Mbunifu na Mwanamitindo mashuhuri duniani kutoka nchini Italia Giorgio Armani, amefariki dunia hii leo Septemba 4, 2025 akiwa na umri wa miaka 91, Kampuni yake imethibitisha.
Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Kampuni ya Giorgio Armani imeeleza “kwa huzuni isiyo na kifani Kampuni ya Armani Group inatangaza kifo cha muasisi wake, mbunifu na nguvu isiyochoka ya kuendesha chapa hii Giorgio Armani”
Armani alikuwa mbunifu na nembo ya mitindo na ustadi wa Kitaliano wa kisasa na alijulikana kwa kuchanganya ubunifu wa hali ya juu na ujasiriamali, akiendesha kampuni iliyokuwa ikipata mauzo ya takribani Euro bilioni 2.3 kwa mwaka.
Kwa muda fulani alikuwa akisumbuliwa na maradhi na Juni mwaka huu alilazimika kukosa maonesho ya kampuni yake katika Milan Men’s Fashion Week ikiwa ni mara ya kwanza katika taaluma yake yote kukosa kushiriki kwenye maonesho ya mitindo aliyoyasimamia.
Kampuni ya Armani Group ndio wamiliki wa bidhaa mbalimbali za mavazi ya kike na kiume ya Emperial Armani pamoja na Perfume za Emperial Armani pamoja na saa zake ambapo kwa mujibu wa jarida la Forbes mpaka anafariki alikuwa na utajiri wa bilioni 12.1.
image quote pre code