Kuhisi vitu vinatembea mwilini,chanzo chake na Tiba
Hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini kwa kitaalam hujulikana kama Formication
Baadhi ya watu hupatwa na shida hii ya kuhisi kama kuna Vitu vinatembea Mwilini Kila wakati,
Je chanzo chake ni nini?
Chanzo cha Kuhisi vitu vinatembea mwilini
Zipo Sababu mbali mbali ambazo huchangia hali hii,na baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na hizi:
1. Ugonjwa wa brucella:
Kwa Asilimia Kubwa hizi ni dalili za Ugonjwa wa Brucella
Ugonjwa wa Brucella ni ugonjwa ambao kwa kitaalam hujulikana kama Brucellosis na chanzo chake kikubwa ni maambukizi ya Bacteria wanaojulikana kama BRUCELLA,
Bacteria hawa hutoka kwa wanyama mbali mbali kama vile; Ng'ombe, mbuzi,kondoo,Nguruwe,Mbwa n.k,
Baadhi ya dalili zake ni:
- Mgonjwa kupatwa na homa ambazo hujirudia mara kwa mara
- Mgonjwa kuhisi kama vile kuna vitu vinatembea mwilini mwake, na wakati mwingine huhisi kama minyoo wakati wa kujisaidia haja kubwa
- Mgonjwa kuanza kutetemeka mwili baada ya kuhisi baridi kali au kuwa na Homa
- Mgonjwa kupoteza kabsa hamu ya kula chakula au kitu chochote
- Mwili kuchoka Sana
- Kupata maumivu ya Viungo,joint n.k.
2. Matatizo kwenye mfumo wa Neva(Neurological conditions):
Kwa Mtu mwenye ugonjwa wowote unaoathiri utendaji kazi wa Neva anaweza kupata dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini, Mfano ni magonjwa kama vile;
- Ugonjwa wa kisukari ambao husababisha hali inayoitwa diabetic neuropathy n.k.
3. Kuwa na matatizo katika afya ya Akili:
Wakati mwingine ukiwa na Msongo wa mawazo mkubwa,Hofu sana,au hali zingine zinazohusu afya ya akili unaweza kupata dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,
4. Matumizi ya baadhi ya Dawa:
Zipo baadhi ya dawa ukitumia unaweza kupata hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,
5. Matatizo ya Ngozi(Skin conditions):
Yapo baadhi ya matatizo ya ngozi kama vile;
- Tatizo la ngozi kuwa kavu(Dry skin),
- Mzio kwenye ngozi(Skin allergic reactions),
- Au matatizo kama scabies wakati mwingine huweza kusababisha hali hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,
6. Upungufu wa Virutubisho mwilini(Nutritional deficiencies):
Baadhi ya tafiti zinaonyesha,Kuwa na kiwango kidogo cha madini kama vile magnesium au upungufu wa Vitamini B mwilini huweza kuchangia pia dalili hii ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini,
7. Mabadiliko ya Vichocheo mwilini(Hormonal changes):
Mfano kwa Baadhi ya Wanawake wakifika kipindi cha ukomo wa hedhi(menopause) hupata mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini, hali ambayo huweza kuchangia dalili hii pia ya Kuhisi vitu vinatembea mwilini.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
image quote pre code