wa mawazo na wasiwasi
  • Msongo wa kijamii/kiafya (hofu ya kushindwa, matatizo ya kifamilia)
  • Unyogovu au depression

3. Sababu za mtindo wa maisha

  • Uvutaji sigara na pombe kupita kiasi – Huharibu mishipa ya damu.
  • Lishe duni na kutofanya mazoezi – Hupunguza afya ya mishipa na homoni.
  • Unene kupita kiasi – Hupunguza testosterone na kusababisha matatizo ya nguvu za kiume.

Ushauri:

  • Angalia mtindo wa maisha (lishe bora, mazoezi, epuka sigara/pombe).
  • Fanya vipimo vya afya (sukari, shinikizo la damu, testosterone).
  • Ongea na daktari wa mfumo wa mkojo au afya ya uzazi (urologist).
  • Ikiwa ni ya kisaikolojia, msaada wa kisaikolojia na ushauri wa kimaisha husaidia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Muhimbili yafafanua namna ya Kuchangia FigoAfyaclass Bongo Social •

Muhimbili yafafanua namna ya Kuchangia Figo

Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga na Mloganzila) imetoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa uchangiaji figo kwa Wagonjwa wanaohitaji huduma ya kupandikiza viungo hivyo, kufuatia taarifa zinazozunguka kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 2, na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa Hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, huduma za upandikizaji figo zilianza kutolewa rasmi Septemba 2017 na hadi sasa wagonjwa 106 wameshanufaika.

Aligaesha amesema hospitali inazingatia Kanuni za Huduma za Figo zilizotungwa mwaka 2017 kwa kuendana na miongozo na maazimio ya Kimataifa yaliyoidhinishwa na Wizara ya Afya, ambayo yanakataza biashara ya uuzaji viungo vya binadamu.

Aidha, ameeleza kuwa ndugu wa karibu wa mgonjwa pekee ndiye anayeruhusiwa kuchangia figo, na uchangiaji huo hufanyika bila malipo.

Ameongeza kuwa kuna Kamati Maalumu ya Uidhinishaji (Authorization Committee) inayojumuisha Wanasheria, Viongozi wa dini, Madaktari na Maafisa ustawi wa jamii, ambayo hupitia maombi yote ya upandikizaji figo.

Kamati hiyo hukagua nyaraka za uthibitisho wa uhusiano wa damu kati ya Mgonjwa na Mchangiaji, ikiwamo Viapo, Vyeti vya kuzaliwa, Picha pamoja na majibu ya vipimo vya maabara.

Hata hivyo Hospitali ya Taifa Muhimbili imesisitiza kuwa itaendelea kuhakikisha huduma ya upandikizaji figo inatolewa kwa mujibu wa kanuni zake na miongozo ya kimataifa.

0 Comment

Vifo vya tetemeko la Ardhi Afghanistan vyafikia 1,400Afyaclass Bongo Social •

Vifo vya tetemeko la ardhi nchini Afghanistan vimefika 1,411 huku zaidi ya nyumba 8,000 zikiharibiwa. Wokoaji wanapambana kufika vijiji vilivyo milimani wakati misaada ya kimataifa ikianza kumiminika.

Idadi ya waliofariki kutokana na tetemeko kubwa la ardhi lililotikisa Afghanistan imeongezeka hadi 1,411, kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu la Afghanistan (Afghan Red Crescent Society). Shirika hilo la kibinadamu limesema pia zaidi ya watu 3,124 wamejeruhiwa na zaidi ya nyumba 8,000 zimeporomoka kutokana na tetemeko hilo.

Katika mkoa wa Kunar, ambako ndiko kitovu cha tetemeko hilo lenye ukubwa wa kiwango cha 6, waokoaji wanafanya juhudi za kufika vijiji vya milimani ambavyo bado havijafikiwa. Kwa mujibu wa Ehsanullah Ehsan, mkuu wa idara ya usimamizi wa majanga mkoani humo, operesheni za uokoaji zimekamilika katika vijiji vinne na sasa zinalenga maeneo yaliyo mbali zaidi.

"Hatuna uhakika ni miili mingapi bado imekwama chini ya kifusi,” alisema Ehsan. "Lengo letu ni kukamilisha shughuli hizi haraka iwezekanavyo na kuanza kugawa msaada kwa familia zilizoathirika.”

Changamoto kubwa inayokwamisha juhudi za uokoaji ni barabara nyembamba za milimani na hali mbaya ya hewa, ambazo zimezuia magari kufika maeneo yaliyoathirika. Mashine maalum zimesafirishwa ili kuondoa kifusi barabarani na kurahisisha upatikanaji wa huduma za msaada.

0 Comment

Zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na magonjwa ya akili: WHOAfyaclass Bongo Social •

Zaidi ya watu bilioni moja duniani wanaishi na changamoto za afya ya akili kama vile msongo wa mawazo na mfadhaiko, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO.



Takwimu hizo zinasema mzigo huu ni wa kibinadamu na kiuchumi, huku magonjwa ya akili sasa yakiwa sababu ya pili inayoongoza kwa ulemavu wa muda mrefu.

“Kubadilisha huduma za afya ya akili ni moja ya changamoto kubwa zaidi za afya ya umma,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus. “Kuwekeza katika afya ya akili ni kuwekeza kwa watu, jamii na uchumi ni uwekezaji ambao hakuna nchi inayoweza kuupuuzia.”

Kujiua ni janga la dunia miongoni mwa vijana

Ripoti hiyo inaonesha taswira ya kutisha ya matukio ya kujiua, ambapo inakadiriwa kuwa watu 727,000 walipoteza maisha mwaka 2021 pekee kwa kujiua. WHO inasema ni moja ya vyanzo vikuu vya vifo miongoni mwa vijana kote duniani, bila kujali kipato au eneo waliko.

Licha ya juhudi za kimataifa, WHO inaonya kwamba maendeleo ni ya taratibu mno ili kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kupunguza vifo vya kujiua kwa theluthi moja ifikapo 2030.

“Kwa mwenendo wa sasa, dunia itafanikisha upungufu wa asilimia 12 pekee,” ripoti inabainisha, ikisisitiza haja ya kuongeza kasi ya hatua.

Gharama ya trilioni ya magonjwa ya akili

Zaidi ya mateso ya kibinadamu, kwa mujibu wa ripoti athari za kifedha ni kubwa mno. Msongo wa mawazo na wasiwasi peke yake hugharimu uchumi wa dunia takriban dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka kutokana na kupoteza uzalishaji.

Gharama za matibabu huongeza mzigo kwa familia na serikali. “Afya ya akili si suala la kiafya pekee ni suala la kiuchumi linalotishia ukuaji na uthabiti endapo litaachwa bila kushughulikiwa,” limesisitiza shirika la WHO.

Uwekezaji usio sawa na pengo linalopanuka

Ripoti hiyo “Ramani ya Afya ya Akili 2024” imeonesha hali ya kusuasua katika ufadhili. Kiwango cha kati cha serikali duniani ni asilimia 2 pekee ya bajeti za afya kinachotolewa kwa afya ya akili, kiwango ambacho hakijabadilika tangu mwaka 2017.

Tofauti ni kubwa imesema ripoti wakati nchi za kipato cha juu zinatumia hadi dola 65 kwa kila mtu, wakati nchi za kipato cha chini zinatumia senti 4 pekee. “Takwimu hizi zinaonesha ukosefu mkubwa wa usawa ambapo mamilioni wanakosa huduma kwa sababu tu ya mahali walipozaliwa,” limesema shirika la WHO.

Hatua za kisera zipo, lakini sheria bado zinasuasua

Kwa upande wa mafanikio, nchi nyingi zaidi sasa zinafanyia marekebisho sera na kuanzisha huduma za kijamii na programu za afya ya akili shuleni. Zaidi ya asilimia 80 sasa zinatoa msaada wa kisaikolojia wakati wa dharura, ikilinganishwa na asilimia 39 pekee mwaka 2020.

Hata hivyo, mageuzi ya kisheria yanayokwenda sambamba yamechelewa, WHO inasema chini ya nusu ya nchi zina sheria za afya ya akili zinazolingana na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu.

“Bila ulinzi wa kisheria, walio hatarini zaidi huendelea kukabiliwa na unyanyapaa, kupuuzwa na hata kudhalilishwa,” ripoti imeonya.

Wito wa hatua za haraka za dunia

Wakati Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Afya ya Akili na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza ukipangwa kufanyika Septemba 2025, WHO inazitaka nchi kuchukua hatua thabiti sasa. Vipaumbele ni pamoja na ufadhili wa haki, marekebisho ya kisera na kisheria, kuimarisha wataalamu wa afya ya akili, na kupanua huduma shirikishi zinazomlenga mtu.

Dk. Tedros ametoa ujumbe ulio wazi “Kila serikali na kila kiongozi ana jukumu la kuchukua hatua kwa dharura na kuhakikisha kwamba huduma za afya ya akili zinachukuliwa si kama heshima ya wachache, bali kama haki ya msingi kwa wote.”

0 Comment

Kuongezeka kwa idadi ya Simba Nchini India yawa tishioAfyaclass Bongo Social •

Kuongezeka kwa idadi ya Simba Nchini India yawa tishio

Japokuwa kitendo cha kuongezeka kwa idadi ya Simba Nchini India kinaonekana kama ni mafanikio kwenye sekta ya uhifadhi, kwa upande mwingine kitendo hicho kinaonekana kuwa tishio kwa maisha ya Binadamu na Mifugo katika Jimbo la Gujarat, Magharibi mwa Nchi hiyo.

Simba hao wamekuwa wakiua Binadamu pamoja na Mifugo ambapo tukio la hivi karibuni linamhusu Mtoto wa miaka mitano aliyeuawa na Simba wakati akicheza na Kaka zake kwenye shamba lililo karibu na nyumba yao ambapo Baba yake amesema Simba huyo alitokea ghafla na kumbeba Mtoto huyo licha ya Familia yake kurusha mawe na fimbo kujaribu kumuokoa na kisha baada ya muda mwili wa Mtoto huyo ulipatikana Msituni.

Mtoto huyo ni mmoja wa Watu saba waliouawa na Simba kati ya Juni 2024 na Juni 2025 ambapo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita zaidi ya Watu 20 wamepoteza maisha kwa mashambulizi ya Simba huku visa vya kushambuliwa kwa Mifugo vikiongezeka maradufu.

Simba wa Asia ambao ni wadogo kidogo kuliko Simba wa Afrika hutambulika kwa manyoya meusi mazito na mikunjo ya ngozi tumboni mwao ambapo inaelezwa kuwa waliwahi kuishi katika maeneo ya Mashariki ya Kati na Asia lakini sasa Jimbo la Gujarat ndilo pekee Duniani lenye Simba pori hao.

0 Comment

Tumia maombi ya Shukurani ili kuingia kwenye Uwepo wa MunguAfyaclass Bongo Social •

Tumia maombi ya Shukurani ili kuingia kwenye Uwepo wa Mungu

Zaburi 100:4 "Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake".

Aina hii ya maombi;

•Humfanya Mungu akukaribie na kukusaidia

•Huleta Ongezeko,Mfano Yesu alitumia maombi ya Kushukuru;Mikate na Samaki wakaongezeka sana(Soma yohana 6:11)

Yohana 6:9-11

Mstari wa 9"Yupo hapa mtoto, yuna mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hivi ni nini kwa watu wengi kama hawa?

Mstari wa 10 "Yesu akasema, Waketisheni watu. Na mahali pale palikuwa na majani tele. Basi watu waume wakaketi, wapata elfu tano jumla yao.

Mstari wa 11 "Basi Yesu akaitwaa ile mikate, akashukuru, akawagawia walioketi; na kadhalika katika wale samaki kwa kadiri walivyotaka.

•Ni Silaha dhidi ya manung'uniko:Nenda mbele za Mungu kwa Kumshukuru hata kama kuna mambo hajafanya kama vile ulivyotaka, Hali ya kunung'unika itaondoka ndani yako,Imani yako kwake itaongezeka Na Mungu atajibu na haja zako ulizonazo.

Tazama Full Video Hapa:

0 Comment

Klabu ya Simba SC imetambulisha rasmi jezi zao mpya zitakazotumika msimu mpyaAfyaclass Bongo Social •

Klabu ya Simba SC imetambulisha rasmi jezi zao mpya zitakazotumika msimu mpya wa 2025/26.



Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wamezindua rasmi jezi zao watakazotumia msimu wa 2025/2026 katika michezo ya Ligi Kuu.

Simba SC wamezindua jezi za aina tatu, nyekundu, nyeupe na bluu, ikiwa ni jezi zao za kwanza za mashindano kutengenezwa na mzabuni mpya Jayrutty kwa kushirikiana na Diadora.

0 Comment

Dalili 8 Ambazo Mtu Huweza Kuzipata Baada Ya Kidonda Chake Kushambuliwa Na BacteriaAfyaclass Bongo Social •

Dalili 8 Ambazo Mtu Huweza Kuzipata Baada Ya Kidonda Chake Kushambuliwa Na Bacteria


1. Homa

 Baada ya upasuaji, ni kawaida kwa wagonjwa kuwa na homa kwa kiwango cha chini ya digrii 100 Fahrenheit. lakini, ikiwa joto la mwili lipo juu hadi 101 au zaidi, hiyo inaweza kuonyesha uwezekano wa maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria katika kidonda. 

 Wagonjwa ambao wana homa wanaweza pia kuwa na tatizo la maumivu ya kichwa na kupungua kwa hamu ya kula.

Vidonda vilivyoshambiwa na Bacteria vinaweza kupatiwa tiba ya antimicrobial drugs n.k.

 2. Mwili kuchoka kupita kiasi

 Kumuuliza mgonjwa jinsi anavyohisi inaweza kusaidia kutathmini uwepo wa maambukizi katika kidonda.

Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi pamoja na mwili kukosa nguvu huweza kuwa kiashiria mojawapo cha uwepo wa maambukizi kwenye kidonda au jeraha ulilonalo.

 3. Kidonda kutoa usaha au maji maji yenye rangi ya Kijani au Njano

 Katika hali ya kawaida kidonda kinatakiwa kiwe na rangi nyekundu, hii ndyo ishara nzuri ya kidonda kuelekea kupona kwa urahisi

 4. Kuongezeka kwa Maumivu katika Jeraha au Kidonda

 Kwa ujumla, mgonjwa anayeendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji au  kuwa na jeraha/kidonda anapaswa kuona unafuu na maumivu yanayopungua na sio kuongezeka.  

Ikiwa mgonjwa ana maumivu yanayoongezeka badala kupungua, hiyo inaweza kuwa dalili ya maambukizi katika jeraha au kidonda. 

 5.Uwekundu Kuzunguka Jeraha au kidonda huku ndani ya kidonda kukiwa na rangi ya tofauti kama vile njano au kijani

 Hapo awali, vidonda vinaonekana vyekundu kidogo kwa sababu ya mchakato wa uchochezi wa asili wa uponyaji, lakini uwekundu huo unapaswa kupungua polepole kwa takribani siku 5-7. 

 Uwekundu zaidi karibu na jeraha huku ndani ya kidonda kukiwa na rangi nyingine ya tofauti kama njano au kijani ni ishara ya maambukizi katika jeraha. 

 6. Uvimbe wa Eneo Lililojeruhiwa

 Kama uwekundu, uvimbe ni kawaida katika hatua za mwanzo za uponyaji wa jeraha. lakini, uvimbe unapaswa kupungua kila wakati.  Uvimbe wa kudumu inaweza kuwa ishara ya maambukizi au shida zingine kwenye kidonda.

 7. Joto La Ngozi Inayozunguka kidonda

 Ingawa inaweza kuwa kawaida kwa ngozi inayozunguka jeraha kuhisi joto kali, Lakini endapo ngozi inayozunguka kidonda huhisi joto sana kwa kugusa bila kupoa, hiyo inaweza kuonyesha kwamba mwili unapanga mashambulizi dhidi ya maambukizi. 

 Joto husababishwa na kutolewa kwa kemikali za vasoactive zinazoongeza mtiririko wa damu kwenye eneo hilo.  Kwa kuongezea, mfumo wa kinga hutoa joto zaidi kwa kutuma lymphocyte kutoa kingamwili kuharibu pathogen na phagocytes kumeza bakteria waliokufa.

 8. Kupoteza uwezo wa kufanya kazi katika kiungo chenye jeraha au kidonda

 Ishara nyingine ya maambukizi kwenye jeraha ambayo inaweza kuhitaji matibabu, ni wakati mgonjwa amepoteza uwezo wa kiutendaji kwenye kiungo au eneo lilithoathiriwa. 

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD